d) Ushuhuda wa Yohana na wa Injili yake (Yohana 21:24–25)
Yohana 21:24
“Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.”
Hapo tunagundua kweli nne za muhimu : Huyu mwinjilisti alikuwa bado anaishi wakati injili yake ilipotolewa, tena ilijulikana sana kati ya makanisa yaliyosema kiyunani (kigriki). Alikuwa akiendelea kuwa mwanafunzi wa Yesu tangu siku za ubatizo wa Kristo hadi kupaa kwake mbinguni.
Yohana alikuwa shahidi wa macho wa Yesu Kristo. Alisikia maneno ya Yesu akayakariri, na vilevile aliandika miujiza yake. Haikuwa mshiriki wa makanisa aliyeandika injili hii, lakini Yohana mwenyewe yule mwanafunzi aliyependwa.
Labda hakuwa mkamili katika lugha ya kiyunani, na hivyo akaandikisha mawazo yake ya juu sana kwa mmoja wa wafuasi wake aliyekuwa naye na mwenye uwezo wa lugha. Maana ya maneno ni wazi, na kweli zote hazikubadilishwa. Wale waliozungusha injili hii kwa makanisa walithibitisha kwa sati moja kwamba, ushuhuda wa Yohana ilikuwa ya kuaminika kabisa. Hiyo thibitisho ilikuwa inapandwa, kwa vile injili ya Yohana ilikuwa tofauti katika mengi yaliyomo, mbali na zike injili tatu zingine. Tunafurahi sana kwa sababu injili hii kipekee kutoka kwa yule mwanafunzi mpendwa ni moja wa hazina zetu kuu za maandiko.
Watu waliotoa injili hii kwa kauli moja walithibitisha kuwepo kwa Kristo katika maisha yao, na ya kwamba wamempokea, wakawa na thibitisho ya kupata kuwa watoto wa Mungu, wakiamini ndani ya jina lake. Roho Mtakatifu aliwashukia, akaishi ndani yao na kuwawezesha kutambua roho baya. Walitofautisha ukweli mbali na uongo au namna ya kukuza mambo (kutia chumvi), wakiwa wamemzoea huyu Roho wa Faraja aongozaye ndani ya kweli zote.
Yohana 21:25
“Kuna mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.”
Kuna watu wanaofikiria kuwepo kwa injili nne ni kikwazo. Tukiongeza na barua za Paulo kama injili nyingine (alivyotamka mwenyewe), basi tungekuwa na tano, - kama vile hata ushuhuda wa Mkristo anayefuata imani kwelikweli ungeweza kuitwa “injili” pia. Mwandishi wa injili ya Yohana anakiri kwamba, alisikia maneno na habari ya matendo mengi mno ya Yesu kutoka kwa wanafunzi wake, hata yeye asingeweza kuyakusanya yote. Ukamilifu wa Mungu huishi ndani yake. Hata siku hizi yeye huishi ndani ya Kanisa lake akiliongoza kwa kufuata nyayo zake. – Kama tungechukua jukumu la kukariri kwa maandiko matendo yote ya Yesu aliyefufuka kutoka kwa wafu hadi siku ya leo, vitabu na magombo ya vitabu visingetosha kutimiza shabaha hiyo. Sisi Wakristo tutahitaji umilele kutambua ujuu, upana, kina na urefu wa upendo wa Kristo unavyofanya kazi katika historia ya binadamu.
Bwana wetu aliye hai hufanya kazi kwa njia ya Neno lake jinsi lilivyoandikwa kwenye Agano Jipya. Twajihesabu sisi kuwa wabarikiwa, kwa sababu twasikia sauti yake, twashika mawazo yake na kufuata wito wake. Yohana anaandika habari ya upendo wa Yesu Kristo, ili wote wapate kukiri, “Tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. Na toka kwa ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema juu ya neema.”
Sala: Tunakushukuru, Bwana Yesu Kristo, kwa kumjalia mtumishi wako Yohana aandike hiyo injili ya upendo wako. Unasema nasi kwa njia ya maneno yake. Twakushukuru kwa rehema yako, matamshi, matendo, maisha na kifo, hata kufufuka kwako. Wewe umetufunulia habari ya Baba, pia na kutusamehe dhambi zetu. Umetupatia maisha mapya kwa njia ya Roho yako. Amina.
Swali 134: Wale waliotoa injili ya Yohana wanashuhudia nini?