Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 077 (Jesus enters Jerusalem)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 3 - Nuru yang’aa ndani ya shirika la Mitume (Yohana 11:55 - 17:26)
A - Utangulizi kwa Juma Takatifu (Yohana 11:55 - 12:50)

2. Yesu aingia Yerusalemu (Yohana 12:9-19)


YOHANA 12:9-11
“Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu. Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye; maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.”

Mji mkuu ukapata uchangamfu kwa habari kwamba, Yesu alimtembelea Lazaro. Wengi wao walikimbilia toka Yerusalemu kuelekea mlima wa mizeituni na Bethania, ili washuhudie mwujiza ule wa mtu kupewa uhai wake tena.

Makuhani wakuu waliegemea kwa Masadukayo, ingawa wao hawaamini habari ya ufufuo, wala habari ya kuwepo kwa roho au pepo ya aina zozote. Hata hivyo walimchukia Yesu na Lazaro kiasi cha kukataa mwujiza, na zaidi hata kutaka kumwua huyu mtenda miujiza. Walikusudia kuwalaza wote wawili makaburini, ili wathibitishe kwamba, hakuna tumaini lolote baada ya kifo. Pamoja na hayo walitaka kubomoa imani yoyote ndani ya huo mwamko wa Yesu, kwa vile makutano walidhania ufufuo wa Lazaro kuwa ndiyo thibitisho kwamba, Yesu ndiye Masihi wa kweli.

YOHANA 12:12-13
“Nayo siku ya pili yake watu wengi waliojia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu; wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!”.

Jina lake Yesu lilikuwa mdomoni mwa kila mmoja, wakahisi-hisi ni jambo gani atakalolitenda, “Atakimbia, au atatwaa jiji kwa kulitawala?” Baada ya kukaa usiku moja Bethania, wachunguzi walimwona asubuhi pamoja na wanafunzi wake wakielekea Yerusalemu; “Mfalme mpya anakaribia, mtukufu mwenye enzi anakuja.” Watu wengi waliinuka ili waone miujiza mingine na ushindi. Wengine walikata majani ya mitende, wakiyabeba ili kumlaki. Wengine waliimba nyimbo zinazotukuza kuingia kwa wafalme na wanaume shujaa. Walilia kwa sauti kuu na kushangilia, “Tunakusifu na kukutukuza. Wewe ni mwenye enzi yote; umekuja katika jina la Bwana, ukijaa mamlaka yake. Twakushukuru kwa baraka unazotuletea. Tusaidie na kutuokoa na aibu zetu zote. Wewe ndiwe Mwokozi wetu, shujaa na kiongozi. Ndiwe Mfalme wetu wa kweli.”

YOHANA 12:14-16
“Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile ilivyoandikwa, Usiogope, Binti Sayuni, tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda. Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo.”

Yesu hakuitika kwa kushangiliwa hivyo, kwa sababu aliwafahamu watu hao wakichangamka, hawawezi kusikiliza wala kutafakari vema, bali wanasongamana katika msululu njiani wakilia na kushangilia. Basi Yesu alisema nao kwa vitendo, akipanda punda kwa kuitikia kuimba kwao, kana kwamba kusema, ”Kweli mimi ni Mfalme aliyeahidiwa na nabii Zekaria 9:9. Usiogope lakini inuka. Mimi sibomoi kuta na malango ya miji. Mimi siui au kutimiza hukumu ya Mungu. Mimi ni mwenye haki, bila upendeleo; nikionyesha haki za yatima na kuwatunza wajane.”

“Kwa sikitiko, sio watu wote ni watenda haki. Wengi wao si waadilifu, wakitanga-tanga mbali na njia nyofu. Msiogope, sitawaangamiza mnavyostahili, lakini nitashinda mabaya ndani yenu. Nitabeba dhambi zenu mwilini mwangu na kuwa mshindi, iwapo wakati huo nitaonekana kama mdhaifu na mwenye kushindwa. Hivyo nitawaokoa na ghadhabu ya Mungu; nami nitatokea kama mshindi katika vita ya kiroho.”

“Ninyi mnamtamani mfalme wa ushujaa, apataye ushindi kwa upanga, lakini ninawajia mnyenyekevu kama kondoo, bila ya kufanya fujo. Nilitoa kabisa mapenzi yangu mkononi mwa Baba yangu. Ninyi mlitazamia nifanye maasi na kuleta ushindi, lakini nawatolea upatanisho, wokovu na amani na Mungu. Angalieni mnyama niliyempanda. Sikupanda farasi au ngamia, bali punda. Msitazamie utajiri au heshima toka kwangu, maana nimekuja na uzima wa milele na kufungua malango ya mbinguni kwenu, nikiwapatanisha wale wenye kutubu na Mungu Baba.”

Lakini mkutano wote, hata na wanafunzi wake, walishindwa kutambua makusudi ya Yesu aliyoonyesha na mfano wa utendaji huo. Baada ya kupaa kwake mbinguni tu, ndipo Roho Mtakatifu alifungua akili zao watambue unyenyekevu wa Kristo na utukufu wa Mungu ndani yake. Hayo yalikuwa kinyume kabisa na yale waliyoyatamani upande wa kisiasa na pia kwa hali yao ya maisha ya kawaida. Lakini Roho Mtakatifu aliwaongoza wafuasi wa Kristo wachangamke na kufurahia kuja kwake, hata kabla ya kutambua wazi maana ya unabii na jinsi ulivyotimia hatua kwa hatua.

YOHANA 12:17-19
“Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua. Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo. Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lolote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.”

Wale waliofuatana naye kutoka Bethania wakakutana na maandamano tokea mji mkuu ili wamkaribishe bondeni mwa kijito cha Kidroni. Wale wa kwanza walilia, “Mnafanya vema kumpokea, kwa sababu Yesu ndiye Masihi aliyemfufua mtu mfu, thibitisho la kwamba ndiye kweli ni Masihi.” Ufufuo wa Lazaro ilikuwa ndiyo msingi wa uchangamfu wa makutano wamfuate Yesu, na pia kule kulishwa watu elfu tano na mikate mitano. Hapo basi kuna makutano mengine wakimjia kwa sababu alimfufua mfu. Katika matokeo yote mawili upendo wa watu kwa Yesu ulikuwa na msingi hafifu wa mambo ya kidunia, wala si kwenye msingi wa kiroho ya haki na ungamo.

Pembeni ya uchangamfu wa makutano basi walisimama Mafarisayo na viongozi wa watu wakikasirika, wakimwonea wivu Yesu, wakimgojea aingie kwa ushindi jijini. Walitetemeka na kujuta kwa kushindwa kwao. Mpango wa kumkabidhi Yesu kisiri mikononi mwao haukufaulu. Aliingia jijini hali amepanda punda pamoja na maandamano makuu ya ushindi.

SALA: Bwana Yesu, nafungua moyo na akili yangu kwako, ili uingie kwa Roho Mtakatifu wako, ukanibadilishe nifanane na hali yako. Uwe radhi kwa makosa yangu, maana sistahili kuingia kwako moyoni mwangu. Lakini naona unakuja, mbali na dhambi zangu. Unanipenda na kuniokoa, kwa sababu umenisuluhisha na Mungu, na kuniingiza ndani ya ufalme wako wa amani. Napenda kulia na wote hao wanaochangamka, “Hosana! Abarikiwe ajaye katika jina la Bwana.” Wewe ndiwe mfalme wangu - mimi ni mali yako. Amina.

SWALI:

  1. “Kuingia kwake Yesu Yerusalemu namna hii ilikuwa na maana gani?”

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on September 01, 2014, at 04:28 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)