Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 030 (Jesus leads his disciples to see the ready harvest)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
C - Kristo kutembelea mara ya kwanza mji wa Yerusalemu (Yohana 2:13 - 4:54) -- Neno Kuu: Kuabudu kwa kweli ni nini?
4. Yesu atembelea Samaria (Yohana 4:1–42)

b) Yesu awaongoza wanafunzi wake waone mavuno yaliyo tayari (Yohana 4:27-38)


Yohana 4:27-30
27 „Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? 28 Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu: 29 Njooni mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je, haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? 30 Basi wakatoka mjini wakamwendea.“

Wakati majadiliano hayo kuendelea, wanafunzi wake walirudi toka mjini na chakula walichonunua. Walishangaa kumwona Yesu peke yake na mwanamke mwenye maisha ya dhambi; naye pia ni Msamaria aliyetupwa. Lakini hakuna aliyethubutu kusema, maana walitambua kuwepo kwa Roho. Walitambua mwujiza tukufu aliyofanya Kristo, maana uso wa yule mwanamke ulikuwa umebadilika kwa kumtazama Kristo na kusikiliza maneno yake. Furaha ya kumtambua Mwakozi ulipata kumtawala.

Mwanamke akaacha chombo chake tupu. Alikuwa hajampatia Yesu kikombe cha maji alichoomba, ila yeye alikuwa ameridhisha kiu chake cha kusamehewa. Akawa amekuwa chemchemi ya maji yaliyo hai kwa ajili ya wengine. Akakimbilia mjini na kuwaambia watu akiwaelekeza kwa Kristo. Mdomo wake uliokuwa kwanza umejaa maneno machafu, sasa ukawa ni chemchemi cha maji safi, ukimshuhudia Kristo. Akawavuta watu kwa Mwokozi, akishuhudia jinsi yeye alivyofunua dhambi zake. Watu wa mjini walihisi kutokana na ushuhuda wake kwamba, jambo lisilo la kawaida limemtukia, ambalo pengine ni kazi ya Mungu ndani ya huyu mwanamke. Walitamani kutazama pia siri yake. Nao wakakimbilia kisimani, ambapo Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakipumzika.

Jambo hilo ni mfano safi wa mambo, ambayo Kristo hufanya ndani ya watu wanaokubali kumfuata. Sisi nasi tuwe tunawajulisha marafiki na majirani kwamba, Kristo alitujia ili kutuokoa. Ndipo hamu ya kupata maji yaliyo hai huinka ndani yao, inayoletwa na nguvu ya Roho Mtakatifu. Je, umewahi kuwa chemchemi ya uhai wa kweli kwa ajili ya wengine?, Kama bado, ukiri upungufu wako kwake Kristo, elekeza maisha yako kwake, ili akusafishe na kukutakasa, ili nawe upate kuwa baraka kwa ajili ya wengi – jinsi ilivyotukia kwa yule mwanamke mzinzi alipoanza kueneza habari njema kwao walioishi naye.

SALA: Bwana Yesu, nakushukuru kwa kunitafuta na kunitambua. Mimi si bora kuliko yule mwanamke mzinzi kule Samaria. Nisamehe dhambi zangu. Nijalie zawadi ya Mungu inayotosheleza kiu yangu ya ukweli na usafi maishani mwangu. Nifungulie macho yangu, ili nimwone Baba wa mbinguni. Nijalie moyo wangu upokee Roho Mtakatifu, ili nipate kuwa mtu wa kufaa, na maisha yangu yawe yakionyesha kukuabudu wewe kwa kujibu neema yako maishani mwangu. Uwaokoe wengi na kuwavuta kwako. Maana wewe huwakatai wanaokujia kwa kweli.

SWALI:

  1. Jinsi gani tunaweza kumiminiwa na maji yaliyo hai?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)