Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 059 (Would that the Salvation in the Believers of the Gentiles incite Jealousy in the Children of Jacob)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 2 - HAKI YA MUNGU HAISOGEI HATA BAADA YA WATOTOWA YAKOBO, WATEULE WAKE, KUFANYA MIGUMU MIOYO YAO (Warumi 9:1-11:36)
5. Tumaini la watoto wa Yakobo (Warumi 11:1-36)

b) Heri kwamba, wokovu katika waumini kutokana na watu wa Mataifa uchokoze wivu ndani ya watoto wa Yakobo (Warumi 11:11-15)


WARUMI 11:11-15
"11 Basi nasema, Je! Wamejikwaa hata waanguke kabisa? Hasha! Lakini kwa kosa lao wokovu umewafikilia Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu. 12 Basi, ikiwa kosa lao limekuwa utajiri wa ulimwengu, na upungufu wao umekuwa utajiri wa Mataifa, je! Si zaidi sana utimilifu wao? 13 Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu, 14 nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi na kuwaokoa baadhi yao. 15 Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?“

Paulo alilipenda taifa lake jinsi alivyowapenda ndugu na dada zake za damu. Hakufikiri kwamba, Mungu atawaadhibu kwa sababu ya kutokutii kwao na hatua yao ya kumkataa Yesu, lakini alitambua kwamba, kuwakataa hao wateule wa agano la kwanza kutatokeza wakati huo uchaguzi mpya kutokana na mataifa yasio safi. Kuanguka kwa Wayahudi kulileta nafasi kwa wale ambao hawakuamini kutoka kwa Mataifa, nafasi ya kipekee kutambua wokovu, ambao ulitayarishwa mapema, na wakapokea wokovu huo kwa njia ya imani ndani ya Kristo.

Kuenea kwa wokovu kati ya Mataifa kulianzisha wivu ndani ya watoto wa Yakobo. Hata hivyo Paulo aliona jambo moja la kufaa katikati ya hiyo wivu uliowaka sana mioyoni mwa Wayahudi; kwamba wangetambua hao wasio safi na wanaishi mbele za Kristo, nao pia wanapokea upatanisho na Mungu, wakijaliwa na furaha ya Roho Mtakatifu, hata wawapende na adui zao. Hapo hao wacha Mungu kati ya watoto wa Ibrahimu wangepata kufahamu kwamba, hao maskini na wa kukataliwa sasa wamepokea jambo bora, si kutokana na utamaduni wao, bali moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Paulo alitamani sana kwamba, hao Wayahudi wenye kuasi na wa kujitosheleza wenyewe wangeshikwa na wivu kwa ajili ya hao wasioamini ambao sasa wamezaliwa mara ya pili, na hapo wangetambua kwamba, baraka za Ibrahimu, Isaka na Yakobo ziliishi na ndani yao. Alitegemea kwamba, watu wake wangebadilika rohoni mwao, ndipo waamue kushiriki ndani ya urithi wao nao, ambayo sasa imetimizwa ndani ya wageni. Katika ufahamu wa namna hiyo Kristo aliwaambia wanafunzi wake: „Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.“ (Mathayo 5.14-16).

Paulo anakamilisha mpango wake wa kuhubiri kwa Wayahudi, akisema: Ikiwa kuvunjika kwa Wayahudi kulipata kuwa chemchemi ya baraka kwa wale waliokataliwa, na ikiwa kupungua kwao kwa baki takatifu kulitokeza wokovu wa umati mkubwa kutoka kwa mataifa, si kubwa sana basi itakuwa kurudi kwao sababu ya kuzidisha mno baraka ya kulipuka kote ulimwenguni! Ikiwa kweli Wayahudi wote wangeamini ndani ya Kristo, nguvu ya imani yao na kina cha kujisikia kwao kungetokeza nguvu ya kuhubiri duniani, ikitokeza chemchemi za maji ya uhai ndani ya majangwa ya dunia yetu, yangemiminwa na kubadilisha ukame kuwa paradiso ya uhai hata kati ya mawimbi ya dhambi.

Paulo kwa mtazamo wake mwerevu aliwahangaisha Wakristo hata pengine wawapende na kuwasamehe watoto wa Yakobo, na hivyo washinde mioyo yao yenye ukorofi na kiburi kwa uvumilivu na unyenyekevu (Mathayo 11:28-30).

Ndipo Paulo akawaelekea waumini toka kwa Mataifa waliokuwa wa kanisa la Rumi, ili awapete na kuwatingisa. Alikuwa akiwaangalia Wayahudi kwa ukweli wa kiroho, akiwaambia kwanza: Yesu hakunituma kuwa mhubiri kati yenu Wayahudi, bali alinikabidhi niwe mtume kwa watu wa Mataifa, katikati ya mamia ya miungu iliyojaa na roho chafu. Kwa furaha naendeleza huduma hii, nikijifunza lugha zao, nikitafakari utamaduni wao na hivyo kuleta uungwana wa Yesu kwa hao waabuduo miungu yao najisi, na pia kwa ukahaba wao wa hadharani.

Paulo aligundua katika huduma yake nafasi ya kuhubiri pia kwa Wayahudi kwa namna ya mzunguko. Alikusudia kuwashangaza watoto wa Ibrahimu kwa mwenendo mtakatifu wa Wakristo na kwa changizo lao dhahiri kule Asia na Ulaya. Alifanya hivyo, ili kuanzisha hamu ya kiroho ndani yao, ili pengine baadhi yao warudi kutoka kwa kosa la njia yao, wapate kujifunza na imani ya watu toka kwa Mataifa, na pia wapate kumfuata Kristo aliyefufuka katika wafu. Paulo alitumaini kwamba, wateule wa agano la awali waliokataliwa sasa, wapokee kwa upya kwa kurudi kwao lile vazi la agano, maana ahadi za Mungu kwao bado zinawafaa na kuwa halali.

Ikiwa kukataa kwao kwa Mfalme wao Yesu ilisababisha upatanisho kati ya Mungu na ulimwengu, kiasi gani zaidi ya hapo kurudi kwao walio na hali ya kufa kiroho kutaleta ukamilisho wa uhai ndani ya Mungu?! Paulo mwenyewe alitambua ushindi wa nguvu ya Mungu juu ya kufa kwake kiroho na makosa yaliyojulikana maishani mwake, na Bwana alimwokoa (pale karibu na Dameski), iwapo alikuwa mkatili katika ushupavu wake. Basi alitazamia yayo hayo kwa ajili ya watu wa taifa lake, na kwa sababu hiyo aliyakinisha kuwafanya wawe washiriki katika uzima wa milele, ili na wao waeneze uhai wa neema ya Kristo katika ulimwengu mzima.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakushukuru na kukuabudu kwa sababu umetumia ule ugumu wa Wayahudi kuwa baraka kwa Mataifa yote. Utusaidie tusiishi kwa kujipendeza wenyewe kiroho, bali tuwahudumie wote kwa njia ya Roho yako Mtakatifu kwa maneno, matendo na maombi, ili tuwaongoze wengi kati ya wale wasioamini pamoja na watoto wa Ibrahimu waingie ndani ya imani hai ya Yesu Kristo. Amina.

SWALI:

  1. Ugumu ule wa Wayahudi ulikuwa na maana gani kwa ajili ya watu najisi ya Mataifa?
  2. Jinsi gani Wakristo wataweza kuwasihi wasioamini waingie kwenye imani ya kweli?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 07:31 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)