Previous Lesson -- Next Lesson
7. Sisi tu watoto wa Mungu kwa ajili ya kuishi kwa Roho Mtakatifu ndani yetu (Warumi 8:12-17)
WARUMI 8:12-14
"12 Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, 13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.“
Roho Mtakatifu hawezi kufanya mapatano na mambo yetu mengi ya kibinafsi yanayoishi ndani yako, bali anaipigania hadi yatakapoondolewa. Roho wa Mungu ataondoka kwako usipokubali kifo cha umimi wako msalabani kwake Kristo, na ufie kiburi chako, hasira, chuki na dhambi zingine zote na maasi. Haimpasi mwumini kufungwa na pesa au mambo ya kujifurahisha, ili aweze kuwa huru na wazi kwa ajili ya Roho wa Bwana wake. Huyu Mtakatifu atafanya kazi ndani yako kama daktari mpasuaji, ambaye anaondoa yote yanayochemka mwilini mwa mtu. Huipasua na kuondoa kwa kukata uchafu wote. Kwa tabia ya namna hii Roho wa Mungu atakusukuma toka gizani hadi nuruni, toka kusema uongo hadi uaminifu, toka mambo ya kujifurahisha hadi usoni pa Mungu. Je, unasikia uongozi wake? Unasikia sauti yake ya huruma? Yeye anakusudia kukubadilisha na kukutakasa kabisa, pia na kukubadili ndani ya sura ya huruma yake. Huu mwujiza wa utakaso kwa njia ya Roho wa Mungu utajionyesha ndani yako kwa upendo, furaha na amani, zilizo na msingi katika uvumilivu, kujinyima na unyenyekevu, pamoja na sifa zote za Kristo, kana kwamba sasa umevishwa na usafi wa Mwokozi wako. Wakati huyu Roho mwema anapotembea moyoni mwako, unapata kuwa mwana wa Mungu. Je, unatambua huo upendeleo kubwa kwamba, hata mbali na hali yako ya mwenye dhambi, umepata kuwa mtoto wa kweli wa Mwumbaji wa walimwengu wote kwa njia ya damu na Roho wa Kristo? Sasa unathubutu kutamka kwamba, wewe ndiwe mwana wa Mungu? Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu (Ndivyo mstari wa 14 unavyosema)
WARUMI 8:15-17
"15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bail mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.“
Roho Mtakatifu huondoa hofu, kukata tamaa, hali ya kuona mambo yote kwa ubaya, shida na hali ya kuvurugwa zote ziondoke kwako. Yeye anakujalia ujasiri, raha na tumaini ndani ya Mungu. Zaidi ya hapo atakufungulia mdomo wako uweze kusema katika jina la Baba. Kwa kukiri hivyo, utatakasa jina la Mungu, maana hii ndiyo mwujiza kuu wa hilo agano jipya; kwamba Mungu ndani ya Kristo alijifunua mwenyewe kuwa ndiye Baba yetu wa mbinguni. Huyu Mwumba wa mbali, aliyekasirishwa na dhambi, sasa hatuchoshi zaidi au kututwisha mizigo kupita kiasi, bali hutuonyesha upendo wake, naye anatuthibitishia wema wake kwa namna ya kibaba. Sura hiyo tukufu na mpya inabadilisha mwenendo wetu kabisa kwa kupindua. Neno hilo „Abba“ ni neno la kiaramayo lililotiwa ndani ya herufi za kiyunani ndipo kutafsiriwa katika kiingereza. Na maana yake ni „Baba“. Hatua ya kuwashirikisha pamoja wote wawili, yaani Wayahudi na Wayunani (wa mataifa) ndani ya Kristo inaonekana wazi katika maneno hayo ya mwanzoni mwa sala ya Paulo kwa wote wawili hao.
Hilo neno „Baba“ linaeleza na kuthibitisha neno la „Abba“. Kristo katika upendo wake mkuu, alitoa mwili wake kwa ajili yetu, na alitufanya tuwe washiriki wa haki zake za binafsi kwamba, Mungu wa utukufu apende kutupokea kama watoto. Basi utambue kwamba jina lako limeandikwa na damu ya Mwana wa Mungu upande wa mbele wa cheti chako cha ruhusa ya kuingia mbinguni; na upande wa nyuma kwenye cheti hiki unaweza kusoma: “Kupokelewa kuwa mtoto wa Mungu“, na yameandikwa na moto wa Roho Mtakatifu pia na kuwekwa sahihi ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Je, utaweza kusahau cheti hiki cha pekee, kuipuuza, au kuitupa mbali? Au utakikubali kabisa, uibusu na machozi ya furaha na ukitunze daima kwa uangalifu wote?
Sasa wewe kisheria na kwa uhakika umepata kuwa mwana wa Aliye Juu, kwa njia ya kupokelewa kama mtoto, au kwa kuzaliwa kwako ndani ya Roho. Mtume Paulo anakueleza tena kwa kurudia ndani ya injili yake, ambayo ni tajiri na kujaa kabisa na neema kwamba, wewe utamrithi Mungu mwenyewe, kwa sababu huyu Mtakatifu amekukaribia kabisa ndani ya Yesu. Naye anatawala ndani yako na ndani ya wote walio wanafunzi wake, naye kwa uzuri kabisa atafunua utukufu wake ndani ya wafuasi wake, maana Mungu ndiye mmoja.
Miujiza hii yote ilianza ndani yetu kwa sababu Roho Mtakatifu alitawala ndani ya makanisa yote yaliyojengwa kipekee juu ya msingi wa Kristo. Je, nuru yake inang‘aa ndani yetu? Umeunganishwa naye Mungu kweli. Je, kwa hiyo umekuwa tayari hata kuteswa kwa ajili yake, jinsi mitume nao walivyoteseka sana kwa ajili ya jina la Kristo?
SALA:
Baba yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
mapenzi yako yatimizwe hapo duniani kama huko mbinguni
Utupatie leo ridhiki yetu,
na utusamehe makosa yetu, kama sisi tunayvowasamehe wale wanaotukosa.
Na usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu hata milele. Amina.
SWALI:
- Jina jipya la Mungu ni lipi, ambalo Roho Mtakatifu atufundisha? Na maana yake ni nini?