Previous Lesson -- Next Lesson
6. Ndani ya Kristo mtu huondolewa dhambi, mauti na hukumu (Warumi 8:1-11)
WARUMI 8:9-11
"9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai kwa sababu ya haki. 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.“
Paulo aliwahakikishia waumini kule Rumi na penginepo kwamba, Roho wa Mungu aliingilia miili yao midhaifu na utu wao wa ukorofi, kwa sababu sasa maisha yao yaliimarishwa ndani ya nguvu na makusudi ya Roho Mtakatifu. Kwa hiyo yeye aliwaumba, kwa kuwafanya wazaliwe mara ya pili na kukua, akawatunza na kuwafariji, pia akawathibitisha na kuwajaza na upendo wa Mungu, mwisho anawakabidhi huduma kadhaa na kuwatia nguvu, ili wafanikishe huduma hizo. Hivyo kila mwumini alifurahia kuwa na Roho Mtakatifu akitawala ndani yake.
Lakini basi, yeye asiye na Roho Mtakatifu akitawala ndani ya moyo wake, huyu si Mkristo, hata kama amezaliwa na Mkristo, maana jina hilo linamaanisha „mwenye kutiwa mafuta na Roho wa Mungu“. Jinsi Kristo mwenyewe alivyotiwa mafuta na ukamilifu wa Roho wa Babaye, ndivyo alivyo mwumini. Si jina, wala si asili ya mtu, wala kupokea ubatizo, wala malipo ya ada ya kuwa mshiriki wa kanisa fulani yanaweza kukufanya kuwa Mkristo. Kipekee ni kwa njia ya enzi ya Bwana inayotawala ndani yako kwamba, utaweza kuwa mshiriki mashuhuli wa Kristo, ukiwa mali yake kabisa, na hivyo kuwa kama jiwe lenye uhai kwenye jengo la hekalu lake. Yeye ambaye hajapokea zawadi hiyo ya uhai na bila kuwa na upendo wa Mungu ndani yake, basi hana lolote kwake Kristo. Ataendelea kuwa mbali naye. Yeye tu aliyezaliwa na Roho Mtakatifu yupo karibu na Kristo na kuwa mali yake na kuishi ndani ya mazingira yake. Wewe basi, usiwe na uvuguvugu, lakini angalia sana kwamba, yeye asiyeshikamana kabisa na Kristo na kuendelea hivyo daima, hatakuwa na sehemu ndani yake. Kristo anakuhitaji kabisa, ndipo ataishi ndani yako kwa ukamilifu wake. Penginepo utakuwa umetengwa naye, kwa sababu imani ya kusitasita sio imani halisi.
Mpendwa ndugu, umwabudu Bwana, maana Kristo anapenda kuishi ndani yako ukipokea kupakwa mafuta ya upendo wake. Wote hao wanaoishi ndani ya Roho, wanashuhudia habari ya mwujiza huo ya kwamba, anawahakikishia kwamba, yumo ndani ya mioyo yao.
Basi, usifikiri kwamba, Kristo na dhambi zaweza kuishi pamoja ndani ya mwili wako. Huwezi kumchukia mtu fulani na kumpenda Kristo wakati mmoja. Hutaweza kujitoa kwa mambo ya uchafu na pia kudai umejazwa na Roho Mtakatifu, maana Roho huyu ni mwenye wivu, naye ataangamiza dhambi yako bila huruma. Dhamiri yako haitatulia hadi utakapokiri dhambi zako zote, kuziungama hata kwa machozi, kuyachukia kwa kirahi, na ukiharibu kiburi chako. Ndipo utakabidhi utu wako uliochafuka kwa upya mkononi mwake Kristo, Mwumba wako. Roho wa Mungu atashughulika dhidi ya dhambi zako, hadi akutakase kikamilifu, maana Yesu amekuita kwa utakatifu wala sio kwa uchafu.
Damu ya Kristo itakusafisha na dhambi zote, ukiamini ndani yake na katika ahadi zake. Nguvu yake itakuzwa ndani ya udhaifu wako. Mapenzi yako au kutaka kwako zitaimarishwa, nawe utajikinahi na kuishi kwake Mungu. Kumbuka kwamba, mwili wako utakufa kwa ajili ya dhambi zako, lakini Roho uliopewa toka mbinguni ataishi daima. Hivyo, tunayo tumaini pasipo na kifani, kwa sababu twabeba ndani yetu uhai wa Mungu ulio hakikisho ya utukufu unaotazamiwa wakati atakaporudi Bwana.
Nguvu ile ile iliyofanya kazi ndani ya Kristo alipofufuka kutoka kaburini ipo hata sasa, ikitembea ndani ya kila mwumini aishiye naye. Mungu ataendesha uzima wake wa sasa ndani yetu hadi kurudi kwake Kristo mara ya pili. Na itatokea kwamba, umati wa watu wasioamini watakuwa na roho bila uhai, wakati sisi tunaoishi na kuwa watukufu kwa neema, kwa sababu Roho wa Mungu anafanya kazi ndani yetu, akitokea katika utukufu, furaha na uwezo, maana ndiye Mungu mwenyewe.
SALA: Ee Bwana uishiye milele, tunakuabudu kwa sababu ulitujalia Roho Mtakatifu wa kwako, ili tuweze kuishi kama watoto wako daima, hali tumejaliwa haki kwa kifo chake Kristo na kushikamana naye. Umetuokoa katika hali ya kutokuamini na kuasi kwetu. Asante kwamba mauti haiwezi tena kutufunga, kwa sababu tumelindwa mikononi mwako, pia na dhamana ya utukufu wako unatawala ndani yetu, ili tuweze kuishi jinsi Mwana wako alivyoishi kati ya wanadamu wakorofi.
SWALI:
- Wale wanaoamini ndani yake Kristo, Roho Mtakatifu anawajalia mambo gani?