Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 03 -- First Commandment: You Shall Have no Other Gods Before Me
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

03 - Amri ya Kwanza: Usiwe Na Miungu Mingine



KUTOKA 20:3
Usiwe na miungu mingine ila mimi!


03.1 - Kuabudu miungu (sanamu) siku hizi

Tukiishi katika nchi ya viwanda vya kisasa na kazi za bidii, itakuwa vigumu kukutana na watu wanaoabudu sanamu, zikiwa za mbao, mawe au hata dhahabu. Lakini tukitembelea Asia au Afrika, kwa vyo vyote tutaona sanamu nyingi pamoja na watu wengi wanaoziabudu kweli kwa hofu sana.

Kwenye gazeti la shirika la ndege “India Airlines” kulikuwa na picha ya Durga, aliye mungu wa kike ya vita, na pamoja naye silaha sita sinazoweza kumwua adui yeyote. Pia na mifupa ya binadamu zilizagaa karibu na Durga. Huyu shujaa wa vitani angemteketeza yeyote amkaribiaye kwa ile moto iliyotokea mdomoni mwake. Tena alicheka wakati wa kuua adui zake.

Utakuta sanamu kubwa zilizichongwa kwa sura ya tembo kule India zikitoa mfano wa mungu Ganahati. Mara kwa mara Wahindi wanaweka maua madogo madogo mbele zao. Kwenye sikukuu za pekee, msongo wa maua zinapamba tembo za plastic, ambazo zaweza kuwa na urefu wa magorofa mawili au matatu kwenda juu. Mati za watu zinasindikiza sanamu hizo zikitembezwa barabarani, ndipo wanazitumbukiza mtoni au ziwani wakitegemea kwamba, uvuvi upate kufaulu, pia na walindwe na mafuriko ya kila mwaka yasiharibu.

Wakati wa sikukuu ya kipekee maelfu ya ng’ombe husukumwa ndani ya mahekalu na kunyunyikizwa maji matakatifu, ili waendelee na afya. Baada ya hapo pembe zao hupakwa rangi mbalimbali kwa alama ya kuwaweka wakfu.

Tungejaliwa kutembelea bonde la Ladakh ng’ambo ya milima ya Himalaya au kusafiri katika nchi ya Wabuddhisti, tungeona sanamu kubwa ya dhahabu zinazochekelea za Buddha, na watu wanaoinama kifudifudi mbele zao kwa uchaji kabisa. - Sehemu ya tatu ya binadamu wote bado huabudu miungu ya aina hiyo, na hivyo kuvunja amri ya kwanza. Waabudu hao huamini ndani ya nguvu ya hizo sanamu pia na katika njia ya kurudia tena uhai katika mwili au kiumbe kingine baada ya kufa. Hesabu kubwa za watu Afrika na Indonesia bado huishi katika vifungo vya kiroho kwa desturi za namna hii. Wengine tena huabudu babu zao wa vizazi vilivyokwisha kufa. - Lakini kama wangejaliwa kutambua mamlaka ya Yesu, wangewekwa huru na hofu zote na namna za kuabudu sanamu na ubashiri. Hapo basi wasingehitaji tena matamshi ya miujiza au lulu za blue na kukataa sanamu zisizo na uhai, kwa sababu wangekuwa na kinga ya kuwalinda na ushawishi wowote wa roho mbaya.

Baba yetu wa mbinguni hutuweka huru na namna zozote za hofu, hata kutoka kwa utawala wa nguvu za giza na kutufungulia na matukio yo yote ya uchawi. Damu ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiyo ulinzi wa mwisho kutoka kwa nguvu zozote baya. Lolote linaloweza kuandikwa au kutamkwa katika jina la nguvu hizo za giza dhidi ya hao wamfuatao Bwana Yesu watakuwa wakikingwa kwa jina la Bwana wetu. Yeye atadumu kuwa ngome imara kwao wote watakaomgeukia.


03.2 - Sanamu za kisasa

Kwa bahati mbaya, kuna namna mpya ya kuabudu sanamu iliyoenea katika nchi za maendeleo ya kisasa, ambapo sanamu za mti, mawe au dhahabu zimebadilishwa na magari, TV, sinema au sifa zozote. Mwanadamu hutegemea zaidi maendeleo za kisasa na za mashine kuliko Mungu aliye hai. Huingia katika gari lake na kuendesha kwa upesi sana kwenye barabara za lami. Gari nzuri imekwisha kuwa sanamu ya kisasa kwa watu wa siku hizi. Wanaingia ndani yake na kujiachilia kabisa kwa nguvu yake. - Iwapo Waisraeli zamani walipiga dansi kwa kuzunguka ndama ya dhahabu, basi ujumla wa wenye maendeleo ya kisasa huzungukia ile gari safi ya kisasa kabisa. Mwenye gari huweka akiba na kutoa sadaka ya mengineyo kwa ajili ya gari, huisafisha na kuing’arisha sana, tena husikiliza zaidi ngurumo ya ingini yake kuliko kuwasikiliza watu walio karibu naye. Hutumia muda mwingi pia na fedha kwa ajili yake - zaidi sana kuliko matoleo yake kwa ajili ya maskini. Je, binadamu amekwisha kuwa mtumwa wa maendeleo (teknologia) ya kisasa? - Msongamano wa watu husukumana ndani ya viwanja vya michezo, ili watazame mashindano ya mbio za magari au matukio yafananao. Lakini wachache tu hukaa kwenye viti kanisani na kushiriki katika ibada ya watu wote.

Kipekee Yesu anatuonya tusipende pesa. Alisema, “hakuna awezaye kumtumikia Mungu na fedha; maana atapenda moja au kuchukia kingine, au kumkataa Mungu na kushikamana na fedha.” “Kupenda fedha ndiyo asili ya maovu yote.” Wa-Socialisti na Wa-Kapitalisti wanao shabaha ile ile; Wa-Kapitalisti ni watajiri na Wa-Socialisti wanataka kuwa watajiri kwa njia za kusukuma au kuvuta mambo kwa namna zao au kwa fitina. Watu hupiga dansi kwa kuzunguka ndama ya dhahabu (mali nyingi) hata siku hizi. Usidanganyike, maana Mungu hawezi kudhihakiwa. Hakuna anayeweza kumtumikia Mungu na fedha. Yesu aliishi kama maskini, lakini aliridhika. Aliwaonya kwa vikali wafuasi wake dhidi ya utajiri: “hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi” (1.Tim.6:9; Math.6:24 na 19:24).

Hata hivyo, sanamu kuu na kutawala juu ya utamaduni na dini zote ndiyo umimi wetu. Kila mtu anaelekea kufikiri kwamba, yeye ndiye bora, anayependeza zaidi ya wengine na kuwa mtu wa maana kuliko wengine. Wasipotafakari vizuri juu ya hayo, basi bila kusikiliza dhamiri zao wanaitamani hali hiyo. Yeyote hufikiri kwamba yeye ndiye kiini cha dunia. Msichana wa miaka mitatu alikuwa anaulizwa, “Je, ungependa kuwa nini?” Alijibu, „Kuwa kama sanamu!“ „Kwa nini basi?“ „Kwa sababu kila mtu atakuwa ananiangalia.“ Kiburi na umimi huwa zinaogelea damuni mwetu. Ila hali hii ni kinyume kabisa na roho ya unyenyekevu wa Kristo. Yesu alisema, “Mwawezaje kuamini ninyi mpokeanapo heshima ninyi kwa ninyi, na ule utukufu utokao kwa Mungu hamwutafuti?“(Yoh.5:44) „Jifunzeni kwangu, maana mimi ni mpole, na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha rohoni mwenu. Maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.“ (Math.11:29-30)

„Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza, na mtu atakayeipoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona“ (Math.16:25). „Je, unajitafutia mambo makuu? Usiyatafute.“ (Yeremia 45:5).


03.3 - Kushinda hali ya kuabudu sanamu

Kwa nini jambo la kukataza ibada ya miungu mingine mbali na Mungu wa kweli liwe ni amri ya kwanza? Kwa kweli, kuna Mungu mmoja tu. Ibada zote za ulimwengu huu ni za muda tu. Mungu pekee aishi milele. Ndiye aliyetuumba, hivyo kwake liwe utukufu na heshima yote. Yeye ndiye kiini cha ulimwengu wote. Umimi wetu ungepasa kuvunjwa-vunjwa kila siku, hadi tuungame na kumtumikia Mungu kwa furaha. Tungetakiwa kuweka nafsi zetu tayari kumtumikia Mungu. Jambo lolote la kwetu lisiwe msingi wa maisha yetu, si akiba yetu ya fedha, si afya yetu, wala si vipawa vyetu.

Ibrahimu alikuwa alimpenda sana Isaka, mrithi wake halali, na mwana wa kongojewa sana. Alimshughulikia sana, hata ikaonekana kwamba, huyu kwake ni muhimu zaidi kuliko Mungu. Ndipo Bwana akamjaribu mtumishi wake. Alimwagiza amtoe sadaka mwana wake mpendwa awe ni dhabihu ya kuteketezwa kwake Mungu. Ibrahimu akawa tayari kufanya lile ambalo lilionekana kwamba haiwezekani, yaani kumtoa sadaka mwana wake na kumpa Mungu utukufu pekee. Hata hivyo Mungu alimzuia Ibrahimu katika dakika ya mwisho asimchinje mtoto wa ahadi yake, akampatia kondoo dume kuwa sadaka badala yake. Katika hali hii ya vurugo rohoni mwake, Mungu akawa ametukuzwa, Ibrahimu alipokuwa tayari kutengana na mwana wake. Hivyo alithibitisha kwamba alimpenda Bwana kuliko mwana wake.

Twahitaji kujipima mara kwa mara na kuchunguza kama kuna sanamu kubwa au ndogo zinazokaa kati yetu na Bwana. Pengine ni vitabu, vito vya dhahabu, picha ya mtu, kumbukumbu ya thamani, jambo la kujifurahisha (hobby), mazoezi fulani, pesa, nyumba na kadhalika. Hata watu huweza kushika mioyo yetu kwa namna isivyopasa.

Jaribu la kuabudu sanamu ni wazi hata ndani ya watu wanaowafanya viongozi wao kuwa kama Mungu. Mati za watu walikuwa wameshikwa na viongozi kama Napoleon, Ataturk, Hitler, Nasser, Khomeini na wengine. Hata hivyo, vitabu vyao na kumbukumbu zao mara nyingi zilichomwa au kuharibiwa mapema baada ya kifo chao. Nabii Yeremia awaonya watu dhidi ya kupumbaziwa na watu au kutia tegemeo ndani ya msaada wa kibinadamu: „Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake“ (Yeremia 17:5).

Watu mara kwa mara hutukuza wabingwa wa sinema au michezo ya aina mbalimbali kana kwamba ni mungu. Wana staajabishwa kwa aina za muziki kiasi cha kushikwa na pepo, hasa wakiwa mati kubwa ndani ya jengo kubwa au uwanja wa michezo. Kwa hayo twahitaji kuwa waangalifu. Hatusemi kwamba kuwatumikia watu na kuwaheshimu ni dhambi. Lakini ni uhalifu wa kiroho kumpenda au kumtegemea mwanadamu kuliko Mungu.

Je, Mungu hakujiunga nasi katika agano la milele? Haishangazi kwamba Kristo huwaita watu „kizazi kibaya na chenye ukaidi“, kwa sababu hawampendi Mungu kwa moyo wao wote, hawamheshimu kwa kina wala kumtegemea yeye pekee.

Siku hizi kuabudu sanamu hutendeka katika namna mbalimbali, na hii ni kutokana na utupu unaoletwa na mwelekeo wa kwenda mbali na Mungu. Bwana ndiye Mungu mwenye wivu, naye atamani kutawala mioyo yetu yeye peke yake. Hataridhika na sehemu au hata sehemu kubwa ya upendo na utii kwake. Anataka tuwe wake kabisa na kwa daima. Kwa hiyo, sanamu za zamani na za siku hizi lazima zipotee kutoka kwa maisha yetu, na tunahitaji kufanya upya hali yetu ya kujitoa kwa Baba yetu ya mbinguni. - Wewe ujiulize, yapi ni sanamu zinazojificha maishani mwako, na unatakiwa kufanya nini kuyaharibu kwa daima?


03.4 - Je, imani ya Kikristo inabishana na Amri ya Kwanza?

Wayahudi na Waislamu waweza kueleana juu ya maelezo ya kikristo kuhusu Amri Kumi hadi hapo. Hata hivyo wao wanashitaki Wakristo kwamba wanagombana na amri ya kwanza kwa kukiri kwao. „Ninyi Wakristo kwa kweli ni wakafiri“ wanatetea, „kwa sababu mnavunja amri ya kwanza, tena iliyo kuu. Mnamtukana Mungu kwa kudai kwamba kuna miungu mitatu, na ya kwamba mmojawao alikufa msalabani.“ Wayahudi na Waislamu huwashitaki Wakristo kwamba wanadharau, kwa sababu wanaamini ndani ya umoja wa Utatu Utakatifu.

Je, jinsi gani Yesu mwenyewe aliitika kwa mashitaka ya aina hii? Yesu alikabiliana na mashambulio ya aina hii kutoka kwa watu wenye mioyo migumu kila siku. Yesu alieleza umoja wake na Mungu wazi kabisa: „Mimi na Baba tu umoja“ (Yohana 10:30). Hakutamka wakati wo wote, „Mimi na Baba tu wawili,“ bali mmoja! Baada ya hapo alitamka, „Mimi ni ndani ya Baba na Baba yu ndani yangu.“ Kabla ya kukamatwa kwake, yeye aliwaombea wafuasi wake, „Ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja“ (Yohana 17:22) Maneno hayo yashuhudia wazi habari ya Utatu Utakatifu. Tamko la „sisi“ hapo lieleweke kuwa „mimi“. Yesu alitoa ushuhuda kuhusu umoja wake kamili pamoja na Baba. Ukweli huo hauwezi kueleweka ki-mahesabu. „ Hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu“ (I.Wakorintho 12:3b). Hii ndiyo ukweli wa kiroho wa milele. Ikiwa hatuwi wazi kwa roho wa Mungu, basi hatuwezi kuelewa kweli hizo za kiroho.

Yesu alisema, „Mtu akinipenda, atalishika Neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake“ (Yohana 14:23). Yesu aliwaahidi wafuasi wake, kwamba, Roho Mtakatifu ataishi ndani yao. Na hapo hapo aliwahakikishia habari ya umoja wake kamili na Baba yake wa mbinguni, na kwamba wote wawili wataishi ndani ya mioyo ya wafuasi wao.

Wakristo hawaamini habari ya miungu mitatu mbalimbali, lakini waamini ndani ya Mungu mmoja, aliyejifunua mwenyewe kuwa Baba , Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa kukiri umoja wa huo Utatu hatuvunji amri ya kwanza, bali tunaitimiza. Roho wa Mungu amemwagwa ndani ya mioyo yetu kama matokeo ya kupatanishwa kwetu na Mungu kwa njia ya kifo cha Yesu Kristo. Huyu Roho mwaminifu hututia moyo tumwite Mungu „Baba yetu“ na kutakasa jina lake hilo la ki-baba. Sisi sote kwa usawa twaamini ndani ya Yesu na kumpenda kwa mioyo yetu yote kwa sababu „pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi“ (Warumi 5:5). Inatupasa kutambua kwamba ule umoja wa Utatu Utakatifu umefunikwa kwa yeyote ambaye hajazaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu na asiyejibidiisha kugundua ukweli huo tukufu.

Kwa kweli Kurani haishambulii imani ya kikristi ndani ya Utatu. Badala yake inashambulia Utatu wa uzushi, ambao hata makanisa yote ya Kikristo yanaikataa na kuishambulia. Kurani inapiga vita dhidi ya Utatu wa baba, mama na mwana (Sura al-Maida 5:116). Kurani pia inakataa imani kwamba Mungu ni Yesu mwana wa Mariamu (Sura al-Maida 5:17,72) au hata kuwa wa tatu katika watatu (Sura al-Maida 5:73). Maana ufahamu kikamilifu wa Umoja Utakatifu ndani ya Biblia ni kwamba Mungu ndiye umoja kikamilifu, umoja wa milele, ule Utatu wa Baba asemaye kwa njia ya Neno Lake na kutenda kazi kwa njia ya Roho yake. Tunakataa ule utatu wa kimwili wa baba, mama na mwana, sawa na dai ile ya kwamba Mungu ni Kristo, mwana wa Mariamu. Tunamkiri Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu anbaye ndiye Mungu mmoja pekee.


03.5 - Agano la Kale lasemaje kuhusu Utatu?

Ndani ya Agano la Kale tunakuta marejeo kadhaa ya kushtusha ya kuhusu umoja wa Mungu ndani ya Utatu Utakatifu. Hata Kurani haiwezi kukataa hayo. Katika Zaburi 2:7 na 12 twasoma habari ya ufunuo wa Mungu kumhusu Yesu miaka kama elfu moja kabla hajazaliwa, „ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa“. Tena anawaonya watu kwa kutamka, „Mbusuni Mwana, asije akafanya hasira, nanyi mkapotea njiani.“

Isaya 7:14 anatamka miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwake Kristo, „Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye ataitwa jina lake Imanueli“ (Maana yake:Mungu pamoja nasi).

Isaya 9:6 anajumlisha ahadi kuu, „Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanaume; na uwezo wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake; Mshauri wa ajabu. Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani“. Maneno hayo matukufu kwenye Agano la Kale yanabeba ushuhuda juu ya uungu wa Yesu na umoja wake kamili na Baba.

Kufuatana na II.Samweli 7:12-14, Mfalme Daudi aliahidiwa kwamba, mmoja wa wana wake, atakayekuwa „akija kutoka katika mwili wake“, hapo hapo pia atakuwa ni Mwana wa Mungu. Na tangu hapo, jina lingine kwa ajili ya Masihi au Mwana wa Daudi likawa ni Mwana wa Mungu.

Kwenye Zaburi 110:1 twasoma, „Neno la Bwana kwa Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, hata niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako“. Je, hapo kuna mabwana wawili? Hata kidogo! Hata hivyo mistari hii inashuhudia umoja ule kamili kati ya Mungu aliye Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.

Tangu mwanzo Mungu alisema katika namna ya zaidi ya moja, „Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu“ (Mwanzo 1:26).

Jambo hilo latuonyesha kwamba, ushuhuda kuhusu umoja wa Utatu Utakatifu haikutengenezwa na Wakristo. Badala yake ni ukweli kwamba Mungu aliufunua miaka elfu kabla ya kuzaliwa kwake Kristo. Nani angeweza kuwa kinyume cha ufunuo wa Mungu?


03.6 - Marejeo ya Kurani kuhusu Uungu wa Kristo

Si torati tu, zaburi na vitabu vya manabii zinazoshuhudia habari ya umoja wa Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, lakini hata Kurani inataja mistari inayothibitisha ushuhuda wa kikristo. Kama kila Mwislamu angesoma Kurani kwa akili iliyo wazi, angesadikishwa kwa mistari hii inayohusu kuzaliwa kwake Yesu na bikira Mariamu. Yesu alizaliwa kama Neno la Allah bila kuingiliwa na mwanadamu. Allah alipuliza Roho yake ndani ya bikira Mariamu, na kwa sababu hiyo Yesu akazaliwa (Suras al-Anbiya21:91 na al-Tahrim 66:12).

Suras Al Imran 3:45, al-Nisa 4:171 na Maryam 19:43 kipekee zinatetea kwamba Yesu ni Neno la Allah mwilini naye ni roho kutoka kwake. Mistari hii ndiyo mwangwi wa kiislamu juu ya Injili ya Yohana, „Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake“ Yohana 1:14a.

Kwenye Suras al-Baquara2:87,352 na al-Maida 5:110 tunasoma kwamba Kristo ametiwa nguvu na Roho Mtakatifu, ili kumwezesha kuunda mfano wa ndege kutoka kwa matope na kumfanya kuwa hai kwa kumpulizia. Aliwaponya vipofu na wenye ukoma na hata wafu kuwa hai tena kwa ruhusa ya Allah. Upatano huo katika utendaji kati ya Allah, Kristo na Roho Mtakatifu umefunuliwa wazi ndani ya Kurani. Kwa nini basi Waislamu wanaasi dhidi ya Mungu na Masihi wake ?

Katika Sura Maryam19:21 tunaweza kusoma, „Tunamfanya kuwa ishara kwa ajili ya watu na kuwa rehema toka kwetu.“ Inashangaza tena na tena kwamba Allah ndani ya kurani kwa namna ya zaidi ya mmoja na kumtaja Kristo kuwa ni Rehema kutoka kwa Mwenye Rehema. Hii inathibitisha kwamba, Yeye ni wa asili ya usawa na asili tukufu.

Kuna marejeo kadhaa ya Agano la Kale na ya Kurani yanayothibitisha umoja wa Utatu Utakatifu. Tunatiwa moyo kuungana na malaika katika kumtukuza Mungu kwa kuimba, „Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.“ (Isaya 6:3). Marudio ya mara tatu „Mtakatifu“ inadokeza kwamba Baba ni Mtakatifu, Mwana ni Mtakatifu na Roho ni Mtakatifu, nao ni umoja katika utakatifu kamili.


03.7 - Imani ya Kikristo ndani ya Uungu wa Kristo

Haikuwa namna ya kutia chumvi, wakati mitume wa Kristo waliposhuhudia kwa umoja habari ya Uungu Wake. Mbali na hatari ya kuuawa Paulo alitangaza waziwazi, „Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana“ (Wakolosai 1:15). Yohana naye anakiri, „Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukuf u kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli“.(Yohana 1:14). Tena mtume Petro anashuhudia, „Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai“ (Mathayo 16:16).

Baraza la Nikea inajumlisha imani ya Kikristo, „Kristo ni Mungu kutoka katika Mungu, nuru kutoka tatika nuru, Mungu kweli kutoka katika Mungu kweli, amezaliwa, hakuumbwa, akiwa na hali moja sawa na Baba.”

Waislamu na Wayahudi huweka mipaka kwenye enzi kuu la Mungu katika mafundisho yao yasiopindikana. Nani awezaje kukataa ufunuo wa Mungu juu yake mwenyewe jinsi alivyo? Nani anayo haki ya kumzuia Mwenyezi asiwe na Mwana na kumtoa dhabihu kwa ajili ya kuokoa ulimwengu? Mungu ni huru kabisa! Kristo alikuwepo kabla ya uumbaji. Ndipo akawa mwanadamu, ili apatanishe ulimwengu na Mungu na kurudisha tena amani ya kimbinguni. Kristo akawa mwanadamu ili auokoe ulimwengu. Naye akaendelea kuwa bila dhambi, ili aweze kutupilia mbali dhambi za ulimwengu wote. Yohana Mbatizaji alirejea habari ya wito huo tukufu, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!” (Yohana 1:29b). Kwa matokeo ya hayo, sisi tumepokewa kuwa wana na kumwita Mungu “Baba yetu uliye mbinguni”, kwa vile dhambi zetu zimesamehewa. Kristo ametengeneza wokovu mkuu kwa ajili ya watu wote, sio kwa ajili ya Wakristo tu. Wokovu wake ni kwa ajili ya Wahindi, Wabudhisti, Wayahudi Waislamu na wasioamini kwamba kuna Mungu. Yeye huthibitisha uzima wa milele kwa ajili ya yeyote atakayemtegemea kabisa na kumkubali Yeye kuwa Bwana na Mwokozi wake. Mwana hutuongoza kwake Baba, tena Baba atuvuta tuje kwa Mwana. Mungu amejifunua mwenyewe wakati wa ubatizo wa Yesu kwenye mto Yordani, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”(Mathayo 3:17). Je, nani ambaye angeweza kuzuia sauti itokako mbinguni?


03.8 - Kusudi la Amri ya Kwanza ni nini?

Kusudi la amri ya kwanza ni rahisi: kumpenda Mungu. Musa alitia mapendeleo hayo ndani ya agizo lililo muhimu kabisa, „Nawe umpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote“ (Kumbukumbu la Torati 6:5). Sisi tunampenda Mungu na kuishi katika amani na Roho yake, au tunamchukia na kuishi kinyume cha Mapenzi yake. Kama tunampenda Mungu, tunatafakari habari zake, tunamsikiliza, tunatenda yanayompendeza, tunaishi kwa ajili yake na kumtamani jinsi Bibi Arusi anavyomtamani Bwana Arusi wake akisoma barua zake tena na tena kwa kurudia. Lakini wale wanaotegemea kiburi chao na kujiangalia kama nusu mungu, wakigeuzia mabega yao kwa Mungu wa kweli, kwa vyovyote watasahau Neno lake; na katika hali yao ya mioyo migumu mwishoni wataangukia kwenye ghadhabu ya Mungu.

Hata hivyo wale wampendao Kristo wako wazi kwa ajili ya Roho wa Mungu. Wao hupokea msamaha wa dhambi zao zote na wanatembea katika nguvu ya Roho Mtakatifu. Wanabadilishwa katika namna ya Baba yao, kwa vile wanaomba kila siku kwamba, jina la Baba lipate kutukuzwa maishani mwao na katika nyumba zao. Ikiwa tunampenda Mungu kweli, tunamgeukia na kupokea neema juu ya neema. Tunapata kutambua kila siku utakaso wa dhamiri zetu, tunaishi katika uhuru wa watoto wa Mungu na kushiriki katika huduma yake ya kiroho. Wale wanaompenda Mungu kweli wanatupa sanamu kabisa nje ya maisha yao na kusimama imara ndani ya agano jipya, ambalo huduma yake imefunuliwa ndani ya neno kuu la imani na maisha yao, tusomavyo, „Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake“ ( 1.Yohana 4:16b).

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:59 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)