Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 07 -- Fifth Commandment: Honor Your Father and Your Mother
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

07 - Amri Ya Tano: Waheshimu Baba Yako Na Mama Yako



KUTOKA 20:12
“Waheshimu Baba yako na Mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana,Mungu wako”


07.1 - Zawadi ya Mungu: Familia

Familia ndiyo lulu ndani ya zawadi ya ukarimu na moja ya salio ya paradise. Mungu alimwumba mwanadamu, mwanaume na mwanamke, ili kurudisha utukufu na upendo wake, na hivyo pia kuzaa na kujaza nchi. Hivyo familia ndiyo chanzo cha uhai wa kibinadamu, tena ni msingi wa utamaduni wote. Inaleta usalama, ulinzi na umoja, na mara nyingi inathibitisha kwamba ina nguvu kuliko mawazo na mipango mapya za maisha.

Kwa jumla dini zote zinakubaliana kwamba, inapasa kuwaheshimu wazazi. Ni ya asili kwa watoto kuwapenda na kuwajali wazazi wao. Wakati Wakomunisti, pamoja na taratibu zao za bila Mungu, walipotia swali juu ya hali ya wazazi, wazo lao lilimpinga Mwumbaji na uumbaji wako, pia na taratibu za asili na za tabia za silika za kibinadamu. Mungu hulinda familia kwa amri ya tano. Inafaa kabisa kumshukuru Mungu kwa ajili ya desturi maalum ya familia, kuwepo kwake na vifungo vyake vya siri katika upendo na ushirikiano.

Ndani ya Amri ya Tano, Mungu anatuagiza kumheshimu si baba tu, kwa kuwa kichwa cha familia na mtunzaji wake, lakini vilevile mama na wanawake kwa jumla.Sawa na mwanaume, mama naye ameitwa kurudisha sura ya Mungu katika maisha yake na kushiriki wajibu katika familia kwa usawa na mume wake. Si ajabu, zote Agano la Kale na Jipya zinapatana katika jambo la kuwaheshimu wakina mama sawa na wakina baba.

Hiyo amri ya kutunza na kuhifadhi familia ni wazi na ya kiasili. Hata katika ulimwengu wa wanyama wadogo wanawafuata mama zao, na kwa ndege mara nyingi wa kike na wa kiume wanatotoa mayai kwa zamu. Wote wawili huwalisha vifaranga wao hadi wanapofaulu kujilisha wenyewe. Kuna vifungu vya asili na husiano zilizopangwa na Mwumbaji, ambazo hakuna awezaye kutukuzijali bila kuadhibiwa. Hata hivyo siku hizi tunasikia sauti za kuasi zinazojaribu na kuzifanya migumu mioyo ya watoto, “Usisikilize wazazi wako wala kuwatii. Bora, tafakari wewe mwenyewe, timiza ya kwako na kuendeleza uasi na utundu kuanzia utoto.” Macho ya watoto kama hao yanaangalia kwa huzuni na kutokutii, na furaha ndani yao imezimishwa. Sehemu malumu ya mioyo yao imeharibiwa kiasi cha kuhuzunisha.


07.2 - Dhabihu ya Wazazi

Wakina baba na mama wanao mapendeleo ya kushiriki katika kizazi kipya. Kila uumbaji wa mtoto ni mwujiza wa ajabu ndani yake! Yawezekana mtoto alitungwa bila kusudi ya wazazi wake. Hata hivyo baba na mama bado walishiriki katika tendo tukufu la uumbaji. Na Bwana aliwaheshimu kwa kuwaruhusu kuzaa na kupitisha urithi wa vizazi vya nyuma kwa mtoto wao ndani ya mama. Kwa sababu hiyo inampasa mwanadamu kuinama mbele ya Mwumbaji, wamwabudu na kumshukuru kwa kila mtoto anayezaliwa.

Mama zetu walitubeba kwa miezi tisa, sawa na usiku na mchana mara 275 ndani ya tumbo lao. Tulikuwa salama na kulishwa mle. Tulishiriki furaha na huzuni zake, masumbufu na uchovu wao. Pengine mama zetu walituombea hata kabla ya kuzaliwa. Kazi ya kutuzaa lazima iliwapatia hofu na maumivu mengi.

Kawaida baba na mama hutusindikiza kwa miaka na miaka. Wanaangalia miguu, mikono na miili yetu zikue na kuitikia kucheka kwetu na maumivu yetu. Pengine wanamshukuru Mwumbaji pia kwa ajili ya kuwepo kwetu na kukua kwetu. Kama wazazi wetu walikulia chini ya mamlaka ya Yesu, kwa vyovyote walitukabidhi ndani ya mikono ya Baba yetu wa mbinguni, wakatufundisha amri zake na kututia moyo kumwamini Mwumbaji na Mchungaji Mwema. Hivyo, walitukuza, kutupenda na kutubariki zaidi ya sisi wenyewe kutambua. Walituchunga mchana na usiku. Walihangaika kutupatia chakula na mavazi. Walijishughulisha kwa ajili ya elimu yetu na uhusiano na marafiki. Tulipokuwa wagonjwa na wenye homa, wao kwa kufahamu vyema walituangalia ndani ya vitanda vyetu. Walifurahi nasi na kulia machozi nasi pia katika masumbufu yetu.


07.3 - Matatizo ya Familia

Kati ya wazazi na watoto kuna fungo la karibu sana kwamba hali ya kupeana upendo na tumaini ni ya wazi. Pamoja na hayo hatuishi tena kwenye paradiso. Hakuna mtoto aliye mwema ndani yake na wazazi nao wako na makosa mbele za Mungu pia. Kwa sababu hiyo watu wazima na vijana wanaisho kwa neema ya Mungu tu na kwa njia ya kusameheana wao kwa wao kila wakati. Hakuna amani ya kudumu ndani ya familia bila msamaha na uvumilivu. Kurudisha amani ndani ya familia haiwezekani bila kukiri na kukubali makosa na kuomba msamaha kwa unyenyekevu. Wabarikiwa ni watoto wanaosimamiwa katika upendo na masamaha kwa wazazi wao.

Sio chaguo la wazazi wenyewe tu kuongoza watoto wao katika imani iliyo sawa, kwa vile Mwana wa Mungu mwenyewe anaagiza watoto wote waletwe kwake ili wabarikiwe. Inawapasa wazazi kuonyesha wazi kiini cha Yesu na uaminifu wake kwa watoto wao, wawaongoze kushika amri zake na kuingiza ahadi zake ndani ya mioyo yao. Wababa na wamama wanawajibika kwa usawa kwa ajili ya elimu ya kiroho ya watoto wao, lakini waelewe pia kwamba, hawawezi kurithisha kwa watoto wao imani yao wenyewe, na zaidi ya hapo hawawezi kuwalazimisha kuipokea. Kila mtoto inampasa kuchagua kwa ajili yake mwenyewe kuwa mtu wa Mungu au kuwa kinyume chake. Hata hivyo ni vema kwa watoto kutambua baraka ya wazazi wao kwamba inaendelea hata kwa vizazi.

Wazazi hawatakiwi kuwaharibu watoto wao au kuwakuza na tabia ya uzembe. Pia wasiwatake kufanya kazi zilizo gumu mno kwa umri wao. Ni ya hekima kuruhusu muda wa kutosha kuendelea kuwa mtoto! Shule na mazoezi ya mara kwa mara ni muhimu, lakini sio muhimu zaidi katika kuwakuza watoto. Ni muhimu zaidi sana kuamsha ndani yao kumstahi Mungu na upendo kwa Mwumbaji wao, ili kujenga dhamiri zao, tabia bora, uaminifu, bidii na usafi. Ni ya muhimu sana kwa wazazi kutumia muda wakutosha pamoja na watoto wao na kusikiliza maswali yao na matatizo yao. Na zaidi ya yote ni muhimu kwamba wazazi wawaombee watoto wao bila kukoma wapate kuzaliwa mara ya pili, hatimaye kuendeleza maisha yao na Yesu.

Watoto watawakabili wazazi wao kwa kuwapima wakiwa katika umri wa kupevuka nay a ujana. Kukua kwao hivi ndani ya utu uzima na uhuru ni wazi kuwa hatua za kukomaa na zisionewe uchungu. Kama wazazi wamewakabidhi watoto wao mapema kwenye utunzaji wa Mungu wa Umoja, basi watafaulu kuwasindikiza na subira katika miaka hii ya uchaguzi, na bila kuwachunga kama kwenye kamba. Pamoja na hayo, vijana wanahitaji kufikia vitabu vya elimu mbalimbali, marafiki wa kufaa, chaguo la vipindi safi vya TV, pia na vikundi vya vijana wa kikristo wanaoendesha na masomo ya ki-biblia yenye uhai. Kuwalazimisha vijana njia za maisha ya zamani itapevusha uasi, pia itafanya mioyo yao kuwa migumu na kufunga mlango wa kufikia mioyo yao.

Kama wazazi twahitaji kukumbuka kila wakati onyo la Yesu: “Bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa katika kilindi cha bahari.” (Mathayo 18:6). “Kukosesha” haimaanishi urejeo wa kukataa au ya hasira, lakini ina maana ya kuwaongoza vibaya hata waseme uongo, kuiba au kuwaruhusu kushiriki katika dhambi fulani ya wazi bila kuwaonya kwa kutosha. Kuwakuza watoto kwa baraka kunatokana na hali ya kicho na upendo kwa Bwana.

Nyakati zetu sizizo na tabia ya asili tena, bali na maendeleo ya ki-sayansi, yawezekana wazazi waaminifu wataonekana kama “watu wa zamani” hata kwa watoto wao. Mara kwa mara katika nchi za maendeleo madogo bado yawezekana kwamba, mama au baba hawawezi kusoma au kuandika. Hali hii haimruhusu mtoto aliyeelimishwa awe na kiburi au kuwacheka. Kufanya hivyo ni kutokuwa na heshima, ni ujinga na upumbavu. Maana uwezo wa kusoma na kuandika haionyeshi kipimo cha akili ya mtu wala thamani yake kwa jumla. Upande wa pili, elimu ya juu haiboreshi wema au utakatifu wa mwanafunzi. Mamlaka ya wazazi haitokani na namba za vyeti na shahada walizopewa, wala si kiasi cha fedha walizoweza kukusanya. Mamlaka yao ina msingi katika kusudi la Mungu na jinsi wanavyowaombea watoto wao mbele za kiti cha neema ya Mungu. Ubaba wa Mungu imejenga polepole upendo wa Rehema mioyoni mwa wazazi. Dabihu ya Kristo huumba hali ya kutimiza huduma bila masharti na ya kujitoa kabisa ndani ya wazazi na watoto pia, wao kwa wao.


07.4 - Kutimiza Amri ya Tano

Jinsi gani watoto watafaulu kuwaheshimu wazazi wao ipasavyo? Dhamiri zetu inatukumbusha tuwapende na na kuwaheshimu, kwa sababu wao ndiyo wenye thamani kuliko yote tunayofahamu au tuliyo nayo hapo duniani. Hii inajumlisha tegemeo na utii kwao, tukijinyima wenyewe, na bila kuruhusu nia za ubovu. Kwa vyovyote mtoto asingempiga baba au mama, iwe kwa kusudi au kwa kukosea. Mtoto hatakiwi kuwa wa kutazamwa kwanza ndani ya familia, lakini ni Bwana Yesu pekee. Yesu alitufundisha habari ya ufunguo wa maisha ya kifamilia yenye furaha aliposema, “ Kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mathayo 20:28). Mwana wa Mungu anawaonya wazazi na watoto kuchunga kwa uangalifu taratibu ya aina hiyo katika maisha ya familia kila siku.

Je, wajibu wa watoto kwa wazazi wao inakwisha mara wanapoanzisha familia zao wenyewe? Hapana! Wazazi wanapoingia umri mkubwa na kuanza kudhoofika kimwili hata kiakili, wanahitaji ushirikiano wa huruma na utunzaji kutoka kwa watoto wao hasa na zaidi. Wana na binti wanaweza kujitolea sehemu ya muda wao kwa wazazi wao, jinsi wazazi walivyojitoa kama sadaka nyakati za siku za kwanza za utoto wao. Hakuna nyumba ya kutunza wazee au pa kuwawekeza inayoweza kulingana na watoto wanaojitoa hasa kwa sehemu ya nafasi na hela zao na bidii za kuwashughulikia wazazi wanaozeeka.

Haya, amri ya tano ndiyo ya kwanza inayotoa ahadi ya wazi kwetu, baada ya kutuangaliza kwenye ubaba wa Mungu aliyotujalia ndani ya agano lake nasi. Yeye anayewatunza wazazi wake kwa wema, anaahidiwa maisha marefu zaidi hapo duniani, kutupunguzi shida na kutubariki tele. Popote adhama ya wazazi inapotunzwa, na ambapowazazi na watoto wanaishi kufuatana na mapenzi ya Mungu, watatambua kutimizwa kwa ahadi hiyo kwa pamoja.

Mungu atukatalia kudharau wazazi na watu wenye mamlaka. Hii inajumlisha dhuluma, kupinda haki, unafiki na udanganyifu. Je, Yesu hakusema, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mathayo 25:40). Unakumbuka habari ya huzuni ya uasi wa Absalomu dhidi ya babaye Daudi? Inaishia na kifo cha mwasi (I.Samweli 15:1-12 na 18:1-18).

Twasoma kwenye kitabu cha Kutoka 21:15-17, “Ampigaye baba yake au mamayake, sharti atauawa. ….. Na yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.” Kitabu cha Mithali 20:20 inasema, “Amlaaniye babaye au mamaye, taa yake itazimika katika giza kuu.“ Kumbukumbu la Torati 21:18-21 inasema, “Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetiisauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi, ….. ndipo waume wote wa mji wake na wamtupie mawe afe.” Yeyote aliyepinga au kufanya fujo dhidi ya wazazi wake, bila kuungama, basi akahesabiwa kuleta hatari kwa watu wote. Usalama wa jamaa ulitegemea upendo wa watoto na utii wao katika siku zile, lakini hata siku hizi!

Kwa uwazi Mungu husema si kwa watoto tu lakini anawaonya na wazazi. Watoto hawatakiwi kuchezewa na watu wazima, kwa vile kila mtoto wamekabidhiwa na Mungu. Hapo ahadi ya Yesu imetimizwa kwa njia nyingine, “Kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi” (Mathayo 25:40). Mtume Paulo naye anaonya dhidi ya kuwakasirisha watoto au kuwalemaza (Waefeso 6:4 Wakolosai 3:21) Wazazi hawatakiwi kuwa wapole mno wala bila kujali. Wasiwe wakali kupita kiasi wala na upuzi. Haifai kusahau kwamba watoto huonyesha ubora wao waliorithi. Hata hivyo, dhambi walizorithiwa na udhaifu hazituruhusu kulalamika kwa ajili ya makosa yao, bali ingewapasa kuwaongoza wazazi wawe wanyenyekevu. Kwa vyovyote unyenyekevu utazaa roho ya upole unaoweza kuwaongoza watoto wao kuwa na adabu ya kufaa. Kwa sababu hizo, wazazi na watoto wanatakiwa kuomba kwake Yesu awajalie maungamo ya kila wakati na nia zao kufanywa upya.


07.5 - Waongofu toka Uislamu na Wazazi wao

Kwa watoto kuna shauri moja tu ambalo linawaruhusu kutokutii wazazi wao: Ikiwa wanawataka kutenda kinyume cha mapenzi ya Mungu. Biblia lasema wazi, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Matendo ya Mitume 5:29). Siku hizi kwa wote, Waislamu pia na Wayahudi, kuna hesabu ya vijana inayoongezeka, ambao hawafuati tena imani ya babazao, kwa sababu wamekutana na Yesu na kumpokea kuwa Mwokozi wao wa binafsi. Hali hii inatokeza mvutano wa kuuma, kwa sababu wameona maishani mwao mbadiliko mkubwa kabisa kiroho na kiadabu, maana upendo wa Munguumemwagwa mioyoni mwao kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hii inawasaidia kuwapenda wazazi wao zaidi kuliko kabla ya mabadiliko hayo. Wanahitaji hekima nyingi, ili waweze kukazana katika kutenda mema kuliko kisema mengi juu ya imani yao mpya. Subira ndiyo moja ya maadili, nao wataoto wanatakiwa kuomba kwa makini kwa ajili ya wazazi wao wasio wakristo bado, ili kwa neema nao wapate kubadilika . Pia wangetakiwa kuwatembelea mara nyingi iwezekanavyo, maana hapo duniani hakuna atupendao kuliko wazazi wetu.

Lakini basi, ikiwa wazazi wanakataa pasipo huruma sauti ya roho wa Yesu na kuwalazimisha watoto wao kumkana tena Mwokozi wao na kuwatisha wauawe kufuatana na mafundisho ya Sharia ya kiislamu, hapo ni wakati wa kuachana. Roho hiyo ya kinyume cha Ukristo ya wazazi kama hao lazima ni kuhukumiwa na ikatazwe. Ila wazazi wenyewe waendelee kuheshimiwa na kupendwa bila kukoma. Hata hivyo, Yesu atuongoza hivi: „Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili“ (Mathayo 10:37). Wazazi wasipofanya kwa haki au kuwatendea jeuri watoto wao kwa sababu za kidini, ndipo vifungo vya kifamilia, zuio la utamaduni au sababu ya kutegemea wazazi kifedha, zinaweza kutumika kushawishi uamuzi wa mwisho wa watoto . Ndiyo sababu ya Yesu kutuagiza kuachana kabisa na jamaa wote walio kinyume cha Injili yake, wasije wakatuvuta tena kwenda mbali na imani. Kwa watu kadha inawapasa kuachana kabisa na wazazi kwa muda kwa ajili ya kuimarika kabisa katika kujitoa kwake Yesu. Inapotokea hivyo, inawaumiza wazazi sawa na watoto pia sana, lakini upendo wa Mungu ni kubwa kuliko kujisikia wenyewe kwa ajili ya wapendwa kuliko wengine wote ulimwenguni.

Waumini wa kanisa wanaitwa kujitoa kabisa kwa kuwasaidia waongofu mapema na kujitolea kwao kama ndugu na dada, baba au mama. Yawezekana hali hii itahitaji kupata hata mafunzo fulani au pengine masomo ya chuo kikuu baadaye, au labda hata kukubali kufunga ndoa na mtu wa namna hii. Jinsi ilivyo vigumu kwa upendo wa wazazi kukoma. Hata upendo wa kanisa kwa ajili ya huyu mshiriki mpya iwe kubwa na bila kukoma, hata ikitokea kwamba huyu mtu hatembei inavyotazamiwa. Upendo na uvumilivu za Kristo ndizo alama za waumini waliokubali kumpokea na kumlea mwongofu mpya.


07.6 - Jumlisho

Upendo ndani ya familia inapasa kuonyesha upendo wa Mungu. Huyu Mungu wa milele ndiye Baba yetu, naye atuita kujiunga na familia yake kwa daima, kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye anatutakasa na damu ya Mwana wake, ili atutunze ndani ya ushirikiano na Yeye na kutuhuisha kwa nguvu za Roho wake Mtakatifu. Kama tutapoteza wazazi wetu katika ajali ya gari au njia zingine zifananazo, hatutakiwi kukata tamaa, lakini tukiri pamoja na Mfalme Daudi, “Baba yangu na mama yangu wameniacha, bali Bwana atanikaribisha kwake” (Zaburi 27:10). Upendo wote wa kibinadamu una mipaka yake, lakini Mungu wetu atukaribisha na upendo wake usio na mfano na anatukumbatia kabisa. Habari ya mwana mpotevu, Luka 15, inatuonyesha kupokelewa kwa mpotevu alipotubu; na jinsi baba alivyojaribu kumshawish yule mwana wa pili mwenye kiburi naye awe na huruma na upendo kwa ajili yake aliyepatikana tena. Baba aliwapenda wote wawili na kujaribu kwa vyovyote kuwaunganisha pamoja. Ushirikiano na Mungu Baba inaendelea kuwa chemchemi ya Amani na utulivu ndani ya maisha yetu. - Mara kwa mara Mungu atupatia nafasi ya kuishi ndani ya ushirikiano wa watakatifu hapo duniani. Ikiwa ni hivyo, tungemshukuru mno Baba yetu wa mbinguni kwa ajili ya familia yetu ya hapo chini, ndipo pia kwa ajili ya kuwa washiriki wa familia yake ya mbinguni.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:57 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)