Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 042 (In Christ, Man is Delivered)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

6. Ndani ya Kristo mtu huondolewa dhambi, mauti na hukumu (Warumi 8:1-11)


WARUMI 8:3-8
"3 Maana yake yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, alihukumu dhambi katika mwili; 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu."

Kristo alianzisha agano lingine jipya, kwa sababu agano la kale lilikuwa dhaifu na halikuweza kushinda tamaa na dhambi ndani ya mwili. Kuingia mwilini kwake Mwana wa Mungu ilikuwa ndiyo mwanzo wa agano hilo jipya, pia na hatua ya kwanza wa ushindi tukufu juu ya huo mwili dhaifu wa kibinadamu, kwa sababu Kristo alifaulu kutawala mwili wake kabisa kwa Roho Mtakatifu aliyeishi ndani yake, ili yule mwovu hakuweza kushtaki dhidi yake. Maisha safi kabisa ya Kristo ilikuwa ya kufunga angamizo na uuaji wa dhambi.

Kristo aliishi takatifu wakati wote, kwa sababu Roho wa Baba yake wa mbinguni alifisha dhambi mwilini mwake, alizorithi kutoka kwa babu zake za kibinadamu. Kwa sababu hiyo aliendelea siku zote bila kosa, na katika upendo na upole wake alitimiza madai yote ya sheria. Kilele cha maisha yake ilikuwa ni wakati alipotwishwa dhambi zetu mwilini mwake, na kutufunika sisi na hali ya kuhesabiwa haki ya Mungu kwa kifo chake. Sisi hatuitambui kwa ndani hiyo zawadi ya kujaliwa haki kwa njia ya imani ya kimawazo au ya kimapokeo tu, lakini inakuwa kweli katika maisha yetu ya kila siku, kwa sababu zawadi ya haki ya Mungu ndiyo upendo wake halali ulio na msingi ndani ya ukweli. Upendo huo kuu ulimiminwa ndani ya mioyo ya waumini, ili waweze kusema: „Kristo anaishi ndani yetu. Anatuongoza, kutuelekeza na kutusukuma kutimiza sheria.“ Mkristo hawezi kuendesha maisha kufuatana na mwili pamoja na tamaa zake chafu, lakini kwa kumfuata Roho na mashauri yake katika shukrani, furaha na faraja.

Hayo ndiyo maswali makuu yanayokuelekea wewe: Je, wewe ni mtu wa Roho Mtakatifu? Kristo anaishi ndani yako? Huyu Mkombozi wa ulimwengu ndiye kiini cha moyo wako? Kifo chake msalabani kilikupatia haki, ili uweze kutembea katika upya wa uhai wake? Imani wakati wowote haiwezi kuwa wazo au jambo la kujifikiria tu. Ni nguvu ya kiroho iliyo hai na kuwepo kwake Mungu ndani ya maisha na miili zilizojaliwa haki.

Mtu wa kiroho anatambulikana na mambo anayoyapenda na kufuata. Anapendelea msamaha na amani. Je, wewe ni mfanya amani? Unatafuta kueneza usuluhisho kwa Mungu na kati ya watu, ili wengi wapate kuwa wapya na kuwa watoto wa Mungu, na hivyo uhai wake tukufu upate kuonekana ndani ya wale ambao bado ni wa kimwili, ili na wao baadaye wapate kuanza kuwa na nia katika mambo ya kiroho?

Haya basi, yeye aishiye pasipo Roho wa Mungu anabaki kuwa ya kimwili, mdhaifu, mgumu wa kufahamika, anatenda kinyume mawazoni na katika mwenendo kinyume cha Utatu Utakatifu, naye anaabudu tamaa zake za kidunia na kuonea uchungu. Mtu wa namna hii atarithi mauti; ni ghadhabu ya Mungu na hukumu ya haki mwishoni. Maana mtu wa kimwili hataki kujinyenyekeza chini ya sheria za Bwana, lakini anaasi dhidi yake kwa makusudi yake ya ukorofi. Wala hawezi kumridhisha Mungu au kumpenda, mpaka atakapoungama, kuokoka na kuamini ndani ya Kristo. Mwanadamu, bila kuishi kwa Roho Mtakatifu moyoni mwake, amepotea. Ataanguka katika upotevu moja hadi nyingine. Kwa maneno mengine, yeyote asiye na huyu Roho mpendwa basi hawezi kuwa mali yake Kristo, bali ni mtumwa wa shetani.

Upande mwingine, mtu wa kiroho ni mwangalifu. Anachunga sana ile amani aliyopewa na Mungu, hupenda hata adui zake, anamwomba Mungu kila siku apate nguvu zake na ulinzi, naye anatamani kwa moyo wake wote kumvuta kila mtu kwake Yesu, aliye kisima cha uhai na amani, ili wao nao wasije wakaangamia, bali wapokee uzima wa milele. Je, wewe umepata kujazwa na Roho wa Mungu, kusukumwa naye, pia na kutambua upendo wake bila kiburi?

SALA: Ee Bwana Yesu, uliye Mungu mpendwa, fahamu zetu haziwezi kushika, wala hatuwezi kumtambua Roho na upendo wako sisi wenyewe. Katika rehema zako kuu wewe umetujalia na uvumilivu wako na mambo mengine ya kwako, ili tupate kukutukuza pamoja na Baba na Roho Mtakatifu na tupate kutimiza mapenzi yako kwa furaha na ukunjufu. Ututunze ndani ya amani yako, na sisi tupate kukufuata katika nguvu ya Roho. Tujalie hekima na makusudi yako, ili tuweze kuwaita wote walio wa kimwili, wajitoe kwako, na hivyo wapate kuokoka, wabadilike na kutakaswa.

SWALI:

  1. Yapi ni mambo ya nia ya mtu wa kiroho? Na ipi ni mapokeo ya wale walio na hali ya kimwili?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 16, 2022, at 05:41 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)