Waters of LifeBiblical Studies in Multiple Languages |
|
Home Bible Treasures Afrikaans |
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hebrew -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Malayalam -- Polish -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Turkish -- Urdu? -- Yiddish -- Yoruba
Previous Lesson -- Next Lesson WARUMI - BWANA NDIYE HAKI au UADILIFU WETU
Masomo kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi
SEHEMU 1 - HAKI YA MUNGU INAHUKUMU WENYE DHAMBI WOTE NA KUJALIA HAKI PAMOJA NA KUWATAKASA WOTE WAMWAMINIO KRISTO (Warumi 1:18 - 8:39)
E - Imani yetu itadumu daima (Warumi 8:28-39)
2. Ukweli wa Kristo unathibitisha ushirikiano wetu na Mungu mbali na matatizo yoyote (Warumi 8:31-39)WARUMI 8:38-39 Paulo alikuwa na uhakika kwamba, hakuna kitu hapo duniani au hata roho ya kidunia ambazo zingeweza kumtenga na upendo wa Mungu uliodhihirishwa ndani ya Kristo Yesu. Kwa tamko hilo kuu la kujumlisha alifunga sehemu hii ya mafundisho ya waraka wake kwa Warumi. Kwa kweli hakuwa akitafakari tu au kuchambua maoni, lakini aliandika mambo yenyewe ya kwenda chini sana kuhusu mateso makuu na mahangaiko kutokana na ushuhuda wa Roho Mtakatifu moyoni mwake. Paulo hasemi, „ikimpendeza Mungu atakuwa nami“, lakini alikiri kwamba, utambuzi wa upendo wa Mungu ndani ya Kristo ulimhakikishia katika tendo la kukiri kwamba, upendo huo hautakosekana hata kidogo. Uaminifu wa Mungu hauna shaka lolote. Paulo hakusema juu ya upendo wa kibinadamu, wala hakutamka habari ya Mungu mwenye rehema na upendo kwa jumla, lakini alimwona Baba kwa njia ya Mwana. Hakufahamu njia yoyote nyingine kwenda kwake Mungu, ila kwa njia ya Kristo. Basi ni tangu Mwana wa Mungu kuingia mwilini tunamfahamu yeye Aliye Juu, Baba yetu ni nani. Upendo wake wa kibaba sio huruma ya kibinadamu, maana Mtakatifu alitoa sadaka ya Mwana wake kwa ajili ya wasio safi, ili sisi tusitie mashaka katika rehema zake, bali tuwe na hakika kwamba, anatukaribisha ndani ya agano lake na kwa hatua ya kupokelewa kama watoto, kwa sababu ya kumwagwa kwa damu ya Mwana wake. Kwa sababu ya msalaba, Paulo alikuwa na hakika kwamba, upendo wa Mungu hautakosekana daima. Hata hivyo, kwa ukweli Shetani yupo, na yeyote anayekana kuwepo kwake, hatambui hali halisi ya dunia hii. Paulo aliona nguvu za kiroho kadhaa zilizokuwa tayari kuangamiza dunia hii na ule ulimwengu mwingine. Paulo hakukabiliana na roho ya mauti tu mara kwa mara, lakini pia alishindana na malaika ya giza, naye alihangaika katika sala zake dhidi ya uovu wa kuzimu hata akatamka: „ Ikiwa kuzimu na mbingu zote pamoja zinanivizia, upendo wa Mungu ndani ya Kristo hautaniacha. Nguvu zote za kunipinga hazikuweza kunishinda, kwa sababu damu ya Kristo ya daima ilinitakasa.“ Paulo alikuwa na kipawa cha unabii. Aliona jinsi yule mwangamizi, mwongo na mwuaji alivyovisia kanisa, lakini hakuweza kulishinda, maana limo ndani ya Kristo, na shetani hawezi kulipokonya mkononi mwake. Hata sheria takatifu haiwezi kusogeza imani ya mitume, hata kwa malalamiko, kwa sababu walifia msalabani pamoja na Kristo, naye anaishi ndani yao na kuwalinda. Hivyo mwumini atalindwa hata kwenye siku ya hukumu ya mwisho, maana Kristo ataendelea kuwa ni Mshindi mwaminifu kwake,. Kwa sababu hiyo tunakuambia, wewe ndugu mpendwa, „Kabidhi roho yako, mwili wako na moyo wako kabisa kwenye upendo wa Mungu, nawe ushikamane na ule Utatu, ili na jina lako liandikwe ndani ya kitabu cha uzima, na upate kuendelea kuwa mtoto wa Mungu daima. Haya na sasa utambue kwamba, Paulo hakuandika wimbo ule wa sifa juu ya upendo uaminifuwa Mungu kwa hali ya mtu mmoja kama yeye tu, alipoandika, „Mimi“, lakini alijumlisha maneno yake kwa kuandika „Sisi“ (wengi), akimaanisha kwa uhakika wale wote waumini walioko Rumi na makanisa kwa jumla yaliyozunguka Bahari ya Shamu. Ushuhuda wa imani yake inatumaanisha na sisi, tunapokubali mvuto wa sura hiyo iliyotangulia. Ndipo hatutaelekeza maccho yetu tu kwenye mambo yanayoonekana kuwa wenye nguvu na kubwa katika dunia hii, lakini tutanang‘ania kabisa kwenye upendo wa Mungu iliyofunuliwa ndani ya Kristo Yesu. Maneno ya mwisho „Bwana wetu“, yanatokea kama mwisho wa wimbo huo. Upande wa pili, yanatuthibitishia ya kwamba, yeye aliyeshinda kule Golgotha, ndiye Bwana wa Mabwana, ambaye ndani ya nguvu yake tunapewa thibitisho la ulinzi wetu. Yeye hunyosha mkono wake wa kulia juu yetu, na hawezi kutuacha, kwa sababu anatupenda. SALA: Ee Yesu, maneno yangu yanashindwa kutamka vema shukurani zangu. Wewe uliniokoa nami nimepata kuwa wako. Nijaze na upendo wako, ili maisha yangu yaweze kuwa ujumbe wa kusifu enzi yako, nami nipate kukutukuza katika uhakika kamili wa imani, nikifahamu kwamba, hakuna jambo linaloweza kunitenganisha na wewe, maana wewe ndiwe mwaminifu. Kwa vile umeketi kwenye mkono wa kulia wa Baba, yeye ndani yako na wewe ndani yake, ndivyo uniimarishe na mimi ndani ya haki yake, ili kitu chochote kisiweze kunitenga na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Amina. SWALI:
QUIZ - 2Mpendwa msomaji,
Ukikamilisha masomo ya mihula yote ya mfululizo kwa Warumi na kututumia majibu ya mwisho wa kila muhula, sisi tutakutumia CHETI CHA ili utiwe moyo kwa ajili ya huduma yako kwa Kristo hapo mbeleni. Tunataka kukutia moyo ukamilishe na mitihani kuhusu Barua ya Paulo kwa Warumi, ili upate hazina ya kudumu. Tunangojea majibu yako na tunakuombea. Anwani yetu ni hii: Waters of Life Internet: www.waters-of-life.net |