Waters of LifeBiblical Studies in Multiple Languages |
|
Home Bible Treasures Afrikaans |
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek? -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish? -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba
WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Maongezo kwa SEHEMU ya 3 - Maelezo ya pekee juu ya msimamo wa Paulo kwa viongozi wa kanisa la Rumi (Warumi 15:14 – 16:27)
8. Wimbo wa Sifa ya Paulo, kama sehemu ya kufunga kwa waraka wake (Warumi 16:25-27)WARUMI 16:25-27 Paulo kwa heshima alifunga waraka wake kwa kanisa la Warumi kwa kumwabudu Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Paulo anamthibitisha yeye kuwa chemchemi ya nguvu zote za mafundisho mema, na kwamba ndiye pekee awezaye kutoa nguvu ya kudumu milele, iwezayo kuanzisha makanisa na kuyaendeleza na kutunza ndani ya Roho ya enzi yake. Paulo alifunga barua yake pamoja na madhubutu yake ya mwanzoni (Warumi 1:16). Kutoa uzima kwa wale waliokufa katika dhambi, jambo hilo limetambulika katika injili hii ya Paulo. Basi hakuna injili nne tu, zinazotajwa kwa majina Mathayo, Marko, Luka na Yohana; bali kila habari njema na tamko la wokovu ndani ya Yesu katika hotuba za Paulo pia ni Injili ya pekee. Huyu Mtume wa Mataifa alikubali kwamba, kutokea kwa Bwana Yesu kwake binafsi kule karibu na Dameski, kwa kumtambua kuwa yule aliye sulibiwa na kuishi tena, na ya kwamba alimtambua kuwa ni yule wa kweli, Kristo aliyeahidiwa; hayo yalikuwa ni shabaha zake za pekee za kuandika waraka wake. Ndani ya injili yake Paulo anafunua ile siri kwa ajili ya yeyote aliye tayari kusikiliza yale yaliyokuwa siri hadi wakati ule, lakini limefunuliwa sasa na kujulishwa kwa maandiko ya manabii wa Agano la Kale, waliokabidhiwa na Mungu mtakatifu na wa milele. Yaliyomo katika siri hiyo ndiyo kwamba, Mungu awatamani hao watu wasio safi na wasioitwa, wa Mataifa, wao nao wajifunze habari ya utii wa imani, kufuatana na Agano Jipya. Hivyo Bwana hutoa msamaha wake wa dhambi kwa wanadamu wote kama neema ya bure, kwa sababu ya sadaka yake ya malipaji ya Yesu. Na kwa sababu hiyo, yeyote asikiaye wito huo, akakubali zawadi hiyo ya Mungu, basi atakuwa ameokolewa. Bali yule asiykubali, anajihukumu mwenyewe. Paulo alimwabudu Mungu, aliye mwenye hekima peke yake. Alishuhudia kwa shukrani na kwa unynyekevu kwamba, Mungu anastahili utukufu na heshima yote; na kuabudu hivyo kibinadamu kuliwezekana tu kutokana na kazi, kifo na ufufuo wa Yesu, atawalaye pamoja na Babaye katika umoja na Roho Mtakatifu daima. Na neno la mwisho „Amina“, ambalo Paulo alilitumia kwa kufunga waraka huu kwa Warumi, linaonyesha kwamba, hilo ndilo ukweli hakika, ambao kwa uhakika utakamilika katika yote. SALA: Tunakushukuru Baba, ndani ya mwana wako Yesu, kwa sababu ulimchagua Paulo, nawe ulimwita kupeleka ukombozi wako kwa makanisa kati ya Mataifa, na pia ateseke na kufa kwa ajili ya huduma yake hiyo. Utusaidie tusiwe watu wa kujifikiria wenyewe tu kiroho, lakini tupeleke wokovu kamili kwa wale wote wanaotamani kupokea ukweli, na tufanye hayo chini ya uongozi wa Roho wako Mtakatifu. Amina. SWALI:
QUIZ - 4Mpendwa msomaji,
Ukikamilisha masomo ya mihula yote ya mfululizo kwa Warumi na kututumia majibu ya mwisho wa kila muhula, sisi tutakutumia CHETI CHA ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni. Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii: Waters of Life Internet: www.waters-of-life.net |