Home
Links
Bible Versions
Contact
About us
Impressum
Site Map


WoL AUDIO
WoL CHILDREN


Bible Treasures
Doctrines of Bible
Key Bible Verses


Afrikaans
አማርኛ
عربي
Azərbaycanca
Bahasa Indones.
Basa Jawa
Basa Sunda
Baoulé
বাংলা
Български
Cebuano
Dagbani
Dan
Dioula
Deutsch
Ελληνικά
English
Ewe
Español
فارسی
Français
Gjuha shqipe
հայերեն
한국어
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
Кыргызча
Lingála
മലയാളം
Mëranaw
မြန်မာဘာသာ
नेपाली
日本語
O‘zbek
Peul
Polski
Português
Русский
Srpski/Српски
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
ไทย
Tiếng Việt
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Uyghur/ئۇيغۇرچه
Wolof
ייִדיש
Yorùbá
中文


ગુજરાતી
Latina
Magyar
Norsk

Home -- Kiswahili -- The Ten Commandments -- 02 -- Introduction: The All-Importance of the Ten Commandments
This page in: -- Afrikaans -- Arabic -- Armenian -- Azeri -- Baoule -- Bengali -- Bulgarian -- Cebuano -- Chinese -- English -- Farsi -- Finnish? -- French -- German -- Gujarati -- Hebrew -- Hindi -- Hungarian? -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Norwegian -- Polish -- Russian -- Serbian -- Spanish -- Tamil -- Turkish -- Twi -- Ukrainian -- Urdu? -- Uzbek -- Yiddish -- Yoruba

Previous Lesson -- Next Lesson

TOPIC 6: AMRI KUMI - Kuta za ulinzi wa Mungu zinazolinda wanadamu wasianguke
An Exposition of the Ten Commandments in Exodus 20 in the Light of the Gospel

02 - Utangulizi Kwa Amri Kumi: Mungu Ajifunua Mwenyewe



KUTOKA 20:2
Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka katika nyumba ya utumwa.

Amri Kumi hazilazimishi watu kufuata taratibu za halali za maagizo fulani au sheria zilizo ngumu, ambazo zilifunuliwa na malaika, hapana.Kwa njia ya hizo Amri Kumi Mungu mwenyewe asema na watu. Mwumbaji awakaribia viumbe vyake, na aliye Mtakatifu asogea karibu sana na watu walio wenye dhambi.


02.1 - Nafsi ya Mungu

Neno la kwanza kwenye Amri Kumi ni „Mimi“. Mungu aliye hai asema nasi akiwa nafsi, si kama roho ya wasiwasi, wala si kama ngurumo ya kutisha inayosikika toka mbali. Lugha yake ni rahisi kusikika. Anatamani kujenga uhusiano wa binafsi nasi, tena unaoaminika kabisa. Anawasiliana nasi kwa neema yake, si kwa sheria au ghadhabu. Ni mapendeleo makuu kwetu kwamba YEYE atuelekea kwa hisani na upendo.

Watu kwa upumbavu wao waweza kutokumjali Mungu mwenye Enzi na kwenda mbali na wema wake. Hata hivyo, Mungu Mtakatifu atuona popote tuendako. Tuko machoni pake wakati wowote. Kwa sababu hiyo kila mwenye hekima ingmpasa kuitika kwa maneno yake. Jambo hilo kwamba atuambia: „Mimi“ linamaanisha kwamba tumeinuliwa kwenye usawa wa kusema „Wewe“, na hivyo kuweza kusema naye kama viumbe wenye nafsi ya kutambuliwa.

Kwa yote hayo ni wazi kwetu mbali na uvuli wowote wa mashaka kwamba, Mungu wa Milele mwenyewe, Mtunzaji na Mwendelezi wa yote, huyu Hakimu asiye na mwisho asema nasi binafsi. Kwa sababu hiyo, tumsikilize kwa makini, na kutunza Neno lake kwa furaha na kushangilia.


02.2 - Kuwepo kwake Mungu

Mungu hufunua kuwepo kwake kwetu anaposema „Mimi ndimi“. Basi, jinsi gani watu waweza kudai kwamba, hakuna Mungu? Kudai kwao wasemao „Hakuna Mungu“ mwishoni hufikinya mbele ya ushuhuda huo wa Mungu, maana huyu „Mimi ndimi“ ndiye sababu ya kuwepo kwetu. Mungu yupo! Yote mengine yatakoma, Yeye pekee ni wa milele. Muda pia na mwanadamu hukaidi dhidi ya Mwumbaji wake,kana kwamba anagongana na mlima mkubwa.

Lakini ukweli hautegemei maneno ya watu wanayosema juu ya Mungu, au maneno yanayoandikwa na wakina sayansi (watu wa maarifa). Yeye ndiye Kweli na Yeye hujaa ulimwengu kote. Watu Fulani walikataa jambo hilo miaka elfu tatu nyuma, enzi za Mfalme Daudi, wakidai kwamba, hakuna Mungu (Zaburi 14). Basi, mtunga Zaburi aliwaita wapumbavu, kwa sababu walipuuza ukweli unaoonekana na kumpita Yeye ashikaye na kutunza ulimwengu wote. Tena wasioamini waliishi katika kutenda dhambi bila kujali dhamiri.

Ushuhuda wa Mungu juu yake mwenyewe hukanusha ule msingi, ambao Buddha alijenga maoni yake ya kidini. Nirvana inayofundisha habari ya kujikinahi na kuweka hamu ya kufa hadi hapo roho wa mtu imemezwa ndani ya ile iitwayo “Hakuna kuu”; hii nayo si hivyo.

Mungu awahitaji watu waishi. Yeye yu hai na kutushuhudia kwamba “Mimi nipo”. Hali hiyo kwamba yupo inatia maana na shabaha ndani ya maisha yetu. Yeye atutaka tuishi jinsi Yeye aishivyo. Lengo lake kwa ajili yetu si kwamba tupate kutokuwepo.

Ushuhuda wa Mungu nao unafisha mafundisho yote ya kanuni kwamba yanayoonekana tu kwa macho ndiyo kweli. Ni mtu tu asiyeona mbali awezaye kukataa kuwepo kwa ulimwengu wa kiroho. Kwa kweli, huyu ni kama jiwe adumuye chini ardhini, wakati ndege huruka hewani. Mungu yu hai naye asema nawe. Naye husema hata na mtu aaminiye tu vitu vinavyoonekana, pia na mtu asiyeamini habari ya Mungu kabisa, pia husema na Kommunisti, ili ikiwezekana mtu awaye yote aweze kuelekeza sikio lake Kwake na kupata kuwa mwenye hekima. Yeyote akataaye kusikiliza na kufanya moyo wake kuwa mgumu, basi atafanana na kipofu, anayedai kwamba hakuna jua, kwa vile yeye hawezi kuliona.


02.3 - Huyu Yahweh ni nani?

Mungu alisema na Musa, “Mimi ndimi Bwana“. „Mimi niko, ambaye niko“, ndiyo tafsiri ya karibu kabisa na maandishi ya Kiebrania katika kitabu cha Kutoka, 3:14. Inaeleza hali ya kuwepo kwake Mungu, ambaye hatakwisha, bila masharti, na asiyehitaji kutegemea mtu au kitu. Mungu yuko kwa namna isiyolingana na hali ya mtu mwingine au kitu kingine. Yeye habadiliki, na hii ndiyo msingi wa imani yetu, tena ni jiwe la pembeni kwa wokovu wetu. Pamoja na mipaka yetu yote na kujaa kwetu na dhambi, Mungu asiyebadilika anadumu kwetu kuwa mwaminifu kabisa. Tumejaliwa kurudi kwake kwa sababu ya uaminifu wake. Hata tunapo kabili mwisho wa ulimwengu huu, Mungu atufariji akisema: „Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.“ (Math.24:35)

(Jina la „Yahweh“ lipo Kut.6:2, ambapo kwa Biblia ya kiswahili twasoma „Yehova“, na penginepo pengi twasoma „Bwana“.)

Mungu mwenye enzi yote huongoza kila kitu: Yeye hufahamu yote, hutambua yote, mwenye kujaa kote na mwenye hekima ya mwisho. Ikiwa milango yote yamefungwa, Yeye hutupatia njia ya kutoka. Yeye hutambua kujisikia kwetu, pia na mawazo yote. Yeye hatuhitaji tudondoke miguuni pake kwa kutishwa. Badala yake Yeye huumba ndani yetu tumaini la kweli na tegemeo ndani yake. Yeye husema nasi, ili tuweze kuinua macho yetu kwake katika hali ya tumaini. Yeye hutamani kuwa Bwana wa maisha yetu. Loo, asingekuwepo mtu anayeficha uso wake mbele ya Mungu wetu mwenye subira, maana Yeye anangojea jibu letu!

Kama fulani anarudi kwa Mwumbaji wake, basi anaitika kwa wema wake wa upendo na rehema. Mungu anaposema, „Mimi ndimi Bwana“, anatamka pia kwamba, Yeye ni Bwana pekee, wala hakuna mwingine. Roho zote zingine au miungu ni upuzi Nyakati zetu, ambamo roho na mafundisho ya kisirisiri hugeuzwa katika dini za kisasa; ila wanaopagawa na mapepo waweza kuwekwa huru, wanapoweka tegemeo lao ndani ya Mungu wa kweli. Siku hizi ambapo hali ya kuwa hakuna Mungu inapungua, basi watu huelekea upande wa pili kabisa na kufungwa katika mazoezi ya kisiri na kushkwa na roho za kishetani.

Matangazo ya roho hizo yako kote kwenye redio, television na magazetini pia.

Katika Injili, Yesu husema „Mimi ndimi“, ambalo ni tamko la kuunganisha kwenye Amri Kumi. Maana kwa kusema hayo, Yesu anathibitisha kwamba ndiye Bwana (sawa na amri ya kwanza); tena kwamba ndiye anayetajwa na Habari Njema za malaika kwa wachungaji makondeni Bethlehemu. Baadaye Yesu aendelea hatua nyingine na kusema, „Mimi ndimi mkate wa uzima“, „Mimi ndimi nuru ya ulimwengu“, „Mimi ndimi mlango“, „Mimi ndimi njia, kweli na uzima“. Yesu pia alitamka, „Mimi ni Mfalme“, „Mimi ndimi mwanzo na mwisho“. Tangu hapo, wafuasi wake wameendelea kushuhudia bila mashaka yoyote, „Yesu ndiye Bwana“. Yeye habadiliki, naye atuokoa na dhambi yoyote. Alithibitisha hali yake na enzi yake alipofufuka kutoka kwa wafu. Daima tangu hapo, mwanzo wa hizo Amri Kumi unasikika kuwa faraja kwetu, tunaposikia, „Mimi ndimi Bwana“.

Musa bado hakuwa na utambuzi wa wazi kuhusu kuja kwake Bwana wake mwilini. Lakini miaka 1,350 kabla ya kuzaliwa kwake Yesu alipokea maneno ya msingi ya mafunuo, ambayo Mungu aliyatumia kujitambulisha kwetu, akisema, „Mimi ndimi Bwana Mungu wako“.


02.4 - Mungu ni nani?

Kwa lugha ya kiebrania Mungu hujiita „Elohim“, ambalo limetafsiriwa kwa kiarabu kuwa „Allah“. „Elohim“ inaweza kusomwa kuwa „“Eloh-im“, wakati „Allah“ ni „Al-el-hu“.

„Al“ ni tamko halisi lenye maana „Ndiye“. „El“ ndilo jina la awali kwa Mungu katika mazingira yatokanayo na Shemu, na maana yake ni „nguvu“. Yesu alitangaza maana ya msingi ya jina „El“ na kulithibitisha aliposhuhudia mbele ya baraza kuu la kiyahudi, „Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu (Math.26:64).

Yale maneno „-im“ na „-hu“ ni sehemu ya neno inayowekwa mwishoni. Neno la kiebrania „-im“ linaonyesha kwamba si moja tu, ambapo „-hu“ kwa kiarabu ni pekee kwa ajili ya moja tu. Hivyo ule umoja wa Utatu Utakatifu kwa neno la „Allah“ limeondolewa kimsingi, iwapo kwa neno la „Elohim“ linaruhusu uwezekano wa Mungu katika Utatu.

Bwana wa milele yeye siye mwenye kujua yote tu, mwenye Hekima yote na mwenye kuwepo kote, lakini zaide naye ni mwenye enzi yote. Yeye pekee ulimwenguni ni mwenye enzi ya kujenga kwa Neno lake la Enzi, aliyeumba ulimwengu wote kutoka katika SI KITU (nothing).

Yeye ni mvumilivu kwa kila mtu. Bwana wetu si wa kubomoa, sio mjeuri, ampelekaye mtu kote atakako au kumpotosha yeyote aonavyo yeye (Suras al-Fatir 35:8 na al-Muddathir74:31).

Kinyume cha hayo, Mungu wetu anatamani „watu wote waokolewe, na kupata kujuayaliyo kweli“ (I.Timotheo 2:4) yenyewe Katika Agano la Kale, tunkuta watu, ambao majina yao na nchi zao zimeunganishwa na jina „El“. Watoto wao walipewa majina kama Samuel, Elijah, Eliezar na Daniel. Pia miji yao wakaita Bethel, Jezreel na Israel. Kwa kufanya hivyo, walijifunganisha kwnye hiyo „Enzi“ inayotawala ulimwengu wote. Katika Agano Jipya watu nao waliunganishwa kipekee na Mungu, kwa vile aliwaahidia wafuasi wake, „Mtapokea nguvu, akiisha kuwajalia juu yenu Roho Mtakatifu (Matendo 1:8). Mungu hawakatai wenye dhambi, lakini anawasafisha, anawatakasa na kuishi ndani yao.

Ni Bwana wetu Yesu Kristo, aliye Mwenye Enzi yote, ambaye kwake mamlaka yote mbinguni na duniani imekabidhiwa. Hata bomu za atomic hazina uwezo kwa kulinganisha na enzi yake ya milele; mamlaka yake haitakuwa na mwisho.


02.5 - Mungu upande wa uislamu ni nani?

Kule kushika miguu kwa Mwenyezi kunawaongoza Waislamu walie „Allahu akbar“, maana yake, „Allah ni kuu zaidi“! Hivyo, Mwislamu anamwona Allah kuwa „mzuri zaidi“, na mwenye „busara zaidi“ kuliko wengine. Basi Allah katika Uislamu anakuwa mkubwa, mwenye nguvu, na wa kutokufikiwa na watumwa wake. Hakuna akili ya binadamu wa kuweza kumjua yeye. Yeye atujua sisi kabisa. Allah katika Uislamu ni aliye mbali mno, tena mbali kwa kuweza kumfahamu. Wazo lolote juu yake halitoshi tena si sahihi. Watu wanaojadiliana, hawataweza kabisa kumtambua Mwenyezi. Waislamu wanaweza tu kumhofu na kumwabudu wanapoanguka kifudifudi.

Wakina Sufi walijaribu kutengeneza madaraja kwa kuweza kumkaribia yule Allah Mkuu asiyeweza kufikiwa, lakini Kurani yenyewe hairuhusu jaribu lolote la kuwaza mfano kwa njia ya mawazo yao ya kibeduin.

Katika Uislamu, Allah adumu katika hali ya kutokuweza kuonekana, wala hakuweka aina ya agano na Waislamu. Muhammadi hahesabiwi kuwa msuluhishi kati ya Allah na Waislamu kwa kusudi la kuwafunganisha kwa Allah katika agano la kiislamu. Yeyey anawaagiza wote kumtii Bwana wao bila kuwa na vifungu.

Waislamu hawamtambui Mungu kwa asili yake. Matokeo yake ni kwamba, hawawezi kuwa na ufahamu juu ya dhambi zao hasa, wala hawatambui neema yake. Ibada katika Uislamu sio shukrani kwa Mwokozi kwa ajili ya kuwaokoa na dhambi, wala si kumtukuza kwa ajili ya kuwaondolea hukumu. Hivyo, ni kuabudu jule Allah wa mbali, mwenye enzi kama watumwa waangukao miguuni pa bwana wao katika hofu na mashaka. Azimio lao ni kumfuata Muhammadi, kwa sababu Uislamu unamkuza Allah, anayewatisha na bila kuwatakasa. Hawamshukuru mwokozi kwa kuwaokoa bure, kwa sababu Uislamu haina mwokozi.Hivyo haishangazi kwamba Mwislamu anadumu kufungwa katika kanuni na taratibu za kuabudu !

Hivyo basi, Mungu wa kweli aliyejifunua mwenyewe ndani ya Biblia hmbali na uumbaji na viumbe vyake. Ametukaribia kabisa na kutengeneza agano na sisi watoto wa Adamu anaposema, „Mimi ndimi Bwana Mungu wako.“


02.6 - Agano na Mungu

Neno „lako“ (letu; wako;wetu) litumikalo badala yangu (yetu) katika tamko hilo, „Mungu wako“ linamaanisha kwamba, „ni letu; ni mali yetu; tumemshika“. Maana yake ni kwamba, Mungu anaturuhusu tumshike, au tumwone kama mali yetu. Twaweza kumtegemea jinsi mtoto anavyomtegemea baba yake. Mwenyezi Mungu ajishusha chini kutuelekea sisi mbali na kuasi kwetu, kana kwamba kusema, „Mimi ni wako; je hutaki kutubu na kurudi kwangu na kujikabidhi kwangu mimi tu kwa siku zote?“ Hii ndiyo habari ya kutamani, kwamba Amri Kumi zinaanza na agano linalowekwa kati ya Mungu na watu. Ni agano ambalo Mungu peke yake alilitoa kwa watu wake. Ndani yake Mungu awahakikishia kuwepo kwake kwetu kwa upendo. Anatutazamia tuitike kwa kuwepo kwake kote kwa imani, tumaini na upendo kwake.

Ndani ya Agano lake na watenda dhambi, Mungu awathibitishia msamaha wake, wokovu na baraka. “Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu (dhidi yetu)” (Warumi 8:31)?

Anatutia moyo kwa kuhakikisha, kwamba yu pamoja nasi daima na kufanya kazi nasi hata kwa udhaifu wetu. Dhambi za watu hazisimamishi uaminifu wa Mungu. Hakuna shaka, yeye Mtakatifu atahukumu kila dhambi, si kitu ni dogo namna gani. Haki yake kamili inadai kuhukumiwa kwa kila dhambi, lakini hata hivyo upendo wake wa daima ndani ya Kristo unasafisha dhambi za wote wanaoingia ndani ya agano lake naye. Kwa kufa kwake badala yetu, Kristo alitupatia hakikisho kwamba hiyo agano tukufu imefanya kazi. Tangu hapo Msalaba ndiyo alama ya uendeleaji wa neema yake.


02.7 - Mungu, Baba yetu

Hali ya binadamu kutengwa na Mungu ilikoma kwa kuzaliwa kwake Kristo. Mungu alitokea ndani ya mwili wa binadamu, ili wafuasi wake wasiendelee tena kama watumwa, kwa vile Yesu aliwaweka huru na mapingu ya dhambi, ambazo ni minyororo ya shetani, huru pia na kifo na hata hukumu ya Mungu. Damu ya Yesu ilimwagika kuwa malipo kwa ajili ya kuwekwa huru sisi. Yeyote aaminiye ndani ya Kristo, atasafishwa na kupokelewa kama mwana au binti wa Mungu. Kwa njia ya Kristo, Mwenyezi Mungu amepata kuwa Baba yetu, kisheria pia na kiroho. Anatuthibitishia kwamba, hata tukianguka katika dhambi baya, “Mimi ndimi Bwana, Baba yako.”

Mungu, aliye Baba wa Bwana wetuYesu Kristo, anahakikisha nguvu ya Roho Mtakatifu kwa yeyote ampendaye na kumfuataYesu aliyesulibishwa na kufufuka. Waumini ndani ya Yesu waliozaliwa mara ya pili wanabeba uzima na hali ya Baba yao wa mbinguni. Hawamo tena chini ya mapingu ya kukata tamaa na ndani ya mshiko wa kifo cha kiroho. Ndani ya Kristo Mungu mtakatifu amejifunganisha mwenyewe na sisi. Ametufanya tuwe hekalu lake, mahali pa kuishi ndani yetu. Yeye ndiye Baba yetu na sisi tu watoto wake. Sisi tu mali yake na yeye amekubali kuwa wa kwetu. Agano hilo mpya limetimia kwa nguvu ya kifo cha Kristo kwa niaba yetu. Tangu hapo mwumini yeyote ndani ya Kristo anatambua uhusiano wa binafsi na Mungu uliyo karibu sana. Anapoomba basi, halii kwenye hewa tupu tu. Badala yake, maombi yake ni kama simu ya kuongea na Mungu, iliyojaa shukrani, maungamo, mambo ya kuhitaji na ya kuombea wengine. Baba yetu wa mbinguni hutusikiliza kwa makini na uaminifu. Katika ubaba wake tunapata kimbilio letu. Yeye hutuzunguka na kutulinda kwa uaminifu wake kama na ngao. Tofauti na Waislamu, wakristo wa kweli hawako mbali na Mungu wao. Hawaabudu jamii ya miungu wengi kama Wahindi, wala hawangojei utupu wa kuogofya jinsi wafanyavyo Wabudhisti.

Mungu Mwenyezi amejifunganisha mwenyewe na wafuasi wa Kristo kwa nguvu ya upendo wake, ili waweze kuishi usoni pake na kubadilishwa ndani ya mfano wake. Baba yetu wa mbinguni hakutaka kutuacha katika hali yetu isiyo na tumaini, lakini aliamua kutuokoa na kutufanya tuwe wapya. Ametuchochea kwa neno la Mambo ya Walawi,11:45: “Mwe watakatifu kwa kuwa mimi ni Mtakatifu”.Ushirikiano na Mungu haimaanishi tu imani ya kiakili, lakini pia matokeo katika mabadiliko kabisa ya tabia. Tunapoishi na Mungu misingi ya utu wetu inatakiwa kubadilishwa, kwa vile Mungu wa milele ameamua kuwapandisha watoto wake kwenye hali ya kawaida ya tabia yake. Baba yetu anatutaka tufanane naye, jinsi Yesu alivyotamka, “Mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.” (Math.5:48). Amri Kumi ndiyo hatua katika njia ya kubadilishwa kutoka kwa watu waliopotea katika hali ya watoto wa Mungu. Kwa kweli, hizo amri ni vizuio vya kutulinda tusianguke mbali, tena kwa nguvu ya neema yake.

Labda unajisikia kwamba haiwezekani kabisa kutimiza maagizo ya Kristo. Jinsi gani tutaweza kuwa wakamilifu, jinsi Mungu alivyo mkamilifu? Je, mnyororo huu haumaanishi hatua ya kurudia jaribu la Hawa kule paradiso, alipomsikia Shetani akisema, “Mtakuwa kama Mungu”? Mwanadamu hawezi kujiokoa mwenyewe, wala hawezi kubadilika kuwa mwenye haki kwa bidii yake mwenyewe. Kila namna ya kuwa haki mwenyewe inajengwa juu ya sheria zinazoamsha maasi na kupeleka kwenye hukumu. - Lakini utakaso wetu hasa ndiyo kazi njema ya Baba yetu wa mbinguni anayoitenda ndani yetu. Yeye hutuongoza kwenye njia ya unyofu wake. Yeye hutuita siku hadi siku kujikana wenyewe, naye anatuhakikishia roho zetu nguvu ya daima inayoshinda maovu ndani yetu. Yeye anatusukuma kusoma Neno lake na kutenda kufuatana nalo. Anatujalia upendo wake, ambao unageuza umimi kuwa utumishi na tuwe wahudumu. Vipawa vya kiroho vya Baba yetu vinakuwa dhahiri sana, hata Mhamadi alivithibitisha na kuwaeleza wafuasi wa Kristo kuwa watu wa pekee bila kujiona, akitamka, “wao hawana kiburi, wanaopokea ndani ya mioyo yao huruma na rehema (Suras al-Maida 5:82 na al-Hadid 57:22)


02.8 - Wokovu uliokamilika

Mungu atamani kutuweka huru na mapingu ya dhambi. Kwa tamko lake la pili katika utangulizi wa Amri Kumi anatueleza kwamba, hatuwezi kujiweka huru sisi wenyewe kutoka kwa mapingu ya dhambi. Ni Mungu mwenyewe atakayeifanya kwa njia ya utii wetu katika imani. Mungu aliwaweka huru watu wake kutoka utumwani Misri wa uchungu sana kwa njia ya Musa na kutengeneza agano tukufu nao. Mungu hakuwakubali kwa ajili ya unyofu wao, bali aliwachagua kwa njia ya neema yake. Aliwatangazia, “Mimi ndimi Bwana Mungu wenu niliyewatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka katika nyumba ya utumwa.”

Wana wa Yakobo walihamia kutoka kwa milima ya miamba yaliyo kavu na tupu, jinsi yalivyo magharibi ya bonde la Yordani. Ni miaka 3600 iliyopita, wakati wa ukame ulipoharibu eneo lao. Walihimizwa na njaa waende kwenye bonde la Naili, kama kilomita 300 mbali na nyumbani kwao. Wakawa na maisha ya unafuu kule. Kila mwaka mto Naili ulifurika na kuleta rutuba ardhini. Watoto wa Yakobo waliongezeka kule kwa haraka na wakawa kama tisho kwa watu wa Misri. Mafarao wakawatumikisha hao Waebrania wageni kuwa wafanya kazi na kuwadhulumu bila huruma. Baadhi yao walimkumbuka Mungu wa baba zao wakiwa utumwani, wakamlilia huyu Mungu awasaidie. Walikuwa wamemsahau Mungu wao nyakati za utulivu na raha, hata hivyo umaskini na haja ziliwarudisha kwa Mwumbaji na Mwopoaji wao. Basi, Mungu akasikiliza vilio vyao na kumtuma Musa, mtumishi wake. Alikuwa amemtayarisha ndani ya jumba la mfalme Farao, pia na jangwani, ili aweze kutimiza wito wake. Mungu alimtokea Musa ndani ya kichaka kilichowaka moto bila kuteketea kwa ile moto. Mungu alijifunua kwa Musa kuwa ni “Mimi ndimi”, maana yake, “Mimi niko ambaye niko”. Na zaidi,”Mimi sibadiliki, bali naendelea kuwa mwaminifu kwako”. Kwa hiyo, “Mtanitafuta MIMI na kuniona MIMI, mnaponitafuta kwa moyo wenu wote.” (Yer.29:13).

Basi Mungu alimtuma Musa kwake Farao mkuu, aliyejiona kuwa mungu wa ki-misri; alienda amtake kuwaruhusu Waebrania hao wafanya kazi wao waliotumikishwa. Lakini mtawala wa bonde la Naili hakutaka kuwaruhusu hao wafanya kazi wake rahisi. Alifanya gumu moyo wake zaidi na zaidi. Farao hata baada ya muda hakuwa tayari kuwaachilia huru hao wana wa Ibrahimu hadi Mungu alimlazimisha kufanya hivi kwa njia za tauni na mateso. Mwishoni waliachiliwa huru kutoka kwa utumwa wa Misri, si kwa sababu ya haki zao wenyewe, lakini kipekee kwa sababu ya utii wao wa kiimani. Hawakuwa na siliaha kali. Wakakimbia usiku kuelekea jangwani wakiwa chini ya kilindo cha damu ya kondoo ya Pasaka iliyochinjwa kwa ajili yao. Kondoo moja alichinjwa kwa kila familia. Walikula nyama ya kondoo, ndipo wakatoroka katika nguvu za Mungu. Kwa kuvuka Bahari ya Shamu na kuangamizwa kwa maadui waliowafuatia ndiyo thibitisho la mwisho kwamba, wameokolewa na utumwa. Siku hizi twaweza kuangalia mumiani ya Farao yule aliyezama akiwa na majani ya maji ya Bahari ya Shamu ndani ya mapafu yake; anaonyeshwa hivi kwenye nyumba ya kuhifadhi mambo ya kale mjini Kairo, Misri.

Waislamu husifu ushindi wao juu ya maadui zao kwa ajili ya Mungu wao kuingilia kati.

Hata hivyo, Mhammadi aliwahi kuwa na ushindi juu ya wafanya biashara wa Makka katika vita ya Badr, wala si kwa ajili ya kuingilia kati kiajabu kwa Mungu wao, lakini kwa sababu ya silaha zao. Wafuasi wake walitoa dhabihu ya kila kitu walichokuwa nacho. Kwa hiyo si ajabu waliwapiga adui zao! Jambo ambalo Musa analieleza kuwa wokovu tukufu la ki-mwujiza (ambapo hakuna hata tone la damu lililomwagika), jambo la namna hii upande wa Uislamu inajulikana kuwa vita takatifu (jihad), na kila mtu anatakiwa kujiunga. Basi kanuni ya kuthibitisha kuwa ni la haki inasimama, wakieleza,”Wewe hukuwaua, bali Allah aliwaua. Haukuwa wewe uliyerusha mshale, bali Allah alirusha” (Sura al-Anfal 8:17).

Haya basi, baada ya Bwana kuwaweka huru Waisraeli kutoka kwa utumwa wa Misri, aliwaongoza kwenye joto kali ya jangwa kavu akawatayarishia sikukuu. Alitaka kukamilisha lile Agano tukufu nao, ili waweze kupata kuwa takatifu katika ushirikiano na yeye. Aliwaita wawe taifa la kikuhani kwa kumtumikia. Walitakiwa kuwa na huduma ya kupatanisha mbele ya kiti chake cha enzi kwa ajili ya watu wote. Hapo Amri Kumi zilikuwa moyo wa kitabu cha Agano, pia kuwa kanuni la dhahabu kwa ajili ya ushirikiano wao na Bwana wao. Mungu aliwekwa kwenye kiti cha enzi juu ya vibao viwili vya amri zake, zilizotunzwa ndani ya sanduku la agano.


02.9 - Wokovu katika Agano Jipya na shabaha ya Amri Kumi

Tunapozingatia juu ya ushindi wa kimwujiza, ambalo Mungu aliwapatia Watoto wa Yakobo miaka 3.300 iliyopita, ndipo kulilinganisha na wokovu, ambalo Yesu alilikamilisha ndani ya Agano Jipya, tunaweza kujumlisha mwanzo wa Amri Kumi jinsi ifuatavyo: “Mimi ndimi Bwana, Mungu na Baba yenu, nami nimewaokoa hata milele.”

Tangu Yesu alipoingia ndani ya dunia yetu na kubeba dhambi ya wanadamu wote msalabani, akifa kama Kondoo wa Mungu kwa ajili yetu, sisi tunatangaza rehema ya Mungu kwa mataifa yote na kumhubiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi kwa ajili ya watu wote.Yesu alivunja minyororo ya dhambi na kushinda utawala wa Shetani kwa njia ya mateso yake na kutufia msalabani. Alimalizisha kabisa ghadhabu ya Mungu na kubeba hukumu kwa niaba yetu. Wokovu wetu kamili ulikamilishwa kipekee kwa njia ya Kristo. Ndiyo maana tunatakiwa kumshukuru sana na kupokea ukombozi wake katika imani.

Ukombozi wa Mungu ni tayari, tena imetayarishwa kwa ajili ya kila mtu. Tumeokolewa kwa njia ya kipekee, ambayo haikutumia silaha. Ni kweli, damu ilimwagika, lakini haikuwa damu ya adui aliyeshambuliwa, bali ni damu ya mwana pekee wa Mungu, aliyejitoa mwenyewe kuwa sadaka kwa ajili yetu.

Hatukuweza kujiokoa wenyewe kwa kushika Amri Kumi; wala hii si kusudi lake. Lakini zinatufundisha sisi tuliookolewa, jinsi tuwezavyo kutoa shukrani kwa ajili ya wokovu uliyopokelewa bure. Yeyote anayefikiri kwamba, anaweza kujiokoa mwenyewe kutoka kwa dhambi, Shetani, kifo na ghadhabu ya Mungu kwa njia ya bidii yake ya kibinadamu, atakuwa amepotea kabisa. Kwa kweli, anajitoa mwenyewe kwa mapingu ya dhambi zaidi na zaidi. Amri Kumi haziwezi kutuongoza kwa kupata wenyewe utakatifu. Bali zinatuongoza kwenye haja ya kutubu na kwenye utii wa imani, tukifurahia habari ya wokovu uliokamilishwa. Twaweza kutimiza kusudi la Amri za Musa, tunapomtukuza Baba wa mbinguni pamoja na Yesu katika nguvu za Roho Mtakatifu. Mungu hakusudii kutuhukumu au kutulaani au kuzifanya Amri Kumi kuwa mzigo mzito wa kutukandamiza. Kwa hakika, sivyo! Bwana wetu alipanga wokovu wetu mapema sana kabla ya ufunuo wa Amri. Alitoa Amri zake ili kuwaongoza waliookolewa wapate kutubu na kubadilisha kabisa uasi wao kuwa unyenyekevu ndani ya upole wa Roho Mtakatifu. Kwa sababu hiyo, kusudi la Amri ni ushirikiano wetu na Mungu Baba yetu, wala si kuangamizwa kwetu katika hukumu ya mwisho.

Sisi tungalielewa bora zaidi habari ya Amri Kumi, kama tungaliwahi kuwa watumwa. Kama watumwa tungaliteseka bila kujali jinsi tulivyojisikia, kuwa wagonjwa au wazima, vijana au wazee. Tungalilazimishwa tu kuchapa kazi kwa hali yoyote ile isiyobebeka. Kama watumwa tungalivaa namba tu, na hakuna kabisa, ambaye angalitujali.

Mungu aliwaweka watu wake huru kutoka kwa hali ya duni na maumivu. Kwa sababu hiyo tunahesabu Amri Kumi kuwa ni kitabu cha kuwaongoza Wakristo waliowekwa huru, ili waweze kujifunza kutenda masafi na yenye hekima katika uhuru wao. Bado kuna majaribu mengi zinazojibanza ndani ya uhuru. Tukiishi pasipo Mungu, haraka tutakuwa watumwa wa tamaa zetu sisi wenyewe na dhambi. Hata hivyo, Mungu alimwumba mwanadamu katika sura yake. Bila Mungu mtu hawezi kuishi maisha ya haki. Hakuna uhuru kamili pasipo Mungu.

Mtu anapoishi katika dhambi, atakuwa ni mtumwa wa ile dhambi. Dawa za kulevya, tamaa za uzinzi, kuiba, uvivu, kunyang’anya au ukorofi zitakuwa ni jela yake. Wengine wako katika maumivu ya ujanja, kama vifungo vya vinywaji vileo, kuvuta tumbako, dawa za kulevya au hata kuzoea kabisa kusema uongo, bila hata kutaja mambo ya ubashiri na roho baya. Shetani huwa anacheza na akili zao. Lakini basi, Yesu amweka huru yeyote amwaminiye, atawaweka huru ndani ya uhuru takatifu ya watoto wa Mungu. Kristo ndiye Mshindi wa kweli, Bwana wa kuokoa, Mganga mwenye hekima, Mchungaji Mwema pia na Rafiki mwaminifu. Hakuna awezaye kumfikia bila kupokea msaada na ushauri.

Amri Kumi ndiyo ukuta wa kulinda kwa wale waliowekwa huru kwa neema. Mungu amepata kuwa Baba yao, Kristo kuwa Mwokozi wao na Roho Mtakatifu Mfariji wao. Wamepata kumwelewa Mungu kuwa Baba yao, ambaye pamoja na Mwana na Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu mmoja. Wamekwisha kutambua namna ya kuwekwa huru kweli ndani yake wakiwa na shukrani na amani. Basi si ajabu, Amri kumi kwao zimepata kuwa alama ya uongozi wa Mungu kwao, ambazo ndani yao inaumbwa wimbo wa sifa kuwavusha kwenye jangwa ya maisha yao (Zab. 119:54).

www.Waters-of-Life.net

Page last modified on August 01, 2017, at 02:01 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)