8. Wimbo wa Sifa ya Paulo, kama sehemu ya kufunga kwa waraka wake (Warumi 16:25-27)
WARUMI 16:25-27
"25 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na Injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, 26 ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. 27 Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina."
Paulo kwa heshima alifunga waraka wake kwa kanisa la Warumi kwa kumwabudu Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Paulo anamthibitisha yeye kuwa chemchemi ya nguvu zote za mafundisho mema, na kwamba ndiye pekee awezaye kutoa nguvu ya kudumu milele, iwezayo kuanzisha makanisa na kuyaendeleza na kutunza ndani ya Roho ya enzi yake.
Paulo alifunga barua yake pamoja na madhubutu yake ya mwanzoni (Warumi 1:16). Kutoa uzima kwa wale waliokufa katika dhambi, jambo hilo limetambulika katika injili hii ya Paulo. Basi hakuna injili nne tu, zinazotajwa kwa majina Mathayo, Marko, Luka na Yohana; bali kila habari njema na tamko la wokovu ndani ya Yesu katika hotuba za Paulo pia ni Injili ya pekee. Huyu Mtume wa Mataifa alikubali kwamba, kutokea kwa Bwana Yesu kwake binafsi kule karibu na Dameski, kwa kumtambua kuwa yule aliye sulibiwa na kuishi tena, na ya kwamba alimtambua kuwa ni yule wa kweli, Kristo aliyeahidiwa; hayo yalikuwa ni shabaha zake za pekee za kuandika waraka wake. Ndani ya injili yake Paulo anafunua ile siri kwa ajili ya yeyote aliye tayari kusikiliza yale yaliyokuwa siri hadi wakati ule, lakini limefunuliwa sasa na kujulishwa kwa maandiko ya manabii wa Agano la Kale, waliokabidhiwa na Mungu mtakatifu na wa milele.
Yaliyomo katika siri hiyo ndiyo kwamba, Mungu awatamani hao watu wasio safi na wasioitwa, wa Mataifa, wao nao wajifunze habari ya utii wa imani, kufuatana na Agano Jipya. Hivyo Bwana hutoa msamaha wake wa dhambi kwa wanadamu wote kama neema ya bure, kwa sababu ya sadaka yake ya malipaji ya Yesu. Na kwa sababu hiyo, yeyote asikiaye wito huo, akakubali zawadi hiyo ya Mungu, basi atakuwa ameokolewa. Bali yule asiykubali, anajihukumu mwenyewe.
Paulo alimwabudu Mungu, aliye mwenye hekima peke yake. Alishuhudia kwa shukrani na kwa unynyekevu kwamba, Mungu anastahili utukufu na heshima yote; na kuabudu hivyo kibinadamu kuliwezekana tu kutokana na kazi, kifo na ufufuo wa Yesu, atawalaye pamoja na Babaye katika umoja na Roho Mtakatifu daima. Na neno la mwisho „Amina“, ambalo Paulo alilitumia kwa kufunga waraka huu kwa Warumi, linaonyesha kwamba, hilo ndilo ukweli hakika, ambao kwa uhakika utakamilika katika yote.
SALA: Tunakushukuru Baba, ndani ya mwana wako Yesu, kwa sababu ulimchagua Paulo, nawe ulimwita kupeleka ukombozi wako kwa makanisa kati ya Mataifa, na pia ateseke na kufa kwa ajili ya huduma yake hiyo. Utusaidie tusiwe watu wa kujifikiria wenyewe tu kiroho, lakini tupeleke wokovu kamili kwa wale wote wanaotamani kupokea ukweli, na tufanye hayo chini ya uongozi wa Roho wako Mtakatifu. Amina.
SWALI:
- Ipi ndiyo siri, ambayo Mungu alimfunulia Paulo, Mtume wa Mataifa?
QUIZ - 4
Mpendwa msomaji,
Baada ya kusoma maelezo hayo kuhusu barua ya Paulo kwa Warumi katika mfululizo huo, bila shaka sasa utaweza kujibu maswali yafuatayo. Ukiyajibu kwa usawa kwa 90% ya maswali, tutakutumia mfululizo ufuatao ya masomo hayo kwa ajili ya maongozo yako mema. Unapotuma majibu kwa Posta, usisahau kuweka jina lako kamili na anwani yako waziwazi kwenye karatasi ya majibu yako.
- Je, umejitoa kabisa mwenyewe kwa daima kwake Yesu, Mwokozi wako, au bado unaendelea na hali ya umimi na kuishi kwa ajili yako tu?
- Zipi ndizo hatua za kuishi maisha matakatifu kwa wafuasi wa Yesu?
- Ipi katika huduma zilizotajwa hapo juu unafikiria ndiyo inayohitajika zaidi siku hizi?
- Aina gani ya matumizi ya upendo wa Mungu unafikiria kuwa muhimu zaidi na kuhitajika sana ndani ya ushirikiano wenu?
- Jinsi gani tutaweza kuwasamehe adui zetu, na kutenda hivyo bila chuki na kisasi?
- Mipaka ya mamlaka ya kila serikali ni ipi, na kwa nini inatupasa kumtii Mungu kuliko watu?
- Jinsi gani Paulo alieleza kwa kihalisi hiyo amri: „Umpende jirani yako kama nafsi yako“?
- Maadili ni yapi, ambayo ufahamu wa kurudi kwake Kristo hivi karibuni, kunatusukuma kuyavaa maishani mwetu?
- Je, inatupasa kufikiri au kusema nini, wakati mfuasi mwingine wa Kristo anayo maoni tofauti juu ya mambo mengine ya maisha yaliyo ya namna ya pili (sio muhimu sana)?
- Ipi ni maana ya mstari Warumi 14:17 „ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu“?
- Je, maana ya mistari Warumi 15:5-6 ni nini
- Jinsi gani Paulo alitazamia kushinda matofauti ya msingi yaliyokuwa ndani ya kanisa la Rumi?
- Paulo aliandika nini katika waraka wake, ambalo aliona kwamba ni sehemu tu?
- Ipi ndiyo siri ya kufaulu katika huduma za Mtume Paulo?
- Kwa nini kabla ya safari yake kwenda Spania, Paulo alitaka kuelekea Yerusalemu, ingawa alijua habari ya tatizo na hatari nyingi zilizomngojea kule?
- Tunaweza kujifunza nini kutokana na majina ya washiriki wa kanisa la kule Rumi?
- Tunaweza kujifunza nini kutokana na majina ya watakatifu wanaotajwa ndani ya orodha?
- Ni wapi ambapo shetani anapokaza majaribu yake kwa uangalifu?
- Nani ndiye mtu ambaye Paulo alimwandikisha waraka wake kwa Warumi?
- Ipi ndiyo siri, ambayo Mungu alimfunulia Paulo, Mtume wa Mataifa?
Ukikamilisha masomo ya mihula yote ya mfululizo kwa Warumi na kututumia majibu ya mwisho wa kila muhula, sisi tutakutumia
CHETI CHA
masomo ya kuendelea katika kufahamu barua ya paulo kwa Warumi
ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni.
Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii:
Waters of Life
P.O.Box 600 513
70305 Stuttgart
Germany
Internet: www.waters-of-life.net
Internet: www.waters-of-life.org
e-mail: info@waters-of-life.net