Previous Lesson -- Next Lesson
1. Kudumu ndani ya Kristo kunaleta matunda mengi (Yohana 15:1-8)
YOHANA 15:5
“Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyu huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neon lolote.”
Jinsi ilivyo heshima kuu Yesu kutujalia hivyo, kwamba tunajumlika kuwa matawi yatokanayo na moyo wake. Yeye aliumba uhai wa kiroho ndani yetu. Jinsi ilivyo na mzabibu, kwanza chipukizi ndogo hutokea, na hiki kinakua liwe mmea unaoendelea kupanuka kuwa mmea mwenye afya na refu. Ndivyo ilivyo na mwumini anayetokea na uwezo wote na vipawa vya kikristo kwa ajili ya Yesu. Si kwa ajili ya uwezo wa imani yetu, bali ni neema juu ya neema. Basi, tunawajibika kudumu ndani ya Yesu.
Ndipo, tunakuta tamko lisilo la kawaida likitokea mara 175 ndani ya Injili, ambalo ni “NDANI YAKE”, na linalopatana, neno la “NDANI YETU” (linapungua kidogo namba hiyo.) Kila Mwumini ameruhusiwa kuunganika na Yesu ndani ya Agano Mpya. Umoja huo ni imara kiasi cha kujisikia kuwa kitu kimoja na Yesu.
Bwana wetu anatuhakikishia kwamba hali ya kila mmoja wetu ya kuwa ni nafsi ya kipekee Haipotei kwa njia ya kuamini; hatuzamishwi ndani ya hali fulani ya kisirisiri. Yeye anaimarisha kutaka kwetu na kujaza maisha yetu na Roho yake. Kristo anatamani kuwaongoza mfikie hali ya kukomaa; naye aunde ndani yetu namna aliyoikusudia kwa ajili yako tangu mwanzo. Uwezo wote wa kwake na zifa zake zaingia ndani ya mioyo ya waumini. Basi, wapi tunakuta imani yetu na upendo wetu?
Ipi basi ni shabaha ya umoja wa Mwana wa Mungu na binadamu? Kwa nini Yesu alikufa msalabani, na kwa nini Roho ilimwagwa ndani ya mioyo ya waumini? Jambo gani ambalo Bwana analitazamia toka kwako? Ndiyo ni matunda ya kiroho tunayojaliwa na Mungu. Na hizo ndizo zawadi au vipawa vya kiroho: Upendo, furaha, amani, subira, wema, ufadhili, uaminifu, huruma na kujitawala.
Twahitaji kujifunza kwamba hatuwezi kujipatia jambo lenye sifa hizo peke yetu. Tunahangaika hata kutokeza na wajibu wetu sisi wenyewe, kama vile kuhema, kutembea na kusema, bila kutaja habari ya kusali, wala imani au upendo. Tunajaliwa kama waumini kufurahia uhai wa kiroho unaotokana na Yesu pekee. Inatupasa kumshukuru kwa ajili ya uhai wetu wa kiroho pamoja na nguvu tukufu anayotia ndani yetu. Nguvu hizi zote na huduma ni zawadi toka kwa Mungu. Bila yeye hatuwezi kufanya lolote.
YOHANA 15:6
“Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.”
Wewe mwenyewe unawajibika kudumu ndani ya Kristo. Upande moja tunaona kwamba, Uhai wa kiroho na kudumu ndani ya Kristo ni zawadi ya neema yake. Upande wa pili tunatambua kwamba, yule anayeachana na ushirika wa Kristo ni kama mtu anayejiua mwenyewe. Mkimbizi kama huyu atazidi kuwa mgumu moyoni mwake, na atapasa kutupwa motoni mwa ghadhabu ya Mungu. Wakati wao malaika watawakusanya wale waliomwacha Kristo na kuwatupa ndani ya giza la nje. Sauti ya onyo la dhamiri zao italia ndani yao na kuwazuia wasipate kutulia. Kwa daima watamwona Mungu katika huruma zake kwa ajili yao, lakini katika hali ya kutengwa naye. Watatambua jinsi walivyotunzwa katika upendo wake kabla ya hapo. - Basi, wakimwacha yeye, watakuwa wamemdharau Mwokozi wao; fungu lao ni kuteketea daima katika jehanamu.
YOHANA 15:7
“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”
Yeye anayedumu kukaa ndani ya Kristo, basi ataishi naye katika uhusiano wa kushirikiana mawazo na utendaji. Jinsi waishivyo wawili katika ndoa ya muda mrefu na kila mmoja kufahamu mawazo na makusudi ya mwenzake. Ndivyo ilivyo na yule ampendaye Kristo, anatambua mapenzi yake na atadumu katika upatano na Bwana wake. Kuchimba chini ndani ya Biblia kila siku kutatujaza na mapenzi yote mema, hata tutatamani kutenda yale apendayo na kuyakusudia; kwa sababu kujisikia kwa ndani yake kutakuwa kumejawa na Neno lake.
Ndipo basi hatutaomba kufuatana na mahitaji yetu ya binafsi tu, bali tutasikiliza kwa bidii kuhusu maendeleo katika ufalme wake. Tutapata kuwa waombezi wenye mzigo katika mashambulio ya kiroho. Ndipo mioyo yetu yatakuwa yanajaa sifa na shukrani, na tutamtolea Mtakatifu mambo yote yanayosumbua, mahitaji na watu wenye shida, ambao Roho Mtakatifu atatusogezea, ilo tuyatambue kwa huruma. - Yesu atenda kazi katika ulimwengu wetu kwa msingi wa sala zetu za kiimani. Anaturuhusu kushiriki katika kazi yake ya kuokoa watu. Je, unaomba? Na unaomba namna gani? Unaomba katika Roho Mtakatifu? Mapenzi ya Mungu yanayo makusudi mbalimbali. Moja ni utakaso wetu; nyingine ni kwamba Mungu anataka kuwaokoa wote na kuwafikisha kwanye utambuzi wa ukweli. Tukitembea katika mwenendo wa unyenyekevu, tunashiriki katika kutakasa jina la Mungu. Umwombe Bwana wako amwage Roho wa kusali ndani ya moyo wako, ili upate kutokeza matunda mengi na kutukuza Baba yako wa mbinguni pamoja na Kristo anayekuongoza.
YOHANA 15:8
“Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana, nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.”
Yesu anatamani wewe upate kutokeza matunda mengi. Yeye hatosheki na utakatifu kidogo katika maisha yako, wala ukivuta wachache katika watu wanaoelekea hata hivyo, wala na shukrani yako ya unyonge tu. Hapana! Anatamani kutakaswa kwako kabisa, uwe kamili, kama Baba alivyo kamili, na kwamba wote wapate kuokolewa. Usiwe ukaridhika na machache na kwa mambo yako ya binafsi tu.
SALA: Tunakupenda, Bwana Yesu, kwa sababu huoni aibu kutukubali tuwe washiriki wako. Tunaombea wokovu kwa ajili ya wote wale, uliowaita waje kwako. Tunataja majina yao mmoja mmoja mbele zako. Tunaamini umewaokoa nao wote msalabani mwako. Wokovu wao umethibitika kwa kushuka kwa Roho Mtakatifu. Jina la baba lipate kutukuzwa ndani ya Roho Mtakatifu. Pasipo wewe hatuwezi kufanya kitu.
SWALI:
- Kwa nini tu ndani ya Yesu na yeye ndani yetu?