Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 067 (Love your Enemies and Opponents)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

4. Wapende adui na wapinzani wako (Warumi 12:17-21)


WARUMI 12:17-21
"17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalia yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. 19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. 20 Lakini adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hayo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.“

Yesu alishinda amri isemayo „jicho kwa jicho, jino kwa jino“. Yeye aliiwekea mwisho (Kutoka 21:24; Mambo ya Walawi 24:19-20; Mathayo 5:38-42), naye alitupatia amri yake ya kupendana, kusaidiana na kubariki adui zetu wote. Kwa kufanya hivyo alitangua mipango yote ya sheria ya Agano la Kale, na anatuongoza kwenye taratibu za kimbinguni hata wakati huu tukiwa katikati ya dunia yetu uliyoharibika.

Mtume Paulo alijitahidi, akiwa chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, atimize na kuishi kwenye maagizo ya Yesu, naye akayafundisha ndani ya makanisa. Kwa hiyo, ikiwa yeyote amekudanganya au kukusengenya, usijaribu kutetea haki na heshima yako kwa ukali au ukorofi, bali upeleke tatizo hili kwa Bwana wako anayeamua haki kwa wanaokandamizwa. Ushuhudie ukweli, wala usiwe mwenye kukwaruza au uchungu. Jibidiishe sana kufanya amani. Kubali kutoa haki zako na muda wako kama sadaka. Omba, ili Mungu aweke amani yake juu yako na juu ya adui zako. Bwana aweza kulainisha moyo wowote uliyo na ugumu, na kuumba ndani yake heshima kwa ajili yako.

Kulipiza kisasi inakataliwa kabisa kabisa kwenye Ukristo, maana Mungu pekee ndiye Mwenye Haki, ambaye, katika utakatifu wake, anaweza kufahamu yote yanayohusika, na hivyo kuamua kwa hekima na haki kabisa (Kumbukumbu la Torati 32:35).

Yesu alipanga kabisa kutuzuia tusihukumu wengine kwa sababu ya ufahamu wetu mdogo tu ya tabia yao. Alisema wazi kabisa: „Usihukumu, au wewe nawe utahukumiwa. Maana kwa namna ile ile unavyowahukumu wengine, wewe utahukumiwa, na kipimo unachotumia, wewe nawe utapimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kile kibanzi katika jicho la ndugu yako“ (Mathayo 7:1-5).

Tamko hilo la Bwana wetu linatutelemsha kutoka kwenye ujuu wetu wa fahari ya umimi na kujidanganya kwetu, na inatuonyesha vema kwamba, hakuna kabisa aliye na haki kamili. Sote tu wenye mapungufu, washiriki kwenye makosa, na wenye haraka kuwahukumu wenye dhambi, huku tukijifikiria wenyewe kuwa bila haja ya maungamo. Paulo alieleza kwa hali ya kimaisha kabisa yale maneno ya Yesu kuhusu kuwapenda maadui zetu, aliposema: Wakati adui yako hana uwezo wa kununua chakula chake, umsaidie, wala usimwache aone njaa. Kama hana maji ya kunywa nyumbani kwake, umtumie kiasi cha machupa yako bure, ili asiwe na kiu. Basi, wewe ni mshiriki katika haja za adui wako, jinsi mfalme Sulemani mwenye hekima alivyosema: „Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa. Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; na Bwana atakupa thawabu.“ (Mithali 25:21-22). Hekima hiyo sio aina ya filosofia mpya. Ilianza kumulika miaka elfu tatu ya nyuma. Tatizo sio kuwa na hekima au kukosa hekima, bali mioyo iliyo migumu na yenye kiburi, ambayo hayainami, hayataki kusamehe, wala kumwomba Bwana atoe msamaha kwa dhambi zao.

Paulo anajumlisha hotuba yake kwa tamko hilo la ajabu: „Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema“ (Warumi 12:21). Kwa mstari huo mtume anataka kukuambia: „Usiruhusu ubaya kudidimia chini ndani yako. Usiwe mbaya ndani yako, lakini ushinde ubaya unaojileta waziwazi dhidi yako kwa wema wa Kristo na upendo wake unaoshinda ufahamu wetu wote.“ Taratibu hiyo ndiyo siri ya injili. Yesu alipeleka mbali dhambi za ulimwengu, na akaishinda kwa upendo wake takatifu na kifo chake cha kutulipia. Kristo ndiye mshindi wa kushangiliwa. Anakutaka wewe nawe ushinde mambo yako maovu, pia na hali yako ya moyo mgumu, ili upate nguvu ya kiroho ya kujitwisha maovu ya wengine na kuyashinda na hayo kwa sala zako na upendo wa kuvumilia.

SALA: Ee Bwana Yesu, tunakuabudu kwa sababu wewe ndiwe upendo wa Mungu mwilini.Wewe hukulazimisha upendo wako, wala kudai haki yako kwa chuki au kisasi, bali uliwasamehe adui zako ukisema: „Baba, wasamehe, maana hawajui watendalo“, ili nasi tupate kujazwa na Roho yako na kuwasamehe adui zetu; wasaidie, wabariki, na uwavumilie jinsi ulivyotutendea.

SWALI:

  1. Jinsi gani tutaweza kuwasamehe adui zetu, na kutenda hivyo bila chuki na kisasi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 11:51 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)