Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 003 (The word before incarnation)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
A - Neno la Mungu kufanyika mwili ndani ya Yesu (Yohana 1:1-18)

1. Asili na kazi ya Neno kabla ya kufanyika mwili (Yohana 1:1-5)


YOHANA 1: 2-4
“Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.”

Kristo hakuishi kwa ajili yake mwenyewe, lakini daima kwa ajili ya Mungu. Hakutengana na Baba yake, lakini alielekea kwake kila wakati, akiishi naye na kudumu ndani yake. Na ushirika huu wa Kristo “ kwa baba yake” ulikuwa wa umuhimu mkuu kwa Mwingilisti Yohana, hata akarundia -rudia umuhimu huu mwanzoni mwa injili yake.Ushirika huu wa kudumu kati ya Kristo na Baba yake ndio siri ya Utatu utakatifu. Hatuamini katika miungu mitatu ambayo inaachana, lakini twamwamini Mungu mmoja aliyejaa upendo. Sasa huyu Mmoja wa Milele hakai kando kwenye Upweke, lakini Mwana kila wakati alikaa naye, wakishiriki katika umoja kamili. Kama mtu hajaonja upendo wa Mungu unaomiminwa na Roho Mtakatifu moyoni mwake, hataweza kukubali ukweli wa asili hii ya Mungu. Upendo tukufu ndiyo jambo linalounganisha Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kuwa Mungu Mmoja.

Wakati Mungu alipoumba dunia mwanzoni, hakufanya hayo peke yake na katika hali ya kutulia, bali alitenda uumbaji huu na viumbe vionekane kwa kutumia Neno lake kwa sauti: “Mungu akasema: Iwe, … na ikawa”. Na kwa sababu Kristo alikuwa Neno la Mungu, Neno likawa hai kupitia kwake. Hii ina maana kwamba Kristo si Mwokozi au Mkombozi na Mwombezi, bali pia ni Mwumbaji..Kwa vile hakuna kitu kilichopo kisichoumbwa na Kristo, yeye ni mwenye enzi yote. Kwa sababu hakuna linalofanyika bila yeye kulifanya, yeye anatawala vyote. Laiti mioyo yetu ingekuwa pana na wazi kwa kutosha, ili kuelewa na kumtambua Kristo alivyo! Utafiti wote wa kisasa wa kisayansi na mambo yote na viumbe vya ajabu, pia na nyota kwa miungano yake kwa ukubwa na umbali wake, ni mambo yasiyotosha kueleza utukufu na nguvu za Yesu. Sauti yako ya pekee, misuli yako na sura ya mwili wako na mipigo ya moyo wako pamoja na mengi mengine, yote hayo ni zawadi za Yesu kwako. Lini unampa Mungu shukrani kwa yote hayo?

Vitu vyote viliumbwa, ila Mungu siye, Neno lake na Roho yake havikuumbwa. Yeye ndiye Uzima, ni wa milele na takatifu. Jinsi Mungu anavyo uzima ndani yake, vile vile Kristo ndiye chanzo cha uzima wa kweli. Ndiye mhimizaji mwaminifu anayetufufua toka kifo cha hatia na dhambi na kutujenga ndani ya uzima wa milele. Maisha matakatifu haya ndani ya Kristo yashinda kifo. Yeye alitoka kaburini kwa nguvu ya uzima wake tukufu. Basi Kristo siye Mwumbaji tu, lakini ndani yake ni chanzo cha uhai. Jinsi alivyo Mtakatifu, hatakufa kabisa milele. Hakuna dhambi yeyote inayoweza kuonekana kwa Mungu au katika Mwana wake. Kwa hivyo yu hai daima. Basi, mawazo juu ya maisha ya Kristo tunakuta mara kwa mara katika sura za injili ya Yohana. Maisha haya ndio msingi wa kueleza Ukuu wake.

Mwangaza wa jua unazaa uhai kwenye sayari yetu iitwayo “Dunia”. Lakini kadiri Kristo anavyohusika, ukweli ni kinyume cha hayo: Uhai wake ndiyo unasababisha mwangaza na vitu hai duniani, na uamsho wa uhai kwa kila kizazi kipya kinatupa tumaini. Imani yetu si imani ya sheria ya kifo na ya hukumu, bali ni ujumbe wa uhai, mwangaza na tumaini. Kufufuka kwa Kristo kutoka kwa wafu unafuta hali ya kukata tamaa. Kutawala kwa Roho Mtakatifu ndani yetu inatuweshesha kushiriki ndani ya maisha ya Mungu.

Dunia imekuwa giza kwa sababu ya dhambi, lakini Kristo ndiye upendo ndani ya nuru. Ndani yake hakuna giza wala ubaya wala kosa. Kwa sababu hii Kristo anaonekana hali amejaa utukufu. Yeye anang’aa kuliko nuru yoyote. Hata hivyo,Yohana Mwinjilisti hakuanza kutaja utukufu wa Kristo wa kung’aa, ila alionyesha nguvu na uhai wake. Maana kwa kufahamu utukufu wa Kristo kunatuangazia maisha yetu, kunatuhukumu na hata kutuangamiza. Lakini kwa kupokea uhai wake nasi tunafanywa hai. Kutafakari juu ya Kristo kunatutuliza na kutuburudisha kweli kweli.

Kristo ndiye nuru ya binadamu. Haangazi kwa alili yake mwenyewe, wala hatukuzi jina lake mwenyewe. Ila anaangaza kwa sababu yetu sisi. Maisha yetu sio chanzo cha nuru, bali cha giza. Wanadamu wote ni wabaya, lakini Kristo atumulikia kwa ndani ili tujitambue na kuelewa hali yetu ya giza. Kwa uweza wa injili yake tunaweza kutoka kwa hali ya kifo na kuingia katika uzima wa milele. Kristo anatuvuta na kutuita kupitia kwa nuru ya maisha yake, ili tuache maisha yasio na matumaini.Tumwendee kwa ukakamavu na moyo wa ushujaa.

SALA: Ee Bwana Yesu, tunanyenyekea kwako kwa sababu wewe na baba yako na Roho Mtakatifu mko Mmoja. Uliumba ulimwengu wote katika ushirikiano na Baba.Ulinijalia na mimi uhai. Nisamehe giza lote maishani mwangu na unimulikie kwa uwezo wa Roho wako Mtakatifu, ili niishi na ukweli na kuagana na giza la dhambi zangu, kisha nielekee kwenye nuru ya uzima wako wa milele.

SWALI:

  1. Ni sifa gani sita za Kristo, ambazo Yohana anazoonyesha mwanzoni mwa injili yake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:51 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)