Waters of LifeBiblical Studies in Multiple Languages |
|
Home Bible Treasures Afrikaans |
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba
Previous Lesson -- Next Lesson WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
A - Ulimwengu Wote Umekaa Chini Ya Utawala Wa Yule Mwovu, Na Mungu Atahukumu Wote Kwa Uadilifu (Haki) (Warumi 1:18 - 3:20)
3. Watu wote ni wapotovu na wenye hatia ( Warumi 3:9-20)WARUMI 3:9-10 Paulo akajumlisha lalamiko lake dhidi ya wote Wayahudi na wa Mataifa katika jina la Mungu, akawahakikishia wote kwamba, hakuna aliye na upendeleo au mafao mbele za wengine. Wote wametenda dhambi, na dhambi zao ni dhahiri. Wametoka kwenye njia ya Mungu iliyonyoka, na wakawa watumwa wa dhambi, hali wamefungwa na tamaa na kujidanganya wenyewe. Paulo alijijumlisha pamoja ndani ya malalamiko hayo, akikiri kwamba, yeye naye alikuwa mwenye dhambi. Je, umewahi kuona wakati wowote jambo fulani lililokuwa la kuchukiza sana kwamba, ukapata kutapika? Makosa yako ni ya kuchukiza mno kwamba, yanafanya roho na moyo wako zitapike. Ujilinganishe mwenyewe na malalamiko ya Paulo, nawe utatambua kwamba, ni wewe mwenyewe unayeelezwa mle. WARUMI 3:11-12 Sisi sote tu wachafu mbele za utukufu wa Mungu unaon’gaa kabisa. Hakuna aliye mwenye haki ila Kristo. Akili zetu zimezungukwa na mvuke mnene, nasi hatuwezi kumwona Mungu, aliye mwimo wetu mkuu, jinsi alivyo Yeye. Hatutambui dhambi zetu zilivyo za kuchukiza kabisa. Heri watu wangekuwa na bidii ya kutafuta utukufu wa Mungu, ili wakapate kuwa wenye akili! Basi tu, kila mmoja achukua njia yake mwenyewe, akishikana na heshima yake mwenyewe, hali amefungwa na tamaa yake, akitafuta tu raha. Watu wote wamepotelewa na njia ya Bwana wao, na hakuna atembeaye katika njia iliyo ya kweli. Wewe sio bora katika tabia yako hata kidogo. Wote wamekwenda upande, wakawa watu wasioleta faida na wanakwenda kupotea. Sisi sote tu wapotovu tangu asili, na dhamiri yetu inatujua kikamilifu. WARUMI 3:13 Uchafu wa watu hujionyesha kwenye ndimi zao. Sote tu wauaji na wachinjaji, kwa sababu tunaleta uharibifu na maangamizi ya heshima, furaha na amani ya wengine kwa njia ya ndimi zetu kali; tunatia sumu kwenye tabia kwa maongo, mashtaka, matukano na maneno ya kuchekesha bila haya; pia tunalalamika dhidi ya miongozo ya Mungu. Upinzani wetu ni kama unajisi chungu midomoni mwetu. Sisi ni wenye kutokutii nidhamu ya Mungu, na hatutambui kwamba, hatustahili lolote ila mapigo mazito na hukumu ya lazima. WARUMI 3:14-17 Chuki yetu haiwezi kubadilika haraka, maana hatuwataki adui zetu, bali twataka tuondolewe na watu wagumu. Watu wanaowachukia adui zao wanamwaga mito ya damu, kwa sababu mwanadamu katika hasira yake hugeuka kuwa kama mnyama mkali. Hakuna amani ndani yetu, mbali na porojo zetu nyingi kuhusu amani. Watu wote ni wauaji tu, na mioyo yao imejaa na dharau, ukorofi na kiburi, kwa sababu hawajui kwamba, Mungu ni upendo, kweli na usafi. Walipoteza akili kuhusu ukweli, wala hawana taratibu au utulivu, lakini walijidondosha wenyewe katika hali ya hatari. WARUMI 3:18 Hao wote wasiomjua Mungu ni wapumbavu; na wote hao wasiomcha yeye wamepungukiwa na hekima, kwa sababu kicho cha Bwana ndiyo mwanzo wa hekima, na kumfahamu Aliye Mtakatifu ndiyo ufahamu wa kweli. Hali ya kutokuamini inazidi kukua siku hizi, na watu wanajiweka kana kwamba hakuna Mungu. Basi, si ajabu kwa sababu hiyo, dhambi imezidi mno, na inainua kichwa chake kwa ushupavu barabarani, ndani ya magazeti na pia mioyoni mwa watu! WARUMI 3:19-20 Watu wa Mungu wakati wa Agano la Kale wote pia ni watenda dhambi, kwa sababu sheria iliwawezesha kutambua dhambi. Ni kweli kwamba, sheria inatuahidi pamoja na baraka zote za mbinguni, ikiwa tutashika maagizo yote ya sheria, lakini hakuna mtu awezaye kutimiza sharti hii. Wakati wowote tunapojitahidi kujijenga kwa bidii yetu sisi wenyewe, mahusiano yetu maovu hutokea ndani ya damu yetu. Sisi sote tunastahili tu adhabu ya Mungu, na matendo yetu mema yote yamechafuka na choyo yetu, wala hatuwezi kumpendeza Mungu. Je, unakubaliana na miongozo hiyo ya Paulo? Rudia tena kusoma yale aliyoyaandika, ili upate kuwa mwenye busara na kuvunjika mbele za Bwana. SALA: Ee Baba wa mbinguni, tunakushukuru kwa sababu ulitujalia tumaini ndani ya Kristo kwamba, tunaweza kufikia hali ya kutokukata tamaa wala kuona yote ya maisha kuwa mabaya. Wote tu wabaya mioyoni mwetu, kwenye ndimi zetu, mikononi, miguuni na machoni; na mioyo yetu imejaa udanganyifu, chuki, tamaa mbaya na maongo. Loo, jinsi nilivyo mtu mchafu sana! Nisamehe dhambi zangu, na uchore utakatifu wako mbele za macho yangu, ili na vipande vyote vya kiburi vivunjwe ndani yangu, nami nipate kukuabudu wewe tu katika ukweli. Ee Bwana niondolee kabisa na dhambi zangu zote. Amina. SWALI:
QUIZ - 1Mpendwa Msomaji,
Ukikamilisha kujifunza vitabu vyote (au masomo yote) ya mfululizo huo juu ya Warumi na kutuma kwetu majibu yako kwa maswali mwishoni mwa kila kitabu, tutakutumia: CHETI CHA ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni. Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii: Waters of Life Internet: www.waters-of-life.net |