Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 12 -- Tenth Commandment: Do Not Covet Your Neigbor's House
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule? -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba?

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

12 - Amri Ya Kumi: Usitamani Nyumba Ya Jirani Yako



KUTOKA 20:17
“Usitamani nyumba ya jirani yako, usitamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako”


12.1 - Majaribu ya kisasa

Yeyote anayetazama TV anaweza kuingia majaribuni kwa vitu vya biashara vinavyopendeza. Pengine utakimbia kununua vitu vya kushangaza, kuweka sahihi kwenye mkataba wa shirika la bima, kununua marashi ya pekee, nguo, hata na gari ya mashindano. Orodha yaweza kuendelea mbali, - na kwa vyovyote huwezi kuwasikia hao watangazaji wa biashara kusema tamko rahisi la Yesu kwamba, “Ujinyime! Uridhike na vitu ulivyo navyo!” Wao daima wanao ujumbe huo; “Tamani kila kitu ukanunue lolote lile ambalo bado hunalo.”

Gazeti fulani ilionyesha picha ya kijana mdogo aliyekuwa amefunikwa hadi masikioni na vitu vya michezo, wanyama wa bandia za aina mbalimbali, magari ya mbao, vibati na plastic, pia na michezo mingi. Huyu kijana mdogo aliwahi kupewa kila kitu alichokitamani. Hakuna alichokitaka ambacho hakupata. Maskini huyu kijana! Jamii ilimwaga kila kitu juu yake hadi alipokinahi na kudidimia ndani ya ulimwengu wake.wa utoto.

Katika jamii yetu ya viwanda na mashine watu huvutwa na mambo yaliyo kinyume cha amri ya kumi. Kwa mfano, mume na mke wake hufanya kazi kwa miaka, ili siku moja waweze kujenga nyumba yao wanaoitamani kwa muda mrefu. Basi wanalemea kwa kazi nyingi, na mama anapoendelea kuchapa kazi huenda atalegea kuwatunza vema watoto wake kwa sababu ya uchovu. Wanazidisha kunywa kahawa na vichocheo vingine wakitazamia vitawaamcha kazini. Matokeo ya mwishi yatakuwa utupu wa ndani kabisa, pamoja na jumlisho la madeni na mavutano ya kifamilia. Kwa nini? Kwa sababu familia hiyo inatumia pesa zaidi kwa vitu ambavyo hawahitaji hasa na kuishi juu ya uwezo wa mapato yao.


12.2 - Je, kuwa na mali kunakataliwa?

Yesu asema, „Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake?“(Mathayo 16:26). Pia alisema, „Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.“ (Marko 8:35). – Wakati wa vita bomu moja inatosha kuangamiza jengo la ghorfa nane kwa sekunde moja, na mwishowe kila kitu kimebakia majivu tu.. Mamilioni wa wakimbizi walipoteza kila kitu walichokuwa nacho. Katika nchi ya kikomunisti, kila mtu aliye na nyumba au mali nyingine ya binafsi inampasa kulipa ushuru iliyo juu ya kodi ya nyumba inayolingana na hiyo anayolipia ushuru, hadi atakapokuwa na hali mbaya kifedha kuliko mtu asiye na kitu. Mungu anatutaka turudishwe kwake na kutuwezesha kuangalia vitu vya dunia hii anavyoyaona yeye. Mambo ya ukweli ya kiroho yako na thamani nyingi zaidi kuliko mali ya kugusika.

Watu wanaogawana urithi basi wangekuwa na shabaha hiyo ya kiroho ndani yao, maana itakuwa na faida gani kujenga chuki katika jamaa kwa ajili ya pesa au mali? Yesu alisema, “Na mtu atakaye kukushika na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia“(Mathayo 5:40“). Mtume Paulo anatuhakikishia kwamba, kuna baraka zaidi kwa ajili ya kutoa kuliko kwa kupokea! Basi hayo ingekuwa daima mwongozo wetu katika kumfuata Yesu. Ni kosa kuthamini mali ya mwingine. Yeyote anayedanganya hati ya nyumba au mali au anayempunja fulani kwa ajili ya unyofu wake, basi anastahili ghadhabu ya Mungu, maana Mungu ni mlinzi wa yatima na wasio na wazazi, pia na wajane.


12.3 - Watu wanaodanganya

Amri ya kumi haikuwekwa tu kwa ajili ya mali uliyopata, lakini inazuia pia kushawishi wafanya kazi pamoja nawe, watumishi au marafiki. Kwa sababu tu waajiriwa wanamchukia mkuu wao wa kazi au kwa sababu kuwa na matatizo kazini, bado hayawaruhusu kuchochea vurugu. Badala yake, tungewatia moyo wakubali kuendelea kwa utulivu; si kitu sisi au wengine wapate nafasi nzuri zaidi kwa njia ya kubadili mahali pa kazi. - Pia tunahitaji kujali amri ya kumi kanisani, katika vyama vya jamii, mashuleni na mashirika ya ufadhili; maana kushawishi ndugu, dada au wafanya kazi pamoja nasi haitaleta baraka yoyote.

Pengine italeta matokeo magumu sana, ikiwa fulani atajiingiza katika mambo ya kifamilia kwa kumjaribu mume au mke kujitenga na umoja wa familia, ambayo Mungu amewabariki nao. Kutamani kubadili, au hata kutokueleana tena au hata mvutano mkali bado haiwezi kuhesabia haki hatua hiyo ya kuumiza sana. Yesu mwenyewe alisema ,“Yaliyounganishwa pamoja na Mungu, mwanadamu asitenganishe.“ Fulani anapojaribu kuharibu nyumba (ndoa) au kujiingiza kwa tendo la kuchukuliana nje ya ndoa, inampasa atubu hapo hapo, abadilishe makusudi yake, pia na awe tayari kuwajibika kwa hasara yoyote katika familia hiyo. Akifanya hivyo basi, maisha yake yaweza kuwa ya maana tena, naye atajifunza kukataa na kuchukia aina zozote za dhambi za eneo hilo. Asingeweza tena kukaribisha mawazo hayo mabovu ya kubadili mwenzake kwa usiku moja, au likizo kutoka ndoa au kujaribu mshiriki mwingine. Badala yake, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu ataishi katika hali ya kujizuia na namna yoyote ya dhambi, maana hapo tena huwezi kufanya lolote mbali na elekezo la Roho Mtakatifu.


12.4 - Mambo gani yanachochea tamaa zetu?

Amri ya kumi inasema habari ya watu au vitu fulani ambavyo twaweza kuyatamani. Siku hizi tunaweza kuongeza kwa orodha ya awali ya mambo ya kutamani mengine kama: magari, vyombo vya muziki, mashine za kufua, barafu na nguo za mapambo. Mwanadamu huelekea kuwaza kwamba, inampasa kuwa na vyote ambavyo wengine wanavyo. Hali ya maisha inayoendelea kupanda, basi inaleta na hatua za kuharibu na kuchakaza. Nchi zinazoendelea zimeanza mipango ya kuharibu tabia, zinazowafanya kutumbukia ndani ya madeni kwa kiasi kikubwa, wala hawawezi tena hata kulipia faida juu ya madeni hayo. Walinunua mashine za kisasa ambazo hazitendi kazi tena kwa sababu hakuna ajuaye namna ya kuzitengeneza zikiharibika, wala kubadilisha chombo kilichoharibika. – Mitume wa Kristo walielewa kwa nini imekuwa muhimu kuridhika na vitu walivyokuwa navyo na kuwa huru na madeni yanayoweza kuongezeka tu.na kuharibu moyo na mwili. Zaidi ya hapo, Yesu alisema, „Mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu“(Mathayo 20:26-27“. Yesu alikuja kurudisha mambo yote ya thamani ulimwenguni kwetu alipoomba, „Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako. …… Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.“ (Mathayo 11:25-30).

Paulo aliandika kwamba, Mungu ataharibu kiburi yote na hali ya kujiona wakati ambapo watajiri wachache na wakubwa walikuwa washiriki wa kanisa la Korintho. Mabadiliko ya malengo maishani na kufanywa upya moyoni iliwapa maana mpya wale washiriki wa makanisa ya kwanza. - Amri ya kumi haikatazi tu matendo yetu maovu na ya kudharau, lakini pia inakemea makusudi yetu yanayojificha moyoni. Kwa kiasi fulani baraza linaweza kuhukumu tendo la kuvunja sheria ya mtu fulani, lakini moyo wa mtu inaweza tu kubadilishwa na Mungu. Hata sisi wenyewe hatuelewi kikamilifu kabisa mioyo yetu. Mara kwa mara tunashindwa kugundua kwa nini rafiki yetu alitenda kwa njia hii au ile. Mara nyingine tu kama siri kwa ajili yetu sisi wenyewe. Biblia lasema, „Kila kusudi analowaza mtu moyoni mwake ni baya tu sikuzote“ (Mwanzo 6:5). Tunapojipima kulingana na utakatifu wa Yesu, tutaona jinsi tulivyo wachafu na kupooza. „Wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu“ (Warumi 3:23). Hali hiyo inaweza kuonekana hata ndani ya mtoto anayejaribu kupata mambo ya kwake kwa kulia bila kukoma. Watoto wanapunjana wao kwa wao, na tunapoona dhambi walizorithi maishani mwao, basi tutakataa mahisi ya kiakili kwamba „watoto hawana hatia“. Mtoto anayeendelea kukua anajaribu kila tamaa, naye aweza kufanya kama kijinga na ya kujiona mwenyewe tu. Kwa kweli, bado kuna tofauti katika kuwaza mabaya na kutenda mabaya. Hakuna awezaye kukwepa majaribu, lakini unaitwa kuzuia mabaya kwa moyo wako wote. Dr. Martin Luther alisema, „Siwezi kuzuia ndege kuruka juu ya kichwa changu, lakini naweza kuzuia wasijenge kioto ndani ya nywele zangu.“

Tunapaswa kuchunga majaribu tangu mwanzo, kuyakataa na hivyo kuyashinda. Paulo mara nyingi anaandika usemi wa kiyunani, „Bora wazo hilo lisizaliwe ndani yangu kabisa!“ Barua ya Yakobo inafuatilia asili ya majaribu. Katika sura yake ya kwanza anahakikisha kwamba, majaribu hayatoki kwa Mungu, maana Mungu hamjaribu mtu yeyote na maovu. Lakini mtu anapojaribiwa, basi anavutwa na tamaa za mwili na damu yake mwenyewe. Hivyo ni wazi, „ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti“. Mtume huyu anaendelea kusema, „Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike. Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake“ (Yakobo 1:16-18).

Mwumini wa kikristo inampasa aruhusu Neno la Mungu limkemee kwa habari ya tamaa zake, pia na shabaha na makusudi yake kila siku. Kushinda mawazo mabovu kunategemea hali yetu ya kujitoa kabisa kwake Yesu na kwa neema yake ya milele, ili tuweze kuomba kwa matumaini, „Usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu“ (Mathayo 6:13). Wakristo wanao uhakika kwamba, dhambi zao zimesamehewa kwa njia ya damu ya Yesu na wanashikamana na haki ya Kristo iliyotiwa ndani yao. Kwa sababu hiyo hawatatenda dhambi kwa makusudi, maana Roho Mtakatifu anatakasa mawazo na shabaha zao. Yesu anataka kuwa Bwana mshindi katika mawazo yote ya mioyo yetu. Anataka kuongoza vita vya maishani mwetu na kutuhakikishia ushindi. Hii sio vita takatifu dhidi ya mtu fulani au taifa, lakini kwa uwazi kabisa ni dhidi ya umimi wetu kuu, pia dhidi ya tamaa zetu za ukorofi inayokaa ndani yetu, na hata dhidi ya majaribu yanayoturukia toka nje. Tuombe kwa makini na kuamini yale tunayoomba, „Ewe Bwana uishiye kuwa Mwokozi wetu mwenye enzi, nakushukuru kwamba, umeniokoa. Tafadhali usiniruhusu kuanguka katika dhambi hii tena, lakini uniponye nayo, pia na kunizuia na maovu yote yaishiyo ndani yangu. Naomba usimruhusu yule Mwovu kupata mahali pa kuwekea mguu wake ndani yangu. Unitawale, Bwana, na kuishi ndani yangu daima. Safisha mawazo yangu kabisa na damu yako na unitakase kote kwa Roho yako, ili makusudi na kutamani kwangu yakupendeze.“


12.5 - Moyo mpya na Roho mpya

Tunapoingia ndani ya vita ya kiroho ya namna hii dhidi ya umimi wetu, basi tutatambua yale ambayo Yesu aliyomaanisha aliposema, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya“. Basi, si jambo la kukingwa na matendo mabaya tu, wala si vita dhidi ya dhambi fulani tu, bali kuna mengi zaidi yanayohitajika kushughulikiwa. Tunahitaji dhamiri safi, mawazo meupe na moyo mpya. Kwa sababu hiyo, tumwulize Yesu akamilishe makusudi yake kwa nguvu za Roho Mtakatifu wake ndani yetu, ili kila eneo la roho zetu, moyo na mwili zipate kutakaswa na Yeye. Maana si mwili wetu tu ulio ovu, lakini pia roho na mioyo yetu. - Shabaha ya Amri ya Kumi ni kumzalisha kwa upya mtu wa kale na kutengeneza kwa upya mawazo na shabaha zake. Nabii Yeremia aliteseka sana kwa ajili ya watu wake waliokuwa wakengeuka sana, naye alipokea ahadi kubwa na tukufu alipoambiwa, „Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hata aliye mkubwa miongoni mwao, asema Bwana; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena“ (Yeremia 31:33b-34).

Mungu alitoa ahadi zilizolingana kwa nabii Ezekieli alipomfunulia, „Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda“ (Ezekieli 36:26-27). Mfalme Daudi aliomba sala lifuatalo la ungamo miaka 30 kabla ya ufunuo wa utabiri huu:

Ee Mungu, unirehemu, sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa na uovu wangu, unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutendea dhambi Wewe peke yako, na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; nawe utanijulisha hekima kwa siri, unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji, unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako. Ee Mungu, Mungu wa wokovu wangu, uniponye na damu za watu, na ulimi wangu utaiimba haki yako. Ee Bwana, unifumbue midomo yangu, na kinywa changu kitazinena sifa zako. Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; moyo uliyovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau. (Zaburi 51: 1-17)

Yeyote atakayeomba sala hii ya ustahifu ya Daudi atapokea jibu la uhakika kutoka kwa Mungu. Yesu alikamilisha unabii huu alipotamka, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12). Pia alisema hivi, “Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyu huzaa sana; maana pasipo mimi hamwezi kufanya neno lo lote” (Yohana 15:5).

Mwanzoni mwa huduma yake, Yesu aliliweka wazi kwa Nikodemu, mzee wa watu wake, akimwambia, ”Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:5). Petro alithibitisha ahadi hiyo siku ya Pentekoste mbele za watu elfu tatu, “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate kuondolewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo ya Mitume 2:28).


12.6 - Vita za kiroho

Roho Mtakatifu anapotawala ndani yetu, bado tutaweza kudhurika na majaribu. Lakini Roho hupigania dhidi ya mwili, na mwili dhidi ya Roho, na mapigano yaendelea jinsi Paulo anavyoyaeleza, “Bali mkiyafisha mambo ya mwili kwa Roho, mtaishi” (Warumi 8:13). Katika barua kwa Waefeso 4:22-24 Paulo anakazia, “Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu, mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli”. Kuvua utu wa zamani inamaanisha kuchukia na kukataa tamaa zetu zote zenye dhambi wakati wowote. Kuvaa utu mpya inamaanisha kumvaa Yesu kama nguo mpya baada ya yeye kutusaidia kushinda umimi wetu wa awali.

Katika vita hiyo inawezekana kuvumilia maangamizi, kwa vile tunatafuta kuishi maisha matakatifu. Basi itatupasa kuinuka mara na kwa haraka kumrudia Yesu, tukikiri dhambi zetu mbele zake kwa uwazi. Kama kiburi chetu na kujitegemea zimevunjwa, basi tutakuwa tumeunganishwa na Yesu tena na tutaona nguvu yake ndani ya udhaifu wetu. Hii ndiyo njia ya pekee kupata tena ushindi juu ya mabaya ndani yetu na kuimarika ndani ya Bwana. Biblia lasema, “Wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndiyo ni watoto wa Mungu.” Katika barua kwa Warumi 8:1-2 Paulo anawafariji wote wanaoshiriki katika vita hiyo ya kiroho, anaposema, “Sasa basi, hakuna ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.” Wakati Agano la Kale linapoweka makusudi na matendo yetu mabaya chini ya hukumu ya sheria, Agano Jipya linatujalia ufahamu wa kina zaidi juu ya hali yetu iliyo ya dhambi kabisa, na wakati uo huo linatushauri kukubali ile haki ya Mungu ya neema kwa njia ya imani ndani ya Yesu Kristo. Yeye anatuwezesha kumpokea Roho Mtakatifu kwa ajili ya kufanya upya akili na kutaka kwetu. Amri za Musa zinajaribu kutuzuia tusianguke, lakini Yesu anatujalia sababu ya kufaa kabisa, pia na nguvu ya Roho ya Mungu, ili tuweze kutimiza maagizo yake. Agano la Kale linapotufunulia maharibiko maishani mwetu kutokana na makusudi yetu mabaya, Baba yetu wa mbinguni hutujalia haki tukufu: hakuna hatia, wala hakuna kuhukumiwa tena! Tayari Yesu amekwisha kulipia bei ya msamaha! Kwa nyongeza ya kutupatia haki anatutia nguvu kwa njia ya Roho yake ya milele, ili tuweze kushinda dhambi. Mungu pekee wa Utatu hutuweka huru na dhambi zetu kuelekea kwenye unyofu wake, naye hutuongoza kutoka kwenye mapigano tufikie ushindi kwa nguvu ya upendo wake unaoishi ndani yetu.


12.7 - Uislamu na Tamaa

Uislamu haufahamu habari ya kutimiza sheria kwa haki kwa njia ya imani au ushindi juu ya mambo ya mwili kwa Roho. Kurani latamka, “Mwanadamu ameumbwa dhaifu” (Sura al-Nisa 4:28). Hivyo Uislamu unasukuma sehemu ya lawama juu ya Allah. Ndiyo maana Mhamadi aliwaruhusu wanaume kuoa suria zao pamoja na wake zao wanne, isipokuwa wanaanguka katika majaribu (Sura al-Nisa 4:26). Mhamadi mwenyewe alimwoa mke wa Zayd, wakati Zayd alikuwa ni mwana wake wa kumlea kuwa mtoto wake. Kuhusu ndoa yake, Mhamadi alipokea mafunuo ya pekee kutoka kwa Allah iliyomruhusu kuoa mke wa Zayd na mwanamke yeyote mwingine aliyekubali kujitoa kwake (Sura al- Ahzab 33:37,50,51).

Kurani pia linafunua mara kwa mara kwamba, Allah humwongoza yeyote amtakaye na kumwongoza njia mbaya yeyote atakavyotaka (Suras Ibrahim 14:4 na Al-Fatir35:8). Kutokana na hayo hakuna wajibu ya adabu zaidi juu ya mtu mwenyewe.

Wakati wa vita takatifu, kuteka nyara na kukusanya mabaki ya vita yalikuwa muhimu sana. Mara nyingine askari walishindwa vitani, kwa sababu walishikwa katika kukusanya mabaki kabla ya wakati wake na kuyapeleka nyumbani. Maraa kwa mara kulikuwa na mahojiano makali sana juu ya kugawanya mabaki ya vita. Kujipatia vitu na kujifurahisha katika tama mara nyingi ni ya muhimu sana maishani mwa Mwislamu. Kwake mamlaka na heshima ni thibitisho la neema ya Allah, ambazo ni wazi kabisa maishani mwa watawala wa Kiislamu. Unyenyekevu na wema wa Kristo ni geni kwa Uislamu.

Zaidi ya hapo, kulipiza kisasi hata kwa kumwaga damu haikataliwi katika Uislamu, kama mapatano ya kulipia haikufanywa. Mhamadi mwenyewe alituma wajumbe kuwaua maadui zake za binafsi. - Tamaa za umimi za binadamu haziwi bora anapokubali kuwa Mwislamu; kila kitu kinabaki bila mabadiliko, isipokuwa hapo ameingia hali ya kutokuweza kuguswa na wokovu ndani ya Kristo. Kwa Mwislamu, imani ndani ya Mungu aliye Baba ni moja wa dhambi isioweza kusamehewa. Kama Mwislamu inampasa kujaribu kujiokoa mwenyewe kwa njia ya matendo yake mema. Na hayo matendo mema kwa jumla sio matendo ya huruma, lakini ni kutimiza wajibu wa kidini, kama vile kukiri imani, sala za kiislamu mara tano kutwa, kufunga mchana wakati wa Ramadhani, kutoa sadaka kwa maskini, kuhiji Makka, kukariri Kurani kwa moyo, mwishowe kupigania vita takatifu (Jihad) kwa ajili ya kueneza Uislamu. Ni wazi kwamba, Mwislamu hajui chochote jinsi moyo wake unavyoweza kufanywa kuwa mpya. Kuwa kiumbe kipya kwake haiwezekani, kwa sababu Roho Mtakatifu wa kweli hajulikani katika Uislamu (Sura al-Isra’ 17:85).

Mwislamu humfahamu Roho Mtakatifu kuwa ni roho aliyeumbwa na Mungu, na kwa kawaida anafahamika kuwa ni malaika Gabrieli. Roho Mtakatifu kwao si roho atokaye ndani ya Mungu. Hivyo utamaduni na ustaarabu wa kiislamu ni matokeo ya kazi za kimwili. Matunda ya Roho, kama vile upendo, furaha na amani hazijaliwi katika Uislamu, kwa sababu msingi wake, ondoleo la dhambi kwa neema ya Msulibiwa, inakataliwa.

Ni rahisi kwa mtu yeyote kupata kuwa Mwislamu, kwa sababu anaweza kuendelea kuishi alivyoishi hadi hapo. Ikiwa mtu anakumbatia Uislamu, anaweza kuendelea kuwa na wake wengi akiwa Afrika au Asia. Tamaa za kimwili na za vitu vya anasa zinaahidiwa pia katika paradiso: kula, kunywa na mapendezi ya kimwili. Mambo ya milele kwa Mwislamu si tofauti na tamaa za binadamu zinazotazamiwa kwa mkamilifu zaidi (Sura al-Waqi`a 56:16-37). Allah mwenyewe hatakuwapo kwenye paradiso ya kiislamu. Hakuna tumaini la ushirikiano wowote na Allah kule, wala hakuna kutengenezwa kwa upya kiroho, wala vita dhidi ya hali ya umimi na kujiona hakuna katika Uislamu. Kimaadili na kiroho Uislamu iko chini sana kulingana na hali ya Agano la Kale, na haiwezi hata kulinganishwa na thamani ya Agano Jipya.


12.8 - Kristo aliye Tumaini letu la Pekee

Twahitaji kuhakikisha kwamba, haturuhusu namna yoyote ya dharau kwa Mwislamu au Myahudi, maana hakuna Mkristo, ambaye ndani yake ni bora kuliko mtu yeyote mwingine. Kwa imani ndani ya Kristo tu tunapokea kuhesabiwa haki, pia na nguvu ya kuishi maisha ya haki na takatifu. Yesu ndiye shina la mzabibu na sisi tu matawi, na kwa kudumu ndani yake tunalindwa na kiburi na kuweza kuleta matunda kutokana na Roho yake. Hatuwezi kufanya lolote bora pasipo Yesu. Yeye ndiye kanuni yetu.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 01:53 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)