Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 047 (The Truth of Christ Guarantees our Fellowship with God)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
E - Imani yetu itadumu daima (Warumi 8:28-39)

2. Ukweli wa Kristo unathibitisha ushirikiano wetu na Mungu mbali na matatizo yoyote (Warumi 8:31-39)


WARUMI 8:31-32
"31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu? 32 Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?“

Baada ya Paulo kutuwekea wazi mfululizo wa mawazo ya Mungu kwa ajili ya wokovu na kuchaguliwa kwetu, ili tupate kuhakikisha habari ya kuchaguliwa kwetu, ndipo akatupatia na mfululizo wa mambo yaliyo kweli juu ya wokovu wetu, ili tupate kujua kwamba, Mungu ameimarisha wokovu wa ulimwengu juu ya matokeo ya kweli ya kihistoria.

Paulo alikuwa na uhakika moyoni mwake na bila shaka lolote alihakikisha rohoni mwake kwamba, Mungu hawezi kuwa adui yake, bali rafiki mwaminifu aliyeishi ndani yake, haidhuru litokee jambo gani, na pia kwa wakati wowote. Na zaidi ya hapo, aliamini kwamba huyu Mwenyezi na Mwumbaji wa mbingu na nchi ndiye Baba yetu. Mtume aliendelea ndani ya upendo wa Mungu na kumheshimu Mwenyezi kwa imani kamili siku zote za maisha yake. Alihesabia mambo yote kuwa ni miongozo ya upendo wa Baba yake na matunzo matukufu ya Mwokozi wake kwa ajili yake.

Jinsi gani Paulo alipata uhakika huo kamili, ulioweza hata kusogeza milima ya dhambi, pia na kuwainua milioni za watu wafu katika dhambi? Msalaba wa Kristo kwake ilikuwa ni thibitisho la upendo wa Mungu. Ndani ya Msulibiwa alitambua kwamba, wema wa huyu Mtukufu umefurikia kwetu, maana alimtoa Mwana wake wa pekee kuwa malipo kwa ajili ya aibu zetu kwamba, yeyote atakayeamini ndani yake asiwe wa kupotea.

Kwa kweli, Mungu alitupatia sisi tuliokuwa bila utii na wavunja amri, moyo wake, mbingu yake, na utukufu wake katika kuja kwake Mwanawe. Hakuna baraka nyingine mbinguni, ambayo Mungu alitunyima katika Kristo, maana alitupatia mambo yote kabisa ndani yake. Je, ndugu iko wapi basi kuabudu kwako? Kwa nini hujajitoa kwake kabisa na mambo yote ya kwako?

WARUMI 8:33-34
"33 Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. 34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.“

Pengine unafikiri kwamba, wokovu na hizo ahadi ni kwa ajili ya watakatifu tu na waumini waliokomaa, wakati ambapo wewe mwenyewe ni mwanafunzi tu, bila kufaulu viziri, anayesitasita na mchafu. Basi unyamaze na kusikiliza uamuzi wa Mungu juu yako. Yeye amekufa na kuwa mwenye haki na bila lawama, na hiyo si kwa sababu ya wema au kufaulu kwako, bali kwa sababu umeamini ndani ya Msulibiwa, ukaunganishwa naye, na pia unatazamia toka kwake tu nguvu ya wokovu.

Labda umesikiliza kidogo kwa uchongezi wa yule shetani, ambayo imekufanya ufikiri kwamba, kunyamaza kimya kwako kumesababishwa na mapenzi ya Mungu. „Hapana“ anasema Roho Mtakatifu. Yeye anakufariji katika makusudi ya Mungu, anamfafanua Kristo aliyesulibiwa mbele ya macho yako na kukukumbusha habari ya ufufuo wake kutoka kwa wafu, ili upate kuhakikishwa kwamba, ukombozi ulithibitishwa kabisa, na Mungu aliridhika. Huyu mshindi juu ya mauti alipaa mbinguni. Anafanya maombezi kwa ajili yako mbele za kiti cha neema, naye anakufanya kuwa mshiriki katika haki za ukombozi kwa damu yake. Hivyo unayo Mwombezi mbele za Mungu. Wewe huko peke yako, mpendwa ndugu yangu, kwa sababu rehema ya Mungu iko pamoja nawe; na shabaha yake ni kukuokoa, wala si kukuharibu. Kristo ndiye dhamana ya ukombozi wako.

Pengine unahofia kifo, lakini kumbuka kwamba, Yesu alishinda kifo, na kwa kweli alifufuka kutoka kwa wafu, naye alithibitisha uhai wa Mungu mbele za macho yetu. Kama umefanywa kuwa mtu mpya, uhai wako wa milele unatawala ndani yako. Hautaisha. Kwa sababu upendo wa Mungu hauwezi kushindwa. Mauti haiwezi kukutenganisha tena na huo Utatu Utakatifu.

WARUMI 8:35-37
"35 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? 36 Kama ilivyoandikwa ya kwamba: Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. 37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda kwa yeye aliyetupenda.“

Paulo hakuwa mtunga mashairi ya kuhisi tu alipotufafanulia mafulizo na mfuatano wa taabu mbalimbali alizovumilia. Alitushuhudia ya kwamba, na sisi tuwe tayari kuteseka kwa ajili ya Kristo, kwa sababu imani ndani ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu hazilindi usalama wetu au hali ya kusikia raha, jinsi uwezavyo kuona kutokana na maisha ya Yesu hapo duniani. Alizaliwa na nguvu ya Roho Mtakatifu naye alisulibishwa na wale waliopagawa na roho ya dunia hii. Paulo alionja umaskini na utajiri, ugonjwa na udhaifu kimwili, hatari na mateso, ndugu za uongo, pia na hatari ya kuzamishwa majini. Hizo zote hazikuwa na uzito kwake, kwa sababu alifahamu upendo na uandalizi wa Kristo, ambao aliiona bora kuliko jaribu lolote la kukatisha tamaa. Kwa hiyo, imani yako itajionyesha na hali ya ushindi hata ndani ya shida za mwisho, hata wakati wa saa ya kufa kwako, maana Roho Mtakatifu ataongeza imani yako hadi utakapobadilishwa, na utaingia katika shule ya Mungu ya kujifunza unyenyekevu, tumaini na sifa hata taabuni. Ndipo utapata kuwa kama kondoo wa Mungu, ukimfuata Kristo. Utavumilia yote bila kulalamika, nawe utafia adhama yako na kiburi chako pia. Hutawahesabia majirani yako matamko yao ya kuumiza, lakini utaendelea kufurahi, kuvumilia na kuwa na subira katika nguvu ya Bwana wako.

Majaribu na taabu zote haziwezi kututenga na Yesu, maana shida zinatufundisha kusoma kwa uangalifu neno (Biblia). Ndipo pia tunatamani kuwa karibu na Bwana wetu Yesu, aliyetutangulia kwenda kwa Baba. Anatufahamu, wala hawezi kutuacha, bali anatusindikiza na kututia nguvu, ili tuweze kutambua upendo wake kuu, nasi tutamheshimu kwa moyo wote, shukurani na upole. Upendo wa Kristo unatuongoza kufikia ushindi tukufu, nasi kwa furaha tutahudumia hata katikati ya taabu na machozi.

SALA: Ee Mungu mtakatifu, wewe ndiwe Baba yangu na mwana wako ni mwombezi wangu, leo na pia kwenye hukumu ya mwisho. Roho Mtakatifu anatawala ndani yangu na kunifariji. Nakuabudu; wewe Baba, Mwana na Roho Mtakatifu aliye upendo hasa. Naamini kwamba, sitakufa, kwa sababu wewe unanizunguka, unanitunza, unanilinda na unanifanya kuwa mpya. Ee Mungu, unilinde na majaribu yote, ili dhambi yoyote isinitenge nawe, ili na upendo wangu, pamoja na upendo wa watakatifu wote ulimwenguni usisogezwe hata kidogo.

SWALI:

  1. Jinsi gani wakristo wanaweza kushinda taabu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 16, 2022, at 07:06 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)