Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 10 -- Eighth Commandment: Do Not Steal
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule? -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba?

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

10 - Amri Ya Nane: Usiibe



KUTOKA 20:15
“Usiibe”


10.1 - Mali ni ya nani? au: Nani ni mwenye mali?

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi na yote yaliyomo. Yeye peke yake ni mwenye yote, ardhi, maji, hewa na moto; pia na mimea, wanyama na sisi nasi pia tu mali yake. Sisi sote tu mali ya Mungu. Hatukuumbwa kwa bahati mbaya, lakini kwa rehema ya Mungu; mawazo na enzi yake zinathibitika ndani ya kila kiumbe. Mungu ndiye mwenye ulimwengu wote. Yeye pekee ni mwenye vitu vyote, hata dhahabu na fedha. Sisi tu mawakili ya yale aliyotukabidhi. Nasi tunawajibika kwa yote aliyotupatia. Muda wetu, afya, nguvu, fedha, utajiri, yote hayo si mali yetu, lakini yote ni yake. Je, unakubali?

Miaka mia moja nyuma maelezo ya watu wasioamini habari ya Mungu(atheists) wanaokataa kuwepo kwa ulimwengu wa roho walipata kuwa mbele. Walikubali tu mambo yanayoonekana, ambao walidai kwamba yote yalijitokeza peke yake. Mungu kwao hakuweza kufikiriwa. Ndiyo sababu wakomunisti wanadai kwamba, watu wanaweza kumiliki ulimwengu, wala si Mungu. Chama kilichotawala kilikamata uongozi juu ya jumla ya mali yote na waliokuwa nayo watu; na kwa kulikubali chama hiki walimaanisha kushirikiana katika mali hiyo yote. Lakini watu mmoja mmoja hawakuridhika na mawazo hayo ya mali ya wote kwa usawa, basi wakapunguza kazi chini ya uwezo wao, na hivyo kufuja fedha na mali ya nchi kadiri walivyoweza. Ndiyo sababu kwamba Uchina na nchi zingine za kikomunisti waliendelea kutenda kazi zisizokuwa za kisosialisti na kazi za binafsi. Kupungua kwa ongezeko la utoaji wa viwanda kulifunua kwamba, hakuumbwa kwa kazi yoyote ya mipango ya kisosialisti. Tuliumbwa kwa kutazamia maisha ya kuwajibika kabisa tangu mwanzo. Mwanadamu anahitaji kujisukuma mwenyewe katika utendaji wake, sio kwa kulazimishwa. Mawazo ya kujitawala wenyewe yalipoendelezwa, mipango ya kikomunisti yalikunjamana.

Katika nchi za Magharibi taratibu ya ukapitalisti (kutegemea mali ya kila mtu) ina maana kwamba, kila mtu ni mtawala wa muda na mali yake. Utaratibu wa kidemokrasia ya kisosialisti unajaribu kuhakikisha sehemu ndogo kwa ajili ya maskini kutoka katika keki kubwa ya mali, ambayo watajiri wanaigawa kati yao wenyewe. Lo, hao wenye mamilioni wangetambua wajibu wao mbele za Mungu na kuungama mbele zake! Ndipo wangewatambua vema walio na haja na kuwafikiria wadogo na kjihusisha zaidi na haja zao.

Kwa kweli, ukomunisti na ukapitalisti zinazo shabaha za kufanana. Zote mbili zataka kutawala mali yote na nguvu zote. Zinatofautiana tu katika njia zinazofuatwa kwa kufikia utawala juu ya utajiri. Kutwaa mali katika nchi za kisosialisti kwa vyovyote ni unyang’anyi. Lakini njia za kupata faida yote iwezekanavyo kutoka kwa maskini zinazotendeka katika nchi za kikapitalisti ni namna za ujanja za kudanganya, inayosaidiwa na vyombo vya mawasiliano ya kisasa.

Mkristo, kwa vyovyote, angekumbuka kwamba mali yote ni ya Mwumbaji Sisi sio wamilikaji au mabwana wa kujitegemea, bali ni mawakili wanyenyekevu tu. Hakuna kilicho cha kwetu pekee. Tulicho nacho si kitu, ila ni baraka kutoka kwa Mungu, nasi tunawajibika kutoa mahesabu juu ya namna tunavyotumia fedha zetu, muda na juhudi zetu. Angalia sana unalolitenda na unalolitumia kwa ajili yako binafsi!


10.2 - Kumpenda Mungu na kutamani pesa

Yesu atuonya, „Hakuna awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu …….Hamwezi kumtumikia Mungu na mali“ (Mathayo 6:24). Mkristo hawezi kufanya kana kwamba yeye ni mtawala wa pesa zake bila kuiweka tayari kwa matumizi ya Mungu; bila kufanya hivyo angekuwa kama mwizi anayemnyang’anya Bwana wake. Kwa sababu hiyo, njia zetu za kutumia fedha zinabadilika kabisa mara tunapokuwa Wakristo. Wakristo tajiri wasingepanga na kuishi kwa ajili yao wenyewe, lakini kwa vyovyote kumwuliza Mungu analohitaji wafanye na fedha alizowakabidhi. Nchi zinazoendelea, ambazo zina viwanda vichache, bado zinahitaji kumulikiwa kiroho kwanza. Imani ndani ya Mungu wa Utatu inaimarisha sana hali ya kuwajibika, bidii na shabaha za kujitolea. Uhusiano wa karibu na Yesu tu inaweza kuwazuia watu wasipate kutumia rushwa au kufanya kazi kwa ajili ya familia zao tu bila kuona na kusikia haja za wengine. Ikiwa malengo yao hayatabadilika, uvivu, wezi na ukatili zitaendelea kutawala. Kristo tu ndiye tumaini la pekee kwa dunia yetu!

Biblia lasema wazi, „Usiibe“, na kwa njia hiyo inathibitisha mali ya binafsi. Basi tusiwe na wivu kwa ajili ya mali ya mwingine, maana hata wajibu wake wa milele inazidi kuwa kubwa kwa sababu ya ongezeko la mali yake. Yesu alieleza agizo hilo aliposema, ”Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu” (Mathayo 19:24). Mali ya watajiri haiwezi kuruhusu kuwa ni haki kumwibia, hata hivyo ni kwamba, kila mtu anayeiba anabeba thawabu ya haki mbele za Mungu yeye peke yake.

Haya, chini sana ndani yetu tunasikia kwamba, tusingechukua chochote kisicho chetu. Dhamiri zetu ni nyepesi kuona na kutuonya tusiibe chochote, kikubwa au kidogo. Tungejipima wenyewe kwa uangalifu na kutazama kama tunacho chote kisicho cha kwetu. Bwana kwa vyovyote atatusaidia kutambua yaliyo ya kwetu na yaliyo mali ya mtu mwingine; ukimwomba atakusaidia kukumbuka chochote kile kisicho cha kwako. Pia tunatakiwa kumwuliza Yesu atujalie ujasiri wa kurudisha kisicho chetu mara moja. Tunahitaji kumwuliza Mungu na wale wenye mali ile tunayorudisha watusamehe ukosefu wetu. Vitu vilivyoibiwa vitadhuru dhamiri yetu, pia na kuharibu uhusiano wetu na Yesu. Katika mkutano wa uinjilisti mahali fulani Afrika, watu walitiwa moyo warudishe vyote walivyoiba. Hapo hapo watu wa polisi waliokuwapo wakacheka na kuangaliana kwa kuchomwa mioyo, maana walijua kwamba kila mmojawao aliwahi kuiba. – Mambo kama hayo hutokea kokote, na ni neema ya pekee ya Mungu kama tunatambua dhambi zetu, kuzijutia na kuzichukia, ndipo kuziungama kwa moyo, kuzikiri hata na kuzilipia. Kwa vyovyote umwelekee Yesu, naye atakusaidia kutengeneza uharibifu ambayo uliusababisha. Rudisha chohcote kile kisicho cha kwako upesi!


10.3 - Kuiba kwa kisasa (kuiba siku hizi)

Tujiulize sisi wenyewe, “Siku hizi kuiba ni nini?” Sio jambo hilo tu la kuchukua vitu visivyo vya kwetu, lakini pia mambo kama kudanganya fedha kwa siri, kuahirisha au kuchelewesha mambo au kutumia vibaya muda wa kazi. Kila namna ya udanganyifu ni kuiba. Kuuza vitu vyenye kasoro kwa bei ndogo au kwa kuzidisha bei ni kumdanganya mteja. Mara kwa mara thamani ya rasilimali hailingani na bei inayoonyeshwa. Kutoa maelezo ya uongo kwa ofisi ya fedha pia ni namna ya kuiba. Kwa kweli kuna njia nyingi za kudanganya kazini au katika maelezo ya biashara. Ukipuuza kuishi mbele za Mungu mtakatifu, basi utakuwa hatarini kudanganya na kutenda dhambi juu Yake na juu ya watu wake.

Zoezi hilo la dhamiri pia lafaa kwa watu wenye kumiliki ardhi, viongozi katika biashara na watu wengine katika nafasi za juu wanapotumia nafasi zao mbele za wakubwa wao, wakidai kuchapa kazi kwa bidii bila kulipa mishahara inayolingana. Pia ni wizi kwa Benki au kwa watu binafsi kudai riba ya juu. Lakini ni dhambi pia kwa mtu kutaka mkopo wakati anapofahamu kwamba, hawezi kuirudisha. Kuna njia nyingi sana za kuiba, kote kibinafsi na katika umilikaji wa raia wote; na tusipozoeza dhamiri zetu katika unyofu wa Roho Mtakatifu, tutakuwa hatarini kupoteza haki zetu na wokovu kwa tamaa ya fedha na wivu ya mali. Paulo afundisha wazi, “Wala wevi, wala watamanio, ……hawatarithi ufalme wa Mungu” (I.Wakorintho 6.10)

Katika mazingira yetu ya kisasa kuiba kunatendeka kwa namna mbalimbali. Watu wengine watatumia simu kazini kwa ajili ya kuongea mambo ya binafsi. Wengine huchukua vitu vinavyoonekana madukani au sokoni bila kulipia. Wengine tena wanafungua magari ya watu na kuyapeleka mafichoni. Kuna wengine tena wanaogawa madawa ya kulevya bure, ili kuwafanya wanaovitumia wapate kujifunga kwa lazima, baada ya hapo wanawalazimisha kununua kwake madawa hayo, ili kutimiza uzoevu wao. Wanawafanya hao wazoefu waibe au kutenda maovu mengine , ili kupate hela za kutosha kwa uzoefu wao. Kuingilia mashine za kuhesabu (computer) za watu au kunakili .maandiko kadhaa bila kulipia pia ni namna ya wizi wa kisasa inayodhuru dhamiri za wengi.

Tusipokubali kupokea moyo mpya kutoka kwa Yesu tunajifungua wenyewe wazi kwa majaribu mengi. Lazima tuhakikishe kwamba, tusikubali tabia ya kufanya pesa kuwa shabaha yetu ya kwanza maishani, au tutapata kuwa watu wa kufikiria mambo ya dunia tu na kupoteza furaha ndani ya Bwana. Usisahau ya kwamba uchoyo na wivu bado ni asili ya maovu yote. Yeyote aangaliaye habari ya pesa tu, anabadilisha nia ya maisha yake. Moyo wake utazidi kuwa mgumu, upendo wake utapoa, na kila atendalo ina shabahaa moja tu katika tamaa ya pesa. Hiyo pesa itakuwa ni kiini cha maisha yake wala Mungu ameondolewa mahali pake. Yesu alipendelea kuishi maisha ya umaskini, kuliko kuangukia katika hatari za utajiri. Hakuwa na mahali pa kulaza kichwa chake. Yuda, aliyemsaliti Bwana wetu, alikuwa ni mwizi aliyeshika mfuko wa fedha (Yohana 12:6) na mwishowe alijinyonga mwenyewe.

Paulo alifanya kazi kwa bidii kwa mikono yake mwenyewe. Hakutaka kutwisha wengine mzigo wa kumtunza. Hakujipatia tu fedha kwa matumizi ya binafsi, lakini aliwasaidia na wengine, ili Injili aliyoihubiri isifunikwe.


10.4 - Kazi na Sadaka

Waumini wapya wengi wanatakiwa kubadilisha hali yao kuhusu fedha na kufanya kazi kwa uaminifu, kwa sababu kuomba au kutegemea msaada wa wengine sio heshima, wala haihakikishi kupata ridhiki kwa kutegemewa. Ombi la nne katika Sala ya Bwana ni „Utupe leo ridhiki yetu.“ Hii ina maana kwamba, tunaomba kwa tegemeo kuu kwa Baba yetu wa mbinguni atupatie kazi ya kufaa na kutubariki na afya na uvumilivu kuifanya hiyo kazi, bila kujali magumu mengi tunayoweza kukabili kazini.

Kama kweli tunaishi chini ya uongozi wa Mungu na kufanya kazi kwa bidii, hatutakuwa na haja ya kuiba au kuwategemea wengine, kwa sababu tutakuwa chini ya baraka ya Mungu kwa kuweza kuendesha familia zetu, na pamoja na hayo kuwasaidia wenye haja, na pia kushiriki kwa matoleo yetu tunayoyaombea katika kazi za Bwana (kanisani) vilevile. Ni yenye baraka zaidi kutoa kuliko kupokea (Matendo ya Mitume 20:35, Waefeso 4:28; I.Wathessalonike 4:11)

Yesu siku moja alikutana na kijana tajiri, aliyekuwa mcha Mungu na kuzishika Amri Kumi kwa uaminifu. Bwana alimpenda na kutaka kumweka huru na vifungu vyake vilivyojificha. Basi akamwambia, „Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni“ (Mathayo 19:21). Huyu kijana alihuzunika kwa kusikia hayo, maana alikuwa na mali nyingi. Alimwacha Yesu aende zake. Pesa kwake ilikuwa na maana zaidi kuliko Mwana wa Mungu. – Mara kwa mara tunatakiwa kujipima wenyewe, ili tuone kama kumfuata Yesu kweli ndiyo kipaombele kwetu, au kama tunategemea yale tuliyo nayo pamoja na akiba yetu ndani ya Benki (Marko 10:19 na Luka 18:10). Yesu anataka kutuweka huru na hali ya kutegemea fedha zetu. Twahitaji kumwelekea Yeye na kufanya sadaka kuwa ni shabaha yetu ya kwanza maishani. Jinsi Bwana wetu alivyojitoa mwenyewe kuwa malipo kwa ajili ya wengi, sisi nasi twahitaji kuwasaidia wengine kwa furaha katika njia nyingi za maisha. Mungu ataka tuwe huru kabisa na tegemeo la fedha na kuimarisha tegemeo letu ndani Yake tu.

Wale washiriki wa kanisa la kwanza Yerusalemu walipendana katika ushirikiano wa kiroho, huku wakingojea kwa shauku kurudi kwa Bwana Yesu Kristo kwa mara ya pili. Waliuza mali zao na kuishi wote pamoja kutokana na mapato hayo. Kwa hiari walihudumiana katika upendo wao kwa wao. Sio kama ukomunisti, hakuna aliyelazimishwa kushirikisha mali yake. Hata hivyo Kanisa la kwanza la Wakristo hawakuweza kuendeleza taratibu hiyo ya kisosialisti kwa muda mrefu. Wakristo wengi wao wakaingia umaskini kwa vile Kristo hakurudi mapema walivyotazamia. Wakati njaa ilipofunika nchi waliteseka vibaya sana. Hadi wakati ule, Paulo alikuwa amekusanya matolea ya kiasi cha ajabu kutoka kwa makanisa ya maeneo, ambayo sasa ni Ugriki na Uturki, akayapeleka hayo kwa Kanisa la kwanza kule Yerusalemu.

Paulo alibadilisha maana na thamani ya kazi alipotamka, „Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu.“ (Wakolosai 3:23). Tangu hapo kila kazi ya heshima inahesabiwa kuwa namna ya kumwabudu Mungu. Hivyo, mama wa nyumbani anapowatunza watoto wake, au kama mfanya kazi wa mji anayefagia barabara, au kama mchungaji anayehubiri Jumapili, basi kila kazi njema ni huduma ya moja kwa moja kwake Mungu. Tunatakiwa kujipima wenyewe na kuuliza, „Tunamtumikia nani? Twajitumikia wenyewe, familia zetu, watajiri wenye kutuajiri, serikali yetu, au tunamwishia Mungu? Kuomba na kufanya kazi pamoja ndiyo ujumla wa maisha ya Mkristo.


10.5 - Uislamu na mali ya Mtu binafsi

Uislamu unathibitisha kwamba, Mwumbaji ni mwenye mali yote aliyoiumba. Pia unakubali umilikiaji wa binafsi ya mali, ambayo Mungu amemjalia kuwa nayo. Mali ni zawadi ya Mungu kwa yeyote anayesali kwa taratibu na kuishi kufuatana na sheria ya kiislamu. Mtu wa Mashariki ya Kati (Oriental) haishi kwanza katika hali ya kujitegemea peke yake kwa kujitenga na wengine, bali anakuwa mshiriki katika ukoo na kabila lake. Mali kubwa kama visima vya mafuta, visima vya maji zinatawaliwa na kusimamiwa na kabila tangu vizazi. Familia imekuwa ni mahali pa salama, ambapo wazee, wagonjwa na wenye vilema, hata na wahalifu wanaweza kujikinga. Hadi juzijuzi hapakuwa na haja sana katika nchi za Mashariki ya Kati kwa ajili ya usalama wa kisosialisti (ya serikali) au za bima za maisha, ila pamoja na mabadiliko ya teknologia ya kisasa wafanya kazi mijini wakawa na hali ya upweke mbali na familia zao, na vyama vya ufadhili vilianza kuhitajika.

Muskiti na mashirika ya kiislamu zinasimamiwa kifedha kutokana na kodi za kidini (zakat) na matoleo ya hiari (sadaqa). Uwezo huo wa kifedha inatawaliwa na kutumika bila uangalizi wa juu toka serikalini, kwa sababu zinatolewa kwa nguvu za taratibu za kidini kana kwamba matoleo hayo yanatengeneza njia kwa Mwislamu kuingia katika paradiso. Mtu akijenga muskiti hapo duniani, anategemea kujaliwa jengo la ngome kule paradiso.

Uislamu ulipoanza mara ya kwanza kugawa nyara za.thamani za vita kwa askari waliokuwa Waislamu, ilikuwa ni njia ya hakika ya kuwavuta watu wasioamini na waliokuwa bado hawajaamua kukubali Uislamu. Mhamadi kwa kusudi kabisa alifuata njia hiyo, hata kwa adui, alivyosema, „ili mioyo yao ipate kuzoea Uislamu“. Ikiwa mpagani hakukubali Uislamu, alitakiwa kuuawa au kufungwa utumwani. Kufuatana na Kurani na sheria ya kiislamu, hao watumwa walikuwa ni mali za Waislamu, na wasichana watumwa wenye umri wa kuolewa walikuwa mikononi mwa mabwana wao, na wazazi wa msichana huyu walilazimika kukubali hayo. Biashara ya utumwa ilistawi kwa muda mrefu ndani ya ulimwengu wa kiislamu. Kule Marekani walipatwa na vita ya wenyeji, ili kukomesha biashara ya utumwa kule.


10.6 - Adhabu kali katika Sharia kwa ajili ya wezi

Uislamu unapasa kusimamia maadhabu mazito kwa ajili ya wizi: Mkono wa kulia hukatwa anapokamatwa akiiba zaidi ya kiasi fulani kwa mara ya kwanza, na mguu wake wa kushoto huondolewa kwa kosa mara ya pili. Ukali huo ulipunguza uwizi katika nchi za kiislamu kwa kiasi fulani. Hata hivyo, hofu ndiyo zuio kuu kwa kushika hiyo amri, na kuna kuiba mara nyingi bado nchini Iran, Sudani na nchi zingine za kiislamu, ambapo mara kwa mara mikono na miguu hukatwa hadharani. Khomeini alitoa agizo kukata mkono wa mwizi bila dawa ya kuzuia maumivu. Sheria hii ya kiislamu nchini Sudan ilifutwa kwa miaka minne. Hapo watu mia moja wenye kukatwa mikono waliunda shirika kwa watu waliotiwa kilema kutokana na sheria. Walidai kwa serikali kuwalipa ukombozi na ujira wa uzeeni, kwa sababu mikono yao ilikuwa imekatwa kutokana na sheria, ambayo haikuwepo tena. Ndani ya kundi hilo walikuwa na watu kama 24 wenye mguu moja tu kwa vile waliiba mara ya pili. Ndani ya gazeti la „Sudan Now“ kulitokea picha ya watu hao wakiinua baki ya mikono yao iliyokatwa bila huruma.

Adhabu kali kufuatana na Sharia haiwapi wezi nia zao kuwa bora au hata kumbadilisha mtu, lakini kwa kweli zinamfanya mtu asiweze kufanya kazi na kumwonyesha wakati wowote kuwa na aibu hadharani. – Basi fikiria yatakayotokea katika nchi zote za dunia, kama kila mmoja anayeiba kitu cha thamani angekatwa mkono wake wa kulia. Watu wangapi wangebakia wakiwa na mikono miwili? Kweli, Sharia haifai siku hizi.


10.7 - Jinsi gani Yesu na Wafuasi wake walishusha moyo wa kuiba?

Yesu alitolea njia bora ya kushinda uwizi. Yeye hakufuta maadhabu ya mataifa dhidi ya uwizi. Badala yake, yeye mwenyewe alijitwisha adhabu ya hukumu ya milele, ili aweze kulipia kwa kila mmoja aliyeiba. Kutokana na shukrani zetu kwa ajili ya kuteseka kwake na sadaka yake sisi hatutagusa kitu chochote kisicho cha kwetu.

Roho wa ukweli ilituweka huru kutokana na roho ya wizi. Yeye huimarisha moyo wetu uliofanywa upya, ili tumtegemee Mungu, Baba yetu tuweze kumwuliza atupatie kazi ya kufaa, ili tuweze kupokea mshahara kwa ajili ya chakula chetu cha kila siku, jinsi tunavyoomba katika Sala ya Bwana. Hatujitumbukizi ndani ya mahangaiko, kwa sababu tuna hakika kwamba Baba yetu wa mbinguni atutunza binafsi, wala hawezi kutusahau. Hivyo mstari unaofuata inafaa sana kwa wafuasi wa Kristo: “Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji” (Waefeso 4:28).

Yesu aliwajalia wafuasi wake na moyo mpya, ambamo ndani yake maisha ya maana haikuangaliwa kwa namna ya pesa au mali nyingi, lakini katika maisha ya kiroho yanayoshikanishwa na upendo na shukrani. Bwana wetu alituweka huru na uchoyo na wivu. Tena anatufundisha kwamba, kila mtajiri anakabili majaribu mazito yanayotaka kumtawala. Basi, inatupasa kufikiria tena namna ya matumizi yetu na kutoa mahesabu kwa Mungu na mbele zetu wenyewe kuhusu kila senti tuliotumia. Tu mawakili juu ya yote aliyetupatia.

Mkristo mwaminifu huwatazama maskini kwa upendo na huruma na kupanga namna ya kuwasaidia, ili waweze kukuza na wajibiko kwa ajili yao wenyewe, hatimaye waweze kufanya kazi kwa uaminifu na kwa bidii.. Tunatakiwa kugundua njia za hekima kuwasaidia wenye haja, ili waweze kujisaidia wenyewe, isipokuwa wale wasioweza kufanya kazi. Kila mshiriki wa Kanisa anaitwa pia kushiriki katika juhudi hizo. “Maana ajuaye kutenda mema, asiitende, anafanya kosa.”

Upendo kwake Mungu ndiyo mwongozo wa kutawala maishani mwa kila Mkristo, wala si hofu ya kuadhibiwa. Ndiyo ile sadaka kuu iliyotolewa msalabani kule Golgotha, wala si matendo yetu mema yanayofuta dhambi zetu. Tunamshukuru Yesu kututia moyo tuwe na maisha ya uaminifu, kwa kuridhika na ya bidii. Badala ya kusimamisha amri nyingi kuhusu mali za binafsi au za serikali, au hata za kudai kodi kubwa, Yesu hubadilisha mioyo na nia za wale wamfuatao kufuatana na shabaha zake, ambazo zaweza kugeuza mazingira ya umri zozote na nyakati zote. “Kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi” (Mathayo 20:28).

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:55 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)