Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 076 (The Secret of Paul’s Ministry)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Maongezo kwa SEHEMU ya 3 - Maelezo ya pekee juu ya msimamo wa Paulo kwa viongozi wa kanisa la Rumi (Warumi 15:14 – 16:27)

2. Siri ya huduma ya Paulo (Warumi 15:17-21)


WARUMI 15:17-21
"17 Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu. 18 Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, 19 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kandokando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; 20 kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine; 21 bali kama ilivyoandikwa, Wale wasiowahi kuhubiriwa habari zake wataona, Na wale wasiowahi kusikia habari zake watafahamu."

Paulo alifurahia na kutukuza huduma yake na ushindi wake hadharani. Hata hivyo, alitangaza mara moja kwamba, kazi na maneno yake hazikutoka kwake, bali kutoka kwa Yesu Kristo, aliyeishi ndani yake, na hivyo kutenda kazi na kusema kwa njia yake. Mtume wa Mataifa hakuwa na ujasiri kusema habari ya matokeo na mabadiliko, ambayo hayakutokana na Kristo mwenyewe, bali alijihesabu kuwa mtumwa wa Mwokozi wake, mwenye utii kwa uongozi wake. Hii ndiyo siri ndani ya maisha ya Mtume, kwamba mwenyewe alikuwa „ndani ya Kristo“. Alikuwa akiwaza mawazo ya Kristo, alitamka yale ambayo Kristo alitia ndani yake, naye akatenda yale ambayo yeye alimwagiza ayatende. Huu ndiyo mstari mwekundu katika kuandika kitabu cha Matendo ya Mitume, na pia ndiyo siri katika hotuba yoyote inayohubiriwa makanisani siku hizi. Shabaha ya Bwana Yesu Kristo aliye hai katika maisha ya Paulo, aliyejifanya kuwa mtumwa wake, ilikuwa hata kuwaongoza watu washenzi wapate kumtii Kristo kwa imani.

Hotuba zote na maandiko ya Paulo hayakutosha kwa huduma hiyo; kwa hiyo basi, ilimpasa kuvumilia safari za taabu, ale chakula kigeni, afanye na kazi sana kwa mikono yake, hata kutenda maajabu. Alishuhudia wazi kwamba, hotuba zake zote, kazi zote za mikono na pia miujiza zilikamilishwa kwa nguvu za Baba, Mwana, pia na Roho Mtakatifu, wala si kwa uwezo wake. Siri ya huduma yake na matokeo yake ilikuwa ni msimamo wake wa kujikinahi mwenyewe, na upande wa pili kumkuza kabisa Kristo Mwokozi.

Paulo alieleza habari ya kuenea kwa huduma yake kuanzia Yerusalemu hadi Anatolia, na hata mpaka Uyunyai wa magharibi. Maeneo hayo yote yalikuwa chini ya Serikali ya Kirumi, na Paulo alisafiri karibu safari zake zote za taabu na hatari kwa miguu, si mbegani mwa farasi au kwenye gari la kuvutwa. Alijichosha mwenyewe katika huduma yake ili kuwafikisha kwake Yesu wale wasioamini, wasiojua, na wapagani. Pia alihakikisha kwamba, heshima ya huduma yake ilikuwa kushirikisha injili ya Kristo kwa jiji kubwa, miji, vijijini na kote katika maeneo ambapo jina la Yesu lilikuwa bado halijajulikana kwao. Yeye hakutaka kujenga juu ya misingi ya wengine, bali alikusudia kuwa wa kwanza wa kuhudumia ambapo hakuna mwingine aliyemtangulia hata katika magumu na hatari ambazo alizivumilia. Kwa huduma yake alitimiza ile ahadi tukufu iliyofanywa na nabii Isaya:

„Ndivyo atakavyowasitusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasioambiwa watayaona; na mambo wasioyasikia watayafahamu.“ (Isaya52:15)

Wayahudi, kwa wengi wao, hawakusadikishwa kwa mpango huo tukufu, kwa vile walijiangalia kuwa wao tu ni watu wa Mungu. Lakini Paulo alieleza ukweli wa huduma yake kati ya Mataifa, uliowekwa kwenye msingi wa thibitisho la kibiblia, pia na ahadi zote za Mungu kwa Mataifa.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakushukuru kwa Yesu Kristo, kwa sababu watumishi wake waaminifu hawakusema katika jina lao wenyewe, wala kutenda kazi kwa nguvu zao tu, bali walisema na kutenda kazi katika jina la Kristo na kupokea nguvu zake. Twaomba, kinga watumishi wako na maneno na matendo, ambayo yametokana na mapenzi yao wenyewe tu, ila uwaimarishe ndani ya mwili wa kiroho wa Kristo daima.

SWALI:

  1. Ipi ndiyo siri ya kufaulu katika huduma za Mtume Paulo?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 12:49 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)