Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 017 (He who Judges Others Condemns Himself)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)
2. Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa dhidi ya Wayahudi (Warumi 2:1-3:20)

a) Awahukumuye wengine hujipatiliza mwenyewe (Warumi 2:1-11)


WARUMI 2:6-11
"6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake; 7 wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele; 8 na wale wenye fitina, wasioitii kweli, bali wakubalio dhuluma, watapata hasira na ghadhabu; 9 dhiki na shida juu ya kila nafsi ya mwanadamu atendaye uovu, Myahudi kwanza na Myunani pia; 10 bali utukufu na heshima na amani kwa kila mtu atendaye mema, Myahudi kwanza na Myunani pia; 11 kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.“

Mpendwa ndugu, unafahamu kanuni zitakazokuwepo katika hukumu ya Mungu? Wanadamu wote wanakimbilia kwenye saa ile ya matata, lakini mtu mwenye busara na hekima ni yule anayejitayarisha kwa ajili ya saa ile. Mtume wa neema anatufafanulia wazi kwamba, katika hukumu ya mwisho matendo yetu mema na mabaya yatapimwa kwa kuweka msingi kwa kuhukumiwa kwetu. Kwa Mathayo 25, Kristo atuwekea wazi kwamba, kutenda kwa upendo kwa watu wale wasiojaliwa, walio wa mwisha, kudharauliwa, maskini na wadogo kati ya watu, ndiyo jambo linalopendeza machoni pa Mungu. Hapo Kristo hakutaja habari ya kufunga, kusali, kwenda kuhiji, na kutoa sadaka kama matendo mazuri, bali alitaka kuona utendaji mwema kwa wale wenye shida.

Kwa matendo yako ya upendo sirini, hapo itajionyesha kama moyo wako ni mgumu au laini, yenye kiburi au huruma. Je, wewe ni msomi, anayeonyesha dharau na udhilifu kwa wale wadogo na wasiangaliwa? Upendo wa Kristo unakusukuma kwenda kwa wale wasiojaliwa, waliotupwa, wajane na yatima? Utapata thawabu tu kwa ajili ya matendo yako ya upendo, wala si kwa ajili ya ibada zako na kushika kikamilifu mambo yote ya kidini.

Paulo akuonyesha njia ya pekee kwa upendo wa Mungu unaojimwaga mioyoni mwetu. Yeye anayeelekeza tabia yake kutazama utukufu wa Mungu, na asiyekimbilia utajiri unaopita tu, au heshima itakayokufa tu, huyu basi atamkaribia Mungu, naye atakuwa anabadilishwa kuwa na huruma. Huyu atafutaye utukufu wa Mungu atakuwa mwenye kuvunjika katika kiburi chake mwenyewe, wala hatadai kupewa heshima kwa ajili yake mwenyewe. Mtu wa namna hii atubuye, atafungua moyo wake kwa msamaha wa Mungu, naye atashikamana na neema yake kama ngao kubwa. Yeyote anayezingatia hali yake ya kufa, atatamani kupewa uzima wa milele, naye ataipokea kiimani, na atashiriki katika mambo ya Roho wa milele. Kwa sababu hii basi, uwe mwangalifu, huokolewi kwa matendo yako mema, bali kutamani kwako umpate Mungu itavuta nguvu yake ndani ya udhaifu wako, na upendo wake utakumba moyo wako, ili uweze kutimiza yale ya tabia ya upendo. Je, utamtafuta Mungu na kuishi milele?

Yule atendaye mabaya, hatendi yale kwa sababu amezaliwa kuwa chombo cha ghadhabu na kuchaguliwa na kutayarishwa kwa ajili ya angamizo, hapana, bali kwa sababu hajakubali kutii ule ukweli. Matendo maovu hayatendeki tu kwa kufumba na kufumbuka. Hayo ni matokeo ya maendeleo marefu yenye makosa. Dhamiri yetu inakataa matendo yote yasiyofaa. Inatukaripia na kutuonya tusimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Hata hivyo, yule anayekuwa kaidi na kukataa sauti ya Mungu, na akijikabidhi kwa roho ya kutokutii, atavunja sheria kwa ushupavu na ugumu wa moyo, akituliza dhamiri yake. Matendo yetu mabaya ni matokeo ya kushawishika na majaribu yanayotuzunguka, pia kutokana na maonyesho mabaya ya sinema, vitabu, urafiki usiofaa, na hata mawazo ya mioyo yetu, yanayotuvuta kwa mabaya.

Yeyote anayezuia mvuto wa Roho ya Mungu ataangukia hukumuni, kwa vile amefunga moyo wake dhidi ya kipawa cha Mungu na kumdharau Aliye Juu na kuchokoza hasira yake. Adhabu ya Mungu kwa uhakika itawaangukia kwa lazima wote wasiotii, wakijipatia matatizo na maumivu. - Je, unaishi na nguvu ya Kristo, kwenye usawa wa upendo, au unadidimia chini ya ghadhabu ya Hakimu wa haki? Huwezi kutoroka jibu kwa swali hilo. Basi uwe tayari kwa kujitayarisha kwa siku ile ya utengano kati ya wema na ubaya.

Kwa tamko lake kwamba, hukumu kwanza itawaangukia Wayahudi, Paulo alimaanisha kwamba, agano la zamani nao liliweka wajibu mazito juu yao, na hivyo Mungu atawaita kwanza watoe taarifa. Yeyote kati ya Wayahudi, kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake, atakayemkaribia Mungu atang’aa na fahari ya utukufu wa Mwenyewe. Lakini yeyote kati yao anayeendelea katika hali yake ya moyo mgumu atashushwa kuzimuni kabla ya wengine, kwa vile hakumruhusu Roho wa Mungu abadilishe roho wa kutokutii ndani yake.

Wayunani, watu wa Mongolia na watu weupe na weusi pamoja na mataifa yote na lugha zote, wote watakuwa na haki ya kumkaribia Mungu, maana ndiye muumbaji wa watu, tena wote, wala yeye hawezi kukaribisha ubaguzi. Mbele zake wote wako sawa. Hata wale wastadi watajiri watapoteza hali ya kujitokeza mbele ya utukufu wake safi. Sisi sote tuko kama si kitu mbele za Muumba wa wote. Wakina mama wanaohudumia manyumbani mwao na ndugu wale wadogo pengine watang’aa zaidi katika Roho wa Kristo kuliko hata maaskofu, viongozi wakubwa au „superstars“ (VIP’s).

Mungu atatupima kwa kipimo cha upendo wake. Awaye yote atakayeruhusu kubadilishwa afanane na tabia ya upendo tukufu, huyu atakubaliwa. Lakini atakayefanya moyo wake kuwa mgumu na kujipenda mwenyewe zaidi ya wengine, atakwenda mbali na Mungu na kunong’ona dharau. Bwana ni mwenye haki na mwaminifu. Kwake hakuna upendeleo kabisa.

Ndiyo, tunathibitisha kwamba, hakuna mwenye haki ndani yake mwenyewe, au mwenye huruma kama Mungu. Lakini yeyote atakayejinyosha kwenye kisima cha upendo, atakuwa mwenye haki, kwa sababu enzi yake Baba wa mbinguni itawabadilisha wote wanaomtafuta. Hata hivyo, usifikiri kwamba badiliko la namna hii na hali ya utayari kwa kazi ya rehema ya Mungu inatendeka haraka. Ushindi juu ya kiburi cha umimi unadai muda, nao ni wachache tu wanaotaka kuwa watumishi wa wale wanaoanguka. Hii ndiyo sababu ya Yesu kutujia na kula na wazinzi na watoza ushuru, ili na sisi tukubali kukataa mioyo yetu migumu, tupokee mioyo laini na kuwapenda wenye dhambi jinsi Mungu anavyowapenda.

Je, unafahamu thawabu ya wale wanaoendelea katika matendo ya upendo kwa uvumilivu usiokoma? Mungu atawavisha hao wote walio wazi kwa roho ya neema na utukufu wake mwenyewe. Kwa hiyo, hitimisho tukufu ya watu wake haitapungua shabaha na sura yake aliyeikusudia mwanzoni. Yeye aliwaumba watu kwa mfano wake, na alikusudia kumwaga utukufu wake wote na tabia za pekee ndani ya vyombo hivi. Aliye Juu huwaheshimu wale walio na huruma na wale wasiofaa machoni pa watu. Amani yake hutawala ndani ya mioyo ya wale waliotupwa na kukataliwa kwa sababu ya uadilifu wake.

Mwisho wa hukumu itakuwa hatua ya kuwatenganisha wenye mioyo laini ndani ya utukufu wa furaha ya Mungu, na wale waliofanya mioyo yao kuwa migumu dhidi ya mvuto wa Roho Mtakatifu, naye atashuka haraka matesoni ya jehanum yasiyokoma Usidanganyike, Mungu hadhihakiwi; maana yote atakayopanda mtu, atayavuna yayo hayo.

SALA: Ee Bwana, upendo wangu ni ndogo na umimi wangu ni kubwa. Mimi ni mchafu mbele zako. Unisamehe dhambi zangu. Nifungulie macho yangu kwa matendo ya upendo wako. Niongoze kwenye maisha ya kukubali kujitoa kabisa na ya matendo mema, maana hakuna ya kufaa ndani yangu. Niokoe na mimi mwenyewe na unijaze moyo wangu na upendo wako, ili niwatafute wale waliodharauliwa, na nikubali kuketi na watu wa barabarani katika upendo, na niwabariki, jinsi wewe ulivyowatafuta wale waliopotelea, ili uwaokoe.

SWALI:

  1. Zipi ni kanuni tukufu zitakazotumika katika hukumu ya mwisho?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 02:59 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)