Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 023 (The Revelation of the Righteousness of God)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
B - Njia Mpya Ya Kuhesabiwa Haki Kwa Imani Iko Wazi Kwa Wanadamu Wote (Warumi 3:21 - 4:22)

1. Ufunuo wa njia hii mpya ya haki ya Mungu katika kifo cha Kristo cha kulipia (Warumi 3:21-26)


WARUMI 3:21-24
"21 Lakini sasa haki ya Mungu imedhihirishwa pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; 22 ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; 23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;“

Je, wewe u mwenye dhambi? Swali hilo lawalenga tu watenda dhambi, ambao wameumia kutokana na matendo waliyoyatenda, kwa sababu wametambua kwamba, damu yao imekuwa ovu, na kuishi kwao kumekuwa kubaya.

Njoo ukasikilize Injili, ambayo inasema kwako katikati ya hukumu ya Mungu kwa ulimwengu.

Paulo amewathibitishia watu wote, walio wacha Mungu na wenye dhambi, waliochaguliwa na waliopotea, waliostaarabika na watu wa kawaida, wazee na vijana, katika nguvu ya sheria ya awali na sheria tukufu kwamba, wote hao ni wenye dhambi na tabia za upotovu.

Mbarikiwe ninyi, ambao mmetambua kwamba bado hamjakamilika katika utukufu wa Mungu, jinsi wanavyopunguka watu wote. Tumepoteza sura ya Mungu tuliopewa wakati wa kuumbwa. Je, unatoa machozi kwa sababu ya ubovu wako ?

Jibu la Mungu ni nini kwa mashitaka ya sheria yake takatifu dhidi yetu? Ipi ni hukumu tukufu dhidi ya umati wa wavunja sheria waovu? Ipi ni hukumu ya haki juu yako na mimi ?

Maneno mazito yalishuka toka mbinguni na duniani katikati ya ukimya na hofu ya ulimwengu wa wafu na walio hai yakisema: Wote wamehesabiwa haki! Hapo akili yetu inainuka na kusema: „Hii haiwezekani!“ na shetani analia kwa sauti: „Hapana!“ Lakini Roho wa Mungu hukutuliza, naye anaelekeza kwake Mwana Kondoo wa Mungu aliyeadhibiwa na kupeleka mbali dhambi za ulimwengu. Mungu alimwadhibu Mwana wake badala ya watenda dhambi wote. Mungu mtakatifu alimwangamiza Mwana wake mtakatifu, ili awatakase waovu. Kristo alitengeneza madeni yetu ya kiroho kwa njia ya mateso yake ya kimwili, ili wewe uweze kuingia bure ndani ya maeneo ya Mungu. Umekuwa huru, kuokolewa na kuachiliwa. Wala dhambi, shetani au kifo haziwezi kuwa na nguvu juu yako. Umekuwa bila lawama na kukubaliwa na Mungu daima.

Je, unaamini hayo na unakubali kwa moyo wote injili ya ukombozi? Ukitazama kwenye kioo, utajiona mwenyewe kama awali, lakini utatambua jambo fulani jipya. Utaona alama za shukrani na furaha ziking’aa-ng’aa machoni pako, kwa sababu Mungu anakupenda, naye amekuweka haki kutoka kwa dhambi zako kwa njia ya kifo cha Mwana wake wa pekee. Basi, utakubali ukweli huo, au utaukataa. Kazi ya kuweka haki ulimwengu mzima ilikuwa imekamilika, wala hakuna haja kwa Kristo afe tena msalabani. Yeye aaminiye hayo ameokolewa, naye anayeshikamana na wokovu huo hataadhibiwa. Imani yako itakuwa imekuokoa.

Kweli, wote walikuwa waovu na kustahili kuadhibiwa kufa na kuangamizwa. Lakini Mungu aliwaweka haki wote, akiwapatia nafasi ya kuishi kwa ajili ya kumtumikia milele. Neema hii ya ki-ulimwengu haipatikani katika dini zozote za duniani. Inaonekana tu ndani ya Injili. Upendo wa Mungu uliwakomboa wanadamu wote; wana-sheria na waliopotea, watu wa heshima na wasioamini kitu, wana-filosofia na watu wa kawaida kabisa, wazee na watoto. Mungu amewajalia haki wote kabisa. Je, muda gani wewe utanyamaza kwa neema hiyo? Njoo basi, waite rafiki zako na kuwaeleza kwamba, mlango wa gereza lao limekuwa wazi kabisa, na kwamba wao nao wana haki ya kuwekwa huru kama kuamriwa ndani ya Injili. Basi, fanya haraka na kuwaonyesha uhuru mpya wa Mungu.

Ndugu mpendwa, umemkubali Kristo wewe binafsi pamoja na wokovu wake? Unamfahamu kwamba ndiye Mwokozi wako mwenye Rehema? Kama ni hivyo, basi nikupongeze na kukuletea shauri kwamba, umshukuru sana Yesu kwa ajili ya mateso na kifo chake kwa ajili yako, maana yeye pekee alikuokoa, kukusafisha na kukuwekea haki. Basi, umheshimu kwa njia ya imani yako, na ukaendelee kumshukuru bila kukoma. Maisha yako unayobakiza yajaae kila siku na shukrani kwa ajili ya neema yake tukufu.

SALA: Ee Bwana Yesu Kristo mpendwa, tunakushukuru na kukupenda kwa sababu umetufia msalabani. Ee Baba mwenye Rehema, tunakuabudu, kwa sababu umetusamehe dhambi zetu zote kwa njia ya kifo chake Yesu cha kulipia. Ee Roho Mtakatifu, tunakushukuru, kwa sababu umetujalia neema ya kuyatambua wazi, ukatukamilisha katika haki kamili na kututhibitishia msamaha wa uhakika. Tunakutukuza, ee Utatu Tukufu, kwa sababu umetujalia maana ya kufaa maishani mwetu. Tufundishe namna ya kukushukuru daima, na utakase maisha yetu, ili kutembea kwetu ing’ae na shukrani kwa ajili ya neema yako kuu.

SWALI:

  1. Yapi ndiyo mawazo makuu ndani ya hali yetu ya kuwekwa haki kwa imani?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 15, 2022, at 10:38 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)