Previous Lesson -- Next Lesson
a) Wayahudi hawakujali haki ya Mungu inayopatikana kwa imani, nao wananing‘inia kwenye matendo ya sheria (Warumi 9:30 - 10:3)
WARUMI 9:30 - 10:3
"30 Tuseme nini basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani; 31 bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria. 32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo, 33 kama ilivyoandikwa, Tazama naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika. 10:1 Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. 2 Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. 3 Kwa maana , wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu.“
Mtume Paulo alijaribu kwa vipengee kuwageuza washiriki wa kanisa la Rumi, wasishikane na uamuzi wao wa mwisho kwamba, wapate kutambua kwamba, haki ya Mungu wanaipata tu kipekee kwa njia ya imani yao ndani ya Kristo, na ya kwamba haki yenye msingi wa matendo inawapeleka wajuzi wa kidini kwenye uharibifu. Swali lake lilikuwa dhahiri. Mtume Paulo alikiri mbele ya baraza la kanisa la kwanza, na hasa hasa mbele za wale walioshika haki kutokana na sheria kwamba, hata mmojawao hakuweza kushika kweli na kutimiza maagizo yote ya Mungu, na ya kwamba hata mmojawao ataokolewa na matendo yake, bali kwa neema ya Mungu, ambayo inapatikana tu ndani ya Kristo (Matendo ya Mitume 15:6-11). Yeyote anayedharau neema ya Kristo anafanana na mtu atembeaye gizani, abaye kwa mstuko atajikwaa kwenye jiwe kubwa njiani kwake, akaanguka chini na kuharibika (Isaya 8:14 na 28:16).
Ingawa Kristo ali wapatanisha Wayahudi na Mungu wao, kwa wengi wao akapata kuwa sababu ya kuhukumiwa, kwa sababu walikataa neema yake ya kipekee. Hata hivyo, wale waliomtambua Mwokozi wao, nao walioamini ndani yake, wakapata kuokolewa.
Paulo alikiri kwamba, Wayahudi wengi walikuwa wenye bidii katika kushika sheria, pia walifanya juu chini, ili kutii maagizo yote. Aliwapenda, kwa sababu ya bidii zao, naye alitumaini kwamba, watatwaa nafasi nzuri za maisha yao, nao wakubali zawadi ile kuu waliojaliwa. Kwa hiyo Paulo alimwomba Mungu sana na kumsihi kwa bidii kwamba, wengi wao wapate kuongozwa kwenye wokovu uliotayarishwa kwa ajili yao. Lakini basi, Paulo alitambua mahali pa kuu pa biashara katika utawala wa Kirumi kwamba, mara nyingi Wayahudi waliendelea kushikana na sheria zao. Walijiona kuwa ndiyo watu wateule wa Mungu, nao wakawaangalia watu wengine kama takataka tu. Hawakutambua haki ile mpya ya Mungu ndani ya Kristo, bali walijaribu kwa kufunga, kwa sala, sadaka, matoleo, pia na kuhiji watimize kikamilifu maagizo yale 613, na hivyo kuthibitisha hali yao ya bila makosa, basi kwa njia hiyo walikataa ile haki ya kweli ya Mungu. Loo, jinsi mawazo hayo yalivyo ya kudanganya! Na jinsi yalivyoleta kwa njia hiyo hali ya maumivu juu yao wenyewe!
SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakuabudu, maana na sisi waumini tunatoka kwa watu wa Mataifa waliokuwa najisi, lakini kutokana na ukuu wa neema yako tumepokea baraka moja baada ya nyingine, nawe umetujalia haki yako mwenyewe kuwa zawadi kuu kwetu. Kwa hiyo tunakuomba utolee baraka hizo nazo kwa wafuasi wa dini zingine, wanaofikiri kwamba, matendo yao yenyewe yataweza kuwapatia haki. Twaomba sana, uvunje kiburi chao, na uwasaidie waamini ndani yako na kukutegemea kama watoto wanaopendwa.
SWALI:
- Kwa nini mamilioni ya waumini kutokana na watu mbalimbali waliweza kupokea haki ya Mungu na kuimarika ndani ya neema hiyo?
- Kwa nini watu walio wacha Mungu wa dini zingine wanajaribu kwa bidii kutimiza sheria zao ili wapokee haki za Mungu?