Previous Lesson -- Next Lesson
c) Tunahesabiwa haki kwa neema, wala si kwa sheria (Warumi 4:13-18)
WARUMI 4:13-18
"13 Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria, bali kwa haki aliyohesabiwa kwa imani. 14 Maana ikiwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. 15 Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira (ya Mungu); maana pasipokuwa sheria, hapan iwe imara kwa wazao wote; 16 si kwa wale wa tohara tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu, aliye baba yetu sisi sote; 17 kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi; mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahusisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako. 18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivynenwa, Ndivyo utakavykuwa uzao wako.“
Alipokuwa amemaliza kunenea tumaini lile la uongo wa Wayahudi kuhusu tohara, Paulo alivunja na tegemeo la pili la hali ya haki mawazoni mwao, ambayo yalikuwa tegemeo lao juu ya sheria.
Hao watu wa jangwani (waliotoka Misri na kutanga miaka 40 jangwani) walifikiri kwamba, Mungu ameketi kwenye vibao vya mawe yaliyoandikwa maneno ya agano, na kutoka hapo anajifunua mwenyewe na kutawala juu ya ulimwengu. Walitegemea kwamba Mungu ataendelea kukaa nao wanapoendelea kutii sheria zake zenye amri nyingi. Pamoja na hayo hawakutambua dhambi zao mbaya mno, wala hawakusikia upendo kuu wa Mungu kwa watu wote. Wakapata kuwa watumwa wa sheria. Mioyo yao ilibadilika kuwa kama mawe, nao walijivuna kama vipofu. Hawakuona hasira ya Mungu juu yao, wala hawakumtambua Kristo, ambaye baadaye aliishi kati yao.
Ole kwa kanisa, au ushirikiano mwingine, inayokuwa yenye bidii kushika mapokeo, kujizuia inayokataliwa na ya kuhukumu watu; heri wangeshika imani rahisi ndani ya Kristo aliye hai! Yule aliye mdhaifu kiimani bado ni bora kuliko mshika sheria asiye na upendo. Kweli, ni siri kuu kwamba, sheria hutokeza hasira, inachochea hatua za kutenda makosa, na pia huleta malipo ya kuadhibu. Hii ndiyo sababu kwa walimu wenye busara kuweka maneno machache tu au masharti nyumbani kwao au mashuleni, maana Kristo alituamuru tuwe na upendo, tumaini, uvumilivu na msamaha, wala si kufunganishwa na sheria au masharti, kuyafuatilia kwa kikamilifu, na pia kwa matisho ya adhabu kali.
Paulo aliwathibitishia watu wa sheria, tena na tena kwamba, Ibrahimu alijaliwa haki kwa njia ya imani, muda mrefu kabla Musa hajaja na sheria au amri 10. Hivyo, Ibrahimu alimtegemea Mungu, kabla sheria haijatolewa. Amri Kumi zilifuata nyuma, ili kuwaongoza waumini, na kwa kuvunja kiburi chao. Imani ndani ya rehema ya Mungu ndiyo nguvu ya kweli, inayoweza kujenga maisha ya kiroho, kuwatia moyo waumini wamtumikie Mungu, pia na kumsukuma atende mema; iwapo upande wa pili sheria inasonga sana, inapatiliza, inahukumu na mwishowe kutuhukumu kufa.
Ndipa Ibrahimu hakuangalia namna ya mwenendo wake au jinsi alivyofuata sheria, bali kipekee alitazama habari ya ahadi za Mungu na kumtegemea Bwana wake. Akapata kuwa mfano na baba wa kiroho kwa waumini wote. Alipoamini ahadi kwamba, ndani yake mataifa yote yatabarikiwa, ingawa wakati ule alikuwa hajawa na mtoto, Ibrahimu aliahidiwa mataifa na watu wengi kiimani, hata Paulo baadaye alimwita „Mrithi wa ulimwengu“.
Kwa taratibu ya namna hii Roho Mtakatifu alianzisha ndani ya Ibrahimu, huyu Bedui, mpango wa baraka, ambamo ndani yake Kristo mwenyewe aliishi, akiwavuta kwake wale wote waliohesabiwa haki kwa imani.
Ibrahimu bila shaka aliwazidi watu wote wa maana wa Agano la Kale kwa sababu ya imani yake kubwa. Mungu aliahidi kwamba, ndani ya uzao wake atabariki watu wote wa ulimwengu tena akimaanisha kwa uzao wake Kristo mwenyewe. Neno la Kiebrania „uzao“ au „mbegu“ linatumika kwa kumwekea alama mtu fulani, na mtume anadokeza kwamba, kulikuwa na mtajo wa pekee kwake Kristo ndani ya ahadi aliyopewa Ibrahimu. Hivyo, wale waliojaliwa haki kwa njia ya Msulibiwa watarithi mbingu pamoja na hazina zake zote, kwa sababu tumaini lao ndani ya Kristo limewaunganisha na uhai, nguvu na baraka za Mungu.
Ndugu we, njoo kwake Mwokozi, ili na wewe uinuke kutoka kwa hali yako ya kifo. Ukidumu ndani ya neno lake, Roho Mtakatifu ataumba maisha mapya ndani yako na kwenye mazingira yako. Ambapo kuna imani ndani ya ahadi za Mungu katika kanisa au ushirikiano wako, imani hiyo itashinda kifo kilicho ndani ya dhambi, na itaanzisha mambo mapya, ambayo hayakuonekana kabla ya hapo, kwa sababu Mungu huumba na kufanya kazi kwa njia ya imani yako, naye husikia mlio wa tegemeo lako. Kibali chako cha neno lake litakubadili wewe, pia na ulimwengu unamoishi.
SALA: Ee Baba wa mbinguni, mawazo yetu ni mwembamba, ya kisheria, na yanaelekea kuhukumu au kupatiliza wengine. Tufanyie nafasi kwa ajili ya kukuamini kikamilifu kwa tumaini na imani imara mioyoni mwetu, na umruhusu Roho wako Mtakatifu atuamuru kwa upendo, ushujaa na mwamko, ili wale waliokufa katika hali ya dhambi wapate kuinuka, na sifa zako zipate kuwa tele katika taifa letu. Umba imani yako ndani yetu, ili uweze kutenda kazi yako ya kuokoa kwa kututumia na sisi.
SWALI:
- Kwa nini tunapokea baraka za Mungu kwa njia ya imani yetu ndani ya ahadi za Mungu, wala si kwa bidii yetu ya kushika sheria?