Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 01 -- Introduction: The All-Importance of the Ten Commandments
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

01 - Utangulizi: Umuhimu kuu wa Amri Kumi


Msafiri wa Ndege arukaye toka Delhi kwenda Srinagar nchini Kashmir huona mapema uzuri wa upeo wa macho ya milima ya Himalaya inayofunikwa na theluji, ikianza kutokea kutoka katika ukungu wa tambarare ya India. Milima ya juu kabisa imegawanyika na mabonde membamba ya kukata chini sana. Baadhi ya vilele vya milima vimefunikwa na mawingu. Ile marefu sana yenye meta 8,000 na zaidi yanapitiliza juu ya yale yenye vilele vya meta 5,000.

Baada ya kutua Srinagar mgeni hukumbwa na mchanganyiko wa dini na utamaduni za kumfadhaisha. Wahindi, Wabudhisti, Wayahudi, Wakristo, Waislamu na wasioamini lolote huishi hapa pamoja. Mahekalu, makanisa, mamuskiti na mbao za matangazo zinashindana kuvuta macho na usikivu wa umati wa watu. Mataifa matano hukutana kwenye eneo hilo dogo la dunia - Uhindi, Pakistani, Afganistani, Urusi na China - na yeyote asafiriye humu kwenye miji na vijiji vya Kashmir na kuongea na wenyeji hapo, basi atasikia mvutano wa mahangaiko. Na kwa hali halisi, vita ya wenyeji ya kumwaga damu sana imeharibu sana bonde hili nzuri tangu mwaka 1991.

Utamaduni na sheria za dini kuu za ulimwengu pamoja na malengo ya siasa za serikali kadhaa zinafunua upeo wa kushangaza kama vile milima ya Himalaya inavyofanya. Lakini maandiko yasiohesabika, liturgia na sheria za kidini zinatoa nafasi kwa ajili ya machache yanayotawala juu ya mengine hayo, kama vilele vya juu vya Himalaya vinavyokaa juu ya yale yanayopungua.

Moja vya hivi vilele vya juu vinavyotawala katika historia ya binadamu ni hizi Amri Kumi. Huyu Mungu mmoja wa kweli alisema na mchungaji Musa, akifunua mapenzi yake kwake na kuandika Amri zake za pekee kwenye mbao mbili za mawe. Wayahudi wanamkumbuka huyu mzee mkubwa mwenye heshima kwa ustahifu sana, maana kwa njia yake Mungu alifanya Agano lake nao juu ya mlima Sinai. Maandiko yake husomwa katika masinagogi yao hadi leo, miaka 3,300 iliyopita.

Wakristo nao wanaona Amri Kumi kuwa ni msingi wa imani yao usiobadilika. Yesu aliwathibitishia wanafunzi wake kwamba, hata „yodi moja wala nukta moja haitaondoka“ katika amri za Musa hadi mwisho wa mbingu na nchi, na hata yote ya amri yatimie (Mathayo 5:18)

Waislamu wanamwita Musa „Kalimu Allah“, msemi wa mMungu. Wanamhesabia kuwa mjumbe wa Allah pamoja na kuwa kiongozi wa kisiasa, aliyekuwa na mamlaka ya kidini sawa na ya kisiasa pia. Kwao anaendelea kuwa mmoja wa watu wakuu katika historia nzima.

Amri Kumi, ambazo Musa alizipitisha kwa wanadamu zilikuwa na mahali pa pekee katika nyakati za Agano la Kale, na pia ni msingi kwa wanadamu hadi leo. Yeyote achunguzaye hizo Amri, akizishika na kuzifundisha, atakuwa mwenye hekima. Watu waliodharau au kusahau hizo sheria wataendelea kuchafuka, watapungua na kupotea. Yeyote atakayekupisha maovu hayo itampasa kujifunza sana hizo Amri Kumi kwa bidii.

Kuzingatia Amri Kumi imekuwa muhimu kule Kashmir kwa sababu dini za awali za dunia zinakabiliwa na mawazo ya kisasa na misimamo yao; hivyo maisha ya kila siku yanamsukuma mtu kurudi kwa sheria za Mungu ilivyo katika Agano la Kale. Kitabu hiki kimekuwa nje ya maongezi na majadiliano pamoja na vijana kule penye nchi ya juu ulimwenguni. Vijana kutoka dini zingine zinazotofautiana walichunguza kupata ukweli na wapate mwongozo kwa maisha yao, pia waliangalia ndani ya uwiano wa Amri Kumi kwa siku hizi. Yeyote atakaye kutafakari na kuzingatia hayo pamoja nao atapokea maoni ya ndani yasiyo na muda, na hayo yatamsaidia katika maisha yake ya siku kwa siku.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 02:02 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)