Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 030 (Peace, Hope, and Love Dwell in the Believer)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
C - Kuhesabiwa Haki inamaanisha Uhusiano mpya kwa Mungu na kwa Wanadamu (Warumi 5:1-21)

1. Amani, Tumaini na Upendo hutawala ndani ya Mwumini (Warumi 5:1-5)


WARUMI 5:1-2
"1 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokaya katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, 2 ambaye kwa yeye tumepata kuwa na njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.“

Mwanadamu wa asili huishi katika hali ya kubishana na Mungu. Watu wote hufanya kinyume cha maagizo ya Mtakatifu, kwa vile makosa yetu yanahesabiwa kuwa tendo la kuvunja sheria. Kwa hiyo, ghadhabu ya Mungu imefunuliwa dhidi ya hali yote iliyo knyume cha Mungu na kutokutenda haki kwa watu.

Sasa baada ya Kristo kufa msalabani na kuwapatanisha tena watu na Bwana wao, ndani ya wakati wa amani, kwa sababu Mwana aliondoa dhambi iliyotutenga, na neema ya Mungu ya kutuokoa ilitokea kwa watu wote. Jinsi baraka zilivyo kuu na za kutuliza, na utulivu ndani ya wale wamwaminio Mungu kwa njia ya Kristo, Mwokozi! Wala hakuna amani kwa wale watendao maovu, pia hakuna utulivu kwa roho zao, ila wao nao wakipata kuamini ndani ya Msulibiwa.

Kristo alitusafisha na kututakasa, ili kila mwumini ndani ya hiyo agano jipya apate kukubali pendeleo hilo kuu, ambalo katika enzi za Agano la Kale ilikuwa imejaliwa tu kwa yule Kuhani Mkuu, aliyeweza kuingia ndani ya Patakatifu pa Patakatifu mara moja kwa mwaka, ili afanye mapatanisho kwa ajili ya watoto wa Israeli kwa dhambi zao zote. Sasa kwa tokeo la kifo cha Kristo basi, lile shela mbele za Patakatifu pa Patakatifu liliraruka vipande viwili, na kwa sababu hiyo sisi tunayo haki tusimame usoni pa Mtakatifu. Sasa yeye humkaribisha yeyote amjie kwa tumaini, na aone kwamba, yeye hatishi, wala si mwenye kuharibu, na pia siye wa mbali sana nasi, lakini badala yake yeye ni Baba na Mwokozi anayejaa upendo na rehema. Anatazamia sala zetu, azisikie, naye atajibu maombezi yetu, naye hututumia kwa kazi ya kueneza Injili ya Mwana wake kwamba, baraka za sadaka ya msalabani zipate kupelekwa kwa wale wote wanaotafuta utulivu kwa roho zao.

Kristo alipokuwa amefufuka kutoka kwa wafu, aliwasalimia wanafunzi wake mara nyingi akiwaambia: „Amani iwe kwenu“, maneno hayo yakimaanisha mawili:

  1. Mungu amewasamehe ninyi nyote dhambi zenu zote kwa sababu ya mateso ya Yesu kwa ajili yenu.
  2. Inukeni basi; na mkaende na kueneza Injili, maana Yesu awaagizeni akisema: „Jinsi Baba alivyonituma mimi, sasa mimi nami nawatuma.“ Yeye amwaminiye Yesu anajawa na amani, na hilo si kwa ajili yake mwenyewe tu, lakini pia awe mmoja wa wafanya amani, akifurahishwa na Kristo, pia na kuitwa mtoto wa Mungu.

Kwa nyongeza ya hiyo amani ya moyo, ambayo imetokana na kuhesabiwa haki, kujitoa kwetu mbele za kiti cha enzi cha Mtakatifu, pia na ujumbe wetu wa kueneza neema, Paulo anatuthibitishia kwamba, tunayo tumaini linalozidi ufahamu wetu wote: Mungu alituumba katika mfano wake, lakini kwa sababu ya dhambi zetu tulipoteza ule utukufu tuliopewa. Ila sasa tumaini hili linaishi mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu anaturudishia utukufu ule ule, ambalo ni la kwake na linalong’aa kutokana naMwana wake. - Je, unaona fahari kwa ajili ya utukufu wa Mungu? Je, unashikamana na tumaini lililowekwa mbele zako? Matazamio yetu ya mbeleni sio wazo tupu tu, la kudhani au la kunuia tu, hapana. Lakini yametimilizwa kwa njia ya enzi ya Roho Mtakatifu ndani yetu, ambayo yeye ni thibitisho la utukufu huo, ambao utafunuliwa ndani yetu.

WARUMI 5:3-5
3 Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; 4 na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; 5 na tumaini halitatahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.“

Hatuishi mbinguni, bali duniani. Jinsi Yesu alivyopita ndani ya aina zote za mateso na dhulumu, ndivyo na sisi tutayapata, pamoja na kukua kwa imani na kupata matunda ya kiroho, basi uchokozi wa watu, magonjwa na kusingiziwa kishetani yatakuja. Hata hivyo Paulo hakuandika habari ya ukweli huo kwa machozi na kuguna, lakini alisema: Sisi pia tunasifu katika mateso yetu, maana hizo ni alama za kumfuata Kristo. Tunapomfuata katika mateso yake, ndivyo tutafuatana naye katika utukufu wake. – Kwa hiyo basi, ufanye yote pasipo manung’uniko; kwa sababu Bwana wetu yu hai na hakuna litakalotupata bila ruhusa yake.

Tunapobeba taabu za kidunia tutaongozwa kujikinahi, hali ya kuchukia kila jambo nyeti ipotee, makusudi yetu yatatakata na tutakabidhi mapenzi yetu chini ya uongozi wa Yesu. Subira itaanza kukua ndani yetu, nasi tutajinyosha zaidi katika tumaini kwake Yesu na kutazamia kujiingilia kwake ndani ya maisha yetu. Katika shule ya mateso, tutajifunza namna ya kuacha wazo la kutokuweza kwetu, nasi tutahakikisha kama vile Ibrahimu kwamba, Mungu anashinda, mbali na makosa yetu.

Ndani ya mashambulio hayo tunafaidika na mazoezi ya Ibrahimu, na kwa sababu wakati huu wa neema, upendo wa Mungu umemwagwa katikati kwenye ya maisha yetu, yaani mioyoni mwetu, kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu wa kweli, tuliyopewa. - Mstari wa 5 kwenye sura ya 5 jinsi ilivyo kuu na nzuri mno, hata tunaahindwa kuitamka. Basi jifunza mstari huo kwa moyo, maana ni tunu kuu la Biblia. Hakuna upendo au huruma ya kibinadamu zilizowahi kumiminwa ndani ya mioyo yetu; lakini badala yake upendo wa Mungu, wenye nguvu, wa milele na bila kuchafuka, ambao ni Mungu mwenyewe. Tangu awali upendo huo haukuishi mioyoni mwetu, lakini ulimiminiwa ndani yetu, si kwa sababu ya wema wetu, lakini kwa sababu damu ya Kristo ilitusafisha. Hii ndiyo sababu ya Roho Mtakatifu pia kuishi ndani yetu na kugeuza miili yetu ya kufa kuwa ni hekalu la Mungu. Jambo hilo la kimbinguni ndilo nguvu takatifu ya Mungu, ambayo Kristo humjalia kila mtu aaminiye ndani yake. Wote wapokeao Roho wa upendo wa Mungu wataonja habari ya kuzaliwa mara ya pili, kufanywa upya na kutambua maisha ya milele ndani yao. Hata hivyo, kuishi kwa Roho tukufu ndani yetu haitokei tu kwa ajili ya kujenga amani kwa ajili yetu, lakini kwa kuimarisha uvumilivu wetu, ili kutuwezesha kwa furaha kuwabeba wale walio wagumu kuwafurahisha, pia na kuwapenda adui zetu kwa matendo, na pia tusikose kufaulu namna ya kushinda taabu zote za maisha yetu. Kristo hakutuacha kama yatima, lakini alitupatia nguvu yake, upendo wake, pia na uhakika wa utukufu, ambao utafunuliwa mara, wakati utakapotimia.

SALA: Tunakuabudu wewe, Ee Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, kwa sababu hukutukataa sisi tulio wa kufa, nyungunyungu maskini, lakini ulimwaga upendo wako takatifu ndani ya miili yetu ya kufa, ili tuweze kuwa na upendo katika nguvu ya Roho yako, na kukuamini, ili kwamba, maisha yetu yapate kuwa mfano wa rehema yako kuu. Tunakushukuru, tunakusifu na kushangilia kwa ajili ya kuwepo kwako mioyoni mwetu. Twaomba utusaidie tutende itupasavyo kufuatana na upendo wako.

SWALI:

  1. Jinsi gani amani ya Mungu inakamilika ndani ya maisha yetu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 11:47 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)