Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 066 (Sheep hear the voice of the true shepherd; Jesus is the authentic door)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 2 - Sehemu ya pili: Nuru inang’aa gizani (Yohana 5:1 - 11:54)
C - Safari ya mwisho ya Yesu kwenda Yerusalemu (Yohana 7:1 - 11:54) Neno Kuu: Kutenganisha giza na nuru
3. Yesu, Mchungaji Mwema (Yohana 10:1-39)

a) Kondoo husikia sauti ya mchungaji wa kweli (Yohana 10:1-6)


Katika sura za 7 na 8 Yesu aliwaonyesha maadui zake ukweli wa hali yao. Ndipo sura ya 9 akawaonyesha upofu wao kwa elimu ya kweli ya Mungu na Mwana wake, hata na juu yao wenyewe. Katika sura ya 10 anawaweka huru walio wake kutoka kwa wajibu wa kuwafuata viongozi wao wenye dhambi, na anawaita waje kwake. Yeye ndiye Mchungaji Mwema, tena mlango wa pekee kuelekea kwa Mungu.


YOHANA 10:1-6
“Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyu ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Bawabu humfungulia huyu, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.”

Wenyeji wa vijiji fulani hukusanya kondoo zao ndani ya kiwanja kilichzungushiwa na ua na kupalinda hapo usiku. Asubuhi wachungaji huja na kuingia ndani wakiwaita kondoo zao. Walinzi huwaruhusu kuingia, ndipo jambo la kushangaza latokea: Hao wachungaji hawawasukumi au kuwavuta kondoo zao watoke kati ya wengine, lakini wanaita kwa sauti ya pekee kila mmoja. Kondo waweza kutofautisha sauti hii na ya mwingine, na hivyo wafuata kila kondoo sauti ya mchungaji wake. Hata kama wachungaji wavae nguo tofauti ya kawaida, kondoo watafuata sauti ya mwenyewe. Kinyume cha hilo, akija mchungaji mwongo, hata kama amevaa sawa na mchungaji wao, kondoo hawatasogea hata kidogo. Kondoo hufuata sauti iliyo sawa, iliyo ya mchungaji wa kweli. Kwa kuwaita huwaongoza walio wake kwenye machungio mabichi na maji ya kuburudisha. Kondoo zake hukusanyika nyuma yake karibu, hakuna hata mmoja anayekawia nyuma zaidi; wanamtegemea mchungaji wao kabisa.

Yesu alitumia mfano huu, ili kutuonyesha kwamba, wote wanaotaka kusikia sauti yake, kwao Yesu atakuwa ni Mchungaji wa ki-mungu. Hakuja kwa watu wa Agano la Kale ili kunyakua au kuiba, bali aliwachagua watu wa Mungu maalum kati yao na kuwaita waje kwake. Aliwaokoa na kuwalisha chakula cha kiroho siku zote. “Wachungaji” wengine wanafanana zaidi kama wezi wakizungukazunguka lile kundi kama mbwa mwitu wakali. Wanaingia ndani kwa utendaji kuwa wasaidizi wa kudanganya. Wananyakua kondoo kwa ajili yao wenyewe na kuwameza. Wao huishi kwa ajili yao wenyewe tu wakijisifu. Hawaihudumii kundi kwa namna ya kweli. - Wachungaji na watumishi makanisani ambao hawakuitwa na Mungu mwenyewe, na wasiodumu ndani ya Kristo kwa kweli, Bwana wetu huwaita wezi. Huwa wanaharibu kuliko kusaidia.

Yesu alitabiri kwamba wafuasi wake wa kweli watajitenga mbali na “wachungaji” wageni na kubaki mbali nao, wakisikia hatari mapema. Naye anawasisitizia wategemee ahadi kwamba Mungu mwenyewe atachunga kundi lake jinsi ilivyoandikwa katika Zaburi ya 23.

Watu hawakuelewa haraka maneno ya Yesu, wakishindwa kutambua kwamba “wachungaji” wao hawakuwa waaminifu, ila waovu (Yeremia 2:8; Ezekieli 34:1-10; Zekaria 11:4-6). Mbali na hayo, Mungu alikuwa tayari kujifanya kuwa Mchungaji wao Mwema, kuwahimiza watu wake na kuwapatia wachungaji waaminifu, jinsi walivyokuwa Musa na Daudi. Biblia hutumia maneno na mifano ya kichungaji; kama vile Mchungaji / Kundi / na Mwana Kondoo wa Mungu, pia na tendo la ukombozi kwa kumwaga damu; yote hayo yanatokana na matamshi ya mazingira ya kichungaji. Mungu ndani ya Mwanawe huitwa Mchungaji Mwema, ili kukaza kwamba, kwake kutuhudumia ndiyo kitu chenyewe hasa.


b) Yesu ndiye mlango hasa (Yohana 10:7-10)


YOHANA 10:7-10
“Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaamieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”

Yesu ajieleza mwenyewe kuwa ni mlango unaoongoza kwenye kundi la Mungu. Hakuna Namna ya kushirikiana na waliokombolewa ndani ya kanisa pembeni ya Kristo. Yeyote anayejaribu kuwa mcha Mungu bila Kristo, anafanana na kiongozi anayechanganya tabia ya kondoo wa Mungu na makosa. Roho Mtakatifu hatatuongoza kwa njia mbalimbali, ila kwenye mlango mwembamba ambao ni Yesu. Yeyote asiyeingia hapo, na hali mwili wake wala kunywa damu yake, basi hana haki ya kuhudumia watoto wa Mungu. Kila mmoja wetu anatakiwa kufia hali yake ya kuridhika na kuingia kwenye kundi la kondoo la Kristo; hivyo tu tutapata kuwa sehemu ya zizi lake.

Wakuu wote waliotokea kabla au baada ya Kristo bila kuishi ndani ya Roho wake Mtakatifu, ni kama wezi wanaodanganya. Yesu asema kwamba wanafilosofia na wenye mawazo makuu na viongozi wa mataifa ni wanyang’anyi, wasipoamini ndani yake na kujinyenyekeza kwake; wanaharibu watu kwa mafundisho na tabia zao. Lakini manabii wa kweli, wanaodumu ndani ya roho ya Kristo na kumtabiri, walikuwa wenye mioyo ya kupondeka, na wameingia kwa Mungu kupitia ule mlango. Yesu alikuwa amewatayarisha na kuwatuma kwa huduma ya uaminifu ndani ya kundi lake na zizi lake.

Hakuna awezaye kuingia ndani ya zizi la Mungu, asipofia nafsi yake ya kawaida na kuambatana na Yesu amwokoe. Yesu huwafanya kondoo zake waaminifu kuwa wafalme na makuhani. Mchungaji mnyofu hutoka nje kwa mlango kwenda ulimwenguni akiwasihi watu wakubali kuokolewa. Ndipo hurudi pamoja nao ndani ya zizi, yaani mwili wa Kristo, ili wao nao wadumu ndani yake na yeye ndani yao. Wachungaji kama hao hawajioni wenyewe kuwa bora kuliko kondoo wengine, maana wote pamoja huingia kwake Kristo. Kila mtu anayedumu ndani ya unyenyekevu, atakuta ndani ya Bwana wake, aliye ukamilifu wa nguvu na ufahamu. Moyo wa kunyenyekea huona ndani ya Yesu malisho yasiokosa chakula.

Yesu mara nne aliwaonya kundi lake dhidi ya Waandishi na Makuhani, kwa vile walitafuta utukufu wao wenyewe na kuwachafua wengine.

Pamoja na hayo Kristo aliwaita watu waje kwake, ili wapatiwe uhai wa kweli na amani, na kuwafanya wawe kisima cha baraka kwa wengine. Yeyote amjiaye Kristo, atapata kuwa chemchemi ya uwezo na maadili akibubujika kwa ajili ya wengine. Wachungaji huwa hawaishi kwa ajili yao wenyewe, lakini wanajinyima siku zao na maisha yao kwa ajili ya kundi lao. Roho wa Mungu hatupatii uhai wa mbinguni kwa ajili ya wokovu wetu wenyewe tu, bali anatuamuru kuwa watumishi na wachungaji katika hali ya kujikinahi na kuwapenda wengine. Pamoja na nyongeza ya upendo itakuja na ongezeko la kufurika. Hakuna linalopendeza zaidi kuliko huduma kwa ajili ya Bwana! Ndiyo hilo linaloonyeshwa kwa tamko hilo: “…..ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele”.

SALA: Bwana Yesu Kristo, asante sana kwamba wewe ndiwe mlango wa kutuongoza kwa Mungu. Tunakuabudu kwa sababu umetuita katika ushirika wako, ili tumtumikie Mungu pia na watu. Utusaidie tujitoe kweli na kufuata uhai wa kweli. Utuwezeshe tuweze kuvuta roho za watu, tukiongozwa na Roho yako, na tuwe baraka kwa wote pamoja na fadhili uzitoazo wewe.

SWALI:

  1. Baraka za Yesu anazoziweka juu ya kondoo zake ni zipi?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on March 18, 2014, at 11:30 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)