Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 048 (The Truth of Christ Guarantees our Fellowship with God)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
E - Imani yetu itadumu daima (Warumi 8:28-39)

2. Ukweli wa Kristo unathibitisha ushirikiano wetu na Mungu mbali na matatizo yoyote (Warumi 8:31-39)


WARUMI 8:38-39
"38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti , wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.“

Paulo alikuwa na uhakika kwamba, hakuna kitu hapo duniani au hata roho ya kidunia ambazo zingeweza kumtenga na upendo wa Mungu uliodhihirishwa ndani ya Kristo Yesu. Kwa tamko hilo kuu la kujumlisha alifunga sehemu hii ya mafundisho ya waraka wake kwa Warumi. Kwa kweli hakuwa akitafakari tu au kuchambua maoni, lakini aliandika mambo yenyewe ya kwenda chini sana kuhusu mateso makuu na mahangaiko kutokana na ushuhuda wa Roho Mtakatifu moyoni mwake. Paulo hasemi, „ikimpendeza Mungu atakuwa nami“, lakini alikiri kwamba, utambuzi wa upendo wa Mungu ndani ya Kristo ulimhakikishia katika tendo la kukiri kwamba, upendo huo hautakosekana hata kidogo. Uaminifu wa Mungu hauna shaka lolote.

Paulo hakusema juu ya upendo wa kibinadamu, wala hakutamka habari ya Mungu mwenye rehema na upendo kwa jumla, lakini alimwona Baba kwa njia ya Mwana. Hakufahamu njia yoyote nyingine kwenda kwake Mungu, ila kwa njia ya Kristo. Basi ni tangu Mwana wa Mungu kuingia mwilini tunamfahamu yeye Aliye Juu, Baba yetu ni nani. Upendo wake wa kibaba sio huruma ya kibinadamu, maana Mtakatifu alitoa sadaka ya Mwana wake kwa ajili ya wasio safi, ili sisi tusitie mashaka katika rehema zake, bali tuwe na hakika kwamba, anatukaribisha ndani ya agano lake na kwa hatua ya kupokelewa kama watoto, kwa sababu ya kumwagwa kwa damu ya Mwana wake. Kwa sababu ya msalaba, Paulo alikuwa na hakika kwamba, upendo wa Mungu hautakosekana daima.

Hata hivyo, kwa ukweli Shetani yupo, na yeyote anayekana kuwepo kwake, hatambui hali halisi ya dunia hii. Paulo aliona nguvu za kiroho kadhaa zilizokuwa tayari kuangamiza dunia hii na ule ulimwengu mwingine. Paulo hakukabiliana na roho ya mauti tu mara kwa mara, lakini pia alishindana na malaika ya giza, naye alihangaika katika sala zake dhidi ya uovu wa kuzimu hata akatamka: „ Ikiwa kuzimu na mbingu zote pamoja zinanivizia, upendo wa Mungu ndani ya Kristo hautaniacha. Nguvu zote za kunipinga hazikuweza kunishinda, kwa sababu damu ya Kristo ya daima ilinitakasa.“

Paulo alikuwa na kipawa cha unabii. Aliona jinsi yule mwangamizi, mwongo na mwuaji alivyovisia kanisa, lakini hakuweza kulishinda, maana limo ndani ya Kristo, na shetani hawezi kulipokonya mkononi mwake.

Hata sheria takatifu haiwezi kusogeza imani ya mitume, hata kwa malalamiko, kwa sababu walifia msalabani pamoja na Kristo, naye anaishi ndani yao na kuwalinda. Hivyo mwumini atalindwa hata kwenye siku ya hukumu ya mwisho, maana Kristo ataendelea kuwa ni Mshindi mwaminifu kwake,.

Kwa sababu hiyo tunakuambia, wewe ndugu mpendwa, „Kabidhi roho yako, mwili wako na moyo wako kabisa kwenye upendo wa Mungu, nawe ushikamane na ule Utatu, ili na jina lako liandikwe ndani ya kitabu cha uzima, na upate kuendelea kuwa mtoto wa Mungu daima.

Haya na sasa utambue kwamba, Paulo hakuandika wimbo ule wa sifa juu ya upendo uaminifuwa Mungu kwa hali ya mtu mmoja kama yeye tu, alipoandika, „Mimi“, lakini alijumlisha maneno yake kwa kuandika „Sisi“ (wengi), akimaanisha kwa uhakika wale wote waumini walioko Rumi na makanisa kwa jumla yaliyozunguka Bahari ya Shamu. Ushuhuda wa imani yake inatumaanisha na sisi, tunapokubali mvuto wa sura hiyo iliyotangulia. Ndipo hatutaelekeza maccho yetu tu kwenye mambo yanayoonekana kuwa wenye nguvu na kubwa katika dunia hii, lakini tutanang‘ania kabisa kwenye upendo wa Mungu iliyofunuliwa ndani ya Kristo Yesu.

Maneno ya mwisho „Bwana wetu“, yanatokea kama mwisho wa wimbo huo. Upande wa pili, yanatuthibitishia ya kwamba, yeye aliyeshinda kule Golgotha, ndiye Bwana wa Mabwana, ambaye ndani ya nguvu yake tunapewa thibitisho la ulinzi wetu. Yeye hunyosha mkono wake wa kulia juu yetu, na hawezi kutuacha, kwa sababu anatupenda.

SALA: Ee Yesu, maneno yangu yanashindwa kutamka vema shukurani zangu. Wewe uliniokoa nami nimepata kuwa wako. Nijaze na upendo wako, ili maisha yangu yaweze kuwa ujumbe wa kusifu enzi yako, nami nipate kukutukuza katika uhakika kamili wa imani, nikifahamu kwamba, hakuna jambo linaloweza kunitenganisha na wewe, maana wewe ndiwe mwaminifu. Kwa vile umeketi kwenye mkono wa kulia wa Baba, yeye ndani yako na wewe ndani yake, ndivyo uniimarishe na mimi ndani ya haki yake, ili kitu chochote kisiweze kunitenga na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina.

SWALI:

  1. Kwa nini Paulo alianza sentenso yake ya mwisho na neno la „Mimi“ na kufunga na „Sisi“?

QUIZ - 2

Mpendwa msomaji,
Baada ya kusoma maelezo hayo kuhusu barua ya Paulo kwa Warumi katika mfululizo huo, bila shaka sasa utaweza kujibu maswali yafuatayo. Ukiyajibu kwa usawa kwa 90% ya maswali, tutakutumia mfululizo ufuatao ya masomo hayo kwa ajili ya maongozo yako mema. Unapotuma majibu kwa Posta, usisahau kuweka jina lako kamili na anwani yako waziwazi kwenye karatasi ya majibu yako.

  1. Yapi ndiyo mawazo makuu ndani ya hali yetu ya kupewa haki kwa imani?
  2. Ipi ni maana ya sentenso: “kuonyesha haki ya Mungu”?
  3. Kwa nini tumepewa haki kwa imani tu, wala si kwa matendo yetu mema?
  4. Jinsi gani Ibrahimu na Daudi walipata kuhesabiwa haki?
  5. Kwa nini mwanadamu huhesabiwa haki si kwa kutahiriwa, bali kwa imani tu?
  6. Kwa nini tunapokea baraka za Mungu kwa njia ya imani yetu ndani ya ahadi za Mungu, wala si kwa bidii yetu ya kushika sheria?
  7. Tunajifunza nini kutokana na mashindano ya imani ndani ya Ibrahimu?
  8. Jinsi gani amani ya Mungu inakamilika ndani ya maisha yetu?
  9. Jinsi gani upendo kuu wa Mungu ulijionyesha?
  10. Paulo anataka kutuonyesha nini kwa njia ya linganisho lake la Adamu na Yesu?
  11. Maana ya ubatizo ni nini?
  12. Jinsi gani tumesulibiwa na Kristo na kufufuka ndani ya uhai wake?
  13. Jinsi gani tutaweza kujileta wenyewe na viungo vya miili yetu ziwe silaha za haki kwa Mungu?
  14. Ipi ni utofauti kati ya mapingu ya dhambi na mauti, na upande wa pili upendo wa Kristo?
  15. Kwa nini waumini wote wameondolewa na madai ya agano la zamani?
  16. Ingawa inatufaa, mbona sheria inaweza kuwa sababu ya maovu na kifo kwetu?
  17. Mambo gani Paulo alikiri juu ya nafsi yake, na ungamo hilo linamaanisha nini kwa ajili yetu?
  18. Maana ya sentenso ya kwanza katika sura ya 8 ni nini?
  19. Zipi ni zile sheria mbili, ambazo mtume alizilinganisha pamoja, na maana yao ni nini?
  20. Yapi ndiyo mambo ya nia ya mtu wa kiroho? Na ipi ni mapokeo ya wale walio na hali ya kimwili?
  21. Wale wanaoamini ndani yake Kristo, Roho Mtakatifu anawajalia mambo gani?
  22. Jina mpya la Mungu ni lipi, ambalo Roho Mtakatifu atufundisha? Na maana yake ni nini?
  23. Ni wakina nani hao wanaougua moyoni kwa ajili ya kurudi kwake Kristo? Na kwa nini?
  24. Kwa nini mambo yote hufanya kazi pamoja kuwa mema kwa wale wampendao Mungu?
  25. Jinsi gani wakristo wanaweza kushinda taabu?
  26. Kwa nini Paulo alianza sentenso yake ya mwisho na „Mimi“ na kufunga na „Sisi“?

Ukikamilisha masomo ya mihula yote ya mfululizo kwa Warumi na kututumia majibu ya mwisho wa kila muhula, sisi tutakutumia

CHETI CHA
masomo ya kuendelea katika kufahamu barua ya paulo kwa Warumi

ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni.

Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii:

Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 Stuttgart
Germany

Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 16, 2022, at 07:22 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)