Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 11 -- Ninth Commandment: Do Not Bear False Witness Against Your Neighbor
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule? -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi? -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam? -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian? -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba?

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

11 - Amri Ya Tisa: Usimshuhudie jirani yako uongo



KUTOKA 20:16
“Usimshuhudie jirani yako uongo.”


11.1 - Nguvu ya ulimi

Ulimi ni kiungo kidogo mwilini na hata hivyo unao nguvu kubwa mno. Mara nyingine unao nguvu zaidi kuliko fedha au hata madawa ya thamani. Neno la ulimi wetu laweza kuwa kama kiberiti unachokiwasha, ili kuweka moto kwenye msitu mkavu. Lakini neno lenye thamani ni kama usukani ndogo ya merikebu inayoweza kuiongoza kufika salama bandarini. Kwa ulimi mtu aweza kusema uongo na kumtukana Mungu au kueleza ukweli, kumsifu Mungu au kumfariji mtu katika hali duni. Kwa nini? Katika sura yake ya tatu ya barua ya Yakobo alitutolea mifano mitatu ya kutusaidia na tuongoza, ili tuungame. Inatupasa kupima maneno ya ulimi wetu, ili yatamkwe katika nuru ya Neno la Mungu; maana kila neno ovu laelekeza kwenye moyo wa uasi, ambayo haujatengenezwa kwa upya. Lakini kila neno linalotamkwa kwa upole linafunua Roho ya Yesu moyoni.


11.2 - Ulazima wa Utakaso wetu

Tunamhitaji sana Mwokozi Yesu kutakasa ndimi zetu na kufanya kwa upya nia zetu, ili tuweze kutambua na kusema ukweli wake. Mheshimiwa nabii-kuhani Isaya alitetemeka aliposimama mbele za Mungu mtakatifu, ili apatanishe watu wake kwake Bwana wa Majeshi wa Utatu. Alipagawa alipoona tu upinde wa vazi la Bwana na kulia kwa sauti, “Ole wangu! Kwa maana nimepotea; Kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, Bwana wa Majeshi” (Isaya 6:5). Ndipo mmoja wa wale maserafi akaruka kwake, akiwa na kaa lililowaka moto mkononi mwake, ambalo amelichukua kwa koleo toka madhabahuni. Ndipo akaligusa kinywa chake na lile kaa la moto na kusema, “Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa” (Isaya 6:7).

Mwanadamu hutambua upotevu na udanganyifu zilizomo moyoni mwake mara anapokutana na Mungu Mtakatifu. Dakika hiyo anatambua kwamba, Mwenye Enzi ndiye kanuni yetu ya mwisho. Katika nuru yake tunaona uchafu, udanganyifu na uasi zinazojaa mle ndani yetu. Mtu huishi kwa juujuu tu bila kukutana na Mungu Mtakatifu aliye hai. Hali hiyo haibadiliki, isipokuwa mwenye dhambi anamkaribia Bwana wake, ndipo kila jambo laweza kufanywa kuwa mpya. Mtume Petro alianguka kifudifudi alipotambua enzi kuu la Bwana wake akalia, “Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana!” (Luka 5:8). Alitambua kwamba Yesu kwa upole alichungulia moyoni mwake na kufichua hali yake ya dhambi. Ingawa Bwana wetu alielewa mapema kwamba, baadaye Petro atamkana, hata hivyo baadaye atakuwa ni mfano wa kila mvuvi wa watu.

Yesu ndiye kweli iliyoingia mwilini, na roho yake kipekee ndiye Roho wa kweli (Yohana 14:17). Huyu Roho wa kweli anahuzunishwa kila mara tunaposema uongo na kupiga domo. Mungu hawezi kusingizia au kudanganya; Yeye ni safi na Neno lake ni kweli na kwa vyovyote litatimia. Anataka kutufanya tuwe wapya na kutuwezesha tuwe waaminifu. Anatushurutisha tuseme la kweli katika upendo. Kutamka ukweli kwa ukali na baridi usoni pa mtu ni kama kumwua. Lakini unaposema blabla kwa ulaini na kuficha ukweli, ndipo pia unasema uongo, si kitu unampenda kiasi gani. Sifa ya uongo na kusingizia mara kwa mara yanaenda pamoja. Hivyo, upendo bila kweli ni uongo, nakweli bila upendo inaweza kuua.


11.3 - Kusema uongo na Asili zake

Mungu wa Utatu ndiye kweli mwenyewe. Lakini Shetani ndiye msema uongo naye ni baba ya uongo wote. Yeye ni mwuaji tangu mwanzo. Yesu amwita “Mwenye uovu wote na mfalme wa dunia hii”. Kila kitokacho kwake ni uongo, si kita hata kikijionyesha kweli namna gani.

Huyu Mwenye Uovu alimdanganya Hawa. Swali lake la ujanja ulipotosha ukweli, na hivyo kumweka Mungu katika mashaka. Alitikisa tumaini la Hawa ndani ya Mungu. Ndipo kiburi cha Hawa, tamaa na uasi dhidi ya Mungu ziliamshwa, na papo hapo ikakua na kuwa uasi.

Mara baada ya ubatizo wake, Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani, ili ajaribiwe na Shetani. Baada ya kufunga na kuomba kwa siku arobaini usiku na mchana, alimshinda mwenye kumjaribu, aliyemjia kwa kuchanganya kweli kwa maswali. Shetani alimwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu . . . . “ Kama angalisema, “Wewe ni Mwana wa Mungu,” angalithibitisha kweli. Lakini alitia yaliyo ya hali halisi katika maswali, akijaribu kutia mashaka moyoni mwake Yesu kwa habari ya uwana wake kwa Baba yake wa mbinguni. Huyu Mwovu alitaka kumtenga na Baba yake na kumwongoza vibaya katika hali ya kumtumikia yeye. Yesu hakujibu na maneno yake mwenyewe. Wala hakuingia kuhojiana na Mwovu, wala hakusema kutoka katika uzoefu wake mkuu wa binafsi. Badala yake akaitika, “Imeandikwa!” Yesu alithibitisha Neno la Mungu lililofunuliwa, na hayo yalikuwa kinyume kabisa na ujanja wa Shetani. Kweli hakuna njia nyingine kumshinda yule baba wa uongo, ila kutegemea kabisa Neno la Mungu, ambalo ni Biblia.

Ni ya dhihaka kwamba, Shetani hufahamu Biblia na kulitumia kwa ujanja. Aliitika kwa haraka kwa kukataa kwake Yesu na kuleta neno kutoka kwa Biblia. Ila alilichomoa katika maneno yaliyotangulia na kufuata, na hivyo akajaribu kuchokoza kiburi kwake Yesu na kumwongoza ajaribu uaminifu wake kwa Baba yake. Tena Yesu akamjibu, “Imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako,” ndipo hapo makusudi ya kudanganya ya Shetani yaliwekwa wazi kabisa katika nuru tukufu ya kweli. Kutokana na mvutano mkuu kati ya Mwana wa Mungu na Shetani, ni wazi kwamba, Ibilisi hasemi neno ila uongo tu, hata ikiwa mara nyingine kuna sehemu ya ukweli ndani yake. Hata hivyo maneno yake yanalisha udanganyifu na uasi dhidi ya Mungu na Mwana wake mwishowe. Eti, chunguza filosofia na dini zilizokuja baada ya Yesu, nawe utatambua jinsi zinavyodanganya, ingawa kuna sehemu fulani za kweli ndani yake. Hata siku hizi Shetani anafanya yayo hayo: Anadanganya waumini nao wanaotafuta ukweli waamini kwamba, Biblia limepovushwa, limebatilishwa, limeandikwa na mikono ya wanadamu na maelfu ya hoja zingine za kutia shaka. Usimruhusu Shetani akunong’onezee uongo za namna hii moyoni mwako. Badala yake, mpinge jinsi Yesu alivyofanya kwa kusema, “Imeandikwa …..”


11.4 - Uongo ulio Kuu

Maoni ya ulimwengu ule mwingine pamoja na mipango ya elimu yake yanabeba maongo ndani yake na pia yanang’aa na kumetameta na madokezo ya kweli na amri zinazoonekana kuwa za muhimu kwa muundo wa ushirikiano. Hata hivyo mwelekeo wa jumla wa maoni hayo ya ulimwengu sio ya kweli. Kinyume cha hayo, sehemu hizo za kweli zinasimamia uwongo zilizo kuu. Pengine Uislamu unaonekana kwa wageni kama “dini ya kiasili ya Allah”, maana maneno yaliyopelekwa kwa kusikika tu na kugeuzwa yanatajwa kutoka kwa Agano la Kale na Agano Jipya. Hata hivyo Waislamu wote wanakataa katakata kusulibiwa kwake Mwana wa Mungu. Hawatambui kwamba, wamepotea na hawawezi kuokolewa kutoka kwa hukumu ya Mungu, ila kwa njia ya Yesu Kristo aliyesulibiwa. - Ingawa ukomunisti na maoni mengine yanachanganya maneno ya uongo yasio yenye tabia ya asili pamoja na kweli zingine zilizogeuzwa na mwishoni yanaongoza kwenye hali ya kupotea ya kutokuamini kabisa.

Baadhi ya wanatheologia wa kisasa au madhehebu ya upotovu huchukua maneno ya Biblia na kuyatumia mbali na mahali pale yalipoandikwa, ili watu wapate kuamini vitabu vyao au mawazo yao, badala ya kukiri kwamba, Yesu ndiye asili ya mawazo yote na ya uhai. Hakuna atakayemfikia Baba, ila kwa njia ya Yeye. Pamoja na hayo ilimpasa Yesu kusulibiwa na kufufuka tena kutoka kwa wafu,ili atimize ahadi zake kuwa Ukweli unaodumu milele. Siku moja sisi sote tutatokea mbele ya huyu Mwenye Utukufu kuwa waongo; lakini yeye aaminiye ndani yake atabadilishwa na kuishi kwa haki na mwenye ukweli na kutoroka katika msitu wa maongo.

Hatuwezi kusimamisha uchafu na wingi wa media zinazoonekana kwenye TV, redio, magazeti ya kila siku au ya wiki au ya mwezi pamoja na sikukuu za sherehe. Madanganyifu hayo yanakusudiwa kuongoza ujumla wa watu wanavyotaka, na matokeo yake wamekwisha kuhisi mapema kwa malengo na faida zao. Kwenye siasa wasemi wengi wanawasingizia wapinzani wao na kusukuma mbele chama chao kuwa ndiyo ukweli wa mwisho na ufumbuzi wa mwisho. Matokeo madogo yatapotoshwa na makosa makubwa yatafunikwa kabisa. Ukweli unaopindika unajaribu kuwashangaza wapinzani na taarifa za habari zilizopindwa kwa hila zinatokeza chuki.


11.5 - Maongo ya Kila Siku

Si kwamba maongo yanatawala maneno ya wana-siasa wengi, lakini pia na maisha yetu ya kila siku. Ukweli hupinduliwa haraka, na watu mara nyingi huwasingizia wengine wakati wa kunywa kikombe cha kahawa na wenzao. Lakini mara huyu anayesingiziwa akitokea, watu hao wanacheka-cheka na kuongea mengineyo katika namna ya unafiki, ambayo namna hiyo ni tabia zetu tangu utoto wetu. Pengine sisi hatujatamka maongo makubwa ya kuumiza, lakini pengine tumemsengenya fulani au kusema singizio ndogo tu, yote yakiwa na uchokozi kutoka kwa “baba wa uongo”. Tunatakiwa kuungama kwa kweli na wakati wowote kusema habari za watu ambao hawapo, kana kwamba wapo pamoja nasi. Hakuna uongo nyeupe! Hakuna kweli nusu! Hayo yote ni ya kufisha tu. Twaweza kukomesha maongezi ya mzozo kwa kumwelekea moja kwa moja yule anayeongelewa na kupata habari kamili kwake, ili kuweka mambo sawa na katika hali ya kweli. Twahitaji kuinuka kwa ajili ya watu wa kusemwa, badala ya kuchukuliwa na jumla ya wote. Amri ya tisa inatufundisha kutenda kama samaki anayeogelea kinyume cha mtelemko wa maji yaliyo mfano wa maongo mengi. Mara nyingine tutajikuta katika hali ya hatari, ambapo tunatakiwa kusema haraka kuhusu jambo lisilopendwa na wengi. Lakini hatupendi kupoteza uso wetu, wala hatutaki kusema juu ya marafiki au jamaa ambao sasa hawapo. Kwa hali hizo mara nyingi tunakimbilia kwa manano ya nusu-kweli au kufunika na maneno mengi matupu na maelezo ya ujanja. Kuna watu wanaopata udhuru haraka kuliko panya anavyopata tundu lake.

Kusema uwongo kumetia sumu katika ushirikiano wetu. Hakuna amwaminiye mwingine kabisa! Wengi wanaelekea kufikiri kwamba, wale wanaosema wanakusudia jambo kinyume kabisa na yale wanayoeleza. Hali ya kutokueleana inatenganisha watu na kuwafanya wawe na upweke, kana kwamba kuna kipande cha kioo katikati yao. Maongo yanawaweka watu katika hali ya upweke! Maumivu ya moyo yanajiinua na kutetemeshwa katika muda hizo za ukimya. Tunatakiwa kutumia nguvu za Yesu na kukiri kwa uwazi maongo yote na masingizio yanayopotosha. Tunahitaji kuwaomba wale waliotendewa yasio ya kweli tupu watusamehe. Hivyo tumaini linajengwa tena na kiburi itabomolewa.


11.6 - Nani ataweza kumfahamu kweli ndugu yake ?

Itafaa sisi tujipime wenyewe tuone, kama kwa kweli tunamfahamu ndugu au dada yetu, jinsi Mungu anavyotutambua vyema. Yesu alichoma hukumu zetu za juujuu na kutuonya, „Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtahukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huliangalii? Au utamwambiaje nduguyo, niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako” (Mathayo 7:1-5).

Yeyote anayetambua ingawa kidogo kuhusu agizo hilo kutoka katika Hotuba ya Mlimani, basi atanyamaza na kwa kujichunguza kwa makini mwenyewe kwanza kabla ya kuwahukumu wengine. Pengine ndugu yetu kweli ametenda kosa kilicho kidogo kama kibanzi jichoni, lakini sisi wenyewe hatutaki kukubali kwamba kuna maboriti mengi katika macho yetu, kutosha kwa kufungua mashine ya kupasua mbao! Yesu angependa kumwonyesha kila mmoja wetu ile chuki, mawazo machafu pamoja na matendo, uchoyo, unyimivu, udanganyifu, unafiki, na kutokuwaheshimu wazazi na pia siku ya Bwana! Yeyote anayejikana mwenyewe chini ya thibitisho la Roho Mtakatifu, hataendelea kuwakataa wengine au kuwasengenya kutokana na kiburi au ukuu fulani, lakini ataanza kuwaza namna ya kuwasaidia hao jinsi Mungu anavyotusaidia sisi sote.

Hatuwezi kuwahukumu wengine kwa haki, kwa vile hatuwezi kuelewa kabisa habari zote na shida za fulani. Je, sisi tungalifanyaje tungalikuwa mahali pake? Au yeye angalikuwaje, kama angalitambua baraka na njia za uongozi tukufu jinsi sisi tunavyozitambua? Kwa kusema, “umpende jirani yako kama nafsi yako” Mungu anatuonyesha jinsi ilivyo ya muhimu sana; tuwe waangalifu mno tunapofikia hatua ya kumhukumu ndugu yetu. Bora tumpende tu.

Mambo hayo yanaleta na tatizo la kuapa kama mshahidi: nani anafahamu kama kweli tuliona mambo jinsi yalivyotendeka kabisa na kuyakumbuka kikamilifu? Kwa kweli hatuwezi kuona mambo kamili jinsi Mungu anavyoyaona. Ikiwa twamhukumu ndugu yetu, uamuzi wetu kwa vyovyote inabaki kuwa ya upungufu. Tunapozingatia hayo vema, hatutarukia maamuzi kuhusu wengine si kwa haraka, lakini tutawaza kwa makini na pamoja na maombi na kujaribu sana kuwaelewa watu kabla ya kutamka jambo. Heri Mungu angetujalia kuwa na macho ya hali ya mama, sio ya hali ya polisi!


11.7 - Jinsi gani tuseme Ukweli?

Tunapotambua upungufu wa uwezo wetu basi tutaweza kufanyaje, ili kutambua yaliyo kweli? Je, tunahesabia kusema uongo kuwa lazima na kweli hasa kuwa mbaya? Hapana, hata kidogo! Kama mashahidi tulioona kwa macho yetu, inatupasa kueleza yaliyo kweli kufuatana na ufahamu wetu. Tunatakiwa kumwuliza Mungu atupatie hekima, ili tusipate kuwa si sawa kwa ndugu na dada zetu. Waumini wanahitaji neema ya pekee wakati wa kuteseka, ili waweze kueleza kweli tupu kwa njia iliyo sawa bila kupotosha mambo. Twahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu, ili tusije tukahatarisha maisha ya waumini wengine. Lazima tuseme ukweli wakati wowote, lakini haitupasi kila mara kusema yote yaliyo ya kweli kwa ajili ya usalama ya wengine. Wale wasiomfuata Yesu pengine watafikiri tunawaambia uwongo kwa vile hawajaelewa roho ya ukweli. Hawawezi kutambua kwamba, Roho Mtakatifu atuongoza kila wakati kusema yaliyo kweli.

Biblia inatusaidia kuzoezwa kila wakati maishani mwetu, shuleni, hadharani na katika familia zetu, kudokeza na kusifu mambo bora maishani mwa ndugu na dada zetu, wala tusilaumu makosa yao yaliyopo nayo. Tutafakari pasipo shaka habari ya rafiki zetu, pia na juu ya adui zetu, na bila kusema uongo. Paulo aliwaeleza Wakorintho, „Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote.“ (I.Wakorintho 13 : 4-8a).

Ikiwa twaishi katika roho ya upendo, hatutawahukumu wenye dhambi hata kidogo. Badala yake tutafanya juu chini kuwaelewa vema, kusaidia, au kusawazisha mambo ya mwenzetu katika roho ya uvumilivu na upendo. Paulo aliwaandikia waumini wa Efeso waliofikia kiasi kikubwa cha kukomaa katika kuendesha huduma za Kikristo alipotaja hivi: “Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha mwenzake.“ (Waefeso 4:25). Kila wakati twajibidiisha kujifunza na kusema ukweli. Lakini hata hivyo tukikomaa kiasi gani katika kumfahamu Roho Mtakatifu, Shetani kila wakati anafanya juhudi kuwajaribu waumini waseme uongo, wahukumu wengine vikali na kuwachukia watu wenye misimamo mingine. Jinsi Yesu mwenyewe alivyopata majaribu, sisi nasi tutajaribiwa. Ndiyo maana Paulo aliwaandikia Waefeso, „Hatimaye, ndugu zangu, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho“ (Waefeso 6: 10-12).

Yohana, mtume wa upendo, kwa maana hasa anatuonyesha mizizi ya kusema uongo maishani mwa mtu akisema: “Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia (I.Yohana 2:22-23). „Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuwamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe“ (I.Yohana 5:10). Kushikamana na kweli kuhusu Mungu wa Utatu kama kiini cha maisha yako inamaanisha kwamba utadumu na ukweli katika maisha yako ya kila siku.


11.8 - Werevu wa Mungu katika Kurani

Uislamu hasa unaonyesha ukweli kama roho ya kigeni. Katika Sura Al Imran tunasoma, „walikuwa na wajanja, na Allah alikuwa mjanja na Allah ni mbingwa wa wote walio wajanja“ Hapo ujanja ulihusika na Wayahudi waliofanya shauri kumwua Yesu. Lakini Allah, kufuatana na ufahamu wa kiislamu, aliwazulisha, akamwokoa Yesu kutoka kwa mateso ya msalaba na kumwinua awe mzima. Hii inamaanisha kwamba Allah hakuruhusu Yesu asulibiwe, lakini alimwinua juu kwake kwa njia ya ujanja wake kuu. Hayo yote ni upotovu kabisa ya mambo yaliyotendeka katika historia yetu, ambapo mahali na wakati zinashuhudiwa kwa uhakika. Allah alihitaji kufunua tabia yake ya kweli mbele ya msalaba, na ilimpasa kuonyesha kwamba yeye si kweli ndani ya nafsi yake, kwamba yeye si Mungu wa kweli, bali adui wa kweli, mkuu wa wajanja wote. Msalaba, kama kilele cha kweli yote, ilimfunua Allah wa Uislamu jinsi alivyo hasa.. Kipekee ibilisi angetaka kukataa ukweli wa msalaba, ili watu wasingepata kuokoka na kupokea uzima wa milele.

Uislamu unamwonyesha Allah ndani ya Kurani kama „mjanja mkuu kuliko wote“, khairul makirin. Hivyo si ajabu, wafuasi wake wanaona ujanja kama nguvu na namna inayokubalika kujipatia chochote wanachotaka, na pia njia ya kusaidia sana ya kutangaza dini ya Uislamu. Mhamadi aliruhusu kusema uongo na udanganyifu katika namna nne: Katika vita takatifu ya kueneza Uislamu (djihad), katika kuwapatanisha adui wawili, mwanaume mbele ya mkewe, na mke mbele ya mumewe. Ndani ya Uislamu huwezi kumwamini rafiki yako wala adui yako. Kila mmoja hamwamini mwenzake, kwa sababu kuna upungufu wa tegemeo kati ya Waislamu.


11.9 - Uongo wa maisha au Ukweli wa Mungu

Ikiwa wewe hutamkubali Huyu aliyesulibiwa na kufufuka kutoka kwa wafu, roho ya ukweli hatakuwa ndani yako. Maisha yako yote yatakuwa ya uongo na kujidanganya mwenyewe kwa sababu ya kukataa kusulibiwa kwake Yesu. Huyu Yesu alimwaga damu yake msalabani ili aweze kulipia kama kuhani mkuu wetu dhambi za watenda dhambi na wasema uongo wanaoungama. Baada ya kufufuka kwake toka kifoni alimwaga Roho ya kweli juu ya wale waliongojea katika maombi, ili wapokee ahadi ya Baba. Roho Mtakatifu alitokea kwao kama ndimi za moto. Hii inaeleza jambo ambalo Yesu alikusudia kuwatendea wanafunzi wake: Wapate kuchomwa ndimi zao za kutamka uongo na kupokea ndimi mpya na za kiroho,zilizoweza kutamka ukweli wa milele. Ni nini ukweli wa milele? Kwamba, Mungu ni Baba yetu, Kristo ni Bwana na Mwokozi wetu na Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu. Mungu wa Utatu ndiye hali halisi wa milele, ambalo roho wa ukweli anaikiri kwa njia ya wafuasi wa Kristo. Hii ndiyo mapendeleo yetu ya kuweza kutamka ukweli Wake kwa upendo, kutangaza kazi Yake ya kulipia msalabani kwa ajili ya wanadamu wote.

Jinsi ilivyo ya ajabu kuwa na rafiki aombaye, anayekueleza ukweli katika upendo! Rafiki wa namna hii ni bora kuliko watu elfu wanaokusifu-sifu kila wakati. Kwa sababu hiyo, tunahitaji kumwuliza Yesu atusaidie kutamka ukweli kila wakati katika upendo na kuwaombea rafiki zetu. Hili ndilo ambalo Yesu anatuagiza: „Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu“ (Mathayo 5:37) Tunatakiwa kumwuliza Yesu atufanye tuwe waaminifu kabisa ndani yake na atuongoze tuweze kusema ukweli Wake katika upendo.

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 05:28 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)