Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 055 (The Aggravation of the Offense of the Israelite People)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 2 - HAKI YA MUNGU HAISOGEI HATA BAADA YA WATOTOWA YAKOBO, WATEULE WAKE, KUFANYA MIGUMU MIOYO YAO (Warumi 9:1-11:36)
4. Haki ya Mungu hupatikana tu kwa imani, wala si kwa kujaribu kutimiza sheria (Warumi 9:30 - 10:21)

b) Uchokozi wa kasirisho la watu wa Israeli kwa sababu Mungu aliwarehemu zaidi kuliko watu wengine wowote (Warumi 10:4-8)


WARUMI 10:4-8
"4 Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. 5 Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. 6 Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), 7 au, ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) 8 Lakini yanenaje? Lile neno ni karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.“

Paulo ashuhudia kwamba, shabaha ya mwisho wa sheria ni Kristo Yesu, kwa maana yeye ndiye njia, kweli na uzima. Hakuna awezaye kumfikia Baba ila kwa njia ya yeye (Yohana 14:6).

Kristo kwa kikamilifu alitimiza madai yote ya sheria, tena pamoja na vipengele vyake vyote, naye akapata kuwa mfano wa kufuata. Kwa hiyo tunapojilinganisha sisi na yeye, tunajikuta tu wachafu. Na tamko hilo lawahusu wote wawili, Wayahudi na Wakristo, maana wote walitenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, maana wote tunapungukiwa upendo na ukweli (Mambo ya Walawi 18:5 na Warumi 3:23).

Basi wakati uo huo, Yesu aliupatanisha ulimwengu wote na Mungu Mtakatifu kwa njia ya kifo chake cha kutulipia (2.Wakorintho 5:18-21). Kristo alitimiza sheria ya awali kwa kikamilifu, na kwa sababu hiyo yeye ndiye sheria yetu mpya, ambaye ndani yake tunaona sheria ya neema. Tangu kifo chake cha kutulipia haki yetu mpya imekamilika kwamba, tunaweza kupokea kuhesabiwa haki kwa neema, ili tuweze kupokea uzima wa milele. Hivyo basi, Kristo ndiye sababu yetu ya kuhesabiwa haki (Isaya 45:24 na Yeremia 23:6 na 33:16), na yeyote amgeukiaye, huyu hatahukumiwa.

Bwana asema ndani ya sheria ya Musa: Yeye atakayeshika maagizo yangu, ataishi. Lakini hakuna aliyezishika maagizo ya Mungu, ila Yesu pekee. Kwa hiyo, hakuna atakayeishi milele kwa nguvu yake mwenyewe. Ndiyo maana Wayahudi wanajaribu, kwa njia ya sala zao, huduma zao, kufunga, na matazamio yao ya kumleta chini Masihi aliyeahidiwa, ili awaokoe na ghadhabu ya Mungu. - Upande wa pili, hawataki kusikia habari ya Masihi wa kweli, wala kumwelekea yeye aliyeshuka kwa mapenzi yake. Haki ya kutoka imani haihitaji Kristo mwingine mpya kushuka toka mbinguni, wala Kristo mpya atakayefufuka kutoka kwa wafu; maana tayari Kristo ameesha kuja chini kwetu (Luka 2:11) naye akafufuka kutoka kwa wafu (Mathayo 28:5+6). Neno hilo la uzima limekwisha kuwafikia watu wengi. Neno la Injili linalohubiriwa linajaa na mamlaka ya Kristo. Yeyote atakayelisikia na kuliamini atapokea baraka ya Injili hii moyoni mwake; na yeyote atakayelitamka atatambua kwamba limo mdomoni mwake. Tu watajiri kuliko tunavyofahamu, na kwa sababu hiyo inatupasa kulitoa kwa wengine wapate kushiriki katika chakula hiki cha kiroho, maana watu wanajifikiria kuwa wakubwa na wenye uwezo, wakati kwa kweli ni wa kutazamia mauti, nao ni wa kufa katika dhambi na chuki.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakuabudu kwa sababu ulimtuma Mwana wako wa pekee, ili atimize amri zako, na hivyo kuondoa dhambi za ulimwengu na kulipia kwa ajili yetu. Tangu kifo chake cha malipo kwa makosa ya dunia yote, sheria haiwezi tena kutushitaki. Yesu kweli amekomesha enzi ya sheria, naye ametuleta ndani ya enzi au utawala wa neema. Amina.

SWALI:

  1. Je, maana ya usemi wa Paulo ni nini, anapotamka: Kristo ni mwisho wa sheria?
  2. Kwa nini Wayahudi wanatazama mbele kwa ajili ya kuja kwa Masihi wao?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 05:54 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)