Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 118 (Jesus appears to Mary Magdalene)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)
1. Matukio siku ya Pasaka asubuhi (Yohana 20:1–10)

c) Yesu anamtokea Mariamu Magdalene (Yohana 20:11–18)


Yohana 20:17-18
“Yesu akamwambia, Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu, naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu, naye ni Mungu wenu. Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba amemwambia haya”.

Mariamu, katika hali ya kumwabudu, akaanguka mbele za Yesu, akijaribu kubusu miguu yake na kumgusa, kumshika bila kumwacha tena. Yesu akamzuia asimguse, kwa sababu upendo wake ni wa kiroho. Alikuwa amemjalia kusikia sauti yake na kuwepo kwake, naye akataka imani yake ikue kwa umoja na Utatu Utakatifu. Hayo alidokezea wazi katika maneno yake ya kuaga kwa wanafunzi wake muda kabla ya hapo. - Si kwa kumgusa, wala kushikamana naye kimwili itaumba umoja naye, bali ni imani ndani ya kuwepo kwake kiroho inayounganisha naye kweli.

Yesu alimwambia kwamba hatabakia duniani baada ya kifo chake; na kutokea kwake itakuwa sio ya kudumu, kwa vile mwelekeo wake ni mbinguni. Lengo lake ilikuwa ni kupaa na kurudi kwa Babaye. Njia ya kurudi kwa Mungu sasa ilikuwa wazi baada ya kujitoa kuwa dhabihu msalabani. Hivyo huyu Kuhani Mkuu aliazimu kutoa Sadaka ya damu kwa Mtakatifu Baba. Basi anamwambia Mariamu, “Usinishike, maana niko nikihitaji kutimiza haki zote; nitakuombea, nami nitakujaza na nguvu ya Roho Mtakatifu.” Naye maneno yake yanamweleza kwamba, yeye hakuja kwa ajili yake tu, bali kwa binadamu wote, “Rudi kwa wanafunzi na ukawajulishe habari ya kuwepo kwangu, makusudi yangu na kupaa kwangu!”

Kwa njia ya ujumbe wake kwa wanafunzi kupitia kwa Mariamu, aliwafariji wote. Akawaita ndugu. - Kwa imani na sisi tutapata kuwa ndugu na dada zake, ni kwa sababu ya msalaba wake na ufufuo, pia na maisha ya bila kufa tena. Anatuita na sisi ndugu, wala si wapendwa tu. Wokovu umekamilika, nasi tumejengwa ndani ya haki zetu za kuwa wana (Adoption). Yeye aliweka sahihi kwenye mkataba wa uwana wetu tukufu kwa damu yake.

Kiini cha ujumbe wa Mariamu ni nini, ambao alitakiwa kuwapatia wanafunzi kwa matamshi yake? Jambo kuu la kwanza ni kwamba, yu hai. Yeye kukutana naye ilikuwa ni jambo la kihistoria. La pili kwamba, hata Baba yake sasa ni Baba yetu; kwa ahadi hiyo Yesu aliwavuta wanafunzi wake ndani ya umoja kamili na Mungu. Yesu hakusema habari ya Mungu aliye mbali, mwenye uwezo wote na mhukumu, bali kwamba ni Baba mwenye kuwapenda na wa karibu kabisa. Kwamba yeye sio Baba wa Kristo tu, lakini pia ni Baba yetu. Alimtaja Baba “Mungu wangu”, kwamba, yeye kwake ni kila kitu. Anaendelea kuwa mwaminifu kwa Babaye, wakati uumbaji wote umetengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi. Lakini sasa yeye si adui wetu kutokana na dhambi zilizotangulia kutendeka, bali atupenda sisi tuliosamehewa kwa ukombozi wa msalabani. Jinsi anavyotawala katika umoja na Baba yake, ndivyo anavyotutaka tuishi ndani ya umoja wa Utatu kwa njia ya kutumwagia Roho yake Mtakatifu, ili na upendo uweze kutiririka kutoka kwetu kwa watu.

Hivyo Kristo akaweka ahadi ya ushirikiano kamili kwenye midomo ya huyu mwanamke, aliyemwona kwanza baada ya ushindi wake juu ya kifo. Mariamu akawa mtii, akaondoka kutoka katika kuabudu miguuni pake akakimbia, ili kuwashuhudia hayo kwa wanafunzi wake, akitangaza na undugu naye na ubaba wa Mungu katika umoja na sisi kwa njia ya neema. Ujumbe huu, kama tarumbeta ya furaha, hujaza hata mioyo yetu yenye huzuni hata leo. – Je, furaha hii ya kukubalika na Mungu na uamsho wako wa kiroho umekufikia? Unaamini ujumbe wa Mariamu kama mtangazaji wa kwanza wa taarifa, kwamba Kristo amefufuka?

Sala: Tunakushukuru, Bwana Yesu, uliyefufuka kutoka kifoni, uliye pamoja nasi sasa, na kwamba unatuita ndugu zako. Sisi hatustahili kuishi katika ushirikiano wa karibu hivi pamoja nawe. Tunasema, Asante kwa kutusamehe dhambi zetu. Twaomba utufanye kuwa wajumbe wa furaha kwa wote wanaokutafuta.

Swali 122: Ujumbe wa Kristo mdomoni mwa Mariamu Magdalene kwetu ni nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 25, 2017, at 02:58 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)