Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 073 (How those who are Strong in Faith ought to Behave)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

10. Jinsi inavyowapasa walio imara kiimani kulinda mwenendo wao wakati wa matatizo ambayo hayakutazamiwa (Warumi 15:1-5)


WARUMI 15:1-5
"1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. 2 Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. 3 Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Matusi yao waliokutusi wewe yalinipata mimi. 4 Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini. 5 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunuia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa kufuata mfano wa Kristo Yesu;"

Paulo alifahamu desturi kuhusu chakula na vinywaji, zilizokuwa na mizizi ya muda mrefu sana. Alikabiliana na wale waliokuwa na nguvu na kuwekwa huru kabisa na sheria, naye alijijua mwenyewe kuwa mmojawao. Lakini mapema aliiwekea mipaka uhuru wake, akisema kwamba, wale walio wenye nguvu na kukomaa inawapasa kubeba madhaifu ya waumini wapya, wakati wote wanapomwamini Kristo. Si vema kuishi tu kwa kujipendeza wenyewe, bali tuishi namna ya kuwapendeza waumini wapya, wasio na uhakika juu ya mambo yote. Kufanya hivyo ni kwa ajili ya wema wao na maadilisho yao, kwa kuwa mafundisho hayo kwa wengine ni muhimu zaidi kuliko kutimiza mapendekezo na haja zetu sisi wenyewe.

Mwongozo kama huu unaondoa uwembamba wa roho ya kujifikiria mwenyewe tu kanisani kwa pande zote. Tusipange maisha yetu, kazi zetu na nafasi zetu kufuatana na ndoto zetu, bali kwa kumtumikia Yesu na wale walio wadhaifu kiimani, maana lengo la mawazo yetu sio „Mimi“, bali „Yesu na Kanisa lake!“ Yesu hakuishi kwa ajili yake mwenyewe, bali alimwaga chini utukufu wake, akawa mwanadamu. Alivumilia mashitaka, matukano na mateso, ili aokoe ulimwengu, na mwishowe aliwafia wote, akidharauliwa kama kuwa mhalifu mkuu, ili kuweza kuwaokoa hata wahalifu na kuwafundisha mema.

Yesu aliishi kufuatana na Biblia Takatifu; maisha yake yakiwa uvumilivu, unyenyekevu na subira ya kupita kiasi. Kutoka katika vitabu vya Agano la Kale alichukua mwongozo na nguvu kwa ajili ya huduma yake. - Yeyote anayetamani kuhudumia kanisani au kati ya wale wanaomkataa Kristo, lazima wawe na mizizi ya chini kabisa ndani ya neno la Mungu, vingine atapungukiwa na nguvu na furaha kwa huduma yake.

Paulo alijumlisha uchunguzi wake mrefu kuhusu mambo hayo kwa kudokeza kwamba, Mungu ni Mungu wa uvumilivu na faraja (Warumi 15:5). Mwumbaji mwenyewe ahitaji subira wa muda mrefu, ili kuwezana na watu wapumbavu na wa kujiona wenyewe tu. Yeye apata kufarijika tu ndani ya mwana wake Yesu, ambaye ndani yake anapendezwa daima. Kwa kugundua hayo, Paulo aliongoza sala za Wakristo kule Rumi ziwe na roho ya uvumilivu na faraja, ili alipatie Kanisa hilo ule umoja usioweza kutokana kwa waumini, bali kutoka kwake Kristo tu; maana kipekee ndani yake mawazo ya Kanisani yaweza kuwa na umoja. Kwa kweli hakuna kushinda au hali ya umoja kanisani, isipokuwa zinatoka moja kwa moja toka kwake Kristo. Hivyo tu wote watashirikiana katika sifa, na wanajifunza kwa uhakika kwamba, Mhukumu mwenye enzi yote na Mwumbaji wa ulimwengu ndiye Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ilikuwa ni Yesu pekee aliyetupatanisha na Mwenye Utakatifu kwa kuteseka na kufa. Alitununua kutokana na kufufuka kwake toka kifoni na kupaa kwake mbinguni, sisi tuweze kupokelewa kuwa watoto wa Mungu na kuzaliwa mara ya pili. Hivyo tujaliwe kufurahi na kumtukuza Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo awe Baba yetu mwenye rehema. Jinsi Yeye na Mwana wake walivyo na umoja kamili kiroho, ndivyo na washiriki wa kanisa inawapasa kushikana, pia na kwake Yesu katika umoja usioweza kutenganishwa tena.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakutukuza kwa sababu Bwana wetu Yesu alitufunulia ubaba wako kwetu, akatupatanisha na wewe, naye akatufunga kwa Roho wako Mtakatifu ndani ya umoja wa upendo wako. Tujalie, upendo huo uweze kutimiza umoja kamili wa kiroho ndani ya makanisa yetu, hata wakati wa maoni yanayoweza kutofautiana kati ya waumini.

SWALI:

  1. Je, maana ya mistari Warumi 15:5-6 ni nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 12:32 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)