Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 066 (We must Learn Brotherly Love)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

3. Tunahitaji kujifunza upendo wa kindugu na kujizoeza sisi wenyewe katika hilo (Warumi 12:9-16)


WARUMI 12:9-16
"9 Pendo na lisiwe na unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. 10 Kwa pendo la undugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; 12 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; 13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. 14 Wabarikieni wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. 15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao, waliao. 16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.“

Kuna maneno mbalimbali ya kiyunani kwa ajili ya „upendo“. Neno la „fileoo“ ina maana ya shauku ya asili ya binadamu kwa ajili ya mwingine au kuvutwa naye. Neno la „eros“ linataja tamaa ya mume na mkewe ya kulalana kutokana na silika au tabia; ndipo neno la „agape“ lamaanisha aina ya upendo kamili na ya juu. Hii ndiyo upendo tukufu iliyo tayari hata kujitoa kabisa kwa ajili ya maskini, na hata kwa ajili ya adui, ikitumia kusudi la wazi na la kuamua, na hivyo kipekee kuwa sehemu ya mafunuo matukufu.

Kristo ndiye alitoa maisha yake kuwa ukombozi kwa ajili ya wenye dhambi katika huu upendo tukufu. Hivyo basi, Paulo anasema habari ya upendo huo katika maisha ya kila siku ya wafuasi wa Kristo, jinsi alivyowahi kuandika: „Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi.“ (Warumi 5:5)

Huu upendo tukufu hautasema uongo, kwa sababu hali yake ni unyofu. Utasema kweli kwa namna ya hekima na rehema. Unafiki sio jambo jema, ndivyo Biblia inavyotuambia. Inatupasa kuungama makosa yetu tena na tena hata mbele za watu, ili kiburi au kujivuna visijifiche ndani yetu. Inatubidi kukiri upendo wetu kwake Yesu, maana yeye pekee alitujalia haki kwa njia ya malipo yake makuu msalabani kwa ajili yetu.

Upendo tukufu huo unachukia maovu yote, ambayo dhamiri yetu inatukemea, na pia yale ambayo neno la Mungu linaeleza kuwa chafu, la uongo, la kupinda na pasipo haki. Upendo hauwezi kukubali mwenendo wa namna hiyo, lakini linapendekeza usafi wote, uaminifu, mwenendo wa unyofu na wa haki kabisa.

Upendo huo tukufu unatuelimisha kwenye upendo kwa ajili ya ndugu na dada zetu katika Bwana, tukivumilia nao kila jambo bila kunung‘unika, na katika kuwachunga. Huduma zetu zote zitendeke kwa makini na kwa moyo, kusudi hata watu wengine watambue kwamba, tunawapenda kweli. Heshima ya mwanaume na mkewe wao kwa wao imejumlishwa katika orodha hii ya adabu. Yeyote anayehudumia injili, kwa maneno au maandishi, huduma yake inapaswa kutendeka katika moto ya kiroho, hata ikiwa ni katikati ya hali ya kupingwa; pia inampasa kuimarika kwa nguvu ndani ya uongozi wa Bwana.

Mtu anapopatwa na makosa asipoteze tumaini lake ndani ya Kristo aliye mshindi; na yule anayekabiliana na mateso au magumu mengine, basi aendelee kwa tumaini na uvumilivu, na ashinde katika kusali kwa imani, bila kuwa na shaka. Bwana hujibu kulia kwetu kwa ajili ya wengine na kwa ajili yetu pia.

Wewe ukiwaona ndugu zako wa imani kwamba wanateseka, inakupasa kuwahurumia na kuchukuliana na matatizo yao. Pamoja na hayo, mara wanapokuja kumtukuza Baba yao, kwa furaha uwafungulie mlango, na Bwana atakuongezea mahitaji yako unapowaridhisha wanaoona njaa kwa ajili ya jina lake. Bwana yu karibu nao wote wampendao.

Ikiwa yeyote anakukabili kwa kukudhulumu kwa matisho, umbariki katika nguvu ya baraka ya Bwana. Usiwalaani wale wanaokulaani, bali umwombe Mkombozi awaweke huru, jinsi waumini wa Dameski walivyofanya wakati Sauli alipowakaribia awatese na kuwapeleka kama watumwa hadi Yerusalemu. Hapo basi Bwana aliposimama katikati ya njia ya Sauli akivunja kiburi chake kabisa.

Wakati baraka ya Msulibiwa huyu aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, inatambuliwa kwelikweli, waumini wengine wanafurahi na kutiwa moyo kiimani, kwa sababu wanatambua ushindi wa Kristo na matokeo yake. Lakini fulani anapolia machozi kwa ajili ya majirani wanaopotea, inatufaa kushiriki na mateso yake. Usione haya kwa ajili ya machozi.

Jibidiishe kuwa kundi moja kanisani kama familia ya Mungu. Usiwaze kwanza mambo ya pesa, heshima, mamlaka na manufaa ya dunia hii, lakini ukubali kuishi na maskini na wasio na tumaini, jinsi Yesu alivyoishi pamoja na wagonjwa wengi na wenye kupagawa na mapepo na hata na wafu.

Usijifikirie mwenyewe kuwa mwenye elimu zaidi au kuwa juu zaidi ya wengine, bali umwulize Bwana wa mavuno atende kazi katika mkutano wenu wa kanisa, aponye, afariji, aokoe na kuleta matokeo kamili katika ushirikiano na huduma zenu.

Jiangalie sana usinung‘unike. Vumilieni ninyi kwa ninyi katika subira, maana Bwana ni mmoja, kafara yake ni moja, na hakuna lolote liwezalo kuwa badala ya Roho yake. Usijifanye kana kwamba unaweza kuumba wokovu bora. Sote twaishi kutokana na neema ya Baba na Mwana na Roho wa upendo wake.

SALA: Ee Baba wa mbinguni, twakushukuru kwa mwujiza wa ushirikiano ndani ya kanisa letu. Wewe ndiwe unatujalia upendo wako, uvumilivu wako na furaha yako kutokana na kuishi kwa Roho yako Mtakatifu ndani yetu, tunapoungama na kuendelea kiimani ndani ya Kristo aliye hai. Twaomba utusaidie kutimiza wajibu wetu katika upendo na uvumilivu, na wala si kwa maneno tu. Udumu nasi, ee Bwana, na ututunze ndani ya tumaini lako tukufu.

SWALI:

  1. Aina gani ya matumizi ya upendo wa Mungu unafikiria kuwa muhimu zaidi na kuhitajika sana ndani ya ushirikiano wenu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 11:48 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)