Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- John - 129 (Future predictions)
This page in: -- Albanian -- Arabic -- Armenian -- Bengali -- Burmese -- Cebuano -- Chinese -- Dioula? -- English -- Farsi? -- French -- Georgian -- Greek -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- Javanese -- KISWAHILI -- Kyrgyz -- Malayalam -- Peul -- Portuguese -- Russian -- Serbian -- Somali -- Spanish -- Tamil -- Telugu -- Thai -- Turkish -- Twi -- Urdu -- Uyghur? -- Uzbek -- Vietnamese -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

YOHANA - Nuru inaangaza gizani
Somo la Injili ya Kristo kufuatana na Mtume Yohana
SEHEMU YA 4 - Nuru Inashinda Giza (Yohana 18:1 - 21:25)
B - UFUFUO na KUTOKEA KWAKE KRISTO (YOHANA 20:1–21:25)
5. Yesu atokea kando ya ziwa (Yohana 21:1-25)

c) Yesu kutabiri habari ya mambo ya mbeleni (Yohana 21:20-23)


Yohana 21:20-22
„Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) Basi Petro akamwona huyu, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi.“

Petro alikabili wito wa Bwana wake kuchunga kondoo na kondoo jike zake. Yohana akiwa mwenye umri mdogo kati ya wanafunzi, Petro alitamani sana kugundua msimamo wa Yesu kumhusu Yohana. Atamrudisha nyumbani kwa ajili ya ujana wake, au atampa cheo cha afisa mdogo katika mashambulio?

Pengine kulikuwa na dalili ya uchoyo ndani ya maneno ya Petro, kwa sababu Yesu alielekea kumpendelea Yohana zaidi ya wengine na kumpenda zaidi. Kwenye chakula cha jioni, kile cha mwisho, Petro alikuwa amemdokezea Yohana awe mjumbe kwa Bwana kutuliza hali ya hangaiko na ataje jina la msaliti.

Wakati wote Yohana alikuwa karibu na Yesu, hata pale penye Msalaba alisimama karibu naye, akihatarisha maisha yake mbele za maadui wa Kristo. Yeye naye alikuwa wa kwanza kuamini kwamba Bwana amefufuka, na wa kwanza kumtambua hapo penye uvuvi ziwani. Alikuwa tayari akimfuata Yesu, wakati Petro alipoitwa kumfuata. Moyo wake ulikuwa umeunganika vema na Kristo. Alikuwa na uhusiano wa karibu zaidi na Bwana kuliko wanafunzi wengine.

Labda Petro alimwuliza Yesu, kama Yohana atakabili mazito mbeleni jinsi yalivyotabiriwa kwake, au kama ilikuwa ni kwa ajili yake pekee. Yesu akamjibu mtume mkuu kwamba, haimpasi yeye kutawala juu ya wengine, lakini kuwa ndugu kati ya wengine walio sawa naye. Haikumpasa kujishughulisha na yale yatakayompata Yohana, aliyekuwa na uhusiano wa mmoja kwa moja kwa Bwana wake, wakati Petro alikuwa ni msemi kwa niaba ya mitume wote. Yohana alibakia kimya, akiimarisha kwa sala na subira maendeleo ya mafundisho ya taratibu za Kanisa, pia na kujaribu kuyasawazisha kwa nguvu za maombi (Mtd.3:1; 8:14; Gal:2:9)

Twatambua kutokana na miadi ya Yesu mapema zaidi kwa ajili ya shughuli ya Yohana kwamba, si muhimu sana, kama tutaishi muda mrefu hudumani mwa Kristo, au kama tutakufa mapema kwa ajili yake. Muhimu zaidi ni uaminifu na utii wetu daima kwake. Yesu hawachukui wafuasi wake kana kwamba wote ni wa namna moja, bali anatayarisha nja ya pekee kwa kila mmoja kwa kumtukuza Bwana wake. Hatusikii lolote kuhusu kifo cha Yohana; inahisiwa kwamba alifia kifo cha kawaida.

Yesu anamwomba Petro amtazame yeye tu, wala asichungulie kwa wanafunzi wengine. – Kwetu inamaanisha kwamba haitupasi kuchokozwe na maendeleo makubwa ya Wakristo wengine, bali tujibidiishe kufahamu zaidi mapenzi ya Mungu ndani ya maisha yetu, na tumfuate mara, bila madai. Ufuasi kwa uaminifu ndiyo lengo la kila Mkristo

Yesu pia alisema na wanafunzi wake habari ya kurudi kwake mara ya pili. Kuja kwake ndiyo lengo la historia ya ulimwengu. Mawazo ya wanafunzi wote yalielekezwa kwenye tukio hilo la mbeleni. Pamoja na kuwepo kwake Mungu kati ya watu, tumaini la vizazi vyote itatimilika: Yesu atarudi katika utukufu. - Wewe je, unamtazamia na kujitayarisha kwa sala, huduma, nyimbo takatifu, pia na ushuhuda wako takatifu? Tutakuta kuwepo kwake katika majeshi ya waumini wanaomfuata kwa karibu kiimani, bila ya kumfuata mwingine.

Yohana 21:23
„Basi neno hilo liliendelea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Walakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe?“

Usawa wa maoni ni kwamba Yohana aliishi maisha marefu, na akawa kama ishara ndani ya Makanisa kuhusu matazamio ya Masihi kurudi. Kati ya wale walioishi naye imani fulani ikakua kwamba hatakufa hadi Bwana atakaporudi. Paulo naye alitazamia kurudi kwake Bwana mapema, na pengine hafi, bali atabadilishwa mara na kuchukuliwa mbinguni. Yohana alikuwa akifikiria mambo yalivyo na kudokeza kwa wazi kwamba ahadi ya Kristo haikuwa na maana kwamba Yohana hatakufa hadi mbingu itafunguka na Mwenye Utukufu atokee. Shabaha na maamuzi yake hayakulingana na matazamio ya Petro. - Bwana husalia kuwa Mchungaji Mwema aongozaye wanafunzi wake kila mmoja katika njia yake ya kipekee.

Sala: Bwana Yesu, wewe ndiwe Mkombozi mwenye utukufu, Mchungaji mwaminifu. Asante kwa kuwaongoza Petro na Yohana katika njia za kumfaa sana kila mmoja, ili wakutukuze wewe maishani na kifoni. Utujalie na sisi tukufuate wewe tu. Waongoze na jamaa zetu na marafiki kwenye lengo la kurudi kwako, ili wao nao wajitayarishe kwa furaha Kwa kuja kwako hivi karibuni.

Swali 133: Maneno ya mwisho ya Krsto ndani ya Injili hii yanamaanisha nini?

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on June 29, 2017, at 06:11 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)