Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 072 (Do not Enrage your Neighbor for Unimportant Reasons)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

9. Usimkasirishe jirani yako kwa mambo yasiyo muhimu (Warumi 14:13-23)


WARUMI 14:13-23
"13 Basi tusiendelee kuhukumiana, bali amueni kuwa mtu asifanye kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. 14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 15 Na ndugu yako akichukizwa kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. 16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya. 17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. 18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu. 19 Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana. 20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. 21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa. 22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali. 23 Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi."

Kwa njia ya huduma yake katika makanisa kadhaa, Paulo alielewa maoni tofauti yaliyoendelea na kuleta ushindani kuhusu vyakula vilivyoruhusiwa au kukatazwa. Alisema, akikariri matamshi ya Yesu (Injili za Marko 7:15-23 na Luka 6:4) kwamba, hakuna kilicho najisi ndani yake yenyewe, bali mambo yanayomtoka mtu ndiyo yanayomchafua. Ni bora kwa mwumini ale vyakula kadhaa yaliyo bora kwake. Pia ni vema kwake kujizuia na vyakula vingine anavyofikiri vinaweza kudhuru afya yake.

Inawapasa Wakristo kuwa wenye mifano bora kwa wengine. Lazima wajizuie na lolote liwezalo kuwa sababu kwa wengine kutenda dhambi. Mwumini alaye na kunywa bila mipaka, na huku kujivuna na uhuru aliyo nayo, anachochea mashaka ndani ya moyo wa yule aliye mwangalifu, na awezaye kusikia kwamba anamdharau. Hivyo huyu aliye na uhuru anakuwa mwenye kosa na amesababisha kumchanganya yule aliye mwumini mpya, maana amesogeza imani yake ndani ya Kristo. Kwake yule aliye imara kiimani upendo unadai asijivune mbele ya yule aliye mdhaifu katika maoni na uchaguzi wake. Inampasa anyamaze, ili asije akawa gogo la kujikwaa kwa ajili ya yule aliyeokoka hivi karibuni.

Paulo alishsuhudia kwamba, ufalme wa Mungu haujengwi kutokana na vyakula na vinywaji, bali unajitokeza kwa matunda ya Roho Mtakatifu. Naye aliyataja kwa majina kama vile uaminifu, amani na furaha, naye aliyataja kuwa jibu kwa ajili ya mambo yanayotofautiana makanisani. Paulo alitamani sana kuimarisha umoja ndani ya kanisa, naye aliwaongoza waumini kwenye msimamo kwamba, jambo la chakula na kinywaji halistahili kuwa sababu kwa kanisa kuhangaika kwa hilo.

Umoja ndani ya roho ni muhimu sana zaidi kuliko makubaliano ya wao kwa wao kuhusu mambo yasiyo muhimu kama vile chakula , kinywaji, mavazi, jinsi ya kukata nywele, au jinsi ya kutumia pesa. Maana Roho wa Kristo kwa njia ya upendo wake na subira yake ya uvumilivu mrefu, anatawala juu ya mahitaji yote ya maisha ya hapo duniani. Paulo alishuhudia ulazima wa kujifungamanisha na upendo hasa, ulio kama chemchemi ya elimu ya Kristo, kwa kujiinua juu ya mambo madogo, huku kujihusisha sana na watu, ambao Yesu naye alikufa kwa ajili yao.

Amani ya Mungu kanisani ni muhimu zaidi kuliko uhuru kamili, na mahitaji ya kutimiza sheria. Kama yeyote ndani ya kanisa hali nyama, au kutokunywa divai, ili atulize dhamiri yake, au kwa sababu ya mipango yake mwenyewe au mashaka, basi inatakiwa kwetu kutembea naye kwa taratibu za upendo bila malalamiko, tukisikia mahitaji ya yule mwingine, ambaye imani yake inaweza kujikwaa kwa sababu ya mwenendo wetu.

Hata hivyo, mwumini mpya anayekula na kunywa kwa mashaka ya dhamiri yake, basi haendi sawa pamoja na watu wote wa kanisa lake, kwa sababu uhakika katika imani ni muhimu zaidi kuliko amani ya juujuu. Imani inayotimizwa katika upendo inashinda juu ya ushirikiano kanisani; na yule atakaye kuonyesha ushupavu wake bila mipaka, atakuwa mharibu wa roho ya ushirikiano.

SALA: Ee Bwana Yesu, tunakuabudu kwa sababu uliwakubali katika kundi la wanafunzi wako wavuvi washupavu, watoza ushuru, wajanja na wajuzi wa sheria na ya mambo yasiyoelezeka. Wewe uliwaunganisha, uliwapa umoja, wala hukuwaagiza lolote ila upendo kamili, pamoja na msamaha, uvumilivu na amani. Utusaidie tuweze kuwasamehe wengine si mara saba tu, lakini sabini mara saba kila siku, na bila kusahau ya kwamba, wao nao inawapasa kutusamehe makosa na dhambi zetu hadi sabini mara saba kwa siku.

SWALI:

  1. Ipi ni maana ya maneno ya mstari Warumi 14:17 „ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu“?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 12:29 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)