Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 041 (In Christ, Man is Delivered)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
D - Uwezo Wa Mungu Hutuokoa Na Nguvu Ya Dhambi (Warumi 6:1 - 8:27)

6. Ndani ya Kristo mtu huondolewa dhambi, mauti na hukumu (Warumi 8:1-11)


WARUMI 8:2
"2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.“

Imani yetu imejaa uhai, kwa sababu Roho Mtakatifu amemiminwa ndani ya mioyo ya waumini, kama wanafungua mioyo yao kwake Kristo. Roho huyu anayetoa uhai na kuhuisha ndiye enzi ya Mungu mwenye kuumba, tena anayefanya kazi ndani yao wanaomtegemea huyu Msulibiwa.

Mwanzoni mwa kuumba ulimwengu, Roho huyu mtukufu alikuwa akielea juu ya ulimwengu uliokuwa bado hauna sura. Siku hizi Roho huyu mbarikiwa huumba uhai wa tumaini ndani mamilioniya watu. Sisi kama waumini hatuishi toka kwa uwezo wetu, bali kwa tunzo lake, makusudi yake na uvumilivu wake. Yeyote anayekubali na kufungua moyo wake kwa kazi ya Roho wa Kristo atajaliwa nguvu kutoka kwa Mungu mwenyewe. Huokoki au kutakaswa kwa mapenzi yako mwenyewe, wala mawazo au nguvu, bali kipekee kwa sababu ya Roho Mtakatifu wa Mungu. Yeye ndiye muumbaji wa imani yako, mwumba wa upendo wako, chemchemi ya furaha yako, pia na asili ya ukarimu wako. Yeye ndiye Mungu atendaye kazi ndani yetu naye anayetusukuma tutende matendo ya rehema, anaendelea ndani yetu kwa uaminifu na kutuongoza tufikie hali ya ukamilifu ndani ya upendo.

Maisha haya ya Roho tukufu hayabadiliki, kama vile upepo unavyogeukageuka na kubadilisha mwelekeo wake kila mara, bali Roho ni mwenye taratibu na makini, pia na mwenye sheria, hata mtume amwita „sheria ya Roho wa uhai“. Au kwa maneno mengine, sheria ya Roho ndiyo uhai wa Kristo ndani ya wale wanaomwamini. Mtakatifu huyu alijifunganisha mwenyewe na wale wanaoamini ndani ya agano lake jipya, na aliwekeza kwa njia ya kifo chake jambo la ukweli linaloendelea mbali na mwisho wa dunia, maana uaminifu wake ni wa milele. Huyu Roho aliyemiminwa kutoka kwa moyo wa Baba; na Mwana hakufikii kwa sababu ya sala zako, kufunga kwako au maisha ya uaminifu wako, lakini kutokana na msingi wa hali ya haki ya Kristo, aliyekamilisha hayo kwa ajili yako msalabani. Mungu mwenyewe amewekeza uzima wa milele ndani yako kwa sababu ya ukweli. Enzi yake haitembei kwa kulipuka wala si katika njia ya kulazimishwa, bali katika upole utakatifu na katika utaratibu unaopendeza. Enzi hiyo hailii wala haingurumi, lakini inaenda kwa upendo na kutumia unyenyekevu jinsi Kristo anavyowapenda wenye dhambi - maana yake anaishi ndani yako na wewe ndani yake. Kwa sababu hiyo usiruhusu roho yeyote geni kuishi ndani yako.

Maisha haya ya kiroho uliyojaliwa haitakuwa ndani yako isipokuwa pamoja na Kristo akiwa mali yako kabisa. Maana hali hiyo inatokana na uhusiano wa daima na umoja wa karibu sana na Mwokozi wako, hata ukawa kiungo cha mwili wake wa kiroho.

Sio sawa kwamba Wakristo walazimishwe kuanguka katika kutenda maovu. Tamko hilo linaonyesha uasi kwa Kristo na kudharau dhidi ya msalaba wake. Kweli, tunakabiliana na majaribu, pengine hata zaidi kuliko kabla ya kuamini, jinsi Kristo mwenyewe alivyopata maishani mwake. Pengine twaweza kuanguka katika maovu kadhaa, au kutenda dhambi bila kusudi. Lakini kwa kawaida, Kristo alituweka huru kutokana na nguvu ya dhambi, na kwa sababu hiyo, mauti sio mshahara wa maisha yetu. Maana sheria kwetu haimaanishi tena jehanumu, wala haitusukumi kuendelea kukosa zaidi, bali sheria inatawala ndani ya mioyo yetu kwa hali ya kutufurahisha. Kwa hiyo hatuwi tena watumwa wa dhambi, bali watoto wa upendo wa Mungu. Hatufi kama watu wasio na tumaini, lakini tunaishi kufuatana na sheria ya Roho wa uhai daima, jinsi Kristo anavyoishi kwa daima. Ujichuvye kwa chini ndani ya maneno ya kitume, yanayojaa na maana muhimu, yatakayokuimarisha ndani ya haki zako, kuachiliwa na sheria ya dhambi, ya kushinda maovu na kuishi katika taratibu na nguvu za Mungu kufuatana na uongozi wa Roho yake.

SALA: Ee Bwana Yesu Kristo, asante sana kwa sababu ulitubeba toka mautini hadi uzimani, ili tupate kutukuza upendo wa Baba yetu, nasi tutembee ndani ya sheria ya Roho. Utuimarishe ndani yako, ili upendo wako upate kutendeka na kuonekana ndani yetu, nasi tupate kukutukuza kwa mwenendo wetu, ili na watu tunaoishi nao wapate kusikia harufu ya uzima, wala si ya mauti.

SWALI:

  1. Zipi ni zile sheria mbili, ambazo mtume alizilinganisha pamoja, na maana yao ni nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 16, 2022, at 04:07 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)