Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 055 (Jesus the light of the world)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
1. Maneno ya Yesu kwenye sikukuu ya Vibanda (Yohana 7:1 – 8:59)

d) Yesu, nuru ya ulimwengu (Yohana 8:12-29)


YOHANA 8:12
„Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.“

Yesu ndiye nuru tukufu. Yeyote atakayemkaribia, atamulikiwa, atahukumiwa, atatiwa na nuru na atapona, na hivyo kuwa nuru na yeye kwa ajili ya Kristo. Hakuna nuru nyingine iwezayo kutumulika kweli na kuponya mioyo yetu miovu, ila ni Yesu tu. Filosofia zote na aina za dini zikipimwa zitaonekana kuwa ni dhaifu, maana zinaahidi kuokoa kimawazo tu na paradiso isiyopo..Kwa kweli ziliwapeleka watu kwenye upofu zaidi na kuwafungia mle. Nuru yake ni kama jua linalowaka na kuhuisha roho. Kupona kwa roho hivyo inayo sharti moja, ndiyo kumwelekea Yesu kwa imani na kumfuata kwa kujikinahi. Na kwa hali hiyo ya kumfuata Yesu siku hadi siku, tunabadilishwa toka gizani kuingia nuruni. Tutaona njia katika nuru yake, ili tufikie salama tuendako, ambako ni utukufu wa Baba na Mwana katika mwangaza wa uhai.

YOHANA 8:13-16
„Basi Mafarisayo wakamwambia, Wewe unajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako si kweli. Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndiyo kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako. Ninyi mwahukumu kwa kufuata mambo ya mwili; mimi simhukumu mtu. Nami nijapohukumu, hukumu yangu ni kweli; kwa kuwa mimi si peke yangu, bali ni mimi na yeye aliyenipeleka.“

Wayahudi walikuwa wamechukizwa na maneno ya Yesu, „Mimi ndimi“, walifikiri kwamba yeye ni wa kujivuna na mwenye kiburi, akijifanya kuwa nuru ya ulimwengu. Walieleza ushuhuda wake kuwa ni kosa na uongo, maneno ya kutia chumvi na kudanganya roho za watu.

Basi Yesu akaitika, „Ushuhuda wangu juu yangu ni kweli, kwa sababu sijipimi mwenyewe, bali kwa ukweli wa Mungu, ambaye nimeungana naye daima. Ninyi hamtambui kwamba nimetoka kwa Baba, na kwake nitarudi. Wala sisemi juu yangu mwenyewe, bali maneno yangu yanapatana na ukweli wa Mungu. Maneno yangu ndiyo kweli, yakijaa enzi na baraka.“

Maneno yenu ni ya juujuu tu, maana mwanadamu huona maganda tu.Mnajihesabu kama mahakimu na kuamini yote mnayoyaweza ili kupita hukumu kwa haki. Lakini mnakosea, hamfahamu kabisa asili ya mambo, wala nguvu zake au matokeo yake. Thibitisho la hayo ni kwamba ninyi hamjanijua mimi. Mnanihukumu tu kwa kuona ubinadamu wangu, ila naendelea kudumu ndani ya Mungu wakati wowote. Kama mgetambua hayo, mgefahamu msingi wa kweli wa ulimwengu.

Kristo ndiye mhukumu wa ulimwengu, na ukweli mwilini wakati uo huo. Hakuja kuhukumu au kutuharibu, bali kutuokoa. Hamkatai fukara yeyote, wala mvunja sheria au aliyetupwa, bali alitamani kuwaokoa na kuwavuta ndani ya upendo wake. Usimdharau mtu yeyote, lakini ukatambue ndani yake mfano ambayo Yesu anapenda kuihuisha au kuiumba ndani yake.

YOHANA 8:17-18
„Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. Mimi ndimi ninayejishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenipeleka ananishuhudia“.

Kwa sababu ya udhaifu wetu Yesu alijishusha hadi kwenye usawa wa sheria. Lakini aliieleza kama sheria yako, ambayo ndiyo taratibu yenu mnayoihitaji kama watenda dhambi. Kufuatana na sheria hiyo, mtu akihitaji kuthibitisha ukweli, alitakiwa kuleta mashahidi wawili watakaosimamia madai yake kinaganaga. Ndipo maamuzi yangeweza kupitishwa kwa msingi kama huo (Kumb. 17:6 na 19:15). Yesu hakulalamika juu ya mahitaji hayo. Alitumia ushuhuda wake kuwa ni ushahidi wa kwanza, na Baba yake ndiye wa pili anayethibitisha ushuhuda wake, anayethibitisha pia na ushirikiano kamili kati yao. Bila ushirikiano huo Mwana hawezi kufanya kitu. Hii ndiyo siri iliyomo ndani ya Utatu Utakatifu. Mungu anamthibitisha Yesu, naye Yesu anamshuhudia Mungu.

YOHANA 8:19-20
„Basi wakamwambia, Yuko wapi Baba yako? Yesu akajibu, Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui; kama mgalinijua mimi, mngalimjua na Baba yangu. Maneno haya aliyasema alipokuwa akifundisha hekaluni, katika chumba cha hazina; wala hakuna mtu aliyemkamata, kwa sababu saa yake ilikuwa haijaja bado.“

Wayahudi walikuwa hawakumwelewa Yesu, wala hawakutamani kumwelewa, bali walitamani kumtega katika unafiki waliofikiri ni wazi; hivyo wakauliza, „Ni nani unayemwita Baba?“ Yusufu (babaye kimwili) alikuwa amefariki tangu siku nyingi, nao walijua ni neno gani ambalo Yesu aliliwaza kwa kusema „Baba yangu“. Lakini walitazamia kupata thibitisho la moja kwa moja kwamba Mungu ndiye Baba yake.

Yesu hakuwajibu waziwazi, kwa sababu kumfahamu Mungu hakuachani na kumfahamu Yesu. Mwana kwamba yu ndani ya Baba, na Baba ndani yake. Yeye amkataaye Mwana, mtu huyu atawezaje kumfahamu Mungu kweli? Lakini yeyote amwaminiye Mwana na kumpenda, kwake Mungu atajifunua mwenyewe; maana amwonaye Mwana anamwona na Baba.

Maneno hayo yalisemwa kwenye pembe la hekalu, ambapo hapo walikusanya matoleo. Bila shaka kulikuwa na walinzi kote hekaluni. Ila mbali na hao askari, hakuna aliyethubutu kumshika Yesu ili kumfunga. Mkono wa Mungu ulikuwa ni usalama wake. Saa ya kusalitiwa iliyothibitishwa na Mungu mwenyewe ilikuwa haijatimia. - Ni Baba yako wa mbinguni tu awezaye kuamua juu ya maisha yako uendako.

SALA: Ee Kristo, tunakutukuza na kukupenda. Wewe hukuja kutuhukumu jinsi tunavyostahili, bali unatuokoa. Wewe ndiwe nuru ya ulimwengu, ukiwamulikia wale wanaokujia. Utubadilishe kwa miali ya upendo wako na ulainishe ugumu wetu, ili tukufahamu bora zaidi.“

SWALI:

  1. Je, ushuhuda wa Yesu juu yake kwamba yeye ni nuru ya ulimwengu, inahusiana namna gani na ufahamu wetu juu ya Baba wa mbinguni?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:12 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)