Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 053 (The Parable of the Potter and his Vessel)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 2 - HAKI YA MUNGU HAISOGEI HATA BAADA YA WATOTOWA YAKOBO, WATEULE WAKE, KUFANYA MIGUMU MIOYO YAO (Warumi 9:1-11:36)

3. Mungu anadumu kuwa mwenye haki, hata kama sehemu kubwa ya Waisraeli (Warumi 9:6-29)

c) Mfano wa mfinyanzi na chombo chake ni kwa ajili ya Wayahudi na Wakristo pia (Warumi 9:19-29)


WARUMI 9:19-29
"19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? Au mfinyanzi je? 21 Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuuthibitisha uwezo wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu; 23 tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; 24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa mataifa pia? 25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu. 26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, Ninyi si watu wangu, hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai. 27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema, Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa. 28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akimaliza na kulikata. 29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena, Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao, Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora."

Mapenzi ya mwanadamu, kiburi chake, na ufahamu wake kuhusu haki inachukia dhidi ya uchaguzi wa Mungu, mapenzi na matendo yake. Mwanadamu mwenye kutokutii ni kama sisimizi anayemwambia tembo: „Kwa nini unanikanyaga?“ (Isaya 45:9).

Mwanadamu hana haki kabisa kumwuliza Mungu au kumkasirikia, kwa sababu upeo wake wa mtu kuona na uwezo wake wa kibinadamu inayo mipaka ya karibu na ndogo sana kwa kulingana na hekima ya Mungu isiyo na mipaka, pia na utukufu wake na upendo.

Mtu awekaye tegemeo lake lote ndani ya Mungu wakati kama huu, ambapo mioyo ya watu binafsi na ya mataifa yamezidi kufanywa migumu, inampasa kuwa na utii kamili kwake Bwana wa ulimwengu huu na kumwinamia kwa shukrani nyingi. Kwa njia hiyo tu tunaweza kupokea jambo hilo kwamba, mtu kama Hitler aliruhusiwa kuua Wayahudi millioni sita ndani ya tanuru zake, bila kuwa na yeyote aliyeweza kumsimamisha au hata kumhoji. Kwa namna iyo hiyo hatuwezi kuelewa kwa nini Stalin aliruhusiwa kuua wakulima millioni ishirini katika muda wa kuimarisha mipango yake ya kisiasa, tena bila kuwa na mtu yeyote kujali.

Paulo anatupatia linganisho, ili kueleza hukumu za Mungu: Mfinyanzi aweza kuumba kutokana na donge la udongo chombo cha kufaa kwa matumizi ya heshima au kuleta sifa, au aumbe kingine cha kudharauliwa kinachofaa kwa kutupia takataka (Yeremia 18:4-6).

Mtume alisisitiza mfano huo na kusema juu ya vyombo vya ghadhabu ya Mungu, ambavyo Mungu aliviweka kwa uvumilivu kwa muda mrefu sana, na mwishoni alividondosha kwa ajili ya uharibifu. Paulo pia alisema kwamba, Mungu alipanga vyombo vya rehema tangu zamani, naye akavitayarisha kwa ajili ya utukufu utakaokuja. Kwa sababu hiyo, vyombo vya rehema zake vinatoka kwenye maeneo ya utukufu wa mwumbaji wao, nao vitarudia kwao.

Paulo hakutengeneza filosofia pasipo na rehema kutokana na yote aliyoyaona maishani mwake, bali anaeleza kwamba, mtengano kati ya wale wanaofukuzwa na ghadhabu ya Mungu, na wale wanaotukuzwa na rehema zake, basi haiwahusu tu watu wa mataifa, lakini pia na hao Wayahudi waliochaguliwa. Ili kuweka wazi kabisa shabaha hiyo, anataja ufunuo wa Mungu kwa nabii Hosea (2:23) kwamba, atawafanya wale ambao hawakuwa watu wake, hao nao wapate kuwa watu wake.

Mtume Petro naye alithibitisha katika waraka wake wa kwanza kwa watu wa mataifa walioamini kwamba: „Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki wa Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema“ (1.Petro 2:9-10)

Kufuatana na Paulo, kusudi hilo ni tukufu na la pekee, kwamba Mungu huwachagua wale ambao kwanza hawakuchaguliwa, naye huwaita wale ambao hawakuitwa wapate kuwa watoto wa Mungu (Warumi 9:26 na 1.Yohana 3:1-3). Wakati uo huo mtume anaweka wazi kwamba, nabii Isaya alitambua kwamba, Mungu atawaongoza waliochaguliwa na hata hivyo wakiwa wa kutokutii awafikishe kwenye dhiki kuu, na kama wataendelea hata hivyo katika kutokutii kwao, ataruhusu wapate kutawanywa, iwapo alitangulia kutamka kwamba, wataongezeka sana kwa hesabu zao kama mchanga wa baharini.

Bwana aliye hai huwatunza watu wake hata wakiwa wabishi. Maana si wote wao walioangamizwa, ila sehemu yao ndogo takatifu ndiyo salio ilidhihirika, ambao ndani yao ahadi za Mungu za kiroho zitaonekana (Isaya 11:1-6); na wakati huo wale wengine wengi katika watu walioitwa, basi watakuwa kama Sodoma na Gomora, ambao waliharibika kabisa (Isaya 1:9).

Paulo katika upendo wake alitamani kuwafundisha Wayahudi walioishi Rumi kwamba, Mungu anayo uhuru kuwaokoa watu wa mataifa wasiochaguliwa, lakini watakaswe kabisa, wakati ambapo aliwafanya wagumu Wayahudi wale walioamini hata wakapata kuangamizwa. Oni hilo halikumjia Paulo kama elimu ya kichwani tu, lakini lilipata kutambuliwa moyoni mwa mtume kwa kuzingatia wale Wayahudi waliojisifu juu ya haki yao wenyewe. Alijibidiisha kuwaongoza wafikie ungamo la kweli, ili ikiwezekana wapate kukiri kwamba Yesu ndiye Masihi aliyeahidiwa na kuwatolea wokovu. Lakini sehemu kubwa ya Wayahudi bado wanamkataa Yesu hata leo.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, utusamehe hali yetu ya juu juu, kama hatukutambua uvumilivu wako kuu sana, ambao wewe uliitumia kwa ajili yetu. Ulitupenda tangu muda mrefu sana, wala hujatuadhibu wala kutuharibu. Ututukuze zaidi na zaidi ili tuweze kutendana kwa upendo wako pamoja na kusema asante na shukrani; na kwa furaha tukubali kutii uongozi wa Roho yako Mtaka tifu kila wakati. Amina.

SWALI:

  1. Nani ndiyo vyombo vya ghadhabu ya Mungu, na zipi ni sababu za kutokutii kwao?
  2. Kusudi la vyombo vya rehema ya Mungu ni nini, na ipi ni mahali pao pa kuanzia?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 29, 2023, at 02:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)