Previous Lesson -- Next Lesson
11. Kristo alishinda tofauti zote kati ya waumini wa Wayahudi na wale waliotokana na Mataifa (Warumi 15:6-13)
WARUMI 15:6-13
"6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. 7 Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe. 8 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu; 9 tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako. 10 Na tena anena, Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake. 11 Na tena, Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana; Enyi watu wote, mhimidini. 12 Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini. 13 Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Mtu asomaye sura za 9 hadi 15 za waraka kwa Warumi, aweza kutambua kwamba, maisha ya kila siku ya kushirikiana kati ya Wakristo wa asili ya Kiyahudi, na wale wa kutoka kwa Mataifa, ilitokeza utofauti bila sababu ya haki. Kiini cha utofauti huo ilikuwa ni tohara na vyakula kutokana na Sheria za Musa, na hapo na kwa hayo namna ya Kiyahudi na namna ya Kikristo. Shabaha ya maneno mema ya Paulo aliyowaandikia Warumi ilikuwa ni kuwaunganisha waumini wa Wayahudi pamoja na wale watoka Mataifa, na ajenge daraja juu ya ufa kati yao, maana Kristo mwenyewe aliwaunganisha: Kwa sababu hiyo, aliandika mwisho wa waraka wake: „Mkubaliane ninyi kwa ninyi, mbali na asili na desturi zenu zilizo tofauti, jinsi Yesu Kristo naye alivyowakubali na kuwaokoa. Na yeyote anayetambua siri ya wokovu huo anamtukuza Mungu, Mwana na Roho Mtakatifu, pamoja na wengine wasio na tofauti, hali ya kujitenga, au hata chuki“.
Upendo hudai huo umoja wa waumini walio tofauti, maana upendo wa Kristo unayo nguvu kuliko tofauti zinazofikiriwa. Paulo aliweka wazi taratibu hiyo kwa waumini wa asili ya Kiyahudi, akawaeleza wazi kwamba, Masihi huyu mtazamiwa akajifanya kuwa mtumishi kwa ajili ya Wayahudi, ili afunue haki na ukweli wa Mungu, na jinsi alivyotimiza ahadi zake kwa maneno na matendo. Kwa hiyo Kristo alitimiza zile ahadi nyingi zilizofunuliwa kwa ajili yake kwa wababa wa imani, ili waweze kutambua kwamba, ukweli hauwezi kupindwa.
Mtume aliwaeleza waumini waliotoka kati ya watu wanajisi wa Mataifa kwamba, iliwapasa kumtukuza Mungu, kwa sababu alikuwa aliwahurumia naye aliwapatanisha, pia aliwapokea kuwa watoto wake na kuwafanya wapya. Sifa kwake Baba na kwa Mwana inayotolewa na wale wasiotoka kwa Wayahudi ndiyo thibitisho kwamba wamemchagua Kristo kweli. Jambo hilo pia ni kamilisho la ahadi za Agano la Kale, maana Kristo naye ni nuru ya Mataifa, na Wakristo kutokana na Mataifa nao wamejaliwa kushiriki katika furaha ya Mungu, maana Kristo aliweka wazi kwamba, alitaka furaha yake ipate kukamilishwa ndani yao (Yohana 15:11 na 17:13). Hata hivyo, waumini toka kwa Mataifa inawapasa wasiwasahau waumini toka kwa Wayahudi, bali inawabidi wamtukuze Baba na Mwana kwa sauti moja na kwa moyo wao wote (Kumbukumb la Torati 32:43).
Ahadi hizo katika Agano la Kale hazikugawiwa kwa ajili ya chaguo ndogo kati ya bara zote za ulimwengu, bali ni kwa ajili ya Mataifa yote yaliyoahidiwa kwamba, wamtukuze Baba ndani ya Bwana Yesu (Zaburi 117:1). Katika ahadi hizo za thamani sana tunakuta mamlaka ya kiroho na wokovu mkuu kwa ajili ya binadamu. Yeyote aaminiye ndani ya Kristo ashiriki katika utajiri wa rehema zake.
Isaya alikuwa ametabiri: „Ndipo chipukizi kitainuka kutoka shina la Yese … Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu; yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta na kutumaini ndani yake.“ (Sura ya 11:10 na penginepo). Unabii huu ukapata kutimizwa ndani ya Yesu, kwa sababu yeye huketi mkono wa kulia kwake Baba, na enzi zote zimekabidhiwa kwake mbinguni na duniani. Yesu pia aliwaagiza mitume wake waende na kufanya wanafunzi kutoka kwa mataifa yote, ili nao waongozwe na kujazwa na Roho yake, pia na ufalme wa Mungu upate kukua kati yao.
Sala ya Mtume wa Mataifa zinalenga shabaha ya kueneza kote lile tumaini, ambalo tokea hapo umoja wa waumini unafanyika. Mtume alitafuta sana ukamilifu wa miili yote miwili (Waumini toka Wayahudi na wa toka Mataifa) washiriki furaha za mbinguni na amani ya Mfalme wa Amani, wapate kujenga imani ya kweli katika umoja wa Utatu Utakatifu, ili wote wapate kutajirika katika tumaini na nguvu za Roho Mtakatifu.
SALA: Ee Baba wa Mbinguni, twakuomba kwa jina la Mwana wako Yesu uwaongoze waumini wa asili ya Wayahudi wasiwadharau waumini watokao kwa Mataifa; lakini waumini wote watambue kwamba, wamepata kuwa umoja usioweza kugawanyika kwa njia ya malipo ya Yesu Kristo. Uwajalie wote utulivu na kusogeana wao kwa wao katika imani, ili wadumu katika umoja kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Amina.
SWALI:
- Jinsi gani Paulo alitazamia kushinda matofauti ya msingi yaliyokuwa ndani ya kanisa la Rumi?