Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 065 (Do not be Proud)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 3 - HAKI YA MUNGU HUJIONYESHA MAISHANI MWA WAFUASI WA KRISTOS (Warumi 12:1 - 15:13)

2. Usiwe na kiburi, bali umtumikie Bwana wako kwenye makundi ya waumini ukitumia vipawa ulivyojaliwa (Warumi 12:3-8)


WARUMI 12:3-8
"3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja. 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani, 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii; mwenye kurehemu, kwa furaha.“

Paulo hakusema kama mchungaji, akiwapa kondoo zake mapendekezo kwa jumla, bali litoa agizo la mwisho, tena wazi kabisa, kwa maadui wote wa kanisa kote duniani.

Na wewe usiwaze juu yako makuu kuliko hali uliyo nayo, lakini ujitambue kwamba, ndani ya nafsi yako wewe si kitu, lakini pengine unaweza kuwa na usumbufu kwa wengine. Bora ufahamu kipawa chako cha kiroho, na utege sikio kwa wito wa Kristo akuonyeshe kipawa chako cha pekee. Usifanye tu yale uyapendayo, bali utii uongozi wa Kristo, si kwa kuchangamka mara moja, bali kwa uangalifu, ukizingatia pia uongozi wa wale waliokomaa kiroho.

Kipimo cha huduma yako sio kipawa chako, bali kwa kweli ndiyo kiasi cha imani yako ndani ya Kristo, maana yeye aweza kukamilisha matakwa yake katika huduma yako. Nguvu yako ndiyo siri ya kazi zako kwa ajili yake. Kwa sababu hizo, ufikiri, useme, na kutenda yote pamoja na Yesu na ndani yake, ndipo utaona matunda ya upendo wake maishani mwako.

Siri ya Wakristo wa kufanikiwa ni umoja wao wa kiroho. Umoja huo sio ya dunia hii, bali ni ya kiroho ndani ya Kristo. Wao ni kama mwili wa kiroho wa Mwokozi wao, maana yake, Kristo hutimiliza kazi zake kwa njia yao. Hakuna kati yao anayetenda peke yake, ili apate kutukuzwa, bali wote ni mamoja katika umoja wa yule Mtakatifu. Kristo ndiye nguvu yako, nawe unakamilishwa ndani yake. Hakuna aliye na vipawa vyote. Ndani ya mwili wa Kristo, mguu huhitaji moyo, mkono huhitaji kichwa, jicho si bila makusudi, na kidole kinangojea agizo la ubongo. Kwa hiyo, mwili wa kanisa unaweza tu kufaulu vema, ikiwa kila kiungo husikiliza kwa vingine, na huku wakimhudumia Bwana kwa pamoja.

Jinsi ilivyo ya kijinga, ikiwa mkono wako unatenda kinyume cha mataka ya akili yako; au ukitembea kuelekea shimo, wakati unaiona kwa macho yako? Yeye asiyejifunza namna ya kushirikiana na viungo vyote vya mwili wake, basi atadumu kuwa na hali ya uchoyo, maskini, mdogo na mpumbavu.

Paulo anavitaja vipawa vya kiroho kwa kanisa fulani. Huyo, atakaye kuwaamsha wale wanaolala, haimpasi kusema tu kwa kuchangamka kibinadamu, akiacha Biblia Takatifu pembeni, bali inampasa kudumu ndani ya mipaka ya neno la Mungu, na hivyo kuvuta watu mmoja mmoja kwake Yesu kwa makusudi ya wazi.

Ikiwa yeyote aliye na kipawa, muda, pia na uwezo kifedha, basi inampasa kuwahudumia wahitaji ndani ya kanisa. Si lazima aseme sana, bali atende kazi kwa bidii na upole na ikiwezekana sirini kabisa na bila kutazamia wengine kumsaidia au kumshukuru, bali kuwahudumia wahitaji kwa hekima ya Kristo. - Mwalimu wa kiroho naye inampasa kupanga mawazo yanayotolewa na Roho wa Mungu na Injili, ndipo ayafundishe hatua kwa hatua kwa wasikilizaji wake, na awasaidie hatua za kuelewa vema, hatimaye waweze kushika kabisa neno la Mungu. Si lazima kufundisha masomo ya aina nyingi, bali kufundisha hatua kwa hatua; wala si kusema kama miporomoko ya maji na mwishoni kuwaacha wasikilizaji wake bila kuelewa makuu ya somo, bali aseme kwa taratibu na upole, na mwisho wa kila somo kujumlisha tena mawazo makuu kwa maneno rahisi na ya wazi.

Ikiwa mwingine anayo kipawa cha kuwatunza kiroho na kuwaongoza wengine, lazima ajifunze kwanza kuwa kimya, asikilize shida za wale wengine kwa makini, ili atambue vema mahali pao pa kiroho. Ndipo asianze kusema kutokana na mawazo yake mwenyewe, bali inampasa aombe kwanza, ili Bwana ampatie maneno yale ya kufaa kwa wakati wake. Ni muhimu sana kwake kuwatembelea wale wanaoguswa na wokovu wa Kristo, aombe nao, na kuwategemea hadi wapate kuwa marafiki ndani ya Kristo.

Paulo alisema pia kwamba, yeye anayetoa (kwa ajili ya maskini au kwa kazi ya kanisa), lazima atoe kwa busara na ukimya, bila hata kumweleza yule mhitaji habari zake na ya msaada wake. Yesu alisema: „Usiruhusu mkono wako wa kushoto ufahamu yale ambayo mkono wa kulia unayofanya“. Kwa hiyo, usitende jambo kwa ajili ya heshima yako mwenyewe, bali yote yatendeke kwa ajili ya heshima ya Yesu tu.

Ikiwa fulani anapokea wajibu wa uongozi ndani ya kanisa fulani, au ndani ya mojawapo ya kamati zake, inampasa asidhurike na upinzani, mateto, au kwa kukawia kwa wengine, bali awaonyeshe kwamba, huduma kwa ajili ya Yesu inabidi kuifanya kwa bidii zote na nguvu, pia na uvumilivu. Lolote ambalo halikuendeshwa na upendo, basi halifai.

Kama jumlisho la vipawa hivi na huduma hizo, Yesu alisema: „Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.“ Luka 6:36)

Paulo anataka kutukaribisha kwa aina hiyo ya wazo tukufu, akisema: „Lolote utendalo, ulitende kwa moyo, kama kwa ajili ya Bwana, wala si kwa ajili ya watu“. Upendo ndiyo alama kuu na shabaha ya Ukristo.

SALA: Ee mpendwa Bwana Yesu, sisi ni watu tunaoanza tu katika tabia ya upendo, huku tukitazamia huruma toka kwa wengine. Twaomba ubadilishe nia zetu, ili tuweze kuhudumia kwa kipawa kile tulichopewa; pamoja na upendo, uvumilivu, uangalifu, imani, bidii, na uhakika, si kufuatana na mawazo yetu, lakini tutende mapenzi yako kwa utendaji kamili. Utulinde na kiburi, ili tusije tukaanguka ndani ya majaribu ya shetani.

SWALI:

  1. Ipi katika huduma zilizotajwa hapo juu unafikiria ndiyo inayohitajika zaidi siku hizi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 17, 2022, at 11:42 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)