Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 002 (Identification and apostolic benediction)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Ufunguzi Wa Barua: Salamu, Shukrani Kwa Mungu, Na Mkazo „Haki Ya Mungu” Kama Neno Kuu La Barua Hii (Warumi 1: 1 – 17 )

a) Tambulisho na Mbaraka wa kitume (Warumi 1:1-7)


WARUMI 1:1
1 “Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu,”

Paulo alipozaliwa, alipewa jina la Sauli, yule mfalme wa kujisifu na aliyekuwa wa kabila la Benjamini. Lakini huyu Paulo, mtesi wa kanisa la kwanza aliposhuhudia utukufu wa Kristo, alitambua kwamba, yeye binafsi hafai kitu. Ndipo alipokea jina la “Paulo”, lenye maana ya “Mdogo”, naye alianza barua yake hii maarufu kwa maneno haya: Mimi Mdogo, niliye mtumwa wa Yesu Kristo.

Katika tamko hilo kwamba, yeye ni mtumwa wa Kristo, Paulo alikuwa amekubali kupoteza uhuru wake, na kujikabidhi kabisa kwa Bwana wake. Kwa hiari moja kwa moja alijimwaga na kujinyenyekeza mwenyewe na kuifia kiburi chake, na kwa sababu hiyo alishi katika nia ya roho ya Kristo, na hivyo alitimiza mapenzi ya Bwana wake kwa furaha kuu. Hii ina maana kwamba, Kristo aliye hai mwenyewe ni mwandishi wa barua hii kwa Warumi, aliyeifunua kwa mtumwa wake msikivu. Hata hivyo, ufunuo huu haikufanywa kwake Paulo dhidi ya mapenzi yake, lakini kwa kuitikia na kukubali kwake. Maana Kristo hawafanyi waumini wake kuwa watumwa bila wao kutaka, lakini anawaachia uhuru wao, waamini na wapende wenyewe, na hata kuwa huru naye. Lakini basi , wenyewe hawataki kutengwa naye, kwa sababu yeye ni chemchemi ya upendo, na kwa hiyo bora wajitumbukize kabisa ndani yake.

Paulo aliinuliwa kwenye daraja la juu na mahali pa adabu na heshima kwa njia ya unyenyekevu wake kama mtumwa wa Kristo. Bwana wake alikuwa amemwita kuwa mtume wake kwa ajili ya kuieneza ufalme wake kati ya mataifa, akimjalia na mamlaka na uwezo, jinsi kama wafalme au marais wanaowatia enzi na mamlaka mabalozi wao, kwa hali ya kwamba wao watawasiliana kila wakati na kutenda kufuatana na mapenzi yao. – Namna iyo hiyo Kristo hata leo akuita moja kwa moja ndani ya utumishi wake. Basi, fungua moyo wako kwa wito huo wa Yesu na kujikabidhi kabisa kwake bila kukawia kwa utii na unyenyekevu, ili nguvu yake iweze kutiririka kutoka kwako kwa wengine nao. - Kama Mtume wa Kristo kwa mataifa, Paulo aliweza kugeuza ulimwengu kwa barua zake. Hakuna mwingine, mbali na Kristo, aliye mkuu kuliko Paulo, aliye “Mdogo”.

Habari Njema ya Paulo, mtumwa wa Kristo, ilikuwa ni jambo gani? Ilikuwa ndiyo Injili tukufu ya Mungu. Paulo hakuja na mawazo yake ya binafsi, lakini alieleza waziwazi hiyo injili kwa dunia hii yenye taabu. Neno hilo “Injili” ilieleweka kwa watu wa Rumi wakati ule. Lilikuwa linatumika katika nyumba ya Kaisari wa Rumi wakati wa tangazo la kiofisi, kama vile amezaliwa na mtoto, au wakati alipopata ushindi juu ya adui zake. Kwa hiyo, neno hilo lilidokeza tangazo la habari njema kwa daraja la familia ya utawala. Zaidi ya hapo, Paulo alileta habari njema ya Mungu kwa ajili ya watu, akishuhudia kuwepo kwake Kristo, ushindi wake juu ya nguvu za upinzani, na matokeo ya ukombozi wake, ili wasikilizaji waweze kutakaswa, na kuingia ndani ya uadilifu (au haki) tukufu.

Mungu mtakatifu alimtenga Paulo, aliyekuwa mwanasheria, na kumwondoa kutoka katika utumwa wa yule mwovu. Alifanya hivyo apate kuwaondolea wale walioweka mabega yao chini ya nira nzito ya sheria na kushikamana na matendo mema, na awalete kwenye enzi ya neema, wasiendelee kujiokoa wenyewe kwa wenyewe, lakini wapate kuingia mbinguni kwa njia ya Kristo, ambaye pekee ni mlango unaopeleka kwa Baba yake wa mbinguni.

SALA: Ee Bwana Yesu Kristo, tunakushukuru, kwa sababu ulimwita mtumwa wako Paulo, na ukamtuma ulimwenguni, ili na sisi tupate kusikia Neno lako kwa njia yake. Utusamehe kiburi na kujiona wenyewe, utusaidie tujinyenyekeze, nasi tupate kuwa watumwa wa upendo wako. Na tuweze kutimiza mapenzi ya Rehema zako pamoja na waumini wote ulimwenguni.

SWALI:

  1. Vipi ni vyeo, ambavyo Paulo alivichukua kwa ajili yake mwenyewe, vilivyo kwenye sentenso ya kwanza ya barua yake?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 14, 2022, at 01:48 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)