Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 037 (Christ raises the dead and judges the world)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
A - Safari ya pili kwenda Yerusalemu (Yohana 5:1-47) -- Neno Kuu: Kutokea kwa uadui kati ya Yesu na Wayahudi

3. Kristo afufua wafu na atahukumu ulimwengu (Yohana 5:20-30)


YOHANA 5:25-26
25 „Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakaposikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. 26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.“

Yesu anaweka wazi kabisa kwamba, yeye ndiye kweli, akitamka, „Amin, amin, nawaambia:“ Yeye anatimiza maneno ya unabii yaliyohusu kuja kwake kwa undani zaidi kuliko watu wa Agano la Kale walivytambua. Yeye huisha wafu leo na kesho. Wote tumekufa dhambini na tu wachafu. Lakini Yesu ndiye aliye mtakatifu, Mwana wa Mungu mwilini, ambaye akiwa mwilini alishinda dhambi, ili na sisi tuwe washiriki wa uzima wake kiimani. Yeyote anayehimiza leo injili ya wokovu, na kuielewa vema na kushikamana na Yesu, ndiye atakayepokea uzima wa Mungu. Kuanzia siku ya ufufuo tunafahamu kwamba imani yetu ni imani ya uhai, wala si dini ya kifo na ya maangamizi. Yesu huweka Roho ya uhai wake ndani ya wale wanaomsikiliza, hata wakishindwa bado kutambua yote kamili, bali wanatamani kushika ukamilifu wa neno lake. Katika maneno yake anaumba usikivu kweli kweli, na ndani yao matamshi yake yatatenda kazi. Wafu hawawezi kufufuka au kusikia habari zao wenyewe. Ila Yesu huleta uhai kwao, na hivyo wanaweza kuhimiza mapenzi yake.

Maisha yetu ya duniani itaharibika, bali uzima halisi tuliohakikishiwa itadumu milele. Jinsi Yesu alivyotamka: „Mimi ndimi ufufuo na uzima. Aniaminiye mimi iwapo atakufa, atakuwa anaishi. Naye kila aishiye na kuniamini, hatakufa kabisa hata milele.”

Kristo aweza kutufufua kwa sababu Baba alimkabidhi ukamilifu wa uzima wa milele. Kristo afanana na chemchemi ya nguvu, na kutoka kwake inamiminika maji ya uzima bila kukoma. Toka kwake tunapokea nuru juu ya nuru, upendo juu ya upendo, ukweli juu ya ukweli. Toka kwake hautokei uharibifu wala giza, wala hamna mawazo maovu. Yeye amejaa upendo, jinsi Paulo alivyotamka: Kristo ni mwenye huruma, na yeye kama rafiki hana wivu wala hawezi kuringa; hatafuti vitu kwa ajili yake mwenyewe na hafikirii maovu juu ya wengine au kufurahia hatia. Anavumilia yote na kuwa mvumilivu kwa wote; upendo wake haukosi shabaha. Hayo yote ametukabidhi kwa njia ya Roho yake. Nasi pia tupate kuwa chemchemi za uhai!

YOHANA 5: 27-29
27 „Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini watasikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.“

Mwanadamu wa asili amekufa kwa sababu ya dhambi. Yeyote asiyejihimiza kwa upendo wa Mungu atajihukumu mwenyewe. Maneno ya Kristo ni ya kupenda, yenye nguvu na safi. Atakayemsikiliza ataishi.Pamoja na hayo maneno na mwongozo wake ndiyo taratibu bora kwa maisha yetu. Mungu amemkabidhi Kristo hukumu; yeye ndiye aliye Mtakatifu, aliyejaribiwa sawa na sisi, lakini bila dhambi. Hakuna mtu atakayekuwa na udhuru mbele ya baraza lake tukufu. Kristo anabaki kuwa wa pekee anayestahili kusimamia hukumu ya ulimwengu. Yeye aweza kuamua itakavyokuwa kwa kila mwanadamu. Huku akiabudiwa na malaika na viumbe vyote.

Ufufuo ni hakika kuwepo siku yake na kwa agizo lake Yesu. Wito wake itachoma dunia yetu; wafu huwa hawasikii miito ya kawaida. Lakini wito wa Mwana itawafanya waliokufa watetemeke. Roho za waliolala wataamshwa na kutoka kwa makaburi yao. Mwujiza juu ya miujiza, roho za wengine wataamka wakiwa hai, na wengine huko wako kama wafu. Kuna kufufuliwa mara mbili, mara moja kwa uzima na mara nyingine kwa hukumu. Saa ile itatokeza maajabu ya kushitusha: Wengine watafunikwa na giza, ambao tuliwafikiria kuwa ni taa za kung’aa. Wengine watang’aa kama jua, ambao tuliwafikiria kuwa watu wa kawaida, bila thamani.

Basi, jamaa walio wema watakaoishi mbele za Mungu, hawakuwa bora zaidi kuliko wabaya. Bali kundi hili ndiyo waliosamehewa na Kristo Yesu na kuitikia kwa kushukuru. Waliishi katika nguvu ya Injili yake. Maisha yao yalionyesha matunda yaliyozalishwa na Roho Mtakatifu. Yesu alifuta aibu zao zote kwa damu yake ya thamani. Na neema hii iliwajia kwa njia ya imani.

Hata hivyo basi, anayejifikiria kwamba kutenda kwake kumetosha mbele za Mungu, watasikia sentenso hili: “Wewe mjisifu, kwa nini ulijishughulisha kwa ajili ya ukombozi wako tu, lakini hukuwapenda wengine, hata adui zako? Kwa nini hukukubali upatanisho kamili uliokamilishwa na Msulibiwa kati yako na Mungu? Na namna gani ulikataa uhai wake wa milele kwa ajili ya utu wako? Kiburi chako kilikufanya kuchagua kifo, basi endelea bila neema iliyotolewa kwako.” - Wale waliofia katika dhambi watafufuka kwa hukumu kali na kupokea hesabu kamili ya maneno, matendo na mawazo yao. Lakini yeye aliyekubali kuvutwa na utukufu wa Kristo kwa imani ndani yake, aliburudika ndani yake na upendo kutoka kwa Kristo. Hayo yalimhimiza kwa huduma ya rehema kwa wengine, ambayo ndiyo dalili ya sifa ya uzima wa milele kwenye maisha yake ya siku hizi.

YOHANA 5:30
30 “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa msababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.”

Kristo anatimiza kazi kuu kabisa kuliko yote; yeye ndiye hakimu wa milele. Kristo alitambua mamlaka hii aliyokabidhiwa. Hata hivyo akawa mnyenyekevu, akijishusha kwenye hali ya chini kabisa ya ubinadamu akisema: “Mimi mwenyewe siwezi kutenda lolote”. Maana yake, siwezi kuhukumu, kutafakari, kupenda , hata kupumua kwa uwezo wangu. Hivyo alimrudishia Baba heshima yote.

Wakati wowote Yesu alikuwa amefungamana na Babaye. Kiungo hicho, kama ya simu, haikukatika kabisa kati ya hao wawili. Sauti ya Mungu ilimjulisha kuhusu roho za watu. Roho ya Mungu anakagua ulimwengu, na hivyo anapima na moyo wako, akifunua mawazo yako na mambo unayoyaficha mbele ya wengine. Roho huyu aliye na ndani ya Kristo atakuhukumu ilivyo sawa. Ubarikiwe ukiungama dhambi zako mbele za Mungu na kupokea msamaha kutoka kwa Msulibiwa. Jina lako litaorodheshwa kwenye kitabu cha uzima. Ndipo kwao wenye haki yeye atasema: “Njooni ninyi wabarikiwa na baba yangu, mkarithi Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu.”

Kristo aliye Ukweli mwenyewe hatasema uongo; anafahamu yaliyomo moyoni mwa mwanadamu. Anafahamu ile tabia tuliorithi toka kwa babu zetu, wala hawezi kutuhukumu haraka haraka. Huwa anangoja kwa uvumilivu toba la mwenye dhambi. Tabia yake takatifu itatenganisha wale waliopata kuwa wenye huruma kwa njia ya huruma yake, kutoka kwa wale waliokataa Roho yake na kudumu na mioyo migumu.

Kristo alionyesha upole wake pamoja na uvumilivu wake. Hakuacha kumwuliza Babaye katika mambo yote aliyohitaji. Hivyo Kristo alitimiza mapenzi ya Babaye katika maneno na matendo hata msalabani. Wakati wa kuamua hasa aliomba: “Siyo mapenzi yangu, bali ya kwako yatendeke.” Kwa hiyo atagawa hukumu za Mungu kikamilifu.

Mahusiano hayo yote kati ya Baba na Mwana yaliyohesabiwa na Mwinjilisti Yohana yanayo shabaha moja, ili kutuimarisha katika msingi wa imani juu ya umoja wa Utatu. Mamlaka ya kufufua watu kutoka kwa wafu ni ya Baba na Mwana kwa usawa. Mungu alimwonyesha matendo yake yote, wala hakuzuia lolote kwa Mwana. Sauti ya Kristo itawaita wafu; maana anayo ufunguo wa mauti na kuzimu. - Imani yetu ni siri kwa akili ya kawaida; kipekee tu, kama upendo wa Kristo unamiminwa ndani yetu kwa unyenyekevu wake, tutatambua maana ya usawa ya kwamba Mungu ni mmoja katika nafsi tatu kwa ajili ya wokovu wetu.

SWALI

  1. Uhusiano kati ya Baba na Mwana ni nini, jinsi alivyotueleza Yesu mwenyewe?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 31, 2013, at 10:10 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)