Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 075 (Paul’s Worthiness to write this Epistle)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Maongezo kwa SEHEMU ya 3 - Maelezo ya pekee juu ya msimamo wa Paulo kwa viongozi wa kanisa la Rumi (Warumi 15:14 – 16:27)

1. Kustahili kwake Paulo kwa kuandika waraka huu (Warumi 15:14-16)


WARUMI 15:14-16
"14 Ndugu zangu, mimi mwenyewe nina hakika juu yenu, kuwa ninyi mmejaa wema, na mmejazwa ujuzi wote, tena mnaweza kuonyana. 15 Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu, 16 ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu."

Baada ya kukamilisha uchunguzi wake kuhusu taratibu za kitheologia, pia na kwa kuongeza maoni yake kwa huduma ya kila siku, Paulo akajumlisha wito na kustahili kwake ya kuandika waraka huo. Alifanya hivyo, ili wasomaji wasije wakawa mateka ya malaumu au mashaka. Paulo aliwathibitishia Wakristo kule Rumi kwamba, wao hawakufuata filosofia ya kitheologia ya mawazo tu, bali kwamba, matunda ya injili yalitambulikana ndani yao. Aliwaita kuwa ndugu zake mwenyewe katika roho na ndani ya familia ya Mungu, ambao wamepata kuwa watoto wa Mungu kufuatana na ukweli na ndani ya roho. Wao walikuwa na sifa hizo kwa sababu walijawa na wema, wala si kwa sababu yao wenyewe, bali walijaliwa na Mungu. Wao hawakusema tu habari za Bwana na uhusiano wao naye, lakini waliishi kweli katika kujitoa kwake katika upendo, unyenyekevu na heshima, ili kwamba hata wale waliokuwa nje ya kanisa walishangaa juu ya wema wao.

Mtume Paulo alihakikisha ya kwamba, mapendeleo hayo ya kiroho na tabia tukufu zinatokana na ufahamu wa Mungu Baba kwa njia ya imani ndani ya Mwana wake. Aliwaambia, kwa kutia chumvi kidogo, kwamba wao walijawa na ufahamu wote. Kweli walijua kwamba, Mungu mtakatifu ndiye Baba, pia kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wake mpendwa, na kwamba wao wametambua nguvu ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu hiyo wao walikuwa wanaishi kwenye daraja lingine kwa kulingana na Wayahudi wengine na Mataifa kwa jumla.

Basi mambo hayo yaliwajalia wajibu wa kuwatengeneza wao kwa wao, si kwa kiburi na choyo, bali kwa uvumilivu wa Kristo na uongozi wa Roho wa kweli. Upendo wa kweli unatambulikana wakati unaposhirikisha ukweli kwa upole na pamoja na upendo kwa wale wanaoonekana wanakwenda kambo. Hata hivyo, maongezi mazuri na ya ukweli yanahitaji mazoezi, utambuzi wa kutosha na utendaji unaofaa hasa kwa heshima. Mtume Paulo aliandika waraka huu mbali na kukomaa kwake kiroho katika taratibu zote za imani ya Kikristo na mwenendo wa maisha, naye aliutaja waraka wake kuwa ni „sehemu“ tu.

Katika sehemu ya 1 ya waraka wake alifafanua habari ya uadilifu au haki ya Mungu, aendeleaye kuwa mwenye haki, hata kama anawahesabia haki watenda dhambi kwa njia ya damu ya Yesu Kristo, na aliwajalia Roho yake Mtakatifu na upendo wa daima.

Katika sehemu ya 2 alikazia sana kuendelea daima kwa hiyo haki ya Mungu, mbali na ugumu wa mioyo ya watu wake aliyewachagua, tena kwa kusudi kwamba, ulimwengu mzima uweze kushiriki katika ukamilifu wa neema yake, ambayo ilikuwa imeahidiwa kwa mababa wa imani.

Katika sehemu ya 3 mtume alieleza namna ya utendaji wa haki ya Mungu maishani mwa wafuasi wa Kristo, jinsi inavyowapasa kuvumiliana bila malalamiko, hata ikiwa baadhi yao waliishi kwa namna fulani tofauti na wenzao.

Paulo aliandika habari ya malengo hayo katika waraka wake fupi: „Misingi ya imani“, „Fundisho kuhusu kuchaguliwa mapema“, na „Taratibu za kushirikiana maisha kikristo“. Aliandika ili kulikumbusha kanisa lililozawadiwa na Roho wa Mungu kwa ukamilifu wa habari zote za Mungu zinazojaliwa kwa waumini. Alikuwa na ujasiri wa kukaza taratibu hizi za msingi katika Ukristo, kwa sababu aliwahi kuona maishani mwake msamaha kamili wa Mungu, ingawa aliwahi kutesa washiriki wa kanisa. Zaidi ya hapo, Mwenye Utakatifu alimwita awe mtumwa wa Kristo, hata aende kutangaza injili kati ya watu wa Mataifa bila masharti. Huduma hiyo haikuendeshwa kwa fujo, upanga au kumwaga damu, wala si kwa maneno ya kushawishi, bali kwa njia ya maombi, imani, pia na kwa kutoa shukrani mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Paulo akapata kuwa kuhani wa kiroho aliyepatanisha majeshi ya watu na Mungu, hao wasiokuwa Wayahudi.

Maneno yake mazito yalilenga shabaha ya kuwatayarisha wale, ambao hawakujua kitu na kuishi katika hali ya kupotea, ili wajikabidhi kwake Kristo kwa njia ya kutoa shukrani katika utii wa imani kwamba, ili wajaliwe kupandikizwa kuwa washiriki katika mwili wa kiroho wa Kristo. Huduma yake ilikuwa inaendeshwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, aliyemwongoza Mtume akamilishe huduma yake kufuatana na mapenzi ya Kristo. Hali ya kumpendeza Mungu ilimsindikiza, kwa sababu alikuwa akitii shabaha za Roho yake.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakuadhimisha, kwa sababu ulimfanya Sauli, aliyekuwa mtaalamu wa Torati asiyetii, apate kuwa mnyenyekevu na mvumilivu kwa kutokewa na Kristo mwenyewe akiwa karibu na Dameski. Wewe ulimwokoa, ukamwita Paulo, ndipo ukamwimarisha kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ili baadaye atangaze wokovu wa Kristo kati ya watu walioishi katika bonde lote la Bahari ya Kati. Na kipekee twakushukuru kwa ajili ya waraka huu wa thamani sana kwa kanisa la Rumi, kwa sababu unakumbusha pia makanisa yote ulimwenguni kwa njia safi taratibu za imani yao.

SWALI:

  1. Paulo aliandika nini katika waraka wake, ambao aliona kwamba ni sehemu tu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 12:46 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)