Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 13 -- Conclusion: The Law and the Gospel
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule? -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba?

Previous Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

13 - Mwisho: Sheria Na Injili



Mwalimu wa kidini siku moja alimwuliza Yesu, “Ipi ni amri kuu ndani ya Torati?” Yesu alijibu na mistari miwili kutoka kitabu cha Kumbukumbu la Torati 6:5 na Mambo ya Walawi 19:18 na kusema, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na mpende jirani yako kama nafsi yako.” Kwa maneno hayo Yesu alijumlisha Amri Kumi kwa kikamilifu. Wakati sehemu ya kwanza ya Amri Kumi inaeleza habari ya uhusiano wetu na Mungu na kumtambua kuwa Mwumbaji, Mwokozi na Mfariji wetu, sehemu ya pili inaonyesha uhusiano wetu na ndugu yetu ya kibinadamu na kutuonyesha wazi huduma yetu kwake.

Yesu hakutoa jibu la kuhangaisha kwa swali la yule mtu wa Mungu. Hakuzungumzia mambo ambayo asingeyafanya. Badala yake, alimwongoza kwa furaha kuelekea kwenye namna ya kutimiza amri kwa hakika. Alitamka kwa kifupi yale, ambayo sisi sote tunahitaji kufanya. Amri hizo mbili zaweza kujumlishwa kwenye lengo moja: Mpende Mungu na watu kwa upendo safi. Basi tujihoji wenyewe na kuona kiasi gani tunampenda Mungu na kama kweli tunawapenda rafiki zetu na hata adui zetu. Mahali kama hapo twaweza kuona vema, ni kwa kiasi gani tunatimiza Amri Kumi.


13.1 - Je, tunampenda Mungu?

Upendo kwa Mungu ndiyo Amri ya kufahamika kabisa na inayotusukuma, ili sehemu zote za muda wetu, fedha na mipango yetu zisiwe kwa ajili yetu, bali kwa Mungu, ikiwa twampenda kweli. Tulipokea roho, moyo na mwili kutoka kwake; tamaa zetu, kutaka kwetu na matumaini yetu yatengenezwe na kujazwa na upendo wake. Tumweke Mwumbaji wetu mtakatifu na Mwokozi wetu wa kutukomboa awe ndiyo shabaha ya maisha yetu. Hakuna kilicho na maana zaidi ya Yeye tu. Yeye ni Mungu mwenye wivu anayetazamia upendo wetu ambayo haikugawanyika na kamili upande wake tu. Hawezi kukubali kuishiriki na mwingine. Kwa hiyo, inatupasa kukabili swali hilo: Je, tunampenda Mungu jinsi alivyotupenda sisi na anavyoendelea kutupenda? Kiasi gani tunampenda hasa? Tunampenda kwa kujisikia, kimawazo, kwa kuzingatia Neno Lake kwa kinaganaga, ili tupate kugundua Mapenzi Yake na kujibidiisha kulitimiza kwa msaada wake? Kuwepo kwetu wote upate kumtukuza kwa neema yake ya kutujalia maisha mapya tunayoishi. Basi, tumheshimu Yeye kwa yale tunayoyatenda na yale tunayojizuia tusiyatende, tukimshukuru kwa msamaha kamili wa madhambi yetu mbalimbali kwa malipo yaliyotayarishwa bure ndani ya Kristo Yesu. Haya, tumsifu Yeye kwa ajili ya furaha, amani na Roho ya kutufariji iliyomwagwa ndani ya mioyo yetu. Hata hivyo, upendo wetu hautoshi. Hatumpendi Mungu sikuzote kwa moyo wetu wote na kwa roho yetu yote. Kwa sababu hiyo twahitaji sana msaada wa Bwana wetu hata kwa kumpenda namna inavyotupasa. Mtume Paulo atuonyesha jinsi Mungu alivyojibu maombi yetu, “Pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Warumi 5:5b). Baba yetu wa mbinguni ametujalia upendo wake mwenyewe, ili na sisi tuweze kumpenda kwa kweli. Upendo wake hujaa mioyoni mwetu jinsi Roho Mtakatifu anavyoishi ndani yetu.


13.2 - Je, tunampenda ndugu yetu kama nafsi yetu?

Roho wa upendo ndiye anayetuwezesha kuwaangalia watu wanaotuzunguka jinsi Mungu anavyowaona kwa macho yake. Kwa hiyo basi tuwashuhudie neema ya Yesu kwao, tukiwaeleza upendo wake wa kuokoa kwa wenye dhambi. Tutawaombea na kuwahudumia tunapowapenda kweli kama tunavyopenda nafsi zetu. Tunapopata njaa, twafanya yote yawezekanayo tupate chakula. Tunapopata hofu, tunajaribu kupata namna ya kutoroka. Tunapopata kuchoka, basi twatafuta kulala usingizi. Namna iyo hiyo upendo wa Kristo hutuongoza kuwalisha wenye njaa, tutawaokoa waliodhoofishwa na kutafuta faraja kwa wale waliochoka na magumu ya maisha. Yesu alimpenda kila mtu kiasi cha kujifanya mwenyewe sawa na wao. Alipata kuwa mmojawetu. Alitangulia kutuonyesha yale ambayo yeye, Mfalme wa wafalme, atakayowauliza wafuasi wake siku ile kuu ya Hukumu: „Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunwesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi“ (Mathayo 25:34-40).

Yesu nafsini mwake anaunganisha upendo wa Mungu na upendo wa binadamu. Tunapomwuliza Yesu, atatuimarisha ndani ya upendo wake, ili tuweze kumtumikia Mungu na vilevile walio na shida. Hatutamtumikia Yeye kwa ajili ya kutuokoa sisi, lakini kwa sababu tumekwisha kuokolewa tunamtumikia Mungu na watu kwa shukrani na moyo wa huruma. Asili ya upendo wetu sio haki yetu ya sisi wenyewe kwa njia ya matendo yetu mema jinsi Waislamu wanavyowaza, lakini kutokana na wokovu uliokamilishwa kwa ajili ya wote ndani ya Kristo Yesu.


13.3 - Maana ya kwenda ndani zaidi

Injili ya wokovu ndani ya Bwana wetu Yesu Kristo inatuongoza kutambua maana ya Amri za Musa iliyo ndani zaidi. Kwa maneno mengine, Amri Kumi zinatuzuia tusijiharibu wenyewe, bali tulinde heri ya furaha yetu. Yesu alimwambia yule tajiri, “Shika Amri Kumi ndipo utarithi ufalme wa milele.” Bila shaka lolote, taifa litakaloshika maagizo ya Mungu na kuishi kufuatana nazo, litaona baraka tele kwa namna zozote zile.

Tena tunapozingatia juu ya amri, itatikisa kiburi chetu na kutoa hoja juu ya kicho chetu. Hizo amri sio namna ya kutuongoza tu, bali zina shabaha ya kutufanya tujitoe kabisa kwake Mungu na kujitenga kabisa na yote ya dhambi. Mara nyingi Bwana alisema,”Mwe watakatifu, maana mimi ni mtakatifu.” Mungu kweli haridhiki na kicho cha kujifanya tu au tabia ya kidini inavyoonekana pia katika dini zingine. Badala yake, Yeye anakusudia kutugeuza kabisa na kutuponya na ukaidi wetu, ili tulingane na mfano wake katika maneno na matendo yetu. Yesu alituagiza, “Mwe wakamilifu, maana Baba yenu wa mbinguni ni mkamilifu.” Hapo alikuwa akimaanisha hasa habari ya kuwapenda adui zetu na kuwahurumia maskini, jinsi Baba yetu wa mbinguni anavyotutendea sisi.


13.4 - Je, Amri zinaweza kusababisha kuharibika kwetu?

Mtu anapoelewa matakwa ya Mungu Mtakatifu na kujaribu kuyatii kwa uaminifu, yawezekana atatetemeka na kuuliza, „Nani mwenye mwili wa kufa ataweza kupenda jinsi Mungu anavyopenda? Na ni nani aliye mtakatifu jinsi Mungu alivyo mtakatifu?“ Kweli, amri inafunua siri zetu; inaweka kioo cha utakatifu mbele ya nyuso zetu na kuonyesha wazi hali yetu yenye dhambi. Sheria inawakemea watenda dhambi wanaoridhika na hali yao, ikiwaamsha wainuke kutoka hali ya kusinzia kwao. Hukumu ya Mungu inamaanisha adhabu ya milele kwa yeyote. Fulani akifaulu kushika sheria zote na kutumbukia ndani ya jambo moja tu, amekuwa mwenye hatia juu ya sheria zote.

Fulani anapochunguza maisha yake katika nuru ya Amri Kumi, akitambua sanamu ndogo na kubwa zinazomwongoza katika maisha yake ya kila siku, anapowaza ni mara ngapi alipochokoza jina la Bwana na kutokutakasa Sabato, basi atatambua kwamba, tayari ameesha kuhukumiwa kifo cha milele na Mungu tangu muda mrefu. Kama fulani atajilinganisha na usafi wa Kristo, atavunjika kabisa, akifikia mwisho wa kufikiri kwake kwamba, kusudi la amri ni kuwaharibu watu wote.

Sheria hufunua uchafu wetu kwa kusudi la kutufikisha kwenye hali ya kuungama tena na tena. Sheria huvunja hali yetu ya kujiona tu wenye haki wenyewe pamoja na kiburi chetu. Basi, twasimama mbele za Mungu mtakatifu tukitetemeka, na tunafahamu kwamba, hatuhukumiwa kwa msingi wa haki yetu sisi wenyewe, lakini kwa ajili ya rehema YAKE kuu tu. Sisi twaweza kukubali maana ya shina la sheria tu, kwa sababu hatuwi tena chini ya sheria kama Wakristo, lakini tuko ndani ya rehema ya Yesu!

Yesu alimjia Yohana Mbatizaji na kufanya wanafunzi kutokana na wale waliokiri dhambi zao, wakabatizwa naye mtoni Yordani. Hakuchagua wanafunzi kutoka kwa wale waliodai kwamba wanashika sheria na kuringa na kicho chao. Badala yake yeye alichagua wale waliokiri makosa yao, na kujaribu kutoroka hukumu ya Mungu iliyo haki, waliokana utu wao wa kale wakaufisha ndani ya maji ya ubatizo. Yesu aliweza kuwajenga kiroho na kuwaondoa kwenye hukumu ya sheria. - Sasa, wao baada ya kuungama kweli, aliwapeleka juu kwenye milima ya Galilaya na kuwaingiza katika ushirikiano na yeye mwenyewe. Sheria ilikuwa imekamilisha lengo lake kwao. Sasa Mtoa-sheria mwenyewe alikuwa amefika na kupeleka mbali hatia zote za wafuasi wake. Yesu alitimiza madai yote ya sheria, na hilo linawaongoza wale wamfuatao Yesu wamsifu daima. Mungu yu pamoja nasi. Yule Mkamilifu aliwajia wale wasio kamili. Hakimu akawa Mwokozi aliyejishusha, ili awaokoe watenda dhambi.


13.5 - Sheria imetimizwa na Yesu

Yesu alifanya nini na Sheria (au Amri) za Musa? Kwa kikamilifu aliitimiza kwa namna, ambayo hakuna mwingine wa kuiweza. Aliendelea kuwa mnyenyekevu na kuridhika. Hakuruhusu kabisa pesa zimtawale. Siku zote alimtukuza Baba yake tu. Yesu alitamka jina la juu sana la Baba yake zaidi ya mara 168 katika maandiko ya Agano Jipya. Ndani ya Injili Baba ndiye lengo la pekee ya maisha yake. Upendo wa Baba pamoja na upendo wa Mwana zilikuwa zimeunganishwa katika umoja Yesu aliposema, “Mimi na Baba tu mmoja. Baba yu ndani yangu, na mimi ni ndani ya Baba.” Upendo wa Baba na utakatifu wake zimekuwa mwili ndani ya Yesu aliyesema, “Yeye aliyeniona mimi alimwona Baba.” Yesu alimpenda na kumtii Mama yake wakati wo wote. Alikuwa naye, jinsi Korani inavyoeleza katika Sura Maryam19:32.

Yesu aliwapenda na adui zake na hakuwasingizia, lakini aliwaambia ukweli. Yeye hakuoa jinsi Daudi au Mhamadi walivyofanya. Alikula na wenye dhambi na watoza ushuru akawaongoza kufikia ungamo. Yesu hakuwa na farasi, na alihitaji kumwomba rafiki yake amwazime punda kwa kuipanda wakati alipoingia Yerusalemu. Aliishi maisha bila kosa na takatifu katika maneno na matendo. Hakuna uongo, tamaa, au hamu ya kinyama hata ya kimawazo haikuharibu utakatifu na ukamilifu wake Yesu. Aliendelea bila dhambi, akiwapenda adui zake na watu wote kwa kujifanya mwenyewe kuwa sawa nao. Alifahamu kwamba, atatoa maisha yake kuwa malipo kwa ajili ya wengi. Kifo chake cha kuokoa watenda dhambi wote kilimaanisha utimilifu wa mwisho wa sheria. “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” (Yohana 15:13) .

Yesu alikuwa amezaliwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, ili aweze kutimiza madai yote ya sheria kwa niaba ya watu wote. Alikuwa tayari kufa kama Mwana Kondoo kamili wa Mungu. Aliondoa dhambi kikamilifu, na hivyo Yesu akawa ni utimizo wa sheria jinsi Paulo alivyoandika, “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki” (Warumi 10:4) Sheria haiwashitaki wale waliokombolewa na kifo chake badala yao, maana wamewekwa huru na nguvu ya sheria. Walikufa pamoja naye kwa upande wa sheria. Hivyo basi, kama Mwana anamweka huru mtu fulani, basi atakuwa huru kweli na ghadhabu ya Mungu mtakatifu haitamwangukia. Wafuasi wake tayari wamepewa hali ya kuwa wenye haki na watapita bila lawama kwenye hukumu ya kutisha siku ile ya mwisho. Kwa sadaka yake ya mara moja tu Kristo amewakamilisha walio wake na kuwatakasa.

Wale wanaomkataa Kristo watasimama mbele zake kwenye siku ya hukumu na kuililia milima, “tuangukie na kutufunika mbele ya uso ya Yule akaaye kwenye kiti cha enzi na kutuficha na hasira ya Mwana Kondoo” (Ufunuo 6:16 na Luka 23:30). Yeyote anayekataa kupewa haki na Mwana Kondoo wa Mungu, anaendelea kuwa chini ya sheria na kuhukumiwa na sheria hiyo.

Hata Mhamadi hakuweza kuonyesha au kuleta uhakika wowote juu ya kwenda kwenye paradiso kwa ajili yake mwenyewe wala kwa wafuasi wake, lakini alisikia hukumu ya kighadhabu ya Mungu alipokiri kwamba kila Mwislamu itampasa kupitia jehanum na kuvumilia mle kwa muda fulani katika miali ya moto ya kuunguza, hata kufuatana na matendo yake mema (Sura Maryam19:71). Hakuna tumaini la wokovu kwa ajili ya Mwislamu yeyote, maana tumaini lao limejengwa juu ya sheria, na hakuna hata mmoja aliyeweza kuishika kwa kikamilifu. Yesu bado anasema, “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36).

Sasa, habari ya Wakristo? Wao ni bora kuliko Waislamu na wengine wote wanaopotea? Wakristo wamekiri makosa yao yote na kuyasikitikia kwa uchungu. Wamevunjika kiroho na hawatasahau walikuwa wakina nani na wametenda nini. Kiburi chao kimefunikwa na damu iliyomwagika ya Mwana wa Mungu, na kwa njia hiyo wamepokea uzima wa milele kutoka kwake Yesu.


13.6 - Sheria ya Kristo ndani yetu

Bwana asifiwe! Yesu, aliye Mtimilizi wa sheria, ndiye aliyewahurumia wanafunzi wake na kuiandika sheria tukufu ndani ya roho na akili zao na kuiweka Roho yake Mtakatifu ndani ya mioyo yao. Baada ya kujaliwa haki yake, si kwamba wanaishi bila sheria, wala hawaendelei kuwa watumwa chini ya sheria. Ni Yesu mwenyewe aliyeweka taratibu mpya ndani ya mioyo ya wafuasi wake alipowaambia, “Amri mpya nawapa, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi, jinsi nilivyowapenda mimi ninyi nanyi mpendane. Kwa jambo hilo wote watafahamu kwamba ninyi ni wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.”. Ndani ya amri hiyo Yesu alijumlisha Amri Kumi zote na kuzifanya ziweze kutendeka. Ndani ya Warumi 13:10 Paulo anaandika, “Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.”

Amri ya pekee ya Yesu wakati wowote haikuwa sababu kwa wanafunzi kuogopa, maana Yesu aliwajalia nguvu ya kiroho ya kuitimiza. Paulo, aliyekuwa msomi wa Torati, alifunua ukweli huu, “Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti” (Warumi 8:2). Roho wa Mungu huleta matunda matukufu ndani ya wafuasi wa Yesu: upendo, furaha, amani, uvumilivu wa muda mrefu, upole, wema, imani, unyenyekevu na kujitawala. Nguvu ya Kristo inaonekana wazi ndani ya watoto wa nuru, “ni katika wema wote na haki na kweli” (Wagalatia 5:22 na Waefeso 5:9b). Wakristo hawawi tena chini ya sheria. Hata hivyo wao si watu bila sheria, kwa sababu sheria ya Kristo inadumu ndani yao na wakati uo huo inawapatia nguvu ya kuitimiza maishani mwao siku kwa siku.


13.7 - Anakaza jambo la kumhubiri Kristo

Upendo wa Kristo huwaongoza wale waliookolewa kwa neema wasiendelee kuishi kwa ajili yao wenyewe, lakini waonyeshe uadilifu wa Kristo waziwazi kwa watu wote. Kuwaeleza watu wote habari za Yesu, pamoja na kumsifu na kumhudumia; hayo ni matokeo ya kwanza ya upendo wa Yesu ndani yetu. Wanafunzi wake tayari wameenda kote ulimwenguni wakihubiri amri na injili. Amri zinahakikisha hali za watu za kimakosa inayostahili hukumu na kupotea, ambapo Injili inamonyesha wazi Yesu mbele za macho ya mioyo yetu. Injili inatuhakikishia kwamba, neema ya Yesu hutuokoa na hukumu ya sheria. Yesu alitimiza kikamilifu madai yote ya haki tukufu kwa niaba yetu, na akatujalia uadilifu wake mwenyewe kutokana na huruma yake usio na mwisho. Kwa sababu hiyo, tunawaendea wanaopotea na wakata tamaa tukiwa na moyo wa shukrani na kuwaonyesha habari ya tumaini isioweza kukoma. Tunawaendea hata Waislamu hata na Wayahudi na kuwatia moyo, „Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu“ (Nehemia 8:10). Tambueni na kufahamu kwamba, wokovu wenu uko tayari hata kwa ajili yenu! Mkaipokee tu! Hamtaendelea tena katika hali ya kukata tamaa kama wale wanaoishi chini ya lawama ya sheria, hata jehanumu haiwezi kuwa na nguvu juu ya kila mmoja anaye

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:54 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)