Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 06 -- Fourth Commandment: Remember the Sabbath Day, to Keep it Holy
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

06 - Amri Ya Nne: Ikumbuke Siku Ya Sabato Uitakase



KUTOKA 20:8-11
“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya mlango wako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa”


06.1 - Siku ya kupumzika ili kumtukuza Mwumbaji

Kwa Wayahudi, Sabato ni moja ya alama ya agano lao na Mungu. Imeamriwa kwa ajili ya ibada, na siku hiyo iliwatofautisha watu wa Agano la Kale na mataifa mengine. Hadi siku ya leo wait wa agano hilo la awali wanaitakasa hiyo siku ya mwisho wa wiki kwa kutokufanya zile kazi wanazozoifanya kwenye siku zingine. Hawawashi hata moto au kwenda kwenye safari ndefu. Badala yake , wanavaa nguo mpya zinazotunzwa kwa ajili ya sikukuu. Sabato inakusudiwa kwa ajili ya shangwe, wakati watu wanapokutanika kwenye ibada na suoma sehemu zilizopangwa kutoka kwa Torati na kuyaongelea pamoja katika mazingira ya shukrani.

Kwenye siku hiyo ya Bwana, waumini wangetakiwa kutumia muda zaidi pamoja na Mungu kuliko siku zingine. Wangemwelekea Yeye kwa mioyo na mawazo yao, maana Yeye ndiye Mwumbaji wao, Mwokozi na Mfariji wao. Tungezoea kusoma Biblia, kusikiliza hotuba safi, na kushiriki katika maombi pamoja na nyimbo za sifa. Hayo yataweza kutudumisha na kutufariji hata katika udhaifu kadha kwenye safari yetu ya jangwani kwenye siku zingine za wiki. – Basi, si mwanadamu wala kupumzika kwake ni shabaha ya siku hiyo, bali Bwana mwenyewe. Kwa njia hiyo Sabato imepata kuwa siku ya Bwana. Ameiweka siku hiyo kipekee, akaitakasa na kuibariki. Siku ya Bwana ndiyo zawadi ya thamani kuu ya Mungu kwa ajili ya Uumbaji wake.

Kuitakasa Sabato ina maana kwamba, tunamsifu Mwumbaji, aliyeziumba mbingu na nchi, nyota zote, nchi kavu na miti kwa neno lake la enzi. Aliwaumba samaki, ndege na wanyama wote wadogo na wakubwa. Uumbaji wake ukafikia upeo kwa kumwumba mwanadamu kwa mfano wa Mungu. Ndani ya uumbaji huo kila kiumbe ni mwujiza wa pekee, uliotengenezwa kwa hekima na nguvu katika namna ya kipekee. Wanasayansi wamefumbuavichache tu vya siri za mwili wa mwanadamu, za uwezo wake na fahari ya akiliyake. Loo, jinsi zilivyo za ajabu kazi za Mungu ! Na ikiwa uumbaji wake ni nzuri sana namna hii, je, kiasi gani uzuri wa Mwumbaji mwenyewe utakavyozidi yote hayo ! Lugha za binadamu haziwezi kueleza kwa ukamilifu ukuu wake, utukufu na uenyezi wake. Kweli, anastahili kuabudiwa na kutukuzwa na wote wa uumbaji wake.

Mungu alipokamilisha makusudi yake yote ya uumbaji, akastarehe. Si kwamba alichoka na kazi zake, maana Mwenyezi hawezi kuchoka, kusinzia au kulala, bali aliridhika sana na kazi zake, alifurahia katika miujiza mikuu isiohesabika alioiumba,naye akaiona kuwa safi sana. Basi ni wajibu wetu kumsifu Mungukwa ajili ya miujiza yake isiyotambulikana ndani ya uumbaji wake.


06.2 - Ulazima wa kupumzika siku ya Sabato

Wakati wa siku ya Sabato, tunapendelewa kushiriki katika utulivu wa Mungu kule mbinguni, iliyokuwa shabaha yake hata kwa ajili yetu. Huwa anatupatia nafasi kufurahia utulivu wa kina na ya ibada. Ukimya huo wa ndani na nje mbele za Bwana ndiyo ufunguo kwa ajili ya kujisikia na afya na rahaHakuna awezaye kushambulia agizo hilo bila kuadhibiwa. – Mataifa kama Urusi wa zamani au hata makampuni makubwa katika nchi za magharibi zilipoteza amani ya nia zilipojaribu kufuta siku ya Bwana. Wale wasiojali siku hiyo wakizunguka katika magari yao hawatambui utukufu wa Bwana ndani ya uumbaji wake. Wamepoteza uwezo wa kuzingatia maana ya maisha, na hivyo shughuli zao zote kwenye siku sita za kazi zinadhoofika. Mtu yeyote, hata wanyama, wanahitaji muda wa kupumzika, na uwezo wa uumbaji haiwezi kujaziwa tena nguvu yake bila kutulia kwanza mbele za Mungu. Basi tusingepuuza agizo la Mungu ya kutakasa siku ya Sabato. Twaweza kuona kwamba amri hii haisemi habari ya masaa 35 au 40 za kazi kati ya wiki, lakini inasema habari ya siku sita ya kufanya kazi kwa bidii. Lakini siku ya saba kikamilifi iwe kwa ajili ya Bwana. Biblia latufundisha kwambamaisha ya uvivu ni mwanzo wa ubaya wote, na kazi ya bidii ya kila siku ndiyo bora kwa kila mwanadamu.

Yesu anatutia moyo kutulia tena na tena, ili kuzingatia habari ya uzuri wa maua bustanini na mimea mingine na kushangaa jinsi ynavyomea. Umeesh kutambua ni muda gani inayohitajika hadi kuchanua maua, majani yakomae, na hata yabebe matunda? Simama basi na kufungua macho yako. Upate kujua nguvu na taratibu zinazotakiwa ndani ya mwenendo wa asili, ndipo basi ndani ya hayo utamtambua Mwumbaji mwenye hekima na wema wake wa ki-baba. Yesu alitushauri tulinganishe uzuri wa maua kwa rangi zake na mavazi ya watajiri (Mfalme Sulemani), ili tutambue kwamba hata wafalme na watawala hawawezi kuvaa kwa uzuri kama haya maua katika umbalimbali wa rangi na sura, ambayo yanafifia na kufa mapema. – Mwanadamu mwenyewe ndiye kiumbe kizuri kuliko vyote katika uumbaji wa Mungu, na uso wake huonyesha tu sehemu ndogo ya utukufu wake. Loo, tungbadili mwenendo wa maisha yetu, tungeacha kukimbia hapo na pale na kuchukua muda wa kutafakari! Tukifanya hivyo, tutaendeshwa na uzuri wa ajabu ya upeo wa uumbaji hata tukamshukuru Mungu na kumtukuza Yeye. Inasikitisha kwamba kuna taratibu za TV zinazoonyesha picha za aibu za uuchi na za ujeuri, wakati Mungu anapenda kufungua macho yetu kwa uzuri wa nyakati za kujipuka kwa mimea, wakati wa kuchanuka, pia wa mavuno na wa baridi na theluji, ili tutambue maajabu yote aliyoyaumba na kutunza hadi leo kwa ajili yetu sisi.

Bwana anapotuagiza kushika Sabato, anadai kwamba, siku hiyo iwekwe kipekee, ili tuitumie kwa kujifunza kuishi mbele zake. Kutakasa siku hiyo ya Bwana siyo jambo la kupumzika tu, kusikiliza au kusoma Neno la Mungu, lakini ni nafasi ya kumwelekea Yeye kwa moyo wetu wote, ili apate nafasi kutubadilisha na kutujaza na wema wake. Yeye ni mtakatifu, naye anatutaka tuwe watakatifu na sisi. Basi, tusonge mbele ndani ya nuru ya upendo wake na kurudisha hiyo nuru ya utukufu wake, maana hakuna kufanywa upya bila ukimya na utulivu


06.3 -- Kutokufahamu vizuri siku ya Sabato

Siku ya Sabato iliwalinda watu wa Agano la Kale wasiharibike na kuwatenganisha na miungu mingi mingine iliyoabudiwa na mataifa yaliyowazunguka. Hiyo kukaza nia zao kwenye siku ya Bwana iliwatayarisha pia kwa ajili ya kuja kwake Kristo, Mwokozi wa ulimwengu. Hata hivyo, Sabato peke yake ilishindwa kubadilisha, kulinda au kufanya upya hao waumini walioishika. Wanadamu wote hufunuliwa kuwa wadhaifu, waovu na bila kustahili mbele za Mungu. Wala sheria yoyote haiwezi kubadilisha ubinadamu huo, wala Sabato haiwezi kumweka huru mwanadamu na dhambi zake. Lakini inaweza kumlinda asiteleze ndani ya hali ya kutokuamini kabisa. Katika Agano Jipya sisi hatuishiki siku ya Bwana ili tupate neema ya Mungu, lakini zaidi tupate kumshukuru kwa sababu alituumba. Aliingia mwilini mwetu na kutujia ndani ya Kristo na kutushughulikia zaidi sana kuliko baba kwa ajili ya watotowake. Kwa sababu hiyo tunampenda na kumheshimu. Kushika amri haitatuokoa na dhambi zetu, lakuini neema ya Mungu ndiyo siri ya ukombozi wetu na kufanywa upya wetu. Yeyote atakaye kuhesabiwa haki kwa njia ya amri, atahukumiwa kwa amri. Lakini ukijinyosha na kuishika mkono wa Yesu aliyoinyoshea kwako, atakuongoza na kukulinda na kuhukumiwa kote.

Siku ya saba Mungu alistarehe na kuangalia kazi yake. Akaona kwamba yote yalikuwa nzuri sana. Hata hivyo, kustarehe kwake Mungu kwa utukufu kulikoma wakati binadamu hawakumtii na kuanguka katika dhambi. Mungu aliacha kupumzika na tangu hapo aliendelea kufanya kazi mchana na usiku ili ikiwezekana aiokoe uumbaji wake uliopotea. Akatamka, “Umenitumikisha kwa dhambi zako” (Isaya 43:24). Yesu naye akathibitisha hayo akisema, “Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi” (Yohana 5:17). Mungu ameguswa kwa ndani sana kwa ajili yetu na dhambi zetu chafu, lakini basi tuko tunamshukuru Mungu kwamba, kuna kuachiliwa kwa ajili ya watenda dhambi wote kwa ajili ya dhabihi ya badala yetu aliyoitoa Kristo. Yeyote aaminiye ndani ya Mwana Kondoo wa Mungu hatakuwa chini ya hukumu ya sheria, badala yake atahesabiwa haki kabisa kwa sababu ya damu ya Yesu. Bwana Yesu alikufa na kuzikwa hapo hapo siku kabla ya Sabato. Akapumzika siku ya pumziko la Mungu katika kaburi la mtajiri. Ndipo akafufuka siku ya kwanza ya wiki kutoka kwa wafu. Na kwa njia hiyo Mungu alitimiza hata mahitaji ya siku ya Sabato. Katika ufufuo wake aliwekesha siku mpya iliyo alama kwa ajili ya uumbaji mpya inayofanikiwa kwa neema ya Mungu na kutokana na nguvu ya Roho Mtakatifu, wala si kutokana na uamuzi wa sheria.


06.4 -- Wakristo wanao haki ya kutakasa Jumapili badala ya Sabato?

Mara nyingi Wayahudi na Wasabato wanawashitaki Wakristo kwamba, wanavunja amri ya nne na kutabiri kwamba ghadhabu ya Mungu itawaangukia wafuasi wa Kristo kwa sababu wanashika Jumapili badala ya Jumamosi (Sabato) kuwa siku ya kupumzika. Basi, Yesu alitamka kwamba Yeye ni Bwana wa Sabato. Yeye Mwana wa Adamu alitimiza matakwa yote ya Sabato kwa niaba yetu. Alizitimiza na kuzikamilisha. Yesu hakupitisha sheria mpya ili aitakase siku nyingine au mwezi au mwaka. Aliwaokoa wafuasi wake na kuwatakasa wao. Watu wasingemwabudu Mungu siku ya Sabato tu na wakati wa sikukuu fulani, bali kila siku. Ndiyo sababu Yesu aliwatakasa watu kadhaa badala ya siku fulani. “Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”(Wakolosai 3:17). Kazi yoyote tunayoifanya chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu ni namna ya kumwabudu Mungu. Hivyo siku hiyo haina thamani ndogo kuliko nyingine. Yesu alituweka haki kwa njia ya damu yake ya thamani na kutufanya tuwe wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu. Yeye aliumba watu waliotakaswa, sio siku zilizotakaswa. Kusudi la kuja kwake hapo duniani ilikuwa kukamilisha yale ambayo Sabato haikuweza kufanya: Kuumba watu wapya, kubadilisha wafanya dhambi waovu ndani ya wafuasi watakatifu, na kugeuza waliojiangalia wenyewe tu wawe watumishi wanyenyekevu.

Yesu alipindua kila sehemu ya uhai wetu wa kiroho. Ndiyo sababu pia ya Wakristo kuchagua Jumapili, siku ambapo Yesu alifufuka, iliwaadhimishe hila Agano Jipya pamoja na uumbaji wake mpya. Lakini Yesu aliwataka wafuasi wake nao wapumzike, na wapate kuzingatia hali ya kujaliwa kuwa sehemu ya uumbaji Wake mpya. Hakutuagiza kushika Jumapili, wala hakutukataza kushika Sabato. Hakukusudia kutufunga na siku au sikukuu fulani, lakini alikuja kuokoa wenye dhambi. Hivyo ufufuo wa Yesu umeweka alama ya mwanzo wa wakati (enzi au millennium) mpya na tutambue kwamba, hatuishi tena chini ya sheria inayotushitaki, bali chini ya neema ya Bwana wetu inayookoa. Wala hii haimaanishi kwamba Wakristo ni watu wasio na sheria (au amri). Roho wa Kristo atawalaye ndani yetu ndiye mwenyewe amri ya upendo, na wakati uo huo inatujalia nguvu ya kuitimiza. Hivyo, Sabato inabakia kuwa alama ya Agano la Kale iliyokuwa dhaifu; lakini Jumapili ndiyo alama ya ushindi wa Kristo inayoanzisha Agani Jipya.

Waumini kadhaa katika nchi za kiislamu hawawezi kupumzika Jumapili wala Sabato. Kwa hiyo wanakutanika pamoja Ijumaa, wakitambua kwamba Bwana mwenyewe yu pamoja nao alivyoahidi, “Kwa kuwa walipo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao”. Yesu hakukusudia kuweka wakfu siku fulani kwa ajili ya Ibada, lakini zaidi ya hapo kutakasa waumini wakati wowote na popote.


06.5 -- Kuadhimisha Jumapili

Jinsi gani Wakristo wataweza kutakasa siku ya Bwana wao? Upendo unawasukuma wakutanike pamoja kwenye Jumapili kuabudu na kusoma Biblia, pia na kumtukuza Yeye ndani ya ushirikiano wa watakatifu. Watoto wetu, wageni, wenzetu wafanya kazi, na hata mifugo zizini, wote wangeshiriki nasi katika siku ya kupumzika na katika furaha tukufu ya ufufuo, unaokumbukwa kila Jumapili na kuingizwa kabisa ndani ya maisha yetu. Msingi wa furaha ya kikristo ina kina zaidi ya ile ya Wayahudi. Yesu alisema, “Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe”(Yohana 15:11). Paulo naye aliandika, “Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini”(Wafilipi 4:4). “Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, …..“ (Wagalatia 5:22).Mistari kama hii inatuonyesha jumlisho la roho wa Jumapili. Pamoja na hayo inatueleza roho wa kazi zetu katikati ya wiki; inatuelekeza pia namna ya maisha ya familia ya kikristo inavyotakiwa.

Basi tufanye kazi Jumapili? Kama watu wengine nao, Wakristo ni watu wa kawaida. Wanao miili inayochoka. Ndiyo maana wanahitaji kutulia na kupumzika. Wao ni viumbe vya kawaida, na pamoja na hayo ni watoto wa Mungu kiroho. Wanaishi mwilini hapo duniani, na kiroho wameketishwa mbinguni pamoja na Kristo. Hawakatai siku ya kupumzika usoni pa Bwana. Tangu mwanzo Jumapili haikukusudiwa kupata nafasi zaidi kulala usingizi, bali kumtukuza Mungu Baba na kumsifu Yeye. Siku hiyo ni mali ya Bwana, na hatutakiwi kufanya shughuli zisizo za lazima. Hata hivyo tusitoroke inapotakiwa kufanya kazi za upendo na huduma zinazowaokoa wengine hatarini. Kuhesabiwa haki kwetu haiwekwi msingi katika kutimiza amri fulani, lakini kwenye kifo tha Kristo kwa niaba yetu, alipoingiza kwa utaratibu mpango wa sadaka ndani ya mioyo yetu. Kwenda kwenye ibada za hadhara na mikutano mingine ya kiroho siku ya Jumapili ndiyo mapendeleo yaliyowekwa kwa ajili ya Wakristo. Lakini haitoshi kwa Wakristo kulishwa tu chakula cha kiroho siku ya Jumapili tu, lakini wanatakiwa kujilisha chakula hichokila siku, pasipo kufanya hivyo, imani yao, upendo na tumaini zitafifia. Jumapili inatupatia nafasi kuimba kwa ushirikiano, kuomba katika vikundi na kushiriki mawazo na washiriki wengine ili kutambua umoja wa kikristo. Waumini wote pamoja ndiyo mwiliwa kiroho wa Kristo. Mwumini mmoja binafsi siyo lengo kuu la uumbaji mpya, , lakini ushirikiano wa watakatifu unaoweza kuonekana siku ya Jumapili hasa.

Na wabarikiwe wala wanaoenda kuwaona wagonjwa, wasiojiweza na maskini kwenye siku ya Jumapili. Waumini kama hao hawataangalia hali ya kupunguza mafuta ndani ya magari yao, au kama bado itatosha kwa kilometa zingine 100.

Roho wa Bwana hutuongoza tutoke kwenye jengo la Kanisa na kuwatafuta waliokufa ndani ya dhambi. Tunaitwa kuwaongoza wafikie ungamo ndani ya Kristo, ili wao nao wainuke kutoka kwa hali yao ya kukata tamaa na ya mioyo migumu. Haisameheki kutokutoa ushuhuda kwa wasioamini habari ya Kristo. Pia tunaitwa kutenda mambo ya kuwahurumia wanaohitaji msaada, pia na vikundi vyenye kuhitaji, hasa siku ya Bwana.

Jumapili pia inatupatia muda wa kumshukuru Bwana, kutengeneza yale yanayopungua kwetu, pia na kuombea mahitaji ya kila namna ya watu wengine. Na kama Mungu ametupatia watoto, tunatakiwa kutumia muda wa kutosha pamoja nao, kuimba nao na kuwatia moyo na furaha kwa nyimbo za kikristo. Na tumwulize Yesu namna ya kutimiza haja za mambo matatu ya mwanzoni mwa Sala ya Bwana, na tufanye hayo hasa Jumapili. Tukishika na kutunza Jumapili kwa vyovyote tutabarikiwa. Yesu ametayarisha mibaraka mingi kwa kila mmoja atafutaye kujazwa na roho wa Kristo aliyefufuka kutoka kwa wafu siku ya Jumapili.


06.6 -- Kukufuru Jumapili

Ni ya huzuni kwamba, madhambi zatendeka zaidi mwisho wa wiki kuliko kwenye siku zingine. Jumapili magari yanafurika nchi za kimashamba. Vituo vya TV vinatoa tu muda mfupi kwa ajili ya Neno la Mungu, huku filamu za kuogofya, za aibu au za siri za roho mbaya zinajaa. Siku za Jumapili watu hufanya kazi nyumbani, bustanini au kibandani, ambapo wangeweza kufanya hayo siku zingine za wiki. Kwenye enzi za Agano la Kale, mtu akikutwa anachapa kazi siku ya kupumzika alihukumiwa kufa. Kama tungeweza kuziona dhambi zote zinazotendeka Jumamosi na Jumapili, tena hadharani na faraghani katika mji moja tu, ingevunja mioyo yetu na kutupotezea akili! Ni upendo wa Mungu tu unaovumilia kuumia kwa muda mrefu na subira inayoendelea kumngojea mtenda dhambi atubu.

Je, umesahao analosema Bwana kuhusu mtu anayedharau siku yake? Tunaposoma kitabu cha Kutoka 31:14-17, tutatambua jinsi ilivyo ya muhimu sana kwetu kuwa na utulivu mbele za Bwana (tazama pia kitabu cha Hesabu 15:32-36 ili kuelewa vema haja ya kushika siku ya Bwana). Heri tungebadilisha mwenendo wa maisha yetu na kuuliza, kwa mfano, wanafunzi wetu wasiendelee na mafunzo yao Jumapili. Bwana anatisha kuchoma mji au kijiji kile ambacho haiheshimu Sabato kama siku ya ibada na kupumzika (Yeremia 17:22). Tusingepuuza onyo hilo kwa urahisi. Nani ajua kama vita za ulimwengu na maangamizi makuu siyo matokeo kwa sababu ya kupuuza kwetu hivyo? Biblia latuambia, „Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu,ndicho atakachovuna“ (Wagalatia 6:7). Hakuna awezaye kuvunja maagizo ya Mungu na kutokea hivi hivi.

Kama Yesu asingalikufua msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na kubeba adhabu kwa niaba yetu, tusingekuwa na tumaini lolote. Hata hivyo, kifo chake sio udhuru kwa ajili yetu kutokutakasa siku ya Bwana. Yesu na wanafunzi wake wakati wo wote walitakasa Sabato. Aliishi kwa ajili ya kumtukuza Baba yake. Baada ya kufufuka kwake siku ya kwanza ya wiki, Yesu aliwatikea wanafunzi wake kwa ajili ya kuadhimisha sikukuu hiyo mpya ya agano lake nao.


06.7 -- Ufahamivu mpya wa Amri (Sheria)

Kwa kutafakari kuhusu njia zisizo sawa za kushika Sabato, tunaweza kuona jinsi ilivyo rahisi kukosa kuelewa amri hii ya Mungu. Yesu alikuwa anahukumiwa kufa kwa ajili ya kuponya wagonjwa siku ya Sabato, na kwa kutamka kwamba, Yeye ni Mwana wa Mungu. Alikuwa amewindwa na viongozi wa kidini wa wakati wake ambao, katika ushupavu wao kwa ajili ya amri za Musa, walikuwa wamepoteza uwezo wao wa kumpenda Mungu na watu. Walikuwa wenye haki kwa nje katika namna ya unafiki na kugeuzia sikio isiyosikia kwa wito wa kuungama. Katika upofu wao walifanya migumu mioyo yao. Hawakuwa tayari kubadili nia zao. Walimkataa Mungu Baba, Mwana na pia Roho Mtakatifu. Hawakujali wale waliokuwa wagonjwa siku ya Sabato. Hivyo shauku yao ya kutimiza amri siku ya Sabato iligeuka kuwa unafiki. Basi, si ajabu ilimpasa Yesu kuwaambia, „Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu“ (Mathayo 15:8+9).

Katika mahangaiko yake ya kutufundisha njia ya kufaa ili tutakase hiyo siku ya Bwana, Yesu hakusema mengi kuhusu kufanya kazi au kutokufanya, bali alikazia shabaha iliyo sawa za mioyo yetu mbele za Mungu. Paulo aliendelea kukazia ufahamu huo wa amri katika roho ya Kristo. Hata hivyo alilaaniwa na kupigwa kwa mawe kwa kufundisha kwamba, waumini wasiokuwa Wayahudi waliwekwa huru na agano la awali. Alitufundisha kwamba, tumewekwa huru na mahukumu ya amri kwa sababu tayari tumekwisha kufia amri kwa njia ya kifo cha Kristo. Kwa sababu hiyo, amri sasa haina nguvu juu yetu. Lakini Roho Mtakatifu aliweka taratibu mpya ya upendo wa Kristo ndani yetu. Amri hiyo mpya ya kiroho ndani ya mioyo yetu imetutakasa na kutuhimiza kutukuza Utatu wa Mungu katika mawazo yetu yote, maneno pia na matendo. Basi, hatulemazwi tena na amri, bali inatokeza toba na imani kwa nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yetu. Tungetakiwa kukumbuka sana kwamba, Kristo hutakasa watu, wala si siku! Hivyo tunajifunza utofauti kabisa kabisa kati ya Agano Jipya na Agano la Kale, na hii ni kutokana na kuelewa vema amri ya nne.


06.8 -- Ijumaa ya Waislamu

Waislamu wameonyesha kwamba, hawaelewi maana ya amri ya nne kwa kuamuru Ijumaa kuwa siku ya mikutano muhimu ya kidini, wala hawaikamilishi hata hivyo. Mhamadi aliendelea hatua moja zaidi, wakati Wayahudi na Wakristo walipokataa ule unabii wake na karibisho lake kuwataka wawe Waislamu. Wala hakukubali habari ya Jumamosi ya Wayahudi wala na Jumapili ya Wakristo. Katika kujaribu kuimarisha imani yake mwenyewe, alikataa taratibu ya Agano la Kale na ya Agano Jipya na badala yake akaamuru Ijumaa kuwa siku ya mikutano ya Waislamu. Hakuna egemezo kwa siku hiyo ndani ya maandiko, wala haina uhusiano na mpango wa ukombozi. Kwa kweli, inatokana na maasi dhidi ya Mungu na Masihi wake. Ijumaa haina msingi au egemezo lolote ndani ya Biblia.

Waislamu hurudi kwenye shughuli zao mara baada ya sala ya Ijumaa. Hotuba za ndani ya muskiti siku za Ijumaa mara nyingi ni za ki-siasa. Si mara chache kwamba, hayo yafuatwa na maandamano ya kuchipuza chuki na kuharibu. Kutakasa siku ya pekee au kumtakasa mwumini mwenyewe, hayo hayajulikani na wafuasi wa Uislamu. Allah anfikiriwa kuwa mkubwa mno hata maana ya utakatifu wake haijulikanina Mwaislamu, isipokuwa jina lake tu. Hayo yaeleza kwa nini Uislamu unsimama chini sana na daraja la agano la kale, hasa kuhusu amri hii ya nne. Wao hawana wazo lolote kuhusu wokovu au uumbaji mpya ndani ya agano mpya.

Lakini tunatoa shukrani kwake yule Mmoja, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, maana alizitenda miujiza yake siku za sabato na pia siku zingine za wiki. Alifufuka kutoka kwa wafu siku ya kwanza ya wiki na kuipatia maana nyingine mpya siku hiyo. Loo, kila Jumapili lingkuwa kama hali ya jua kuchomoza asubuhi, sawa kwa kila wiki mpya na kung’aa na maneno ya kuhuisha ya Bwana wetu, „Amri mpya nawapa,Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi“ (Yohana 13:34-35).

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:57 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)