Waters of Life

Biblical Studies in Multiple Languages

Search in "Kiswahili":
Home -- Kiswahili -- John - 012 (The Sanhedrin questions the Baptist)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 1 - Kuangaza kwa nuru tukufu ya Mungu (Yohana 1:1 - 4:54)
B - Kristo anaongoza wanafunzi wake kutoka hali ya kutubu kwenye furaha ya karamu ya arusi (Yohana 1:19 - 2:12)

1. Utume kutoka kwa baraza kuu (iitwayo Sanhedrin) unamhoji Mbatizaji (Yohana 1:19-28)


YOHANA 1: 22-24
22 “Wakamwuliza, Wewe ni nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? 23 Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani: Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile nabii Isaya alivyosema. 24 Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo.”

Wale wajumbe walichoma maswali yao makali kama mishale ya moto kumwelekea Mbatizaji. Hayo maswali yalihusikana na mafundisho ya uongo yaliyotarajiwa kutokea kabla ya kuja kwa Masihi wa kweli. Lakini baada ya Yohana kukataa kwamba yeye ni Masihi au Eliya au nabii aliyesemwa na Musa, umaarufu wake ulipotea wala hakuwa na hatari kwa maoni yao. Hata hivyo waliendelea kusisitiza kumwuliza, yeye ni nani na ni nani aliyempatia ujumbe wake. Shabaha yao ilikuwa, wasirudi barazani bila kugundua ukweli wa mambo na malengo yake Yohana.

Maswali hayakuwa na uhusiano wowote na unabii wa Isaya (Isaya 40:3), lakini Roho alimwongoza Mbatizaji kwa ujumbe huo. Alijieleza kuwa, yeye ni sauti inayolia jangwani itengenezeni njia ya Bwana. Kama asingewapa dhihirisho fulani kutoka kwa maandiko matakatifu, wangemlaumu kwamba anafanya kazi kwa mamlaka yake na kuunda mafunuo yake mwenyewe. Wangemhukumu kwamba anafukuru. Kwa hiyo Yohana alinyenyekea na kuchukua nafasi ya mdogo kuliko wote katika Agano la Kale, akisisitiza kuwa yeye si kitu ila ni sauti iliayo nyikani.

Sote tunaishi katika jangwa la ulimwengu wetu. Tumezungukwa na hali ngumu na kilio. Lakini Mungu hataacha dunia ya umaskini na watu wenye kurusha ndani yake bila kuleta msaidizi. Anakuja ulimwenguni kwa wanadamu ili kuwaokoa. Hatua hii kuu kutoka mbinguni hadi duniani ni neema ya ajabu. Mtakatifu hatatumaliza kama vile tunavyostahili, lakini anatutafuta sisi na wenzetu waliopotea. Upendo wake ni kuu kuliko mawazo yetu yanavyoweza kufikiria. Wokovu wake wa ajabu unabadilisha jangwa kuwa mabustani yaliojaa na majani mabichi.

Mbatizaji alielewa kupitia kwa Roho Mtakatifu kwamba Mungu ndani ya Kristo anakuja katika dunia yetu. Kwa hiyo alianza kuwaita watu wajirudi na kujitayarisha kwa kumkaribisha yule ajaye. Juhudi zake za kutengeneza mapito ya Kristo ilimfanya kuwa sauti katika jangwa la dunia yetu. Hakujitaja kuwa ni nabii au mjumbe, lakini sauti tu. Lakini sauti hii ilithibitishwa na Mungu bila kuwaacha watu kustarehe, bali wahukumiwe na dhamiri zao kwa sababu ya dhambi zao.

Sauti hii ya jangwani ilikuwa inasema nini? Lengo lenyewe la ujumbe huu ilikuwa: Inukeni, mpate kutambua kwamba, ufalme wa mbinguni umekaribia! Tengenezeni maisha yenu! Mungu ni mtakatifu na atakuhukumu. Kwa uongo wote, wizi, tabia mbaya na mambo machafu Mungu atakuita utoe hesabu na kwa makosa upate sentenso ya jehanum. Mungu hawezi kutokujali makosa yako. Mwovu atadhihirishwa na dhambi zake zote. Na mtu anayejidhania tu kuwa mwema, hatakuwa bora kuliko mtu mwovu. Maana hakuna mtu aliye bila lawama mbele za Mungu.

Ugumu wa madai ya Mbatizaji uliwaelekeza watu wajikague wenyewe. Wajitambue kuwa wenye ukorofi, wanaohitaji kufuta kiburi na kuacha kuringa na kubadilisha mawazo yao. Ndugu, unajihesabu kuwa mwema na anayekubaliwa kuwa mwadilifu? Uwe mwaminifu na kutubu dhambi zako. Kama umedanganya mtu hata kitu kidogo, mrudishie bila kukawia. Ufe kwa kiburi chako na kumwishia Mungu. Nyoosha yalio kombo katika mwenendo wako. Inama chini mbele za Mungu kwa sababu ya makosa yako.

Wengi katika wajumbe wale walikuwa ni Mafarisayo. Walipata kuchokozwa kwa sababu ya unyofu wa Mbatizaji. Walijihesabu kuwa wenye haki, wa dini na wema. Watu wa tabia nzuri lakini walikuwa wanajidanganya wenyewe, walijifanya wazuri. Kwa uangalifu sana walijitahidi kushika kila agizo la sheria. Lakini walijidanganya wenyewe. Walijifanya tu kuwa wasafi, lakini ndani yao walipotoka na kujaa picha za maovu mawazoni mwao. Mioyo yao ilijaa kisasi, kama kioto cha nyoka.

Nyuso zao zenye kujaa ukali hazikumwogofya Yohana, asiwakemee na kuwakumbusha kwamba wote tunahitaji sana kumrudia Mungu, ili kujitayarisha tutengeneze njia ya Mungu anayetujia hivi karibuni.

SALA: Bwana, unajua moyo wangu, mambo yangu yaliyopita na dhambi zangu. Ninaona haya mbele zako kwa sababu ya makosa yangu, yale ya wazi na yaliyofichwa. Nakiri maovu yangu yote mbele yako na kuomba nsamaha. Usinifukuze usoni mwako. Nisaidie kurudisha chochote nilichomdanganya mwenzangu, pia niweze kuomba radhi kwa yeyote niliyemwumiza kwa usemi wangu. Vunja kiburi changu, unitakase na makosa yangu yote kwa neema yako, ewe mwenye huruma kwa wanaohitaji neema.

SWALI:

  1. Ni jinsi gani Mbatizaji alivyowaita watu kutengeneza njia ya Bwana?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on July 24, 2013, at 07:52 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)