Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- Romans - 003 (Identification and apostolic benediction)
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
Ufunguzi Wa Barua: Salamu, Shukrani Kwa Mungu, Na Mkazo „Haki Ya Mungu” Kama Neno Kuu La Barua Hii (Warumi 1: 1 – 17 )

a) Tambulisho na Mbaraka wa kitume (Warumi 1:1-7)


WARUMI 1:2-4
“2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu, 3 yaani habari za mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi, kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uwezo kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu,”

Jinsi mto Nile inavyolainisha na kuleta rotuba kwenye maeneo makavu na ukame na kuigeuza iweze kuzaa mazao, ndivyo na injili inavyofanya kazi ndani ya waumini na kuwawezesha kuleta matunda na kuwa na furaha. Siri kuu ya injili ndiyo kuja na kufanya kazi kwake Yesu Kristo. Unakaribishwa uamini si ndani ya kitabu, lakini ndani ya mwenye sifa kuu, asiye na muda. Maelfu ya miaka iliyopita Mungu alijulisha kwa njia ya manabii wake, kwamba mtu atazaliwa kutokana na Roho wa Mungu na bikira safi, na jina lake litakuwa Mwana pekee wa Mungu. Torati imejaa na unabii kuhusu tukio hilo. Kwa hiyo, kila nabii wa kweli anakiri ndani ya ujumbe wake kwamba, Kristo ndiye Mwana wa Mungu. Nani basi, atathubutu kumpinga Mungu mtakatifu, anapotangaza mwenyewe katika umoja wake, ya kwamba yeye ni Utatu Utakatifu, kwa kusudi la kugeuza mawazo yetu mabovu na kutuinua kwenye ufahamu mpya na wenye kina zaidi? Basi, tangu Kristo alipokuja mwilini, tunafahamu kwamba, Mungu ni Baba mwenye huruma na upendo, kwa sababu sura ya Mwana mwenye huruma alitutolea sisi wazo au fundisho mpya kuhusu Mungu – kwamba Yeye ndiye Upendo.

Haya, Mwana wa Mungu akawa mwanadamu kweli, aliyezaliwa kutokana na uzazi wa Mfalme Daudi, aliyekuwa nabii na mtunga zaburi, na aliyepokea ahadi toka kwa Mungu kwamba, mmoja katika uzazi wake atakuwa ni Mwana wa Aliye Juu (2 Samweli 7:14). Kwa kuingia kwake mwilini, huyu Kristo wa milele alijivisha mwenyewe udhaifu wa miili yetu naye akajaribiwa kwa namna zote, sawasawa na sisi.

Hata hivyo alikuwa bila dhambi, na mauti hakuweza kuwa na nguvu juu yake, kwa sababu Roho Mtakatifu, aliyeishi ndani yake pamoja na uwezo wake wote na kushinda mwili wa dhambi. Yesu alithibitisha uwezo wake kikamilifu na bila kuweza kupingwa alipoinuka kutoka kaburini, akishangilia na kuthibitisha ukuu juu ya mauti, adui wa binadamu. Kwa njia ya tukio hilo la mwujiza Mungu alithibitisha Uwana wa Yesu, akamwamuru kuketi mkono wake wa kulia kama Bwana wa kweli, ambapo sasa anatawala, jinsi Yesu alivyosema: “Enzi yote nimekabidhiwa mimi mbinguni na duniani”, naye anaishi pamoja na Baba na roho Mtakatifu; Mungu Mmoja wa milele.

Enzi wa Kristo iliruka kutoka kwa Paulo na kwenda mbio ndani ya makanisa; na enzi ya Kristo hutenda kazi hata leo ndani ya wale wanaokiri kwamba, Yeye aliyezaliwa na bikira ndiye Bwana mwenyewe aishiye milele. Tamko hilo: “Yesu Kristo Bwana wetu” ni jumlisho la Imani yetu tangu mwanzo wa Ukristo. Inachukua maana zote za siri za Utatu Utakatifu, nguvu za wokovu na tumaini lote.

SALA: Tunakuabudu, Ee Mwana wa Mungu, kwa sababu ulikuja kuingia mwilini kwa njia ya upendo wako, na ulishinda dhambi na mauti ndani ya mwili wako. Tunaomba ukubali maisha yetu ya kimauti iweze kuwa shukrani kwako; na utusafishe kwa njia ya Roho yako Mtakatifu, ili tuweze kufaa kwa ufalme wako wa upendo. Twakuomba utawale mawazo yetu, usemi wetu na mwenendo wetu, ili tuwe mashahidi waaminifu kwa ajili yako pamoja na watumwa wa uaminifu wako ndani ya taifa letu.

SWALI:

  1. Nini ni maana ya tamko kwamba, Kristo ni Mwana wa Mungu?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on November 14, 2022, at 02:03 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)