Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 074 (The raising of Lazarus)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
4. Kumfufua Lazaro na matokeo yake (Yohana 10:40 - 11:54)

c) Kumfufua Lazaro (Yohana 11:34-44)


YOHANA 11:38-40
“Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba, ukiamini utauona utukufu wa Mungu?”

Kwenye eneo la Yerusalamu watu huzika maiti zao kwenye kichumba kilichuchimbwa ndani ya mwamba, ndipo kuweka jiwe kubwa la mviringo penye njia nyembamba ya kuingia. Iliwezekana kuvingirisha lile jiwe upande wa kulia au kushoto kwa ajili ya kufunga au kufungua kaburi.

Hapo ndipo walipomlaza Lazaro ndani ya kaburi ya namna hii ya mwambani. Yesu akakaribia na kutambua tisho la mauti kwenye nyuso za wote. Katika kifo Yesu alitambua ghadhabu ya Mungu inavyomwagwa juu ya watenda dhambi wote, kana kwamba Mungu aliwaachilia wahai wote mikononi mwa mwenye kuharibu. Lakini Mwumbaji hatamani kifo cha wenye uhai, bali kuungama kwao na kuokoka kwao kwa uzima.

Yesu aliagiza kuondolewa kwa jiwe lililoziba kaburi. Watu wakashituka vibaya, kwa sababu kugusa maiti ilifanya unajisi kwa siku kadhaa. Kuoza kumeanza sasa siku ya nne. Kwa namna Martha alitaka kukataa, akisema, “Bwana, si sawa kugusa tena mabaki ya mfu, ananuka.” Martha, imani yako iko wapi? Ulishuhudia sasa hivi kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu na Masihi, awezaye kufufua wafu. Tokeo la kifo na sura ya kaburi zilififisha macho yake, wala hakujua jambo ambalo sasa Bwana wake alikusudia.

Hata hivyo, aliimarisha imani yake na kutia moyo tumaini lake la kupitiliza uwezo wa kawaida ya kibinadamu. Alidai kwake tegemeo kabisa kwamba astahili onyesho la utukufu wa Mungu. Yesu hakusema, “Amini, nawe utaona nikifanya mwujiza mkuu.” Mapema zaidi aliwaambia wanafunzi wake kwamba ugonjwa wa Lazaro haikuwa ya kufa, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu (Yoh. 11:4). Yesu alijua la kufanya kufuatana na ushirikiano wake na mapenzi ya Babaye. Alijaribu kuvuta uangalifu wake kutoka kwa hali halisi mbaya ya mauti, atazame utukufu wa Mungu, unaofunuliwa kwa imani. Shabaha yake haikuwa heshima yake mwenyewe, bali enzi ya Babaye na utukufu wake zionekane.

Vivyo hivyo Kristo akuambia wewe, “Ukiamini, utaona utukufu wa Mungu” Geuza macho yako mbali na matatizo na taabu zako. Usihangaike kwa ajili ya hatia zako na maradhi, na umtazame Yesu tu, amini kuwapo kwake, ujielekeze kwake kama mtoto anavyomkumbatia mama yake. Uruhusu mapenzi yake yatendeke kwako; anakupenda sana.

YOHANA 11:41-42
“Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.”

Tumaini la Martha ndani ya maneno ya Yesu ilikubaliana na imani katika agizo lake. Akawataka wale wa karibu waondoe lile jiwe. Wasiwasi ilipanda kati ya umati wa watu. Je, Yesu ataingia kaburini na kukumbatia maiti ya mpendwa, au atafanyaje?

Lakini Yesu alisimama kimya mbele ya kaburi. Aliinua macho yake katika kusali, akitamka maneno ya kusikika. – Hapa tunayo moja ya sala za Yesu iliyoandikwa. Alimwita Mungu kuwa Baba. Alimshukuru Baba, kwa sababu maisha yake yote ilikuwa ni namna ya kutukuza na kuadhimisha ubaba wa Mungu. Kwa uwazi alimshukuru Mungu kwa kujibu ombi lake kabla Lazaro hajafufuliwa. Wakati wengine walipolia machozi, Yesu alisali. Alimwomba Baba yake kumfufua rafiki yake, ishara ya uhai tukufu inayoshinda kifo. Baba alikubali, akampatia uweza wa kumwokoa aliyemezwa na tisho la mauti. Yesu aliamini kwamba sala zake zitajibiwa, bila shaka lolote. Maana wakati wowote alisikiliza sauti ya Babaye. Kwenye kila hatua ya maisha yake Yesu aliendelea kusali, ila hapo aliomba kwa sauti, ili na watu wapate kutambua ajabu itakayotukia hapo. Alimshukuru Baba yake kwa kujibu kila mara maombi yake. Hakuna dhambi iliyoweza kuwatenganisha, hakuna kizuizi kilichoweza kuinuka katikati yao. Mwana hasisitizi kutimiza mapenzi yake mwenyewe, wala hadai heshima kwa ajili yake, wala kuonyesha nguvu yake kwa ajili yake mwenyewe tu. Ukamilifu wa Baba hutenda kazi ndani ya Mwana. Mapenzi yake ya ki-baba ilimwinua Lazaro kutoka kwa wafu. Yote hayo Yesu alikiri mbele za makutano, ili wao nao watambue kwamba, Baba alimtuma Mwana kwao. Hivyo kumfufua Lazaro inakuwa ni kumtukuza Baba, ishara ya mwujiza kutokana na umoja wa Utatu.

YOHANA 11:43-44
“Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.”

Mara Yesu alipolia kwa sauti kuu, “Lazaro njoo nje”, baada ya kumpa Mungu utukufu, mfu akasikia (wakati kawaida wafu hawasikii lolote). Nafsi yenyewe ya mwanadamu haiangamizwi wakati wa kufa. Mbinguni majina ya waamini yameandikwa. Wito wa Mwumbaji, sauti ya Mwokozi, na utendaji wa Roho Mtoa-Uhai ukaingia kwa undani kabisa wa kifo na kushinda. Namna Roho Mtakatifu alivyoanza “kutamia” gizani mawazo na maamuzi hapo mwanzo, hapo alipoanza kuumba mambo kutoka katika utupu. (Mwanzo 1:2)

Lazaro alikuwa amezoea sauti ya Yesu na kutii. Kaburini namo akasikia na kutii kwa imani. Mamlaka ya uzima wa Kristo ikamiminwa ndani yake; moyo wake ukaanza kazi tena, macho yake yakafumbuka, miguu ikatembea.

Ndipo hatua nyingine ya mwujiza ikatendeka, maana Lazaro alikuwa amefungwa ndani ya utambaa kwa nguvu. Mfu alikuwa kama nyungunyungu ndani ya ukoko, bila uwezo wa kusikia kitu. Hakuweza kutumia mikono yake iliyofungwa, ili aondoe vifungo vingine na leso usoni mwake. Basi Yesu akawaagiza watu wamfungue kabisa.

Wote walishangaa kuona uso nyeupe wa Lazaro; alitembea iwapo bado alikuwa na vitambaa vya sanda. Wote walimkazia macho wakati alipomkaribia Yesu.

Baada ya kufunguliwa Lazaro alitembea katikati ya watu na kuelekea nyumbani. Yohana hatuelezi lolote, kama watu waliinama mbele za Yesu, wala hamna habari ya majonsi ya furaha au kukumbatiana. Wala halinganishi habari ya ufufuo huo na kipeo cha furaha ya waumini juu ya Yesu wakati wa kuja kwake mara ya pili. Yote hayo yalikuwa na maana ndogo kwa kulinganisha na ufufuo huo. Yohana anachora picha ya Yesu, mtoa uzima, ili ikiwezekana sisi tupate kuamini na kupokea uzima wa milele. Mwinjilisti Yohana alikuwa kati ya mati wa watu wakati huo; kiimani aliona utukufu wa Mungu ndani ya Mwana, kwa sababu alisikia sauti ya Kristo na kukubali enzi yake. - Je,- wewe umefufuka kutoka kifo cha dhambi kwa imani ndani ya Kristo?

SALA: Mpendwa Bwana Yesu, nashukuru kwa kumfufua Lazaro kwa jina la Baba yako. Na wewe nawe umefufuka kutoka kwa wafu. Twakushukuru kwa uhai wako ndani yetu. Kwa imani nasi tumefufuka nawe. Tunakusihi uwafufue walio wafu katika taifa letu, ili na wasioamini wapate kukutegemea, nao katika umoja na wewe wapokee uzima wa milele.

SWALI:

  1. Jinsi gani utukufu wa Mungu ulijionyesha wakati wa kumfufua Lazaro?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:40 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)