Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 018 (The Law, or the Conscience Condemns Man)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)
2. Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa dhidi ya Wayahudi (Warumi 2:1-3:20)

b) Sheria au dhamiri humhukumu mwanadamu (Warumi 2:12-16)


WARUMI 2:12-16
"12 Kwa kuwa wote waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na wote waliokosa wenye sheria, watahukumiwa kwa sheria. 13 Kwa sababu sio wale waisikiao sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki. 14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. 15 Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea; 16 katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu.“

Kanisa la Rumi lilichanganywa na makundi mawili: Wakristo wenye asili ya kiyahudi na waumini toka ulimwengu wa kiyunani na kirumi. Wa kwanza walikuwa na ufahamu wa ahadi na sheria, wakiendelea kufuata desturi zao kufuatana na Agano la Kale; wakati ambapo Wakristo toka kwa Mataifa hawakufahamu taratibu lolote tukufu kwa maisha yao, lakini walitembea katika nguvu ya Roho wa Kristo.

Paulo aliwathibitishia Wakristo kutokana na Wayahudi kwamba, Mungu atawahukumu kufuatana na sheria ya zamani, iliyo mfano wa utakatifu wake. Kusikiliza tu neno la Mungu hakutaokoa, na mawazo ya kiroho na sala ndefu hazitatosha, maana Mungu anadai utii wa moyo na wa maisha. Anatutaka neno lake lipate sura ndani yetu na maisha yetu yabadilishwe kabisa kutokana na neno lake. Myahudi atahukumiwa kwa kila analotenda kwa kuvunja sheria, maana matendo yote mabaya yanahesabiwa kuwa uadui dhidi ya Mungu.

Paulo alipoandika ukweli huu, alisikia rohoni mwake, utetezi wa Wakristo waliokuwa wa asili ya kiyahudi wakisema: „Sisi hatuna sheria nasi hatujui Amri Kumi; basi jinsi gani Mungu atatutendea katika siku ya Hukumu? Sisi tuko huru na hukumu“.

Ndipo aliwajibu waziwazi kwamba, haki ya Mungu haibadiliki kwa kesi yoyote, hata ikiwahukumu wale walioachia mbali Sheria, wale ambao hawakusikia Amri Kumi na ahadi za Mungu, wala kuelewa habari ya upendo na utukufu wa Mungu; maana Muumbaji aliweka ndani ya kila mwanadamu dhamiri iliyo nyepesi kuona, angalifu, wa kupima na kuonya, wa kukaripia na kulaumu. Mwonyaji huyu pengine mara kwa mara atanyamaza kana kwamba amefungwa katika hali ya kutokutumika kwa muda. Lakini kwa hakika atainuka kwa upya kwa kukuonyesha makosa yako. Pengine mvutano utachipuka ndani yako. Baki hilo la sura ya Mungu ndani yako haliwezi kunyamazishwa kwa wakati wowote. Dhamiri yako inakuhukumu. Wala huwezi kupata utulivu isipokuwa katika neema ya Mungu. Hii ndiyo sababu kwa watu wengi waonekane wenye huzuni na wepesi wa kushtuka, kwa sababu wanaishi katika uadui na dhamiri yao, wala hawaungami makosa yao, ingawa dhamiri yao inaangalia kazi zao na kuwaonya. Je, unamshukuru Mungu kwa dhamiri yako, ile sheria ya nidhamu iliyoumbwa ndani yako? Basi, uinoe dhamiri yako ndani ya Injili, na kuichuvya ndani ya mawazo ya upendo wa Mungu, ili iendelee kukuonya kwa ukamilifu zaidi na kukuongoza kufuatana na taratibu za Mungu, na pengine hivyo utapata kustahili na kuwa tayari kwa kila kazi njema. Ndipo hutaanguka ndani ya hukumu ya mwisha, kwa sababu uliishi katika upatano na sauti ya Mungu moyoni mwako.

Lakini usipoingilia kwa chini ndani ya neno la Kristo, na usipojiweka huru mwenyewe na malalamiko ya dhamiri yako, lakini kuendelea katika ukaidi, na kujiweka haki mwenyewe kwa mwenyewe, ndipo dhamiri yako itainuka dhidi yako kwenye siku ile ya mwisho. Itampa ukweli Mungu na kukuhukumu wewe. Basi huna ufumbuzi nyingine kwa kutokutulia kwako ila kujiweka kwenye Injili, itakayokuonyesha kwamba, hakimu yako ni Mwenyewe, Mwokozi wako. Basi, njoo kwake Kristo sasa hivi, nawe utapata hali ya kutulia moyoni mwako.

Umewahi kujua kwamba, hukumu ya Mungu ya mwisho itakuwa imewekwa mikononi mwa Yesu Kristo? Unafahamu kwamba jina kamili la hakimu huyu si Kristo tu, lakin pia ni „Yesu“? Utofauti kati ya majina hayo ni kwamba, „Yesu“ ni jina lake la binafsi, wakati „Kristo“ ni kielelezo la cheo chake. Yesu ndiye Mtiwa Mafuta, aliyejawa na vipawa na tabia zote za Mungu, aliye na mamlaka kamili na ya juu, na aliyekabidhiwa yote ya hukumu na ya wokovu.

Hivyo, mtume aliweza kutamka kwamba, Mungu atahukumu ulimwengu na siri zake zote kufuatana na Injili, ambayo Paulo aliitoa kumhusu Yesu. Basi ni lazima kwetu kupata kufahamishwa yote yaliyofunuliwa ndani ya injili ya Paulo, jinsi ilivyo ndani ya waraka wake kwa Warumi, hasa yale ya kuhusu Siku ya Hukumu.

SALA: Ewe Mungu mtakatifu, wanijua zaidi kuliko ninavyojifahamu mwenyewe. Shughuli zangu zote ziko wazi mbele zako. Nayakiri dhambi zangu, nakuomba unifunulie hatia zangu zilizofichika, ili niyalete kwenye nuru ya mwana wako kabla ya siku ya kuogofya inayokuja. Nisamehe kama sikuitii sauti ya dhamiri yangu mara moja, au kama nilipuuza kwa makusudi sauti yako. Nijalie bidii na nguvu kutimiza maagizo ya upendo wako. Amina.

SWALI:

  1. Jinsi gani Mungu atawashughulikia watu wa Mataifa katika Siku ya Hukumu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 03:05 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)